ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 13, 2023

OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 600 NA DOLA ZA KIMAREKANI ZAIDI YA MILIONI 37

 

Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Boniphace Luhende akizungumza wakati akifungua kikao cha cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika Jijini Tanga.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mark Mulwambo  akizungumza wakati wa akifungua kikao cha cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika Jijini Tanga.

Na Oscar Assenga, TANGA

SERIKALI kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh Bilioni 600 na dola za Kimarekani milioni thelathini na saba nukta tatu nne ambazo zingelipwa kwa wadaiwa endapo Serikali ingeshindwa kwenye mashauri hayo.

Hayo yalibainishwa leo na Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Boniphace Luhende wakati akifungua kikao cha cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika Jijini Tanga.

Alisema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuiendelea kuiwezesha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza vema majukumu yake ya kuiwakilisha Serikali na Taasisi zake kwenye mashauri ya madai na usuluhushi ndani na nje ya nchi.

Aidha alisema majukumu hayo ni kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi yanayofunguliwa dhidi au kwa niaba ya Serikali na Taasisi zake ndani na nje ya nchi.

“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwani amekuwa akiendelea kuiwezesha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza vema majukumu yake ya kuiwakilisha Serikali na Taasisi zake kwenye mashauri ya madai na usuluhushi ndani na nje ya nchi”Alisema

Aliongeza kwamba katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2022/2023 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeendesha mashauri 7,392 ambapo kati ya mashauri hayo 7,255 ni ya madai na 137 ni ya usuluhishi ambapo kati ya mashauri hayo 7,350 ni ya ndani ya nchi na 42 ni ya nje ya nchi.

Dkt Luhende alisema kwa kipindi hicho hicho Ofisi hiyo imemaliza jumla ya mashauri 620 ambapo mashauri 579 yalimalizika kwa njia za kimahakama na mashauri 41 yalimalizika kwa njia ya majadiliano nje ya mahakama.

Alisema kwamba wameshuhudia ongezeko la bajeti yao bungeni kwa ajili ya uendeshaji wa majukumu ya Serikali kuwatumikia wananchi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo katika kipindi hicho ofisi ya wakili mkuu wa Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ilifanikiwa kuongezewa bajeti kutoka zaidi ya Bilioni 12 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi kufikia zaidi ya Sh.Bilioni 17 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo ongezeko hilo ni asilimia 25.

Awali akizungumza katika kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mark Mulwambo alisema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 ofisi hiyo imejiwekea vipaumbele mbalimbali ni pamoja na kuendelea kuratibu, kusimamia na kuiwakilisha serikali na taasisi zake katika kuendesha mashauri ya madai yanayofunguliwa dhidi ya Serikali kwenye mahakama au mabaraza mbalimbali ndani na nje ya nchi .

Alisema pia kuendelea kukamilisha ujenzi wa makao makuu ya ofisi ya wakili mkuu wa serikali unayoendelea mji wa serikali Mitumba mji Dodoma wanaishukuru serikali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo.

Alisema pia wataendelea kuwajengea uwezo watumishi kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ikiwemo mafunzo ya kibobevu katika maeneo maalumu ikiwemo ya sekta ya mafuta na gesi pamoja na usuhuluhi wa kimataifa kuimarisha ofisi za mkoa na hivi sasa wanaendelea kufungua ofisi nyengine mkoani Manyara.

WATALAKA NA WATALAKIWA WAPEWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 MKUU wa Idara ya Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Tanga Sharifa Coshuma akizungumza wakati akifungua mafunzo ya watalaka na watalakiwa yaliandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR)yaliyolenga kutoa elimu kwa kundi hilo la watalaka na watalakiwa ya ujasiriamali kwa lengo ka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirika hilo Lulu George na kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Rodgers Chamani



MKUU wa Idara ya Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Tanga Sharifa Coshuma akizungumza wakati akifungua mafunzo ya watalaka na watalakiwa yaliandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR)yaliyolenga kutoa elimu kwa kundi hilo la watalaka na watalakiwa ya ujasiriamali kwa lengo ka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kushoto


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR) Rodgers Chamani akizungumza wakati wa mafunzo hayo kulia ni Katibu wa shirika hilo Lulu George

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR) Rodgers Chamani  akizungumza wakati wa mafunzo 

Katibu Mkuu wa Shirika hilo Lulu George akisisitiza jambo wakati akitoa mada katika mafunzo hayo






Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi

Na Oscar Assenga, TANGA

MKUU wa Idara ya Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Tanga Sharifa Coshuma  amefungua mafunzo ya watalaka na watalakiwa huku akifichua siri ya wanawake wengi kuishi marefu kuliko wanaume kwamba ni uvumilifu na kutoishi na viny’ongo moyoni.

