Diwani wa kata ya Butimba Dismas Makungu kwa niaba ya Mstahiki Meya wa jiji hilo, akikabidhi bendera ya jiji kwa Afisa Utamaduni wa jiji la Mwanza Mama Makenke kwaajili ya ushiriki michuano ya SHIMISEMITA inayotarajiwa kuanza rasmi kesho mjini Dodoma.
Timu hiyo inaondoka leo kuelekea mjini Dodoma kwaajili ya michuano hiyo inayoshirikisha michezo mbalimbali kama Football, Netball na michezo mingine ya ndani kama vile Bao, Kuvuta kamba na Karata.
Mwanza City team ikiwa na jumla ya wachezaji 22, kocha wawili na kiongozi mmoja pia imekabidhiwa bango la Mwanza.
Diwani wa kata ya Butimba Dismas Makungu kwa niaba ya Mstahiki Meya wa jiji hilo, akikabidhi mpira wa mazoezi kwa kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Mwanza city Amidu Juma, kwenye makabidhiano yaliyofanyika mchana huu katika viwanja vya Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Diwani wa kata ya Butimba Dismas Makungu kwa niaba ya Mstahiki Meya wa jiji hilo, akikabidhi mpira wa mazoezi kwa kocha Rehema Menzukwa wa kikosi cha netiboli cha Mwanza city, katika makabidhiano yaliyofanyika mchana huu kwenye viwanja vya Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Mwanza city.
Kikosi cha netiboli cha Mwanza city
Mkuu wa msafara huo ambaye ni Afisa utamaduni wa jiji la Mwanza Mama Makenke akizungumza na waandishi wa habari ameahidi kurudi na kombe la ushindi wa kwanza kupitia michezo hiyo ya Serikali za mitaa (Shimisemita) akisema sababu kuu ya kujiamini kwake ni ushiriki vyema wa timu hiyo kwenye michuano ya Polisi jamii iliyomalizika hivi karibuni kwa wilaya ya Nyamagana ambapo timu hiyo ilitwaa kombe ikizigalagaza baadhi ya timu kali za jiji la Mwanza.