ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 20, 2018

HIKI HAPA KICHUPA KIPYA ALICHOSHIRIKISHWA DIAMOND PLATNUMZ NA MORGAN HETITAGE - "AFRICA JAMAICA"For Immediate Release 
Oct 19TH 2018 ... 

PRESS RELEASE:

MORGAN HERITAGE RELEASE “AFRICA JAMAICA” FEAT. DIAMOND PLATNUMZ & STONEBWOY 

Grammy-award winning music group: Morgan Heritage have released “Africa Jamaica”—the anticipated music video and collaboration featuring East Africa’s top music act: Diamond Platinumz and Ghana’s music gem / Dancehall King: Stonebwoy.

An elated Morgan Heritage talk on what makes their latest release special: “Releasing ‘Africa Jamaica’; our first video shot in Africa is a historic moment in our career, that will forever live in our hearts. It was a joy to work with Diamond Platnumz and Stonebwoy— Africa’s best from East to West. We hope the people in Africa and around the world will love the music video,” adding, “We love discovering new sounds and making connections through our music and I believe we are doing just that moving on.” 

Watch: “Africa Jamaica” on YouTube

They also added, “The video is an exciting fun display of where our culture comes from in Jamaica. The spirit, the dancing and the culture all comes from Africa. It truly captures your attention from start to finish. It was also an honour for us to work with Stonebwoy for a second time since our Grammy-nominated album Avrakedabra.”

Morgan Heritage and Diamond Platnumz first linked up for the “Hallelujah” collaboration that garnered over 1 Million YouTube views in 24 hours. Diamond says, “It is always a vibe working with my brothers Morgan Heritage. This is our second song together and I am excited that we have made yet another mega-hit for our fans. Last time we made a world-class hit so you definitely have to watch out for this new video. 

“Africa Jamaica” is the lead single off Morgan Heritage’s upcoming album set for release in 2019. Directed by Jordan Hoechlin and Morgan Heritage, the music video of “Africa Jamaica” was shot in Ghana with captivating scenes from Cape Verde taken during Morgan Heritage’s trip to Ghana.

FOR MORE:

Follow Morgan Heritage:

#AFRICAJAMAICA

To schedule an interview with Morgan Heritage, Africa media can contact Anyiko PR via email: press@anyiko-pr.com | Whatsapp No. +254 770 360 087 or call + 254 721 368 983


NDOTO ZA MBUNGE WA KWIMBA NI KUONA SHULE ZA VIJIJINI ZINAGEUKA KUWA KIMBILIO LA ELIMU BORA.

NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR, amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 4 kwa ajili ya kukarabati na kuboresha miundombinu ya Shule ya Sekondari Ngudu iliyopo wilayani humo. 

Akipokea mchango huo wakati wa mahafali ya 2 ya kidato cha 4 Mwenyekiti wa shule hiyo, FEISALL YASIN, amempongeza mbunge huyo, kwa namna ambavyo amekuwa akijitolea katika masuala mbalimbali ya maendeleo, na sasa amerudi tena kuikwamua shule hiyo ili vijana wanaosoma shuleni hapo wapate nafasi ya kutimiza ndoto zao.

"Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi nakumbuka Mhe. MANSOOR, alitumia zaidi ya shilingi milioni 100 toka kwenye mshahara wake, wakati akiwa diwani wa kata yetu ya Ngudu kuhakikisha swala la elimu linasonga mbele. Hii leo amerudi tena, huu ni moyo wa kizalendo na wakipekee" alisema FEISAL na kisha akaongeza.

"Shule nyingi vijijini zina vijana wengi wenye akili na wabunifu lakini wanakwamishwa na changamoto zilizopo kwenye shule zetu, kama vile ukosefu wa maabara na vitendea kazi vyake, vitabu vya kutosha, miundombinu ya kutosha yakiwemo majengo ya ofisi za waalimu na madarasa, uchache wa shule za sekondari ni chanzo cha kushindwa kupata matokeo mazuri ambapo husababisha wanafunzi wetu kusafiri umbali mrefu na kufika shuleni wakiwa wameshachoka"
Licha ya kuipongeza Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI, kwa kutoa elimu bila malipo, Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. SHANIF MANSOOR, amesema ni kwa kipindi kirefu amekuwa na ndoto ya kuona jimbo lake likifanya vyema katika utoaji wa elimu na ufaulu na hata baadaye kuwa mfano wa kuigwa sanjari na kugeuka kuwa kimbilio kwa wazazi wa wilaya na mikoa mbalimbali nchini linapokuja suala la elimu. 

