ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 18, 2017

ARSENAL YABAMIZWA 3-1 NA WEST BROMWICH, HOFU YATANDA KAMA WATACHOMOZA TOP 4.

 
 Craig Dawson akiwa hewani juu ya Nahodha wa Arsenal, Laurent Koscielny kuifungia West Bromwich Albion bao la kwanza dakika ya 12 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya timu ya kocha Mfaransa, Arsene Wenger katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa The Hawthorns. 

Dawson alifunga mabao mawili na la tatu dakika ya 75, huku la pili la West Bromwich likifungwa na Hal Robson-Kanu dakika ya 55 na la kufutia machozi la Washika Bunduki wa London, likifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 15 

 Alexis Sanchez mpachika mabao wa klabu ya Arsenal's akionekana kuchoka mara baada ya timu yake kuelemewa.

Kwa masikitiko akiwa benchi  Alexis Sanchez mkono kichwani akisikitika mara baada ya kutolewa dakika za lala salama huku timu yake ikiwa nyuma ya matokeo.

YANGA HAINA CHAKE TENA LIGI YA MABINGWA.


YANGA SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanaco jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia.

Matokeo hayo yanamaanisha Yanga inatolewa kwa mabao ya ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga wataumia zaidi kwa kutolewa na Zanaco, kwani bao la kusawazisha la Wazambia hao Dar es Salaam lililopatikana dakika ya 78  kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame lilikuwa la kuotea.

Na pamoja na hayo, wachezaji wa Yanga walikuwa wamezubaa kusubiri wapinzani wao watoe nje mpira kiungwana (Fair Play) baada ya mchezaji mwenzao, Obrey Chirwa kuangushwa.

Siku hiyo, Yanbga ilitangulia kwa bao la winga Simon Happygod Msuva dakika ya 39 baada ya kuwachambua mabeki wa Zanaco kufuatia pasi nzuri ya kiungo Mzambia, Justin Zulu.

Na ushindi huu unaifanya Zanaco iendeleze rekodi ya kuitupa nje Yanga kwenye michuano ya Afrika, baada ya mwaka 2006 pia kuwatoa katika hatua kama hii ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakishinda 2-0 Lusaka baada ya kufungwa 2-1 Dar es Salaam.

Yanga sasa itamenyana na timu iliyofuzu hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho kuwania tikeit ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, wakati Zanaci inakwenda moja kwa moja hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya/Emmanuel Martin dk56.

Zanaco; Toster Sambata, Ziyo Tembo, George Kilufya, Zimeselema Moyo/, Chongo Chirwa, Saith Sakala, Taonga Bwembya, Ernest Mbewe, Boyd Musonda, Attram Kwame na Augustine Mulenga.

Friday, March 17, 2017

VACFT YAITUNUKU CHETI 'KAZI NA NGOMA' YA JEMBE FM.

 Aksante sana kwa Victory Against Cancer Foundation Tanzania kwa kututunukia cheti cha Uhamasishaji team #KAZINANGOMA ya @jembefm kupitia zoezi la hivi karibuni kupima, kuchunguza afya na ushauri wa tiba kwa Afya ya magonjwa ya kansa na moyo kulikofanywa na Madaktari Hospital ya Rufaa ya Bugando eneo la Bugarika jijini Mwanza. 

Mtangazaji wa kipindi cha 'Kazi na Ngoma' toka Jembe Fm Mwanza Mansour Jumanne (kulia) akipokea cheti cha kutambulika kama mmoja ya wanaharakati waliosaidia zoezi la Upimaji na Uchunguzi wa Afya kwa wanannchi kata ya Bugarika iliyopo wilayani Ilemela jijini Mwanza @kennyhirly (wa pili toka kulia)  @Tinomihayo toka (wa tatu) #Vacfoundation_tz @chrissthedj (kushoto) Picha by @gsengo Aksante #jembefamily Kwa sapoti ya pamoja.

Picha ya pamoja.

UN: SERIKALI YA SUDANI KUSINI YALAUMIWA KWA BAA LA; INGALI INANUNUA SILAHA.