Mafunzo yaliandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR)yaliyolenga kutoa elimu kwa kundi hilo la watalaka na watalakiwa ya ujasiriamali kwa lengo ka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Sharifa alisema Wanawake wengi ni wepesi kuzungumzia matatizo yao tofauti na wanaume hatua inayowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo na kuweza kuishi kwa muda mrefu bila chuki wala vikwazo.

“Kwa kweli kuzungumza na kuwa wawazi ndio tiba sahihi katika jambo lolote katika kumuweka mtu huru lakini viny’ongo havisaidii na vinakuwa vibaya sana katika jamii na hatarishi kwa afya“,Alisema Afisa huyo.

Aliwataka wanawake hao kuzingatia mafunzo wanayopewa kwa mustakabali wa maisha yao na familia hasa kwa kuzungitia kuwa jukumu la malezi ya watoto bado lipo mikononi mwao


Awali akizungumza katika mafunzo hayo Katibu Mkuu wa Shirika hilo Lulu George alianza kuwashukuru TPA kwa kuwapa nafasi ya kushirikiana na wakina mama hao ili kuwawezesha kupata mafunzo ya kujikomboa kiuchumi.

Lulu alisema wanaamini kama taassi mbalimbali zilizopo Mkoani Tanga zikiendelea kuwashikia mkono itawezesha Shirika hilo kusambaza elimu ya ujasiriamali,kujitambua,maisha baada ya talaka sambamba na changamoto ya ukomo wa hedhi kwenye makundi mbalimbali kwa jamii.

“Tunaamini wakina mama hao wakiwa na akili iliyotulia wanaweza kufanya mabadiliko mazuri ya kiuchumi,kupitia wamama hawa hawa wataweza kuitumia Bandari yetu ya Tanga kufungua fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi na hatimaye kuongeza pato la mtu mmoja mmoja,mkoa na Taifa kwa ujumla”,alifafanua.

Katibu Mkuu huyo alisema baada ya mafunzo hayo wanatarajia kuunda vikundi vitakavyowezesha wamama hao kufanya shughuli zao kwa pamoja na hatimaye kufikia malengo waliyokuwa wamejiwekea katika kukidhi mahitaji yao.

“Yapo mambo mengi wanaweza kufanya kwani Mkonge peke yake wakitumia fursa iliyopo katika kuongeza thamani kwa bidhaa zinazotokana na zao hilo watafika mbali kwa sababu uhitaji wa bidhaa za zao la Mkonge ndani na nje ya nchi bado ni mkubwa sana ,tunatarajia wamama hawa wafike kwenye soko la dunia”,alisema.

Hata hivyo aliisihi jamii kuondoa dhana kwamba mtu aliyetalakiwa ni mtu mwenye laana au aibu kwani unyanyapaa huo husababisha watu waliotalikiana kuishi katika maumivu makubwa na kushindwa kujisamehe.

“Lakini tuwashukuru Bandari ya Tanga kwa kuwaezesha kuendelea kuwapa matumaini kundi hili ambalo kwenye jamii lilionekana kwamba mtu akipewa talaka amelaaniwa au hafai lakini mara baada ya kuwapa mafunzo kuna maisha baada ya talaka wakina mama hawa wamekuwa watulivu na wameweza kurudisha tabasamu la matumaini”alisema.

Lulu alisema Shirika la Msamaria Mwema linaendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kumkomboa mwanamke kwenye nyanja zote ikiwa ni pamoja na kulinda afya ya akili changamoto inayowakabili wanawake wengi kwa sasa.