Katika kukuza michezo shuleni hapo Mbunge huyo amewapatia mipira 8, pamoja na kuwajengea magoli katika  uwanja wao wa soka.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, NIKIA ALLY, amewataka wazazi kuacha mara moja kuoza watoto kwani ni moja ya vyanzo vinavyo warudisha nyuma kimaendeleo na kuchangia umasikini, akisisitiza kuwa hato muonea haya yule yeyote atakaye kutwa na hatia ya kujihusisha au kushiriki kufanikisha vitendo hivyo.

Zaidi ya wanafunzi 50 wilayani Kwimba mkoani Mwanza, wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na mimba zisizo tarajiwa.

Pamoja na kufanya vizuri katika masomo ya sayansi, shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa waalimu kumi wa somo la Sayansi.


Shule ya Sekondari Ngudu inazaidi ya wanafunzi 1100 huku wanafunzi 400 wakiishi bweni.

VIDEO: SILAHA ZA KIVITA ZAKUTWA KWENYE GARI LILILOTUMIKA KUMTEKA MO DEWJI.


Kamanda wa jeshi la polisi nchini, IGP. Simon Sirro amethibitisha kupatikana kwa silaha hatari kwenye gari ambalo linalodaiwa kuwa ndio lilitumiwa na watu waliomteka mMohammed Dewji. Miongoni mwa silaha hizo zilizopatikana kwenye gari hilo ni bunduki aina ya AK-47 pamoja na risasi zake 19, pastola tatu pamoja na risasi zake 16.

TAARIFA YA AWALI.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu Mo, aliyepatika leo baada ya kutekwa Oktoba 11, 2018, amesema watu waliokuwa wamemteka walikuwa wanataka fedha.

Akiongea leo nyumbani kwa baba yake Mo ambako alifika kumuona mfanyabiashara huyo, amesema amemweleza kuwa moja ya sababu ya kutekwa kwake ni fedha ambapo watekaji walikuwa wanataka wapewe fedha.

''Mo ameniambia tangu alipotekwa alikuwa amefungwa mikono, miguu na kufunikwa macho, lakini pia walimsimamia sana kwenye suala la kula lakini sababu kubwa watekaji walikuwa wanataka fedha ila walikuwa na hofu ya kumpigia baba yake wakiamini jeshi la polisi litawafikia'', amesema Mambosasa.

Mambo sasa ameongeza kuwa baada ya taarifa za jana kutoka kwa IGP Sirro kubaini gari lililotumika kumteka, zimesaidia kumpata mfanyabiashara huyo kwani wahusika waligundua wamekaribia kunaswa.

Kamanda Mambosasa pia amethibitisha kuwa gari lenye namba za usajili T 314 AXX, ambalo walilibaini kutumika kumteka Mo, likiwa na namba za nchi jirani AGX 404 MC, ndio hilo limetumika kumtelekeza katika eneo la Gymkhana jijini Dar es salaam.


Amemaliza kwa kusema baada ya kutupwa pale Gymkhana, walinzi wa eneo hilo walimuona na kumtambua kama ni Mo, ndipo wakamfungua kamba alizokuwa amefungwa kisha akawatajia namba za simu za baba yake na walipompigia mzee Dewji akafika na familia kumchukua.

Friday, October 19, 2018

VIDEO:- MWANAFUNZI NA MWALIMU MAJERUHI WA RADI GEITA WASIMULIA KILICHOTOKEAGSENGOtV

MWANAHABARI wetu Albert G. Sengo tayari amesharejea jijini Mwanza kutokea mkoani Geita ambako huko Kazi na Ngoma iliweka Kambi ya Siku Moja tu (JANA) kuripoti taarifa ya ajali ya radi iliyouwa wanafunzi 6 na majeruhi kadhaa. 

