ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 7, 2016

SERIKALI YAIPONGEZA TAASISI YA DHI NUREYN KWA KUOKOA MAISHA YA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO

DSC_3050

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation na washirika wake zilizofanikisha zoezi la kambi ya Moyo kwa watoto iliyokuwa katika Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo imemalizika juzi.
DSC_3073Baadhi ya wageni waalikwa na Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia tukio hiulo.
DSC_2859
Wageni waalikwa wakifuatilia tukio hafla hiyo
DSC_2872Baadhi ya Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakifuatilia hafla hiyo na wakati huo Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akitoa hotuba yake kwa wageni waalikwa (Hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo.DSC_2873Baadhi ya Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakifuatilia hafla hiyo.
DSC_2892Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI),Profesa Mohamed Janabi akitoa shukrani zake kwa taasisi zilizofanikisha zoezi hilo.
DSC_2902 DSC_3035Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akiabidhi tuzo kwa mgeni rasmi, Mh. Dk. Kigwangalla kwa namna Serikali inavyothamini mchango wa taasisi binafisi hapa nchini.
DSC_2908Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi katika kuthamini taasisi hiyo
DSC_2923Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete , Dk Peter Kisenge akitoa cheti maalum kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri
DSC_2928Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi akipokea tunzo maalum kama mchango wa JKCI katika kuthamini na kuokoa maisha ya watoto hapa nchini.
DSC_2944Prof. Jameel Alata ambaye ni kiongozi wa Madaktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto akitoa tunzo maalum kwa Viongozi wakuu waliofanikisha taasisi zao katika zoezi la kambi ya moyo hapa nchini
DSC_2953
Picha chini ni baadhi ya Madaktari waliokabidhiw vyeti vya shukrani:
DSC_2995 DSC_2999
DSC_3089Picha ya pamoja ya madaktari na wageni waalikwa akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla wakati wa hafla hiyo ya kufunga kambi ya Moyo Muhimbili.
Serikali kupitia WIzara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imepongeza juhudi za Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Kiislam ya hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn Islamic Foundation kwa juhudi zake za kuunganisha nguvu na taasisi zingine za nje  katika kuokoa  maisha ya watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.
Akizungumza wakati wa hafla maalum ya kufunga kambi ya Moyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali inatambua juhudi za taasisi binafsi katika kusaidiana nazo hivyo kwa hatua hiyo, suala la magonjwa ya moyo ambayo awali yalikuwa yakitibiwa nje kwa sasa yatashughulikiwa hapa hapa nchini.
“Tunaishukuru taasisi ya Dhi Nureyn na taasisi zote kwa kushirikiana na taasisi ya JKCI, kwani zimeweza kusaidia kuokoa maisha ya watanzania ikiwemo kuokoa vifo ambavyo vingetokea kwa watoto wenye matatizo ya moyo.
Zoezi hili limeweza kuvuka lengo la asilimia 70. Kwa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu hayo ya moyo.  Tunaamini mwaka huu tukaongeza malengo,  na tayari wameweza kufanya operesheni takribani 200. Hii ni misheni ya pili na kwa maana hiyo wameweza kuvuka malengo ya asilimia 70 yale tuliyowapa.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Na kuongeza kuwa, Awali kabla ya utaratibu  wa JKCI, wagonjwa 250 walikuwa wanapelekwa nje kufanyiwa operesheni hizo za magonjwa ya moyo. Lakini kwa mwaka huu hata miezi sita bado haijafika, Wagonjwa zaidi ya 200 wameshafanyiwa hapa hapa nchi operesheni hizo. Kwa hatua hiyo wameweza kuvuka lengo la asilimia 70 na wanataka wafikie angalau wagonjwa 400 hadi 500 kwa mwaka” alimalizia Dkr. Kigwangalla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri  alieleza kuwa, taasisi hiyo imekuwa kiungo kuzitafuta taasisi zingine za nje ya nchi na kuleta wataalam hao wa bingwa wa magonjwa ya moyo hapa nchini ni faraja kubwa kwa taasisi hiyo na Watanzania wote kwani imeweza kuokoa maisha ya watoto hapa nchini.
Miongoni mwa taasisi hizo  zilziofanikisha kambi hiyo ya Moyo hapa nchini ni pamoja na Taasisi ya  Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktai kutoka Saud Arabia, Taasisi ya RAF kutoka Qatar, Taasisi ya Dhi Nureyn (Tanzania) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Tanzania). Zoezi hilo la kambi ya magonjwa ya moyo ni la pili kufanyika hapa nchini  likiwemo la kwanza la mwezi Mei mwaka jana (2015) na kufanikiwa kuwatibu watoto 66 wa Kitanzania ambao walipangiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na kufanya kuokoa mabilioni ya shilingi ya Serikali kwa ajili ya gharama za matibabu hayo.
“Tunaishukuru sana taasisi ya Muntada Aid, kwa kujali, kuthamini na kujitolea kufanya kazi hii iliyookoa maisha ya Watoto weyu. Pia iliyowaondoshea maumivu watoto na wazazi wao na kuwapa matumaini mapya ya maisha. Pia tunaishukuru Serikali ya Saud Arabia, Taasisi ya Jakaya Kikwete  na Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla pamoja na washirika wetu wote wakiwemo Taasisi ya Al Akhlaaq na wanahabari na wote kwa ujumla pamoja na mdaktari wa hapa ndani. Nashukuru sana” alimalizia Sheikh Said Ahmed Abri wakati wa kutoa hutuba yake hiyo kwa wageni mbalimbali pamoja na madaktari hao.
Aidha, madaktari hao pamoja na taasisi zote zilizofanikisha zoezi hilo, zilitunukiwa vyeti na tunzo maalum kwa ajili ya shukrani.