SERIKALI ya Sudan Kusini ndiyo inayobeba lawama kubwa kwa baa la njaa linaloshuhudiwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo iliyoharibiwa na vita huku Rais wa nchi hiyo Salva Kiir akiendelea kutumia mamilioni ya dola zinazotokana na mauzo ya mafuta kuimarisha vikosi vyake vya ulinzi.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la umoja huo na jopo la waangalizi wa vikwazo dhidi ya nchi hiyo.
Waangalizi hao wa UN wamesema, asilimia 97 ya mapato yanayotangazwa rasmi ya serikali ya Sudan Kusini yanatokana na mauzo ya mafuta huku asilimia isiyopungua 50 ya mapato hayo ikitumika kwa masuala ya usalama.
Jopo hilo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limefafanua katika ripoti yake hiyo kuwa mapato yaliyotokana na mauzo ya mafuta yaliyouzwa kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi hadi Oktoba 2016 yalikuwa karibu dola milioni 243, lakini licha ya ukubwa wa matatizo ya kisiasa na hali mbaya ya kibinadamu na kiuchumi iliyopo serikali ya Rais Kiir imeendelea kununua silaha kwa ajili ya jeshi lake la Ukombozi la Wananchi wa Sudan (SPLA), vikosi vya huduma za usalama wa taifa, vikosi vingine tanzu pamoja na wanamgambo watiifu kwa serikali hiyo.
Raia wa Sudan Kusini wanaokabiliwa na ukame.
Umoja wa Mataifa ulitangaza baadhi ya maeneo ya taifa hilo changa zaidi duniani kuwa yamekumbwa na baa la njaa ambapo watu wapatao milioni tano na nusu, ikiwa ni takriban nusu ya raia wote wa nchi hiyo wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Machafuko na vita vya ndani vilizuka nchini Sudan Kusini Desemba mwaka 2013 baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake, Riek Machar kwamba amehusika na jaribio la kutaka kupindua serikali yake

TAASISI YA USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE (UDI) YACHANGIA MAENDELEO WILAYANI LUSHOTO

 Wanafunzi wa shule ya secondari viti kata ya shume wilayani Lushoto wakipokea mifuko ya saruji yenye thamani ya shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo kutoka kwa taasisi ya USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE (UDI) ikiwa ni katika kuchangia juhudi za Mh. Mbunge wa Mlalo mh. Rashid Shangazi za kuleta maendeleo jimboni hapo.
 Diwani wa kata ya Vuga wilayani Lushoto mh. Dhahabu jumaa akipokea miche ya miti kutoka kwa taasisi ya USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE , ikiwa ni juhudi za kuendeleza na kutunza mazingira wilayani Lushoto, pichani anayekabidhi ni katibu Mkuu wa UDI DIckson shekivuli na naibu katibu Mkuu Frank shempemba
Diwani wa kata ya vuga wilayani Lushoto mh. Dhahabu Ijumaa, akipokea dawa kutoka kwa taasisi ya USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE (UDI) kwa ajili ya zahanati ya vuga.

MAGAZETI YA LEO:- LISSU APIGA HODI JELA, BULEMBO AFICHUA SH MIL 50 ALIZOPEWA NA LOWASSA, MEYA KUMSHTAKI MAKONDA KORTINI KUHUSU VYETI VYAKE.


 Lissu apiga hodi jela, Bulembo afichua Sh. Mil. 50 alizopewa na Lowassa, Meya kumshtaki Mkonda kortini kuhusu vyeti vyake.
                                                   
 DCI aita polisi wa kimataifa msako msaidizi wa Mbowe, Hakuna ndoa bila cheti cha kuzaliwa, Mahakama yamganda Yusuf Manji. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa. 

Thursday, March 16, 2017

TANGAZO LA KUPOTEA KWA KIJANA ERICK RAPHAEL MSYALIHA ,ANATAFUTWA NA NDUGU ZAKE.



Pichani ni Kijana anayefahamika kwa  jina la ERICK RAPHAEL MSYALIHA anayeishi Sinza-Mugabe ametoweka Ghafla Tarehe 13.03.2017 majira ya usiku alipochukuliwa na watu wasio famika akiwa mitaa ya  nyumbani kwake. Mpaka sasa hajarejea nyumbani, hivyo anatafutwa na ndugu zake, Tunaomba  yeyote atakayemuona au kupata Taarifa zake atujulishe kwa namba +255718105959 au atoe Taarifa katika Kituo cha Polisi kilicho jirani nae,Tunatanguliza Shukurani zetu

MKAZI WA KIJIJI CHA ISENGULE MKOANI KATAVI FATUMA ISSA (22) AJIFUNGUA WATOTO WANNE.