SHIRIKA LA AMEND TANZANIA LAPONGEZWA KWA KUTOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WANANCHI

 

 

NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Rehema Kasim Muhina akizungumza wakati wa kikao cha kuhitimisha mradi wa usalama barabarani kupitia Tanga Yetu uliokuwa ukiendeshwa na Shirika la Amend Tanzania chini ya Ufadhili Shirika la Botnar Foundation ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2023, kuhusiana na suala zima la usalama barabarani.

NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Rehema Kasim Muhina akizungumza wakati wa kikao cha kuhitimisha mradi wa usalama barabarani kupitia Tanga Yetu uliokuwa ukiendeshwa na Shirika la Amend Tanzania chini ya Ufadhili Shirika la Botnar Foundation ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2023, kuhusiana na suala zima la usalama barabarani.


Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mradi huo


Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mradi huo


Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mradi huo


Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga Shadia Ally akieleza namna walivyonufaika kupitia mradi huo



Sehemu ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakiwa kwenye kikao hicho




Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho


NAIBU meya wa Jiji la Tanga Rehema Kasimu kushoto akimpatia cheti cha kutambua mchango wa Mwalimu wa Shule ya Msingi Usagara Faraja Mwajike kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya usalama barabarani mapema leo












Na Oscar Assenga, TANGA

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga limelishukuru Shirika la Amend Tanzania kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu usalama barabarani sambamba na uboreshaji wa miundombinu katika shule za Msingi hatua iliyowezesha kupunguza ajali

Elimu hiyo ilitolewa kupitia mradi wa Usalama Barabarani kupitia Tanga Yetu chini ya Ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika rasmi mwaka 2023 ambao umekuwa na manufaa makubwa.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mradi huo ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2023, Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow amesema katika kipindi cha miaka minne wamekuwa na Amend katika kushirikiana kuhusiana na suala zima la usalama barabarani.

“Amend ni miongoni mwa mashirika yanayofanya kazi kwa ukaribu katika program ya Tanga Yetu , ni miongoni mwa miradi 17 tuliyokuwa nayo katika miradi ya Tanga Yetu na moja ya mradi huo ni mradi wa usalama barabarani.Katika mradi huu waliokuwa wamepata kazi ya kuusimamia na kuendesha ni Amend.

“Mradi huu umefika mwisho na umefanyika kwa miaka minne ukiwa unafadhiliwa na Shirika la Botnar chini ya mradi wa Tanga yetu na leo tumekuja kuwapa taarifa wadau tuliokuwa tunashirikiana nao tangu mwanzo kama.

“Ni mradi ambao umekuwa na mafanikio makubwa ndani ya miaka hii minne kwa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani imetengamaa na imejitosheleza katika jiji letu la Tanga, kwasababu mradi huu pia uligusa uboreshaji wa miundombinu,”amesema Shiloow.

Amefafanua wameboresha miundombinu katika Shule ya Msingi Usagara, Shule ya Msingi Chuda, Shule ya Msingi Mwazange na Shule ya Msingi Mabawa. “Tumeboresha miundombinu hii ambayo imetengenezwa maeneo mahususisi ambayo watoto wanaweza kupita kwa usalama na kuepuka kupata ajali za barabarani.

“Lakini kuweka alama za barabarani, tumeweka matuta, kingo, zebra na alama mbalimbali za kuashiria watumiaji wa vyombo vya moto kwamba wako katika maeneo ya shule.Amend pia wametoa elimu kubwa kwa watoto wa shule za msingi, sekondari, madereva wa bodaboda, maofisa wa maendeleo ya jamii , askari wa kikosi cha usalama barabarani.

“Elimu hiyo imetolewa ya kutosha katika Jiji la Tanga na zimetolewa kwa nyakati tofauti lakini hawakuishia hapo wametoa elimu kwa madereva zaidi ya 900 ambao nao walipewa elimu sahihi ya matumizi ya barabara lakini jinsi gani ya kumlinda mtumia barabara ili na yeye awe salama.”

Ameongeza kikubwa zaidi ambacho Amend walikifanya na kuvutia zaidi ni kuwa kuanzisha Mahakama Kifani ya Watoto iliyokuwa ikiendesha kesi za madereva waliovunja sheria za usalama barabarani na madereva hao walihukumiwa.