WANAFUNZI WALIOFARIKI 

1. YUSRA AUNI 
2. GLORY GILBERT
3. ABDUL BUNDALA
4. CHRISTIAN ORICK
5. JACKLINE JOSEPHAT
6. WILLIAM EMIL

LEO ni nafasi ya kumalizia yaliyojiri jana baada ya mazishi ya baadhi ya watoto, hali ya majeruhi inaendeleaje, kipi kinachoendelea leo na vipi hatua gani zilizochukuliwa kwa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa ili watoto warejee na masomo bila woga.

MKUU WA WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA SENYI NGAGA, AMPONGEZA MANSOOR.

 NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV


Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga, ameambana na mbunge wa jimbo la kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR, kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mwamashimba kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na Serikali kwa kiasi ya shilingi milioni 400.

Licha ya kujitolea nguvu kazi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati Mhe. NGAGA amewataka wananchi wa Mwamashimba kusimamia kimilifu mradi huo, katika kuulinda kuondokana na uharibifu wa wachache wenye nia ovu.

NGAGA, amepongeza Mhe.SHANIF MANSOOR, kwa jitihada zake binafsi za kuisaidia Serikali kuchochea maendeleo ya Jimbo lake akisema kuwa  hakika huo ndiyo uzalendo ambao iwapo ungeigwa na watanzania wengi taifa hili lingekuwa kama peponi.

Sanjari na kuahidi kusimamia vyema miradi ya maendeleo, wananchi wa Mwamashimba wamepongeza juhudi za Mhe. SHANIF, kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ikiwa ni pamoja na kufungua barabara za ndani na zinazoingia katika tarafa ya Mwamashimba, hali ambayo wameitaja kuwa itachochea kasi ya maendeleo katika jimbo lao.

Mbunge wa jimbo la kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR, akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajenzi mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mwamashimba.
Uongozi ni mfano safu ya viongozi walioambatana kwenye ukaguzi ilifanya usaidizi kupanga matofali ya ujenzi wa kituo cha afya Mwamashimba, huku akishuhudiwa na Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR na wadau wengine.
Hatua za ukaguzi zikiendelea.
Wananchi wa kata ya Mwamashimba wakiwa kwenye kusanyiko la kujadili shughuli za maendeleo yao.Mbunge wa Kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR akizungumza na wananchi kata ya Mwamashimba mara baada ya kutembelea kituo cha Afya Mwamashimba kujionea maendeleo ya ujenzi.
Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga, akizungumza na wananchi kata ya Mwamashimba.
Safu ya mbele ni akinamama na nyuma akinababa kwa umakini ndani ya kusanyiko wakifuatilia kinachoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga, akizungumza na wananchi kata ya Mwamashimba.

DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO


Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mtambo wa kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018. Mwingine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), alipotembelea na kukagua kiwanda cha Darsh jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.

Na Mathias Canal-WK, Mseke-Iringa

Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250 za nyanya kwa siku.

Waziri Tizeba ametoa mwito huo jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Kiwanda hicho kinafanya shughuli za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.

Waziri Tizeba, aliwataka wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza tija katika kipato chao na jamii kwa ujumla.

“Wakulima wa nyanya hapa Igwachanya na hata katika maeneo mengi nchini wanalima kwa kutegemea mvua na uzalishaji huwa mdogo na usiokidhi mahitaji ya soko hivyo nawasihi kuongeza uzalishaji wa nyanya kwani soko la uhakika lipo” Alikaririwa Dkt Tizeba

Kadhalika, Waziri wa kilimo aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza wigo wa ununuzi wa nyanya katika mikoa mingine ya uzalishaji ikiwemo mkoa wa Dodoama na Singida.

Awali akisoma taarifa ya kiwanda hicho mbele ya mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhimiza sera ya uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto chache zinazojitokeza hivyo kuendelea kulinda maslahi mapana ya Taifa.

Alisema uanzishwaji wa kiwanda hicho ulitokana na ushawishi uliopatikana kutoka kwenye muunganiko wa wajasiliamali vijijini (MUVI) na Techno Serve walipotembelea kiwanda cha Darsh Mkoani Arusha.

Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alimpongeza waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba kwa kutenga muda wake na kukubali kufanya ziara Wilayani Iringa ili kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa nyanya nchini.

OPRAS NI NJIA MUHIMU YA KULETA UFANISI WA WATUMISHI.

 Mkurugenzi wa Utawala wa Tume wa Utumishi wa Walimu Moses Chitanda, alipokuwa akifungua mafunzo ya OPRAS kwa Maafisa Elimu wa Mkoa wa Manyara jijini Dodoma.
 Mwakilishi kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma, PS3 Geoffrey Lufumbi, akitoa maelezo ya utangulizi na jukumu la mradi huo wakati wa mafunzo hayo ya OPRAS (Picha zote na Atley Kuni-OR TAMISEMI).
 Mmoja ya Wawezeshaji wa Kitaifa kuhusu Mafunzo ya Mfumo wa OPRAS Nicodemas Tindwa akitoa mada katika Semina hiyo ya siku mbili jijini Dodoma
 Mmoja ya Washiriki wa Mafunzo hayo Bibi Tarimo, Afisa Elimu Sekondari kutoka Wilayan Hanang mkoani Manyara akichangia mada katika mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo ya OPRAS Yanayo wakutanisha Maafisa Elimu wa mkoani Manyara wakifatilia kwa makini Mafunzo hayo.


MASAUNI AZISHUKIA SHULE ZENYE MAGARI MABOVU ZANZIBAR

 Naibu   Waziri   wa   Mambo   ya   Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti waBaraza la Taifa la Usalama  Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati   ya   Uzinduzi     wa   Kampeni   Maalumu    ya   Usalama   Barabarani  na Udhibiti     wa     Ajali     katika     Uwanja     wa   Skuli   ya   Jang’ombe,   leo   VisiwaniZanzibar. Picha na  Wizara  ya Mambo ya Ndani  ya Nchi.

 Mwanafunzi   wa   Shule   ya   Msingi   Jang’ombe, Aisha Abdallah Haji, akiulizaswali  linalohusiana  na  uvukaji  wa  barabara kwa watu wenye ulemavu wakatiwa   Uzinduzi   wa    Kampeni   Maalumu   ya Usalama Barabarani na Udhibiti waAjali katika  Uwanja  wa  Skuli  ya  Jang’ombe, iliyozinduliwa  leo Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae  pia  ni  Mwenyekiti  wa  Baraza la Taifa laUsalama   Barabarani,   Mhandisi   Hamad   Masauni   (hayupo   pichani),   VisiwaniZanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Wanafunzi  wakifurahia  jambo wakati  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndaniya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza   baada   ya   kuzinduaKampeni   Maalumu   ya   Usalama    Barabarani   na     Udhibiti wa  Ajali   katikaUwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo   Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara  yaMambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu   Waziri   wa   Mambo   ya   Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti waBaraza     la     Taifa     la     Usalama     Barabarani,   Mhandisi     Hamad   Masauni,akimkabidhi   Mwalimu   Mkuu   wa   Shule   ya   Msingi   Jang’ombe,   Tiffy   Mustafa(kushoto),   moja   ya   kikoti   maalumu   watakachokua   wanavaa   wanafunzi watakaoteuliwa     kuwasaidia     wenzao   kuvuka   barabara     baada   ya   kuzinduaKampeni   Maalumu   ya   Usalama   Barabarani   na   Udhibiti   wa   Ajali katika Uwanja   wa   Skuli   ya   Jang’ombe,   leo   Visiwani   Zanzibar.   Picha   na   Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi     wa   Taasisi     inayojishughulisha     na     masuala     ya     usalama barabarani, Pily   Hamisi     Layda   (kushoto)    akimkabidhi    Naibu    Waziri     waMambo    ya   Ndani ya Nchi,  ambae pia  ni  Mwenyekiti wa Baraza  la Taifa laUsalama  Barabarani,  Mhandisi    Hamad     Masauni,   mpango   kazi   wa   KampeniMaalumu   ya Usalama   Barabarani   na   Udhibiti wa Ajali iliyozinduliwa   katikaUwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo   Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, amewatadharisha wamiliki wa shule zinazotumia magari mabovu kubebea wanafunzi ikiwa ni kinyume na sheria za usalama barabarani hali ambayo inaweza kupelekea ajali.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni Maalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, Naibu Waziri Masauni aliwataka wamiliki wa shule kuhakikisha wanatumia mabasi imara ili kuepusha ajali na kuwaasa madereva wa magari hayo kufuata sheria za barabarani “Wamiliki wa shule wanatakiwa wafuate sheria kwa kuacha kutumia mabasi mabovu na kujaza wanafunzi kupita kiasi na tutatumia kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha wanafunzi wanakua salama muda wote wakiwa wanaenda shule na kurudi nyumbani.