Watoto wanne walizaliwa  na  mwanamke   aitwaye  Fatuma  Issa  22   Mkazi wa   Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema   mwambao  mwa  Ziwa   Tanganyika  Wilaya  ya  Tanganyika  Mkoa wa  Katavi wakiwa katika   chumba  maalumu  katika   Hospitali ya  Manispaa ya  Mpanda.
Huyu  ndiye  mwanamke   aitwaye   Fatuma  Issa  22  Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule   Tarafa ya  Karema   Wilaya  ya   Tanganyika    Mkoa wa  Katavi   akiwa   katika  chumba  maalumu  katika  Hospitali ya  Manispaa ya   Mpanda     baada ya kujifungua  watoto wanne kwa wakati mmoja  ambapo alijifungua  watoto hao  hapo machi 12  katika   Hospitali  hiyo  kati ya watoto hao mmoja ni wakike na watatu ni wakiume.

Mkuu  wa  Wilaya ya   Mpanda  Lilian  Matinga  akiwa  katika wodi ya  wazazi    katika   Hositali ya  Manispaa ya  Mpanda   aliwajulia  hali watoto wanne   mapacha  waliozaliwa hapo  Machi  12  mwaka huu kwa  wakati mmoja  na  mwanamke  aitwaye   Fatuma  issa  22   Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema  Wilaya ya  Tanganyika   Mkoa wa   Katavi
Picha  Na  Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog


  Na  Walter  Mguluchuma .
    Katavi yetu Blog
MKAZI wa kijiji cha Isengule , mwambao mwa Ziwa Tanganyika  katikawilaya ya Tanganyika  mkoani Katavi , Fatuma Issa (22) amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya  Manispaa ya Mpanda mwishoni mwa wiki.
 
Muuguzi  Mkuu wa Hospitali hiyo , Alexanda Kasagula alisema mama huyo alijifungua watoto hao wanne mwishoni mwa wiki  kwa  njia ya kawaida ambapo mama na watoto wake hao  wote wakiwa na afya njema.
 
“Mtoto wa kwanza ambaye ni wa kike alizaliwa akiwa  na uzito wa kilo moja na gramu 800 ,mtoto wa  pili alizaliwa akiwa na uzito wa kilo moja na gramu 500 , watatu alizaliwa akiwa na uzito wa  kilo moja na gramu 800 huku wanne alizaliwa akiwa na kilo  moja na gramu 700.

 
Kati ya watoto hao watatu ni wakiume  hali ya mzazi na watoto wake wote  wanaendelea vizuri  bado wamelazwa  katika  wodi ya wazazi hospitalini hapa “ alieleza .

Kwa upande wake , Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Jafar Kitambwa alieeleza kuwa  mama huyo na watoto wake wataendelea  kuwa chini ya ungalizi hospitalini hapo  hadi hapo watakaporuhusiwa rasmi kwenda nyumbani

 
Mama huyo alieleza kuwa yeye na mume aitwae Agustino Andrew (25) kama wanando huo utakuwa uzao wao wa tatu ambapo wana idadi ya watoto watano .
 
“ Mie na mume wangu  sasa tuna idadi ya watoto  watano  uzazi wangu wa kwanza  nilizaa mtoto  mmoja ambaye yuko hai.Hii itakuwa mara yangu ya pili  kujifungua  watoto zaidi ya mmoja  katika uzao wangu wa pili   nilijifungua mapacha  lakini mmoja wao alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa na pacha mwenzake  alikufa  miezi mitatu  baada ya
kuzaliwa.

 
Nimejifungua watoto  wanne  lakini tangu nijifungue sijapata tatizo lolote la  kiafya  naendelea vizuri mie na watoto  wangu wote nawashukuru  wauguzi ambao wamenisaidia  hadi nimejiufungua salama bila ya matatizo yeyote yale “ alieleza
Alieleza kuwa  mama yake mzazi ndie anayemwangalia hospitalini hapo huku akimsadia kuwalea watoto hao .