Meya Shiloo amesema Mahakama ya Watoto imewasaidia watoto hao kuwa na ujasiri na kufahamu haki zao kuwa sheria za barabarani zipo na zinatakiwa zifuatwe na zinaweza kutolewa hukumu na watu wakahukumiwa.Pia amesema kupitia mradi huo kumekuwepo na mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uelewa wananchi.

“Tunawashukuru Amend walitutengenezea mpango kazi wa Jiji letu la Tanga kuhusu suala zima la usalama barabarani, ni suala kubwa kwetu .Niwaambie tu Amend wamekuwa na sisi kwasababu tu ya kufadhiliwa na Fondation Botnar na sasa mradi umekwisha.

“Jambo la kufurahisha mradi huu umekwisha lakini Amend wamepata mfadhili mpya ambaye ni Serikakali ya Uswiss ambao wameona umuhimu wa kuendelea na Amend katika Jiji la Tanga pamoja na Jiji la Dodoma ambako nako watapata huduma kama ambazo zimetolewa kwetu.

“Amend wanafanya kazi kwa uhalisia na linafanya kazi na watu wenye uhitaji, watu ambao wanahitaji kusemewe na sisi kama viongozi wa umma tunawasemea watoto wetu ili tujenge taifa nzuri lisilokuwa na watoto wenye ulemavu kwa miaka ijayo na ili tujenga taifa lenye upendo ni lazima tuwajali hawa watoto ikiwa pamoja na kuangalia usalama wao,”amesema Shiloow.

Awali akizungumza katika kuhimitisha mradi huo Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo alisema mafanikio tokea kuanzishwa mradi huo mwaka wa 2019 wamefanya kazi mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika shule za msingi 11.

Alisema katika uboreshaji huo ulikuwa ni pamoja na njia za miguu, madaraja ya waenda kwa miguu, alama za barabarani, matuta, alama za pundamilia, na zaidi;

Meneja huyo alisema pia walitoa mafunzo kwa waendesha pikipiki kwa waendesha pikipiki zaidi ya 900, kwa kushirikisha Polisi wa Trafiki na viongozi wa vyama vya bodaboda;

“Lakini pia utekelezaji wa Mahakama ya Watoto katika shule tano za msingi (Usagara, Mwanzange & Martin Shamba, Mwenge, Mwakizaro),Elimu ya usalama barabarani kwa zaidi ya watoto 12,000 wa shule za msingi,Uwezeshaji wa mafunzo kwa Polisi wa Trafiki”Alisema Meneja huyo.

Alisema kwamba kampeni hiyo ya uhamasishaji wa usalama barabarani ilikuwa ikijumuisha kampeni ya vyombo vya habari, ujumbe kupitia kwa maafisa wa maendeleo ya jamii na ujumbe kupitia wanasiasa wakiwemo madiwani,

Warsha zaidi ya nane za wadau na wadau muhimu zikiwahusisha wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mkurugenzi wa Jiji na Mkurugenzi, Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani.

Jumla ya maofisa wa serikali 139, taasisi za elimu 14, wanafunzi 12,894, walimu 128, askari polisi 29 na madereva 1,220 wameguswa moja kwa moja na mradi huu.

Kutengeneza Mpango Kazi wa Usafiri Salama na Endelevu wa Jiji la Tanga.

Awali akizungumza Naibu Meya wa Jiji la Tanga alilishukuru Shirika la Amend Tanzania kwa usimamizi na utekeleza mzuri wa mradi huo ambao umekuwa na tija kubwa kwa kuwezesha kupunguza ajali zilizokuwepo awali.

Alisema kwamba Amend wamewatenda haki na waliyoyafanya yanaonekana na hivyo kuhakikisha usalama kwa watoto wa Tanga wanakuwa salama wakati wanapotumia barabarani kwenda shuleni na kurudi nyumbani

“Lakini pia niwapongeze Botnar kwa kujali watoto kwa kufadhili mradi huo miaka minne na kufadhili miradi 17 kwa jiji la Tanga ambayo imelenga kuboresha mazingira ya watoto na vijana na kuwajengea vijana uwezo ili wasiwe kuajiriwa bali wajiajiri “Alisema

Hata hivyo alisema miradi hiyo imekuwa na matokeo makubwa sana yanayoonekana, na shughuli hizo zimeweza kupunguza ajali kwa watoto huku akieleza jukumu la Amed wamefanya ya muhimu katika kuboresha miundombinu ambayo imehakikisha usalama kwa watoto .

