ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 25, 2010

HAYA HAYA..

AJALI HII NILIKUTANA NAYO NJIANI NIKITOKA SENGEREMA KUELEKEA WILAYA YA GEITA AMBAPO ROLI JINGINE LA MIZIGO LILIGONGANA UBAVU KWA USO KWENYE KONA NA ROLI HILI LA MIZIGO CHANZO KIKIWA NI MWENDO KASI NA UFINYU WA BARABARA KWANI BARABARA HII NI YA GARI MOJA NA NUSU HIVYO YAHITAJI KUSUBIRIANA WAKATI MKIPISHANA.

DREVA WA GARI HILO ALIYEVAA OVAROLI INASHANGAZA AMEWEZAJE KUSALIMIKA KATIKA AJALI MBAYA KAMA HII HASA UKIZINGATIA KUWA ROLI LILIGONGA UPANDE WAKE.

GARI LILIPOTEZA UELEKEO NA KUGONGA KISIKI NA KUJICHIMBIA.

KUNA MENGI YALIYO YA KITALII YAKUJIVUNIA NDANI YA ZIWA VICTORIA.

WATALII TUNAWAKARIBISHA.

JAMANI NISAIDIENI NDEGE YUHU NDEGE GANI?

Thursday, September 23, 2010

HAPA NA KULEEEE!

TATIZO LA MAJI SAFI YALIYO SALAMA LIZIDI KUENDELEA KUWA SUGU HAPA NCHINI, JEH! TUNAHOJI WAGOMBEA AU TUNACHUKULIA POA AKA YAANI FREEESHII!!? PICHANI NI WATOTO WA KIJIJI CHA NKOME WILAYANI GEITA.

KISIMA CHENYEWE.

UMIA UJAE.

KIJIWE CHA KAHAWA KEMONDO JIJINI MWANZA.
UKITAKA BREAKING NEWS ZA MJINI NA HABARI ZA SIASA AMBAZO ZAMA HIZI KILA MTANZANIA AMESHIKIA BANGO HAPA NDO PENYEWE, NASKIA PIA KUNA DEGREE ZINAZO TOLEWA BURE KWENYE VIJIWE VYA KAHAWA.

KITUO CHA MAFUTA MWALONI KIRUMBA CHANUSURIKA KUTEKETEA.

KITUO CHA MAFUTA CHA MWALONI KIRUMBA JIJINI MWANZA JIONI YA JANA MAJIRA YA SAA 12 KASORO KIMENUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO MARA BAADA YA MOTO KUZUKA WAKATI WA USHUSHAJI WA MAFUTA KUTOKA KTK ROLI MOJA KWENDA KWENYE VISIMA VYA KUHIFADHIA MAFUTA KITUONI HAPO.

MARA BAADA YA KUMALIZA TENKI LA 1 NA LA 2 DEREVA WA ROLI HILO ALLY HAMZA WA KAMPUNI YA 'EHANDO RAD HURAGE' ANASIMULIA KUWA WAKATI AKIWA ANAENDELEA KUSHUSHA MAFUTA KATIKA TENKI LA 3 MOTO UKAZUKA TOKA KISIMA ANACHO MIMINA MAFUTA UKIPANDA JUU KUFUATA MKONDO WA MAFUTA, NDIPO ALIPOAMUA KUSITISHA ZOEZI LA UMIMINAJI HUKU AKIJARIBU KULIONDOSHA GARI ENEO LA MOTO JAMBO AMBALO ALIFANIKIWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA SIMON SIRO AMELIPONGEZA JESHI LA ZIMA MOTO KWA KULIWAHI TUKIO NA KUSHIRIKI VYEMA KATIKA KUUZIMA MOTO HUO HASA UKIZINGATIA KUWA ENEO KITUO HICHO KIKO KARIBU NA MAKAZI YA WATU, SOKO KUU LA MWALONI BIASHARA YA SAMAKI NA VYANZO VINGINE VYA MAPATO NA UCHUMI KAMA BANDARI NDOGO NA NK.

WAKAZI WA MWANZA NA WAFANYABIASHARA WAKIDHIBITIWA ILI WASISOGEE ENEO LA TUKIO.

MOJA KATI YA HASARA ZILIZO PATIKANA KUTOKANA NA MOTO HUO.