RAIS DKT MAGUFULI ATEMEBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU MPYA KIJIJINI CHAMWINO, DODOMA.

  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wahandisi na maafisa wa Wakala wa Majengo ya Serikali wakati alipowasili kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Sehemu ya matofali katika eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakati walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza wakati  Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea na wafanyakazi wa TBA  wakati wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskasi Muragili,akitambulishwa  kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiangalia ufyatuaji wa  matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakichanganya mchanga na saruji na kusaidia kufyatua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakikagua mchanga unaotengezewa matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakimwangalia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Jenista Muhagama (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akiagana na  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga   kagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017.
PICHA NA IKULU

QUALITY GROUP KUANZISHA KAMPUNI LUKUKI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

 Ofisa Mtendaji Mkuu  wa Kundi la Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Nicholas Ralph akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Ralph akielezea jinsi uongozi ulivopanga mikakati ya kuboresha kampuni zilizopo na kuanzisha nyinginezo nchini na nje ya nchi.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo

Suleiman Msuya
KAMPUNI ya Quality Group Limited (QGL), imesema inaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni hiyo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa QGL, Nicholas Ralph alisema katika kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi wameanzisha mfumo unaotambua na kudhibiti uhalifu huo kwenye taasisi (e-Governance).

Alisema mfumo huo wa utambuzi na udhibiti unapaswa kuwepo katika idara zote za Serikali kwani una utija ni salama zaidi hasa katika kulekea katika Tanzania ya maendeleo endelevu.

Ralph alisema QGL imewekeza katika sekta mbalimbali  kama afya ambapo wanatarajia kujenga vituo 4,000 vya afya nchini kote pamoja na vioski vya kutoa afya ili kuendana na teknolojia ya sasa na kurahisisha kila mwananchi anapata huduma bora ya afya.

Alisema pia wamekubaliana na kampuni kutoka nchini Urusi ili kusambaza vifaa tiba na kampuni nyingine kutoka Marekani itatoa huduma ya ndege katika huduma ya dharura.

“Pia kampuni ya QGL imeingia makubaliano na kampuni kutoka nchini Ireland kujenga na kuwekea uongozi katika utawala ambapo itasaidia kuongeza teknolojia kwa kampuni za ndani,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kampuni ya QGL imekuwa ikisadia wavuvi katika Kanda ya Ziwa kwa kuwapatia vitendea kazi na matibabu, kusaidia elimu na pia ilisaidia mapambano ya ugonjwa wa Ebola.

Alisema kampuni yao imefanikiwa kuongeza ajira, mafunzo, kukuza uchumi ili kuhakikisha inaunga mkono  mpango wa maendeleo wa Serikali wa 2025.

Ralph alisema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa viongozi na waajiriwa vijana kupitia program ya Moreh Derech ambayo imekuwa na mafanikio makubwa.

Aidha, alisema katika kuhakikisha kuwa wanapanua ushirikiano na taasisi za kimataifa wamesaini makubaliano na Kampuni ya  Solanika International Tractors Limited ya India ambao watakuwa wanaingiza matrekta 1,000 kwa mwaka hivyo kuongeza ajira 1,200 ifikapo mwaka 2018.

“Pia tumesaini barua katika miradi ya madini ambapo tunarajia kuuzungumzia vizuri pindi hatua zote zikiwa zimekamilika,” alisema.

Halikadhalika alisema wamewekeza katika viwanda vya sukari na maziwa ambapo wananchi wengi wa Kitanzania ndio watafaidika kwa kuuza bidhaa husika katika viwanda hivyo vyenye teknolojia ya kisasa na uongozi kutoka Israel, Ulaya na Afrika Kusini.

Ralph alisema QGL imekuwepo kwa zaidi ya miaka 30 ambapo inashirikiana na kampuni kubwa duniani kama General Motors (GM), Honda, Isuzu, Bridgestone na Chevrolet.

Alisema kutokana na ushirikiano huo QGL imeajiri zaidi ya watu 667,300 na kupata faida ya dola za Marekani bilioni 348.6 hayo yakichangiwa na uwajibikaji, uwazi, uaminifu na mafanikio.