“Nitoe rai kwa watu wote kuendelea kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabara kwa watumiaji, kuheshimu vivuko vya watembelea kwa miguu vilivyopo hata kwa waendesha pikipiki,uvaaji kofia ngumu kwa waendesha pikipik kwao na abiri”Alisema

Hata hivyo alisema kutokana na uwepo wa mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali kutokana na maboresha hayo hivyo ni taarifa njema huku akiwataka wasibweteke waendelee kuhamasisha matumizi salama ya barabara kwa Jiji la Tanga

Wednesday, October 11, 2023

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA WIKI YA VIJANA KITAIFA SAMBAMBA NA KITABU CHA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI MANYARA

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Manyara sambamba na Wiki ya Vijana katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga.

Na Cathbert Kajuna -MMG/Kajunason, Manyara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amezindua kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Manyara sambamba na Wiki ya Vijana katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Muongozo huo unaelezea kwa kina fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo Mkoani Manyara na Dira ya Mkoa kwenye eneo la Uwekezaji na Maendeleo.
Uzinduzi huo uliofanyika katika Wiki ya Vijana Kitaifa 2023 iliyoanza Oktoba 8, 2023 inatarajiwa kumalizika Oktoka 14, 2023 ambapo itaenda Sambamba na Uzimaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika mkoa huo.

Akizungumza katika Uzinduzi huo Waziri Mhagama ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Khasim Majaliwa amefurahishwa na mwamko wa Vijana jinsi walivyojitokeza kuhudhuria katika Wiki yao inayowapa fursa ya kutambua mambo mbali mbali yanayofanywa na vijana wenzao Tanzania nzima.

"Binafsi nimefurahishwa na muamko wa vijana jinsi mlivyojiyokeza na kuonyesha kazi zenu, nimepita katika mabanda mbali mbali nimejionea kazi zenu za mikono na kwakweli vijana ni nguvu kazi ya Taifa letu," amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama alitoa pongezi kwa Viongozi wa Mkoa wa Manyara unaoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Queen Cuthbert Sendiga kwa jinsi walivyojipanga kusimamia na kufanya maandalizi ya shughuli mbalimbali za kiserikali ikiwemo Wiki ya Vijana, Ibada ya Kitaifa ya kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amesema kuwa mkoa wa Manyara unamaono makubwa sana katika kupambanua fursa zilizopo hivyo ni vyema vijana wakawa msitari wa mbele katika kuchangamkia fursa hizo.

"Nawashukuru timu nzima ya Mkoa wa Manyara kwa kazi nzuri na kubwa tulioshirikiana kwenye uzinduzi wa jarida hili, tunaweka mazingira rafiki kwa kila atakayetaka kuwekeza ndani ya Mkoa wetu wa Manyara, tumeanza kutangaza fursa hizi kwa vijana wetu waliofurika mjini Babati kutoka pande zote za Tanzania," amesema Mhe. Queen.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama ,Taasisi, na Dini.

Wiki ya Vijana Kitaifa 2023 yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yakiwa na Kauli mbiu, "Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu"
Wageni mbali mbali ikiwemi wakuu wa taasisi za kiserikali na binafsi pamoja na mashirika ya maendeleo waliohudhuria hafra hiyo.
Wanahabari.
Meza kuu.
Wadau wa maendeleo wakipokea kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Manyara
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kateshi "A" (Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu) wakitoa ujumbe kwa viongozi ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2023 yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yakiwa na Ujumbe "Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu"
Msanii Shoro Mwamba akitumbuiza.