YANGA YATISHA AFRIKA, MSUVA NA MATHEO MASHUJAA… WAANGOLA CHALI KIFO CHA MENDE

Simon Msuva akikimbia kushangilia baada ya kufunga bao la kwanza jioni ya leo Uwanja wa Taifa 
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imeshinda 2-0 dhidi ya Sagrada Esparanca ya Angola katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shukrani kwa wafungaji wa mabao hayo, Simon Happygod Msuva na Matheo Antony Simon, yote kipindi cha pili na sasa Yanga itahitaji sare katika mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kuingia kwenye makundi.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Ghana, Joseph Odartei Lamptey aliyepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera David Laryea na Malik Alidu Salifu, Yanga ilipoteza nafasi nyingi za kufunga kipindi cha kwanza.
Simon Msuva akitia krosi mbele ya beki wa Sagrada Esperanca Roadro Juan da Semero
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akimtoka beki wa Sagrada Esperanca, Antonio Kasule
Kikosi cha Yanga kilichoanza leo dhidi ya Sagrada Esperanca
Kipindi cha pili pia kilianza kwa ugumu, Yanga wakiendelea kutengeneza nafasi nzuri na kushindwa kuzitumia, hali iliyoufanya mchezo uwe mgumu upande wao.

Kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Amissi Joselyn Tambwe ndiye ambaye hakuwa na bahati kabisa siku ya leo kutokana na kupoteza nafasi nyingi za wazi.

Baada ya kosakosa za muda mrefu, hatimaye vijana wadogo wazawa, Msuva na Matheo wakawainua mashabiki wa Yanga mfululizo kwa mabao safi.

Msuva alianza dakika ya 72 akimalizia krosi maridadi ya winga Godfrey Mwashiuya aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Malimi Busungu, kabla ya Metheo kufunga la pili dakika ya 90 kwa shuti la mbali. 

Pamoja na ushindi huo, Yanga ilionekana kabisa kuathiriwa na kuwakosa nyota wake wawili Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma ambao walikuwa wanatumikia adhabu za kadi za njano walizopewa mfululizo kwenye mechi dhidi ya Al Ahly mwezi uliopita.

Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela/Mbuyu Twite dk46, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Malimi Busungu/Godfrey Mwashiuya dk53, Amissi Tambwe na Deus Kaseke/Matheo Anthony dk77.

Sagrada Esperanca; Yuri JKose Tavazes, Roadro Juan da Semero/Paul Camufingo dk64, Dennis Conha Morais, Asenio Cabungula, Antonio da Silva Oliveira/Evanildo de Jesus Pedro dk64, Ntaku Zabakaka, Manuel Paulo Joao, Alentua Tangala Rolli, Osvaldochitumba Palana/Aderito Chosolla dk80, Manuel Sallo Conha na Antonio Kasule. 

FNB SASA RASMI JIJINI MWANZA.

 Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema mkoa wa Mwanza una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji mkubwa wa sekta mbalimbali za kiuchumii karibuni ni ishara kuwa Mwanza inakua kwa kasi.

"Tunakaribisha uwepo wa FNB  na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha huduma zenu hapa na  mikoa mengine," alisema Mkuu wa Mkoa.