MKUU WA KITUO CHA KIRUMBA MAMA MATOLA PAMOJA NAE KAMANDA WA POLISI JIJINI MWANZA SIMON SIRO WAKIPATA MAELEZO.

JESHI LA POLISI JIJINI MWANZA LIKO KATIKA MIKAKATI KUBAINI SABABU ZA MATUKIO YA MOTO AMBAYO YAMEKUWA YAKIJITOKEZA MFULULIZO ENEO HILI LA MWALO WA KIRUMBA IKIWA NI PAMOJA NA MATUKIO MA3 YALIYO RIPOTIWA MWAKA HUU IKIWA YA KUUNGUA KWA BOTI ZA MAFUTA KATIKA YADI ZA MWALO WA KIRUMBA.

Wednesday, September 22, 2010

PUMZIKA KWA AMANI BIBI YETU JOSEPHINA LEMY ZAKAYO MANGA.

NI KAMA MSHUMAA UWAKAO KATIKA UPEPO MKALI. ILIKUWA TRH 19.9.2010 SAA NANE MCHANA BIBI YANGU MZAA BABA ALIAGADUNIA.

DADA ZAKE MAREHEMU BIBI JOSEPHINA AMBAO NI WADOGO ZAKE WAKIAGA MWILI WA MAREHEMU KWA PAMOJA.

MOJA KATI YA KITUKUU WA MAREHEMU.

SHANGAZI YANGU SALOME SIMBIRA AKIUAGA MWILI WA MAMA YAKE.

KWAYA YA AIC NKOME GEITA ILIUFARIJI UMATI VYA KUTOSHA SIKU YA MAZISHI HATA KATIKA MKESHA WA MATANGA.

MWILI WA MAREHEMU UKISHUSHWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE.

"ULIUMBWA KWA MAVUMBI NA MAVUMBINI UTARUDI" NI KAULI YA SIMANZI SANA.

WAJUKUU (NAMI NIKIWA MMOJA WAO) TUKIWEKA MASHADA YA MAUA.

BIBI JOSEPHINA ALIFARIKI 19.SEPT.2010 KTK HOSPITALI YA WILAYA YA GEITA MWANZA NA KUZIKWA NYUMBANI KWAKE NKOME GEITA TAREHE 21.SEPT.2010. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Monday, September 20, 2010

MWANZA MWANZA NA MAMBO YA WEKEEND.

NI PITA PITA ZA STAREHE NDANI YA CLUB MAARUFU JIJINI MWANZA VILLA PARK, HAPA NI DJ MALINZ NA AY.

WADAU WA BLOG HII ..... WAKILA RAHA NA KUPATA MUZIKI WA UKWELI NDANI YA CLUB ILIYOREJEA UPYA STONE CLUB MWANZA.

FLOWERS DOIN.. EEENH ALAJIIIII NDANI YA STONE CLUB.

WADAU NAMBA MOKO.

MIE NA MANAGER WA PASSION FM MR. HILL.

EEEEEENH! THIS IS HOW WE DO! NDOMANAKE...

AFYA YA KID BWAY YAENDELEA KUIMARIKA.

Afya ya mtangazaji wa radio FREE AFRIKA KID BWAY inaendelea kuimarika kadri anavyoendelea kupata matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Maendeleo ni ya kuridhisha yanayotia matumaini makubwa sana tofauti na awali. Kwa hivi sasa mshkaji anaweza kula mwenyewe ingawa chakula anachotumia ni kile rojorojo kama uji, supu na vyakula vilivyopondwapondwa kwani nguvu ya taya kutafuna inampa maumivu.

Kutokana na maumivu ya kichwa anapatiwa dawa maalum na amepewa ushauri kuwa asifanye maongezi zaidi ya kujuliwa hali na kusikilizwa juu ya huduma anayohitaji, pia anapaswa kupumzika muda mwingi, hivyo amekuwa akishinda kitandani akiwa amelala.

Nimepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa madaktari wa hapa ameniarifu kuwa bahati iliyoje kuna madaktari wataalamu wa upasuaji kutoka nchi za mbali ambao wamekuja kitambo sasa kwa ajili ya kutoa huduma za upasuaji bure nao wamemtembelea na kumfanyia uchunguzi na wamemweka katika ratiba na sasa wako katika mikakati ya kumpa huduma, ingawa daktari hajanitamkia wazi kwamba wameona nini na watakwenda kufanya nini. Lakini kwa ufupi hali inaridhisha.