Tuesday, October 10, 2023

WATAALAMU WA KUPAMBANA NA UJANGILI WAKUTANA ARUSHA

 Na Mwandishi Wetu-Arusha


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) amesema ili kupambana na uhalifu wa wanyamapori kunahitaji ushirikiano, kuchangia rasilimali fedha na kupashana habari pamojag na kuwa na operesheni za pamoja kikanda

Hayo ameyasema wakati akifungua mafunzo kwa Wahifadhi Wanyamapori kutoka katika nchi za Afrika na Asia ambao wamekutana Jijini Arusha kwa lengo la kupeana uzoefu juu ya mbinu mpya na bora za kupambana na changamoto ya ujangili na usafirishaji haramu wa Nyara zitokanazo na wanyamapori na misitu.



Mhe. Kitandula aliongeza kuwa wahifadhi wanyamapori wanatakiwa kutambua kuwa utekelezaji wa sheria za wanyamapori kwa ushirikiano ni muhimu na ni moja ya mahitaji muhimu ya kupambana na ujangili kwa ufanisi na kuongeza utaalam katika kudhibiti uhalifu kwenye maeneo ya wanyamapori.

Vilevile, Mhe. Kitandula alifafanua kuwa mafunzo hayo yanawapa washiriki nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu, kukuza ujuzi na maarifa yanayohitajika katika kujenga mtandao wa ufanisi kwa utekelezaji wa sheria za wanyamapori na udhibiti wa vitendo vya ujangili wa Wanyamapori na Misitu.

“Kutokana na viwango vya sasa vya uhalifu wa wanyamapori katika Bara, na bidhaa haramu hasa pembe za tembo, pembe za kifaru, na magamba ya pangolin kusafirishwa nje ya nchi katika siku za hivi karibuni, kuna haja ya kuimarisha uwezo na kukuza ushirikiano kati ya vyombo vya utekelezaji wa sheria kupitia kuongeza ufuatiliaji na kushirikishina habari ” aliongeza Mhe. Kitandula

Naye Mkurugenzi wa mkataba wa LATF(LUSAKA AGREEMENT TASK FORCE) Edward Phiri alisema kwamba mafunzo hayo yanaonyesha ushirikiano uliopo katika kukabiliana changamoto ya usafirishaji wa nyara zitokanazo na wanyamapori pamoja na misitu.



Aidha, aliongeza kuwa wataalamu hao wanaenda kupata mafunzo ya kinadharia na vitendo yanayoendana na mazingira ya sasa kwa sababu wahalifu wameongeza ubunifu hivyo ni bora wataalam hao wakapata mbinu mpya za kukabiliana na ujangili wa wanyamapori na misitu.

Mafunzo hayo yanajumuisha wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali zinahusika na uhifadhi wa wanyamapori na mazao ya misitu Barani Afrika na Asia.

DKT. BITEKO AZINDUA MPANGO MKAKATI KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII PANGANI

NA ALBERT G. SENGO Asisitiza Wakuu wa mikoa, Wilaya kuwa wabunifu kutangaza fursa za utaliii Awahimiza Watendaji kutimiza wajibu wao kuwahudumia Watanzania Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua mpango mkakati wa kutangaza fursa zilizopo Sekta ya Utalii katika wilaya ya Pangani, mkoani Tanga ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuikuza sekta hiyo nchini. Dkt. Biteko amefanya uzinduzi huo Oktoba 7, 2023 jijini Dar es salaam katika Kongamano la Uwekezaji la Swahili International Tourism Expo lenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko katika wilaya hiyo ikiwemo utalii katika mbuga ya Saadani, fukwe, kilimo biashara pamoja na uchumi wa Buluu katika wilaya hiyo. Vile vile, alisisitiza kuwa, Kongamano hilo litumike kuitangaza wilaya ya Pangani na kubadilishana mawasiliano ili fursa zilizoko Pangani ambazo hazipatikani kwengine zishawishi watu wengine kuzifuata. "Niwapongeze sana watu wa Pangani kupitia Mkuu wa wilaya kwa ubunifu huu wa hali ya juu na nitoe wito kwa wilaya zingine kuiga Pangani na kufungua fursa za utalii na uwekezaji kwenye wilaya zao" Alisema Dkt. Biteko. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula alisema kuwa, sekta ya utalii kwa sasa mchango wake katika Pato la Taifa ni asilimia 17. Alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira rafiki katika sekta hiyo ili kuendelea kuvutia utalii nchini katika maeneo mbalimbali hususan wilaya ya Pangani. Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Pangani Mhe. Zainabu Abdallah alisema, wilaya ya Pangani imejikita kwenye uwekezaji wa maeneo matatu ikihusisha utalii , kilimo mkakati na uchumi wa bluu na kuongeza kuwa wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya ya kimkakati yenye mazingira mazuri ya uwekezaji. " Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji na tunawaomba wawekezaji kufika wilaya ya pangani kujionea fursa hizo muhimu "alisisitiza Mhe. Zainabu Uzinduzi wa mpango huo ulikwenda sambamba na Kongamano la uwekezaji chini ya maonyesho ya wadau wa Sekta ya Utalii kuunga mkono fursa za uwekezaji. Wengine walioshiriki hafla hiyo ni Viongozi mbalimbali wa Serikali, watendaji wa taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na wadau wa sekta ndani na nje ya nchi.

Rais Samia Suluhu kuhudhuria Ibada ya kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Manyara.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria ibada maalum ya kumbukizi ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, 2023 mjini Babati - Manyara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa katika Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Parokia ya Roho Mtakatifu Babati imesema kuwa ibada hiyo itaanza saa 1.30 asubuhi na itaendeshwa na Mhashamu Baba Askofu Anton Lwagwen.

"Tunawaomba waumini muhudhurie kwa wingi ibada ya Kitaifa itakayofanyika kanisani kwetu, tunapata ugeni mzito ni vyema na sisi tukajitokeza kwa wingi," katibu wa kanisa.

Ibada hiyo itahudhuriwa na Mama Maria Nyerere pamoja na viongozi mbali mbali watakaokuwa wameambatana nae.

Vile vile baada ya kumaliza kwa ibada kutakuwa na hafla katika uwanja wa Tanzanite Kwara kwa ajili ya uzimaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023.

Monday, October 9, 2023

KUKATIKA KWA UMEME NATAKA KUWE HISTORIA KWA TANZANIA

 NA ALBERT G. SENGO/BUKOMBE/GEITA

Kupitia kipindi Cha Mchakamchaka, Naibu Waziri Mkuu, Waziri Wa Nishati na Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mheshimiwa amezungumza namna alivyoipokea simu ya Rais Wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt @samia_suluhu_hassan wakati Wa sherehe ya Siku ya Walimu Dunia katika Uwanja Wa shule ya Sekondari Ushirombo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita. Aidha Mhe. Biteko amewakaribisha wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali kuzichangamkia fursa zilizopo wilayani Bukombe. Kuhusu suala la tatizo la umeme na kukatika katika kwake Mhe. Naibu Waziri Mkuu, ambaye pia ni Waziri Wa Nishati na Mbunge Wa Jimbo la Bukombe ameahidi haya.............. . . Full interview iki hap YouTube channel yetu @jembefmtz

CCM TANGA YAWAONYA WALIOANZA KUJIPITISHA KUSAKA UBUNGE, UDIWANI

 

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akiwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga 
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati akiwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga 
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege Tanga kwa ajili ya ziara ya kichama mkoani Tanga 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed  Suleiman Abdulla kulia akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema mara baada ya  kuwasili uwanja wa ndege wa Tanga tayari kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani Tanga
 

 Na Oscar Assenga, TANGA.


MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amewaonya makada wa chama hicho mkoani Tanga ambao wameanza kujipitisha pitisha kutangaza nia ya kutaka Ubunge na Udiwani waache mara moja maana wakiendelea wanajimaliza wenyewe.

Hemed ambaye pia Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga aliyasema hayo Octoba 8,2023 wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara yake ya kichama kwenye mkoa huo.

Alisema kwenye mkoa huo wapo watu wameanza kujipitisha pitisha wakitangaza nia ya kusaka udiwani na ubunge wakati wakidhana kufanya hivyo ni kosa hivyo niwatake walipofikia wasimame.