“Nawaagiza askari wa usalama barabarani kusimamia sheria ili wamiliki watakao kiuka sharia hizo waweze kuchukuliwa hatua pamoja na madereva watakaobainika kuendesha magari mabovu ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi,” alisema Masauni

Akitoa ripoti ya matukio ya ajali za barabarani Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Shukuru Amir Ally alisema jumla ya ajali 229 zimeripotiwa ndani ya mwaka huu tofauti na mwaka 2017 ambapo jumla ya ajali 391 zikiripotiwa huku akitoa siri ya kupungua kwa ajali hizo ni ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau wa usalama barabarani.

Akisoma risala ya uzinduzi huo Mkurugenzi wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya usalama barabarani ya New Vision, Pily Hamis Ladya alisema wamedhamiria kufikia mikoa yote ya Zanzibar na katika awamu hii ya kwanza wanaanza na shule kumi huku akiahidi kuzifikia shule zote katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi.

“Tunategemea kutoa elimu hii ya usalama barabarani ili kuweza kuwaepusha na kuwalinda wanafunzi wetu na majanga ya barabarani ili waweze kwenda shule na kurudi nyumbani salama,”  alisema

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WACHEJAZI WA TIMU YA TAIFA STARS.IKULU DSMGSENGOtV

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anakutana na wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) na baadaye kula nao chakula cha mchana Ikulu Jijini Dar es Salaam.Oktoba 19,2018

Thursday, October 18, 2018

"LAITI KAMA NINGEMSIKILIZA MWANANGU YASINGENIKUTA HAYA" ASEMA BABA WA MMOJA WA WATOTO 6 WALIOFARIKI KWA RADI GEITAGSENGOtV

Baba wa marehemu Yusra Ayuni aitwaye Auni Idrisa Ramadhani anasema tukio la kifo cha mwanaye mara ya kwanza wakati akipata taarifa alilipokea kwa mshtuko mno.

"Ingawa kifo si jambo geni lakini mazingira yake wakati mwingine yanaweza kukufanya ukajiuliza maswali mengi na kuishia kujilaumu" Anasema Auni
Marehemu Yusra Ayuni mwanafunzi wa darasa la pili aliyefariki kwenye ajali ya radi shule ya msingi Emaco iliyopo mkoani Geita..

Na kisha kuongeza "Siku ya tukio Yusra alikuwa akijibizana na mama yake, kwamba yeye hataki kwenda shule......lakini mwishoweikabidi aende.........Labda asingeenda asingefariki......"


Wengi wamejitokeza nyumbani kwa wazazi wa Marehemu Yusra Ayuni mwanafunzi wa darasa la pili aliyefariki kwenye ajali ya radi shule ya msingi Emaco iliyopo mkoani Geita kwaajili ya shughuli za mazishi..
Taratibu zinaendelea nyumbani hapa.
Akinamama wakiwa kwenye majonzi kwenye ibada ya marehemu Yusra Ayuni..
Mazishi yamefanyika leo kwenye makaburi ya waislamu Mkoani Geita. 
Sehemu ya wahudhuriaji katika mazishi ya Marehemu Yusra.
Hatua ya mazishi ikiendelea kumzika marehemu Yusra Ayuni mwanafunzi wa darasa la pili aliyefariki kwenye ajali ya radi shule ya msingi Emaco iliyopo mkoani Geita..
Safiri salama.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA 5 AJINYONGA SENGEREMA.


Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Shule ya Sekondari ya Sengerema aitwaye Ayoub Yahya Petro (19), mwenyeji wa Kyerwa mkoani Kagera, amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya chandarua aliokua ameifunga kwenye mti uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa shule hiyo, iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Tukio hilo limetokea leo Oktoba 18, 2018 majira ya saa 12: 00 asubuhi, hii ni baada ya wanafunzi wenzake kupita eneo la uwanja wa shule kisha kuona mwili wa marehemu Ayoub aliyekuwa akisoma mchepuo wa PCB, ukiwa unaning’inia juu ya mti na kutoa taarifa kwenye uongozi wa shule ambao ulifikisha taarifa hizo kituo cha polisi.

Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya DDH Sengerema kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na kwamba linatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

MKUU WA SHULE WALIOFARIKI WANAFUNZI 6 KWA RADI ANASEMA ALIGUNDUA TUKIO HILO MARA BAADA YA KUHISI HARUFU ILIYOMTATIZA.GSENGOtV

Taarifa ya vifo vya wanafunzi 6 wa shule ya msingi Emaco mjini Geita na wengine 25 kujeruhiwa, baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani imestua wengi.

Jembe fm kupitia kipindi chake cha #KAZINANGOMA mapema kabisa leo imekuwa mjini Geita na kupeperusha matangazo LIVE kutoka eneo la tukio.

Sanjari na kutoa pole, kungumza na Uongozi wa Shule, Waathirika na familia zilizopoteza watoto pamoja pia tumefanya juhudi kujaribu kuona nini kifanyike kwa majanga haya yasije jirudia.

Kuhusu tukio:- Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Octavian Lawrian anasema wakati akikagua mazingira ya shule kuhakikisha kwamba wanafunzi hawachezi kwenye mvua aligundua tukio hilo mara baada ya kuhisi harufu iliyomtatiza.

MIFUGO INAYOZAGAA MJINI SASA KUPIGWA BEI.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza imetangaza kukamata na kuuza kwa mnada mifugo kama vile Ng'ombe, Punda, Mbuzi, Kondoo na mingine jamii hiyo endapo itakutwa imezagaa ovyo maeneo ya mjini.

Katika taarifa yake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani hapa, John Wanga imeeleza kuwa kwa mujibu wa ufuguji wa mifugo hiyo itaendana na kibari kutoka halmashauri ambapo anayefuga mifugo aina hiyo anaamriwa kuiondoa mpaka kufikia Oktoba 31, 2018,  atakayekiuka atawajibishwa kisheria bila taarifa zaidi.

Wanga ametahadharisha endapo itatokea mtu au taasisi yoyote itaachia mifugo aina ya Ng'ombe, Mbuzi, Kondo, Punda na mingine inayofanana na hiyo kuzagaa ovyo katika maeneo ya mjini, halmashauri itawakamata wanyama hao ikiambatana na  utozwaji wa faini kiasi cha shilingi 50,000/= kwa kila mfugo na kila siku ambapo mfugo utakuwa umehifadhiwa, huku ikiuza kwa mnada baada ya siku tano tangu kukamatwa.

Aidha katazo hilo limeendana na sheria ndogo za usafi (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, tangazo la serikali NA. 364 la mwaka 2014 pamoja na kanuni za kuondoa adha na usumbufu mijini, (Tangazo la Serikali la Mwaka 2008).

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi  vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019 katika kanda za magharibi, kati na nyanda za juu kusini.

Maeneo yatakayoathirika na mvua hizo za juu ya wastani hadi wastani ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kusini mwa Morogoro, Lindi na Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 18, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi amesema  utabiri huo ni kwa mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.

"Katika kipindi cha mvua za msimu hali ya unyevunyevu wa udongo kwa ustawi wa mazao na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi,” amesema.

"Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi kama vile mahindi, maharage na mtama yanaweza kuathiriwa na hali ya unyevunyevu wa kupitiliza na maji kutuama.”

