BILIONI 1 KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA MABATINI NA UJENZI WA NJIA NNE BARABARA YA UWANJA WANDEGE WAJA.
WAKALA wa Barabara Mkoa
wa Mwanza (TANROAD) kutumia iasi cha shilingi bilioni 1.3 kukamilisha ujenzi wa
Daraja la juu kwa watembe kwa miguu eneo la Mabatini Kata ya Mbugani Wilaya ya
Nyamagana Mkoani hapa.
Hatua hiyo inatokana na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuri kumwaagiza Mkandarasi Kampuni ya Nordic
Consstruction Ltd ambapo garama zote zimetolewa kiasi cha
shilingi milioni 888,530,039/= kwa ujenzi na Mkataba wa Usimamizi
akilipwa kiasi cha shilingi milioni 135,350,000/= na kufanya thamani
kuwa bilioni1.
Akizungumza na mamia ya
wananchi na viongozi mbalimbali wa Mkoa ,Wilaya ya Nyamagana, Jiji la Mwanza
leo kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi katika eneo la mradi huo,
alisema kwamba Mkandarasi anatakiwa kutekeleza mradi huo kwa wakati na kuzingatia
Mkataba wake kutokana na kulipwa fedha yote.
Dkt. Magufuri alisema
kuwa serikali kupitia Wizara yake ya Ujenzi itaendelea kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa uboresha wa miundombinu ya barabara na vivuko
vya majini na watembea kwa miguu ikiwa ni madaraja.
“Tuliahidi na sasa
tumetekeleza, mnaona leo tumeweka jiwe la msingi na kazi ya ujenzi inaendelea
naamini kufikia Desmba 25 daraja hili litakuwa likifunguliwa na sherehe za
Chrismas watu watapita hapa na kupata frusa ya kupiga picha kama wanavyofanya
kwenye eneo la samaki ikiwa ni kuongeza ajira na utalii”alisema.
“Tumedhamiria kupunguza
msongamano wa magari kuingia mjini na kupunguza vifo ambapo takwimu za ajari
zinaonyesha zaidi ya watu 12 wamekufa na wengine 20 wamepata majelaha na vilema
vya maisha hivyo serikali kuchukua hatua ya kutoa pole kwa waliopoteza maisha
na kuwatakia majeruhi kupona haraka amina” alisema.
Aliongeza kuwa serikali
sikivu ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete itaendelea kuboresha Miundombinu ambapo hivi
sasa Mkandarasi yupo eneo la mradi wa Ujenzi wa barabara ya Lami ya Usagara
hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita 17 kwa garama ya shilingi bilioni 17.9
zilizotolewa na serikali kwa asilimia 100.
“Tumedhamilia kuondoa
msongamano wa magari na watu kulazimika kutumia barabara kufika miji tayari
Wizara yangu tayari imeanzisha mchakato wa kujenga kivuko cha kisasa ndani ya
ziwa Victoria ambacho kitatoa huduma ya usafiri kuanziaia eneo la Pansiasi
kupitia maeneo ya Kirumba mwaloni hadi Nyegezi” alisisitiza
Huku pia akisisitiza
kuweka kwenye mipango ya ukarabati wa ujenzi wa barabara za Isamilo, Mabatini
hadi zahanati ya Kata ya Mbugani na maeneo mengine yaliyosahulika kwa kuongeza
kwenye bajeti ya mwaka ujao kupitia fedha za mfuko wa barabara ili kuiwezesha
halmashauri ya jiji kuzijenga na kuziboresha.
Awali Meneja wa Tanroad
Mkoa wa Mwanza Injinia Leonarld Kadashi akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo
alisema kuwa Mkandarasi kwa sasa ameisha tekeleza kwa asilimia 60 ya kazi yake
na tayari fidia ya shilingi milioni 9.5 imetolewa kwa uhamishaji nguzo za
Tanesco maeneo yote.
“Ujenzi wa daraja hili
la kisasa unaenda sambamba na upanuzi wa njia tatu badala ya mbili kwenye
barabara ya Nyerere kuanzia eneo la Nata hadi Buzuruga lengo ikiwa ni kupunguza
msongamano wa magari kuingia mjini wakati wa asubuhi na kutoka jioni kwani
mkandarasi yupo eneo la mradi na utatumia bilioni 2 kwa awamu ya kwanza”alisema
na kuongeza.
Kuwa awamu hiyo ya
kwanza itaishia eneo la Sinai na awamu ya pili itaanzia Sinai na kuishia kwenye
daraja la Buzuruga ikiwa ni pamoja na kuweka taa za kuongozea magari na
watembea kwa miguu eneo la makutano ya barabara ya Barnaba na Mahina kwa garama
ya bilioni 2 na kufanya thamani kuwa zaidi ya bilioni 4.
Kwa upande wake Meya wa
Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula aliomba kwa Waziri Dkt. Magufuri daraja hilo
kuwekewa uzio ili kuzuia watoto kuvuka kiholela hivyo kuhatarisha maisha yao na
kumpongeza kwa juhudi kubwa ya kuendelea kusaidia Jiji la Mwanza ambapo kiasi
cha bilioni 1 alichokitoa kwa jiji hilo kinatekeleza ujenzi wa barabara za mawe
ambazo ni Mkuyuni-Nyakurunduma, Capil point-Idara ya maji, Sweya-Ihumilo,
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Injinia Evarist Ndikilo ametoa ombi maalumu kwa Waziri Magufuri kuweka
mkakati wa kuipanua barabara ya Makongoro inayouelekea Uwanja wa Ndege toka
mjini kati kuwa ya njia nne kutokana na kujengwa jengo la kisasa la kitega
uchumi la Kituo cha Biashara eneo la Ghana na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege
unaoendelea kujengwa kwa sasa kuwa na hadhi ya kimataifa.