ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 30, 2019

MSANII WA MAREKANI NIPSEY HUSSLE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI.


Rapa wa Marekani,  Ermias Davidson maarufu kama Nipsey Hussle ameuawa kwa kupigwa risasi mapema leo nje ya duka lake la nguo lililoko Los Angeles.

Nipsey mwenye umri wa miaka 33, alipigwa risasi kadhaa mwilini mwake na alipofikishwa hospitalini alibainika tayari alikuwa ameshafariki, kwa mujibu wa CNN.

Watu kadhaa walijeruhiwa pia katika tukio hilo ambalo kwa mujibu wa polisi lilihusisha makundi mawili kushambuliana kwa risasi, Kusini mwa Los Angeles.

Nipsey alikuwa mmoja kati ya wakali wa rap waliotikisa ulimwengu mpya wa michano, ambapo albam yake ya ‘Victory Lap’ ilifanikiwa kutajwa kwenye kipengele cha albam bora ya rap/hiphop kwenye tuzo za Grammy mwaka huu, kipengele ambacho rapa wa kike Cardi B alifanikiwa kushinda na albam yake ‘Invasion of Privacy

MSINGI WA MAENDELEO YA NCHI NI MAENDELEO YA KWELI KWA WANYONGE ASEMA KIKWETE.

Mkakati wa kuhakikisha maendeleo yanawafikia watu wa Hali ya Chini ndiyo msingi utaowafanya Wananchi waendelee kuipenda na kuichagua Ccm. Maneno hayo ameyasema leo Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaweza jiwe la Msingi la Zahanati ya Kitongoji Cha Chahua huko mjini Chalinze mapema hivi leo.

Akiweka jiwe la Msingi , Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alieleza furaha yake juu ya mafanikio ambao Halmashauri yake imepata kwa upande wa Afya,Elimu,Maendeleo ya Jamii na kusisitiza kuwa haya yanatokana na msimamo ambao Chama Cha Mapinduzi kinasimamia inapofika katika utekelezaji wa ilani yake ambayo inawalenga kuwapelekea Mabadiliko ya Kweli wananchi wa hali za chini kabisa.Mheshimiwa Mbunge Ridhiwani hakusita kueleza jinsi Raisi Magufuli anavyoendelea kupambana kuwasaidia Watanzania hasa katika kuwapatia huduma bora hasa kwa Upande wa Afya. 


"Katika Halmashauri ya Chalinze tumejenga zaidi ya Zahanati 86 katika vitongoji na Vijiji ,Vituo vya Afya zaidi ya 13 na Sasa tunakamilisha Hospitali ya Wilaya ambayo fedha Kiasi cha Shilingi Milioni 500 zinatarajiwa kuletwa kumalizia Ujenzi pamoja na kununua vifaa tiba. Tunachopaswa wana Chalinze wenzangu ni kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ambazo Raisi Magufuli anafanya akishirikiana nami Mbunge wenu,Diwani wetu na Mwenyekiti wetu wa Kitongoji." Mbunge Ridhiwani Kikwete alisisitiza.

“Katika Kata yetu ya Bwilingu, mambo mengi ya kimaendeleo tunayatekeleza ikiwa ni pamoja na kumalizia ahadi za Mheshimiwa Raisi alizozitoa kipindi cha kampeni. Katika Upande wa Elimu ,tunapambana kupunguza wingi wa Wanafunzi pale Shule ya sekondari ya Chalinze kwa kumalizia shule ya sekondari ya pera na mkakati mwengine wa kuanzisha ujenzi wa Shule ya sekondari ya Chahua." Mheshimiwa Mbunge pia aligusia juu ya Ujenzi wa Maabara ya Kisasa katika kituo cha Afya Chalinze ili kusaidia vipimo vya ziada vya Kiafya.

Akizungumza kabla ya Mbunge kuweka jiwe la Msingi Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Sadallah Maisha alimshukuru Mbunge kwa Msaada anaowasaidia Watu wa Chahua hasa katika maendeleo ya Jamanii. " Mheshimiwa Mbunge tunakushukuru kwa Kutupatia Nondo 80 na fedha taslimu Shilingi Milioni Mbili,LAki Mbili na Nusu. Pamoja nawe Halmashauri na Nguvu zetu Wananchi."


Mbunge wa Chalinze anaendelea na Ziara ya kuangalia Shughuli za Maendeleo na Utekelezaji wa Ilani katika Vijiji,Kata na Vitomgoji mbalimbali Vya Halmashauri hiyo. Katika Hali nyengine Mvua kubwa iliyonyesha kuanzia Alhamisi imeharibu Miundo mbinu katika Mji wa Chalinze na pera na Vitongoji mbalimbali.

MRADI WA MAJI MLANDIZI MBOGA KUANZA KATIKATI YA MWEZI WA NNE

MBUNGE wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametembelea kiwanda cha mabomba cha Tanzania Steel Pipes kinachotengeneza mabomba ya kusafirishia maji kwenye mradi wa maji wa Mlandizi- Chalinze- Mboga.

Akitembelea kiwanda hicho, Ridhiwani amefurahishwa na maendeleo ya utengenezaji wa mabomba hayo ambapo takribani mabomba 321 yameanza kusafirishwa kwa ajili ujenzi wa meadi huo unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi April.

Akizungumza baada ya kumaliza kukagua mabomba hayo, Ridhiwani amesema kuwa imechukua miaka 16 kwa wananchi wa Chalinze kupata majisafi na salama na imani yake kubwa ipo kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA wafanikishe mradi huo.

“Sikuwahi kuona namna wananchi wanatumia maji pamoja na wanyama kama ng’ombe ila kukamilika kwa mradi huu kutawezesha watu wangu kupata majisafi na salama ila na amesema mradi huo utawanufaisha wakazi wa maeneo hayo ikiwa pamoja na wananchi wanaoishi kwenye eneo la mradi.

Joseph amesema Mradi wa maji wa Mlandizi -Mboga unatarajiwa kusafirisha maji lita milioni 9.3  (mita za ujazo 9300) kwa siku kiasi kianchokisiwa kuweza kutosheleza mahitaji ya walengwa kwa sasa na ongezeko la matumizi kwa siku za usoni.

“Hadi sasa, kiasi cha mabomba ya umbali wa km 3.7 yameshazalishwa katika kiwanda cha TSP na yameanza kupelekwa kwenye maeneo ya mradi ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza katika Vijiji vya Mboga na Msoga,” amesema Joseph.

“Katika usanifu wa mradi huo, umetilia maanani ongezeko la watu na mahitaji ya miaka 20 ijayo na kutosheleza idadi ya watu hadi kufikia 120,912 ndani ya eneo la mradi na utakuwa kwa umbali wa Kilomita 58 ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji na utagharimu bilion 14 hadi kukamilika kwake,”amesema Joseph.

Maeneo yatakayohudumiwa na mradi huo ni pamoja na Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.

Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzireli ya kisasa (SGR)

Afisa Utawala wa Kiwanda cha Mabomba cha TSP, Elly Bohela amesema anashukuru sana kwa Mbunge Ridhiwani Kikwete kufika kwenye Kiwanda chao kuona namna wanavyotengeneza mabomba hayo ambayo yanaenda kuwekwa kwenye mradi uliopo katika jimbo lake.

Amesema, kiwanda cha TSP ni cha wazawa na wamejizatiti kwenye kutengeneza mabomba yenye ubora aidha ameishukuru dawasa kwa kuweza kuwaamini na kuwapatia kazi hiyo muhimu.

 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa ndani ya gari lililobeba mabomba yanayoelekea kwenye jimbo lake kwa ajili ya mradi wa maji wa Mlandizi Mboga baada ya kutembelea kiwanda cha Mabomba cha Tanzania Steel Pipes leo Jijini Dar es Salaam.

 Gari iloyobeba mabomba kwa ajili ha ujenzi wa mradi wa maji wa Mlandizi Mboga likiwa tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea Chalinz

 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) kwenye kiwanda cha Mabomba cha Tanzania Steel Pipes leo Jijini Dar es Salaam.

 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.

 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Chalinze akielezea kwa umakini ramani ya mradi wa Mlandizi Mboga unaotarajiwa kuanza kujengwa Katikati ya mwezi April mwaka huu utakaohudumia wakazi wa jimboni kwake akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph  na Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Lydia Ndibalema.

Shirika la AGPAHI latoa mafunzo ya saikolojia kwa watumishi wa afya Mwanza

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka Vituo vya Afya mkoani Mwanza, yanayolenga kuwajengea uwezo katika kutoa msaada na huduma za kisaikolojia kwa watoto na vijana wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Mafunzo hayo ya siku tano yalianza jumatatu Machi 25, 2019 hadi Ijumaa Machi 30, 2019 katika ukumbi wa “Isamilo Lodge” Jijini Mwanza ambapo yamewashirikisha wataalam wa afya zaidi ya 60 kutoka Halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo Nyamagana, Ilemela, Misungwi, Magu, Ukerewe na Buchosa.

Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona amesema mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma za afya katika vituo vya tiba na matunzo kutambua namna bora ya kuwahudumia wateja wao hususani watoto na vijana.

Amesema mafunzo hayo yatawasaidia pia kuwatambua watoto na vijana wenye changamoto kisaiklojia na namna ya kuwasaidia huku wakizingatia upatikanaji wa huduma bora na rafiki kwa wateja kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo michezo.

“Tunatarajia pia wataenda kuanzisha vikundi vya akina mama wanaoishi na maambukizi ya VVU ambao wako kwenye kitengo cha kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili nao waweze kujifunza kupitia uzoefu wao huku vikundi vilivyopo vikiimarishwa zaidi”. Amesema Yona.

Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walikuwa wakikumbana na changamoto ya kutambua mazingira halisi yanayowakabili watoto na vijana kupitia klabu zao.

Shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia taasisi ya Centres for Disease Control (CDC), linashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutekeleza afua mbalimbali za kupambana na maambukizi ya VVU pamoja na kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi hayo.
Mmoja wa Wawezeshaji, Margaret Safe kutoka Kibaha mkoani Pwani akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji, Margaret Safe akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona.
Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti akiendelea kutoa mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti kutoka mkoani Iringa.
Wataalam wa afya walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa umakini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Timu ya wakufunzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo pia walipewa mtihani na hapa wakiwa kwenye chumba cha mtihani ili kupima uelewa wa kile walichofundishwa.
Washiriki wakijibu mtihani kuhusu walichofundishwa.
Baada ya mafunzo ya nadharia darasani yaliyofanyika Isamilo Lodge, washiriki walielekea Lesa Garden kukutana na baadhi ya watoto na vijana kutoka klabu za elimu na makuzi kwa ajili ya kucheza na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwasili Lesa Garden iliyopo Luchelele Jijini Mwanza.
Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
Inaelezwa vijana hujifunza na kuelewa vyema kupitia michezo na hapa michezo imepamba moto.
Michezo mbalimbali ikiendela.
Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
Washiriki wa mafunzo wakifurahi pamoja na vijana.
Michezo ikiendelea Lesa Garden.
Watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo kufikisha elimu kwa watoto na vijana.
Inaelezwa michezo husaidia watoto na vijana kuelewa vyema yale wanayofundishwa hivyo watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo pia kuwaelimisha vijana na watoto.
Washiriki wakifurahia pamoja na vijana.
Pia kulikuwa na burudani ya muziki ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo ambapo husaidia watoto na vijana kuwa huru kwa watoa huduma za afya.
Burudani ya muziki.
Washiriki wa mafunzo wakifurahia muziki pamoja na watoto/ vijana.
Michezo na burudani ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Friday, March 29, 2019

BAADA YA KIFO CHA MWANANCHI KUANGUKIWA MAWE DC APIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA UCHIMBAJI



HALI ya mazingira hatarishi kwa shughuli za uchimbaji mchanga kwenye eneo la vilima vya Mahina tambukareli wilayani Nyamagana mkoani Mwanza imemlazimu Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Philis Nyimbi kupiga marufuku wananchi au mtu yeyote kufanya shughuli za uchimbaji kwenye eneo hilo.

Mwili wa Ndalahwa Mashauri aliyeangukiwa na mawe akiwa shimoni kwenye machimbo ya udongo wa mfinyanzi al maarufu MABUMBA tangu Jumatatu ya tarehe 24 mwezi Machi 2019 hatimaye  Alhamisi ya tarehe 28 Machi 2019 umefanikiwa kutolewa  shimoni humo.

Kwa muda wa siku nne waokoaji wamekuwa katika eneo la ajali kwenye vilima vya kata ya Mahina, Tambika reli wakijaribu kwa kila namna kuona ni jinsi gani wanafanikiwa kuutoa mwili wa marehemu Mashauri ambaye alikuwa ameangukiwa na mawe pamoja na kisusi cha udongo mita kadhaa ardhini wakati akichimba udongo.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MASHINE ZA KISASA ZA TIBA YA MIONZI, SARATANI LINAC.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu mara baada ya kuwasili katika viwanja vyaTaasisi ya Saratani (Ocean Road) kuzindua mashine mpya za tibaya mionzi LINAC, kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage, Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohammed Bakari Kambi, Mwnyekiti wa Bodi, Taasisi ya Ocen Road, Prof Hamis Ndehenga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu mara baada ya kuwasili katika viwanja vyaTaasisi ya Saratani (Ocean Road) kuzindua mashine mpya za tibaya mionzi LINAC, kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage, Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohammed Bakari Kambi, Mwnyekiti wa Bodi, Taasisi ya Ocen Road, Prof Hamis Ndehenga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohammed Bakari Kambi, mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Taasisi ya Saratani (Ocean Road) kuzindua mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC , kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Julius Mwaiselage na kushoto kwake ni Mwnyekiti wa Bodi, Taasisi ya Ocen Road, Prof Hamis Ndehenga
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (hawapo Pichani), kabla ya uzinduzi wa mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC, uliofanyika leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kathe Kamba, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kufungua mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC, leo katika Taasisi ya Saratani Ocaen Road, Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kufungua mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC, leo katika Taasisi ya Saratani Ocaen Road, Dar es Salaam
Moja ya Mashine za tiba ya mionzi LINAC (CT-STIMULATOR) iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Raod, Jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI UVCCM AKEMEA SIASA ZA MAKUNDI

 Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara akemea Siasa za makundi na kudhoofishana

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Mara, Ndg Kheri D. James (MCC) amekemea vikali tabia ya baadhi ya Wanachama cha CCM kuanza kampeni mapema na kuchafuana. 

Ameyasema hayo leo, Alhamis tarehe 28-03-2019  akiwahutubia wajumbe wa halmashauri ya CCM Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara. Ndg Kheri D. James (MCC) alionya kwamba, chama hakitamuhurumia yeyote anayeendesha makundi na siasa za kudhoofishana zinazolenga kuwagawa wanachama na kukosesha ushindi kwenye chaguzi.
Awali akiongea na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya, Comrade Kheri D. James alieleza juu ya watendaji na viongozi wa CCM kuheshimu katiba na kanuni zingine za Chama. 

Alisisitiza kushirikiana na kupendana huku wakizingatia mgawanyo wa majukumu uliowekwa ili kuepuka migongano isiyokuwa na sababu.

Ndg Kheri D. James alitumia ziara hii kukumbusha viongozi wa ngazi mbalimbali kuwa na mikakati ya kuweza kujitegemea kiuchumi. Alieleza kwamba ni wakati sasa CCM na Jumuiya zote ziweze kujiendesha zenyewe kwenye ngazi za Wilaya.

Amewaomba Viongozi  na wanachama wa CCM kuungana na Rais wetu, Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli katika vita dhidi ya Rushwa. Amewataka kukemea vitendo vya Rushwa kwani vinapelekea kuzorota kwa utolewaji wa huduma za kijamii, Ujenzi wa miundo mbinu isiyo na Ubora na pia kupatikana kwa viongozi ambao hawana uwezo kuleta matokeo chanya. Vile vile Rushwa inapelekea kushamiri kwa dhulma,ongezeko la urasimu katika upatikaniji wa haki na fursa.Na wahanga wakubwa wa rushwa ni sisi Vijana.

Comrade Kheri D. James ameanza ziara ya kikazi kama Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara kukagua uhai wa chama kwa kukumbushia taratibu na kanuni zinazoziongoza Chama cha Mapinduzi,kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na kuweka mikakati kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019. 

Ziara hii itakuwa ni kwa Wilaya za Mkoa wa Mara kwa kuanzia Serengeti, Tarime, Rorya, Musoma Vijijini,Musoma na Bunda.       _Mwisho

Thursday, March 28, 2019

WATUHUMIWA WA SHEHENA YA DHAHABU MWANZA HUKUMU YATOKA DPP ANENA.



Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza imewahukumu wafanyabiashara wanne wa madini ya dhahabu kwa pamoja kutumikia kifungo cha miaka 38 jela au kulipa faini ya shilingi millioni 529.8 baada ya kukiri makosa 9 yakiwemo ya uhujumu uchumi, rushwa pamoja na utakatishaji wa fedha yaliyokuwa yanawakabili.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa mwanza Rhoda Ngimilanga  baada ya watuhumiwa hao Sajid Abdalah, Kisabo Nkinda, Emmanuel Kija na Hassan Sadick kukiri makosa yaliyokuwa yanawakabili.
Aidha watuhumiwa wengine wa 8 ambao ni askari polisi wamekana mashtaka yanayowakabili na wamerejeshwa rumande hadi April kumi mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Akizungumza nje ya mahakama Mkurugenzi wa mashtaka nchini Biswalo Mganga anafafanua zaidi. (TIZAMAVIDEO)

BankABC YATOA MSAADA WA MABATI WILAYA YA KILINDI.


Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo


Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)


Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)


. Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.

Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo


Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo baada ya kukabidhi msaada wa mabati 200. Wengine katika picha ni Asmah Abubakar na Raphael Kalinga wa BancAbc.

BancABC kupitia Huduma yetu ya Mkopo Rahisi imejidhatiti kuweza kuhakikisha kwamba tunainua kuendeleza mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hii inafanya shughuli zake kupitia miradi yetu ya kusaidia jamii inayotuzunguka. 

Sisi BancABC tunaamini kwenye umuhimu wa elimu bora katika jamii zetu hapa Tanzania na kwa hivyo tunaunga mkono Serikali ya Awamu ya 5 na hususani Rais wetu Mhe. John Pombe Mafuguli Katika miradi mbali mbali ya elimu kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kuweza kuwafikia kila jamii na hasa maeneo ya vijijini kwa wale ambao wako kwenye hali duni. 

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Emmanuel Nzutu ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi alisema; “Kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania kuanzia chekechekea hadi kidato cha nne, Leo Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo.” 

Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha Bancabc na pia kuwajulisha kuwa benki yetu tunatoa huduma ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa ule wa awali. 

Uzuri wa mkopo huu tofauti na mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo anaweza kuchagua ni mradi gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa karo ya shule, kununua gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi ya nyumba au kumalizia ujenzi. 

Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya. 

‘Mkopo huu utakuwa na bima ya maisha pale ambapo mwenye Mkopo anapofariki, familia yake inapewa pesa taslimu Tzs500, 000 kwa ajili ya kugharamia mazishi.’ 

Tunatoa wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na Bancabc na kuchangamkia Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto zako.