Kutokana na mvua hizo, Kijazi amewatahadharisha pia wachimbaji wa madini hasa wadogo kuwa makini na ongezeko la maji linaloweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi au maji kujaa kwenye mashimo.

Pia, amezishauri mamlaka za miji na majiji kuchukua tafadhali kwa kuhakikisha mifumo ya kupitisha maji inafanya kazi ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko yanayogharimu maisha ya watu na uharibifu wa miundombinu.

HONGERA MWANA FA + RICHIE KWA UTEUZI HUU WA MWAKYEMBE. Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe ameteua wajumbe watano wa BASATA  akiwema Msanii wa Bongo Flava Hamis Mwinjuma, Mwana FA pamoja na msanii wa Bongo Movie Single Mtambalike, Richie.Wednesday, October 17, 2018

HIVI NDIVYO MILA NA DESTURI ZINAVYOCHANGIA ONGEZEKO LA MIMBA ZA UTOTONI NA KUSHUKA KIWANGO CHA ELIMU WILAYANI TARIMEGSENGOtV

Mila na Desturi zinatajwa kuchachangia kwa kiwango kikubwa mimba za utotoni na kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani Tarime nini sababu, wapi tunakosea kama jamii?

Wakizungumza wakati wa mkutano baina yao na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana la KIVULINI, wazee hao wameahidi kumfichua yeyote atakayebainika kumkeketa mtoto wa kike ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wazee wanaosimamia mila na desturi kutoka koo 12 za Kabila la WAKURYA Wilayani TARIME Mkoani MARA pamoja na Mangariba kutoka koo hizo wametangaza kuachana na ukeketaji wa watoto wa kike baada ya kutambua kuwa vitendo hivyo vinamuondolea haki utu na heshima mtoto wa kike.


Madiwani,Viongozi wa Dini, Wanaharakati, Wazee wa Mila, Mangariba, Viongozi wa kata pamoja na Maafisa elimu wilayani Tarime wacha wenyewe wafunguke. 

WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI.

Kwa mujibu wavyombo vya habari vya ndani zaidi ya watu 6 wahofiwa kufariki na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa baada ya treni kuacha njia  karibu na mji mkuu wa Morocco, Rabat, siku ya jumanne.

Ajali ilitokea katika mji wa Sidi Bouknadel uliopo katikati ya Rabat na mji wa kaskazin magharibi wa Kenitra.

Picha zilizosambazwa kwenye kurasa za kijamii zinaonyesha mabehewa yakiwa yamepinduka, pia baadhi ya video zinaonyesha raia wema wakijaribu kutoa msaada.

"Uchunguzi umeanza kufanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo" ilisema taarifa iliyotolewa na mahakama kuu ya Morocco.

MHE.PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA, JAJI MKUU WA TANZANIA ATEMBELEA MAHAKAMA YA WILAYA YA KWIMBA..


 NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. IBRAHIM HAMIS JUMA leo ametembelea mahakama ya wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza, kujionea mazingira na changamoto zilizopo ainazokwamisha utendaji katika maeneo mbalimbali  ya mahakama ya mwanzo wilayani humo.

Akiwa katika ziara yake ya siku 4 ya kikazi mkoani hapa, Prof. IBRAHIM, amekutana na watumishi wa mahakama hizo ili kupokea mawazo na na kuona jinsi gani Serikali inaweza kutatuwa changamoto zinazowakabili.

Kwenye ziara yake hiyo Prof. IBRAHIM HAMIS JUMA, amepokelewa na mwenyeji wake Mhe. Shanif Mansoor, Mbunge wa Jimbo la Kwimba na Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo Senyi Ngaga.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiteta jambo na  mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR,

Mmoja kati ya watendaji wa mahakama wilayani Kwimba akitoa maelekezo.
 Moja kati ya changamoto alizozibaini kwenye ziara hiyo ni pamoja na upungufu wa watumishi, uchakavu wa miundombinu, uhaba wa majengo ya mahakama na ofisi za watendaji wake pamoja na vitendea kazi kulingana na kasi ya maendeleo ya teknolojia. 

, Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Hamis Juma akipata picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama.