ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Showing posts with label HABARI MWANZA. Show all posts
Showing posts with label HABARI MWANZA. Show all posts

Thursday, October 13, 2022

WAZIRI MKUU KUFANYA ZIARA JIJINI MWANZA

 

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa anaetarajia kufanya ziara Mkoani Mwanza 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima (kulia) akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya ujio wa Waziri Mkuu.



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambapo ata kagua miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 13,2022  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima, amesema Waziri Mkuu atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Daraja la Magufuli,mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),mradi wa stendi ya kisasa ya mabasi Nyegezi na kuzindua jengo la huduma ya macho kwenye Hospital ya Kanda ya Rufaa Bugando.

“Oktoba 17,2022 Waziri Mkuu atatembelea Wilaya ya Ukerewe ambapo atawasili kwenye kisiwa cha Irugwa kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya,ujenzi wa shule ya sekondari Irugwa”, ameeleza Malima

Katika hatua nyingine Malima ametoa rai kwa madereva na wamiliki wa magari kuwa na utaratibu wa kuondoa magari pindi yanapoharibika barabarani ili kuepusha msongamano unaoweza kusababisha ajali zisizokuwa za lazima.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi, ameeleza mikakati mbali mbali iliyopo ya kuhakisha wanapunguza ajali za barabarani ikiwemo askari kusimamia maeneo ya watembea kwa miguu.

Thursday, September 15, 2022

ALICHOSEMA MBUNGE WA NYAMAGANA MBELE YA MAKAMU WA RAIS

 NA ALBERT G SNGO/ MWANZA

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Jijini Mwanza Stanslaus Mabula haya ndiyo aliyoyawasilisha jana Tarehe 14 September 2022 mbele ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, akihitimisha ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi Mradi wa Maji Butimba, Mwanza. Mahitaji ya maji kwa sasa kwa jiji la Mwanza ni lita milioni 160 lakini uwezo wa kuzalisha maji wa chanzo cha maji Capripoint ni lita 98 tu, hivyo baada ya mradi huu kukamilika ifikapo mwezi Disemba 2022 (kama ahadi ya kuharakisha) utaongeza lita milioni 48 na kuwa suluhu ya uhakika kwa changamoto ya upatikanaji wa maji hadi mwaka 2040.