MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KWENDA CHA TANO KITAIFA NA MKOA WA MWANZA .
*Kitaifa sekondari ya wavulana imeshika nafasi ya Pili kati ya sekondari 2,322 na Mkoa imekuwa ya Kwanza kati ya sekondari 174.
*Kitaifa sekondari ya wasichana imeshika nafasi ya 13 kati ya sekondari 2,322 na Mkoa imekuwa ya Pili kati ya sekondari 174.
*Wanafunzi wamepata daraja la Kwanza na Pili (Division one na two) hakuna la tatu, nne au waliofeli.
* Masomo waliofanya vizuri ni Uraia, Historia, Biologia, Kemia, Kingeleza, Hesabu na Biashara.
SEKONDARI za Alliance, Wavulana na Wasischana za jijini Mwanza zimeongoza nafasi ya kwanza naya pili kwa shule za sekondari za serikali na binafisi mkoani Mwanza, baada ya kutangazwa hivi karibuni.
Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya Nyamwaga Ltd ya jijini Mwanza inayopilikia Shule za Sekondari, Msingi, Awali na Kituo cha Michezo vya Alliance, James Bwire, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa alisema kwamba, matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2014/2015 sekondari ya wavulana Kitaifa imeshika nafasi ya Pili kati ya sekondari 2,322 nchini na Mkoa ya Kwanza kati sekondari 174.
Bwire alisema sekondari hiyo kwa Mkoa wa Mwanza imeshika nafasi ya Kwanza kwa kufaulisha wanafunzi 43 kwa daraja la kwanza (Division one) na daraja la pili mwanafunzi mmoja (Division Two) kati ya watahiniwa 44 waliofanya mtihani wa Taifa katika sekondari hiyo mwaka 2014/2015 na hakuna aliyefanya vibaya na kupata GPA alama 4.4937 huku wakifaulu masomo ya Uraia (Civics), Historia, Geografia, Engilishi, Fizikia (Physics), Kemia (Chemistry),Biolojia na Hesabu (Basic Mathemastic).
Mkurugenzi huyo alisema sekondari ya wasichana Alliance kwa Mkoa wa Mwanza imeshika nafasi ya 13Kitaifa na Mkoa wa Mwanza imeshika nafasi ya Pili kati ya sekondari 174 kwa kufaulisha ambapo wanafunzi waliopata daraja la Kwanza ni 42 (Division one) na daraja la pili ni 11 (division Two) na hakuna waliofanya vibaya kati ya watahiniwa 53 waliofanya mtihani wa Taifa mwaka 2014/2015 na kupata GPA alama 4.1866 huku wakifaulu masomo ya Biashara (Commerce), Biolojia, Kemia, Fizikia, Kiswahili na Book Keeping.
Bwire alisema siri ya mafanikio ya shule za sekondari Alliance wavulana na wasichana kufanya vizuri ni pamoja na kuwa na walimu wenye sifa na weledi wa kufundisha kwa kujituma, ubunifu wa walimu kutekeleza mikakati ya shule na usimamizi mzuri wa uongozi kwa utekelezwaji wa malengo yanayowekwa kwa walimu na wanafunzi na mazingira bora ya shule kuwa rafiki kwa walimu na wanafunzi.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo , kumekuwa na motisha kwa walimu kwa kila somo ambalo wanafunzi wanapata alama za juu katika mitihani ya kawaida na ile ya kitaifa, kuwanjengea uwezo walimu na kuwapatia mikopo ya magari, mishahara mizuri na kuwapatia nyumba za kuishi katika eneo la shule jambo ambalo huchangia uwajibikaji wenye tija kwa wanafunzi.
“Kama ilivyo kwa walimu pia shule hutoa motisha kwa wanafunzi wanaofaulu vizuri katika madarasa yao kwa kupata alama za juu kwa kuwalipia ada yam hula mmoja au miaka miwili kulingana na mwanafunzi anavyofanya vizuri jambo ambalo pia limewapa fursa wanafunzi kujituma ili kupata ufaulu mzuri kwa kujisomea wakati wa likizo yam hula na mwaka,”aliseama.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba kutokana na uongozi mzuri wa shule zote za Alliance kufanya utafiti na kujiwekea mikakati iliyo na utekelezaji umefanya baadhi ya shule za msingi na sekondari kutoka mikoa ya Mbeya, Dar es salaam, Arusha, Dodoma na Morogoro kuja kujifunza ikiwemo Vituo vya michezo ili kuona Alliance inavyoweza kufanya vizuri zaidi kitaaluma na kimichezo.