Alisema mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanakuwa ni sehemu sahihi ya kuchochea maendeleo ya nchi na wananchi wa Tanzania. 

KITUO CHA EATV NA TAASISI YA HAWA YAWASHUKURU WATANZANIA KWA KUFANIKISHA KUCHANGIA KAMPENI YA 'NAMTHAMINI'

Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akizungumza mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusua mafanikio yaliyopatikana kupitia kampeni ya 'NAMTHAMINI',Basilisa amebainisha kuwa kupitia EATV na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na pakiti za pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673 kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.Pichani kulia ni Mratibu wa Vipindi Eastafrika Radio,Irene Tillya na kushoto ni Mratibu wa Vipindi EATV,Sophie Proches.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akifafanua jambo kuhusiana na mafanikio makubwa waliyoyapata kupitia kampeni hiyo ya 'NAMTHAMINI',Kiria emesema kuwa Katika kampeni hiyo ambayo wananchi walijitokeza kuichangia katika kuonesha kumjali mtoto wa kike aliyepo shuleni zilichangwa jumla ya shilingi 20,176,110, ambazo fedha taslim shilingi 11,774,610 na pedi za thamani ya shilingi 8,401,500.
 Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na mafanikio ya kampeni hiyo 'Namthamini',iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za Kike) kwa wanafunzi wa Sekondari,ambapo takwimu zinaeleza kuwa karibia asilimia 45 ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi kutokana na kukosa pedi za kujistiri.
 Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika mapema leo jijini Dar.

-------   ------   ------  ----------


Kituo namba moja kwa vijana East Africa Television (EATV) Limited kikishirikiana na Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA foundation) kinapenda kutoa shukrani za dhati, kwa umma wa watanzania  kwa  kufanikisha kuchangia kwenye kampeni ya Namthamini.

Namthamini  ni kampeni iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za Kike) kwa wanafunzi  wa Sekondari, kutokana na takwimu kuonesha karibia asilimia 45 ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi kutokana na kukosa pedi za kujistiri.

Kwa wastani wanafunzi wa kike wengi hupoteza siku tano hadi saba kila mwezi kutokana na ukosefu wa pedi za kujisitiri, na kwa mwaka inakadiriwa kukosa masomo kwa takribani siku 60 hadi 70.

EATV na East Africa Radio katika kufikisha mchango wake kwa jamii, na kwa kuangalia Siku ya Wanawake Duniani, Machi mosi tuliamua kuanzisha kampeni hii kwa kuishirikisha jamii ili kumuwezesha mwanafunzi wa kike asikose masomo yake na kumfanya kutofikia lengo lake kimasomo kwa kukosa pedi pale awapo kwenye hedhi.

EATV na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na pakiti za pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673 kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.

Katika kampeni hii ambayo wananchi walijitokeza kuichangia katika kuonyesha kumjali mtoto wa kike aliyepo shuleni zilichangwa jumla ya shilingi 20,176,110, ambazo fedha taslim shilingi 11,774,610 na pedi za thamani ya shilingi 8,401,500.

Michango yote ya fedha iliyopatikana itatumika katika kununua pedi na zitaelekezwa moja kwa moja katika shule za Sekondari 20 zenye uhitaji zilizoteuliwa kupata msaada huu, katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Lindi, Pwani na Tanga.

Uongozi wa EATV Limited na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa Foundation) inapenda kutumia nafasi hii kwa dhati kuwashukuru wananchi wote walioguswa na tatizo la pedi kwa wanafunzi wa kike na kuichangia kampeni ya Namthamini na kuonyesha kuwa kwa pamoja tunaweza. Sisi EATV husema Together Tunawakilisha.

Mwisho kabisa tunapenda kusisitiza kuwa tatizo la wanafunzi wa kike kukosa kuhudhuria shuleni kutokana na kukosa pedi za kujisitiri ni la kwetu sote hivyo East Africa Television Limited pamoja na Taasisi ya Haki za wanawake inatoa wito kwa jamii kuendelea kuungana kwa pamoja katika kusaidia watoto wa kike kupata mahitaji muhimu wawapo shuleni, ili wapate kusoma kwa amani pasipo kukosa kuhudhuria darasani.