“Katika hili niwaonye watu ambao wameanza kujipitisha na kusaka ubunge na udiwani wakati viongozi hao bado wapo hapo walipofika wasimame wakiendelea wataendelea kujimaliza mimi ni mjumbe na wale sitamuoenea aibu mtu wa namna hiyo kwa maana sasa wabunge tunao achene wafanya kazi zao hatutakubali hili”Alisema

Mlezi huyo alisema ukiona mtu ana ndoto ya kuanza kuona anafaa kuwa mbunge na diwani sio pekee yake ana watu huko nyuma wanampa sapoti acheni hizo tabia chama kina utaratibu wake muda ukifika wataangalia nguvu yako .

Aidha alisema kwa sasa kwenye mkoa huo na yeye akiwa mlezi ameona aliseme mapema na kama kuna watu wanawatuma watu hizi hazikubaliki kutokana na taratibu za chama hicho.

“Kama hukufuata nidhamu ya chama haustahili kuwa kiongozi achene jambo hilo sasa tulenge kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tufanye kazi na tuweke nguvu kwenye uchaguzi wa mkuu wa 2025”Alisema

Alisema pia katika mkoa huo hawatakuwa tayari wala kumvumilia mtu ambaye anakwenda kuufanya ushindi wao uwe na tatizo wakati CCM haina tatizo.

Aidha alisema mtu huyo yeye ndio atakuwa tatizo atatupisha yeye kama ni wa serikalini wataangalia utarartibu kwa kumfikishia Taarifa Mwenyekiti wao Taifa Dkt Samia Suluhu kwamba hapa hatuendi vizuri na amekuwa hodari wa kufanya hivyo.

Kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Makamu huyo wa Pili wa Rais alisema wakati wanaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kauli mbiu ya mkoa huo ni wapo tayari kwa ajili ya uchaguzi huo wa 2024.

Alisema pili ili waende kwenye uchaguzi huo wakiwa vizuri lazima waendelea kuzidisha umoja na mshikamano baina yao wenyewe kwanza hilo anazungumzia kwa viongozi wakishikamana wao wanapokwenda kwa wananchi wanazungumza lugha moja ya ushindi wa CCM.

Alitumia wasaa huo kuwaomba viongozi wa wilaya na mkoa pale penye changamoto wewekane sawa ikiwemo kuondosha tofauti za na wasimame kwenye mstari utakaowaongoza wanachama wao kuelekea kukipigia kura chama hicho kwenye ngazi zote.

Alisema ili kuhakikisha wanashinda kwenye ngazi zote na wakifanya hivyo huo utakuwa ni ujumbe mzuri wa kuelekea 2025 huku akiwaomba wamuomnyeshe Rais Dkt Samia Suluhu na watanzania kwamba Tanga wakiamua wanamaanisha.

Hata hivyo aliwataka waende wakatimize lengo lao huku akiwahaidi kuwa mstari wa mbele kwa sababu hapendi kushindwa.

Makamu huyo wa pili wa Rais aliwataka Mwenyekiti anayehisi kwenye kata yake atashindwa awasamehe mapema kutokana na kwamba hawatakuwa tayari kupoteza chochote kwenye jambo hilo lazima wahakikishe wanashinda.

Kuhusu upinzani.

Alisema kwamba kwa mkoa huo wapinzani watatulia kama wanapakwa hina huku akiwataka kila mtu kwenye wilaya yake huo mkakati wanaimarisha kwenda kushinda kwenye serikali za mitaa.

Makamu huyo wa pili alisema wana malengo ya kwenda kushinda kama kuna jambo halikajaa sawa wawambie kutokana na kwamba chama hicho ni kikubwa na hawawezi kufanya mchezo kuingia kimasihara lazima waingie na wapate matokeo.

Umoja na Mshikamano alisema kwamba suala la umoja kamisaa yupo hapa kaa vizuri na kamisaa wako wa wilaya wote washauriane vema changamoto wamalize huko wakija wanakwenda kwenye utekelezaji na wanakwenda kumaliza shughuli zao na wao wanaendelea kubaki kuwa kidedea.

“Hakikisheni hilo mnalifanyia kazi kwani mkiniona nipo Zanzibar msifikirie ya Tanga siyajui na yanayojiri kwenye vikao najua kila siku nimekuja nikijua Tanga kuna nini niwaombe mshikamano huo ndio utatupelekea ushindi wa CCM.