Alisema mbali na mkoa wa Mwanza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi bali pia inazalisha mali nyingi na ina utajiri mkubwa wa rasilimali. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya FNB Tanzania la Mwanza jana jijini humo huku akiambatana na Mkuu wa Biashara wa FNB Tanzania, Francois Botha (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma (kulia) na Alex Mziray, Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo.
 “Tunatarajia kuwa mtatoa mchango mkubwa katika utoaji huduma za kifedha mkoani Mwanza kupitia huduma zenu mbalimbali kwa kutumia ubunifu na utaalamu wenu,” Mongella alisema.
Wadau wa kibiashara na wawekezaji.
 First National Bank ni benki inayotoa huduma kwenye nchi mbalimbali barani Afrika tangu mwaka 1874.
Hivi sasa FNB inatoa huduma zake kwenye nchi za Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zambia, Mozambique, Lesotho, Swaziland na Tanzania na mpango wake ni kuwa benki inayohudumia watu wengi zaidi barani Afrika.



 Benki ya First National Bank Tanzania (FNB) imeendelea kupanua wigo kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akisalimiana na mmoja kati ya wadau wa FNB baada ya kutinga ndani ya Benki hiyo kama sehemu ya ufunguzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma akisalimiana na mmoja kati ya wadau wa FNB baada ya kutinga ndani ya Benki hiyo kama sehemu ya ufunguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na benki ya FNB Tanzania kutoka kwa Asmini Gambo, Mshauri wa Huduma kwa Wateja na Mauzo wa benki hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua huduma za benki hiyo jijini Mwanza.
 Mkuu wa Biashara wa FNB Tanzania, Francois Botha akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma (kulia)  jinsi ya kuhamisha fedha na kupata huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi. 
 Mkuu wa Biashara wa FNB Tanzania, Francois Botha akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella jinsi mashine ya kisasa ya kutolea fedha inavyofanya kazi baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua huduma za benki hyo jijini Mwanza.  Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumza na waandishi wa habari.
Yapi manufaa kwa ujio wa FNB.
Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma alifunguka jinsi jamii itakavyoufaika na shughuli za kibenki.
Pamoja sana.
Sehemu ya kusanyiko la uzinduzi.
Uzinduzi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Francois Botha alisema uzinduzi wa tawi la FNB Mwanza umelenga kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za kibenki na za kifedha katika mkoa huo.

  “Uzinduzi wa tawi la Mwanza ni sehemu ya uwekezaji endelevu na mkakati wa kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia tumezingatia ukuaji wa haraka wa mkoa wa Mwanzaambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.”

Botha alisema tawi Mwanza ni la tisa miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati  wa kupanua mtandao wa matawi ili kuyafikia maeneo yote nchini.

“ First National Bank daima tunafikiri njia mbalimbali za  ambazo tunaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la  Mwanza litatoa ufumbuzi wa kina kwa wateja wanao ishi Mwanza na maeneo jirani  yenye biashara inayokua kwa kasi” Botha alisema.

Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishi jijini Mwanza na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi,” alisema Botha.
Picha ya pamoja.
G.Sengo.
Tawi hili lililofunguliwa kwenye jingo jipya la Rock City Mall litatoa huduma za kawaida za kibenki pamoja na huduma za dijitali kwa masaa 24 ili mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.

First National Bank Tanzania ilifungua milango yake rasmi nchini Tanzania tarehe 27 Julai 2011, tawi la Mwanza likiwa ni la tisa, matawi mengine ni pamoja na tawi la makao makuu, Mbezi Beach, Sinza, Mbagala, Quality Centre, Peninsula, Kariakoo na tawi la Kimweri. 

Kwa taarifa zaidi tembelea www.fnbtanzania.co.tz au tuma barua pepe info@fnb.co.tz

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO May 7, 2016.


Neno Baby lachafua hali ya hewa bungeni, Rais Magufuli kugawa bure sukari iliyofichwa, Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.  

Magufuli kutaifisha sukari iliyofichwa, Mbunge CCM azua tafrani, Muarobaini wa walioua viwanda upo karibu. Pata dondoo hizi hapa. 
 Simba kushushwa daraja, Stand United yagongea jezi, Yanga na Experance vitani leo. Dundika na habari za michezo hapa. 

Friday, May 6, 2016

MAJAMBAZI YATIKISA TENA KATA YA KISHIRI/IGOMA JIJI LA MWANZA, YAPORA MADUKA MAWILI NA KIBANDA CHA M-PESA YAMJERUHI MMILIKI WAKE KWA RISASI AJIJARIBU KUYATOROKA.


NA MWANDISHI WETU, MWANZA.

JIJI la Mwanza lazidi kutikiswa na majambazi ambapo safari hii ilikuwa ni maeneo ya Kata ya Kishiri zamani Igoma ambapo walivamia na kupora fedha huku wakibuni stahili mpya ya kuimba wimbo “tumekuja kuchukua pesa zetu hatutaki kuuwa” hali iliyoleta wasiwasi kwa wananchi jijini Mwanza.
 
Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamis Mei 6 majira ya kati ya saa 3 hadi 4 usiku ambapo watu wanaodhaniwa majambazi wakiwa na silaha za moto waliweza kuzingila kwa muda eneo la Kishiri kwenye maduka zinapogeuzia dalalala na kufanya uporaji wa fedha kutoka katika maduka mawili ya bidhaa mbalimbali na kisha kuhamia kibanda cha jirani cha M-Pesa.
 
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo huku wakiomba majina yao kutotajwa walieleza kwamba majambazi hao wakiwa wamevalia makoti marefu na kufunika nyuso zao yakitumia silaha walivamia maduka mawili na kuamuru kupatiwa fedha bila ubishi kwa kuwa lengo lao ni fedha si kuuwa .
 
“Waliku na wimbo wao walioimba “tumekuja, tumekuja kuchukuua fedha zetu hatutaki kuuwa towa pesa” huku baadhi wakitoa bunduki na kuwatishia wamiliki na wauzaji kuwapatia pesa bila kufanya ubishi na baada ya kupora waliondoka katika maduka hayo na kuelekea eneo ambalo kulikuwa na kibanda cha mihamala ya fedha cha M-Pesa huku yakifyatua risasi hewani kutishia wananchi,”alieleza mmoja wa mashuhuda. 
 
Alieleza kwamba baada ya kukaribia kibanda cha M-Pesa huku aliyekuwa ndani ya kibanda hicho akiwa tayari amefunga baada ya kusikia mlio wa risasi kwa majirani zake wa maduka ya alihisi hali si shwari na kufunga haraka ili kuondoka katika eneo hilo ambalo tayari hata hivyo lilikuwa limeisha zingilwa na watu hao waliokuwa wakiimba na kufyatua risasi hewani.
 
“Ilikuwa kama sinema hivi na baadhi hawakujua kinachoendelea na wananchi wengine walianza kukimbia baada ya kusikika milio ya risasi haku mmiliki wa kibanda cha M-Pesa akiamuliwa kusimama na majambazi hayo akijaribu kukimbia kutoroka lakini yalifanikiwa kumpiga rirasi ya muguni na kumjeruhi vibaya,”alisema. 

Aliongeza kuwa watu hao ambao ni majambazi walionyesha dhalau kubwa kwa kufanya uhalifu huo huku wakiimba nyimbo mithili ya kutokuwepo vyombo vya ulinzi na usalama na kusababisha wananchi wengi kuwa na hofu ya usalama wa maisha yao pamoja na mali zao kutokana na watu hao kufanya matukio mapema na kuondoka bila hata Polisi kufika pamoja na taarifa kutolewa na wananchi juu ya matukio yanapotokea hata kusikia kuwa wamekamatwa baada ya kutokea matukio ya uhalifu jambo ambalo wananchi wameanza kuhoji kazi ya Polisi nini kwa sasa?.

 
Kufatia tukio hilo ikiwa ni siku chache tangu kutokea tukio jingine la ujambazi katika eneo la Ibungilo Wilaya ya Ilemela ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na silaha walivamia duka la kufanya mihamala ya fedha (M-Pesa) na wakala wa benki ya CRDB na kumuua mmiliki wake huku watu wengine watatu wakijeruhiwa kwa risasi.
 
GSENGO BLOG ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC), Hemerd Msangi, kwa njia ya simu ya mkononi haikuwa hewani na kuamua kumtafuta Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO), Augustine Senga naye simu yake ya mkononi haikupatikana ili kuweza kutoa taarifa za tukio hilo na hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi na mali zao kuwa shakani.
 
Kwa upande wake alipotafutwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye simu yake ya mkononi majira ya saa 9:30 alasiri alipokea na kuomba apigiwe tena badae kwa kuwa alikuwa kwenye kikao ambacho yeye ndiyo alikuwa akikiendesha kwa wakati huo na kushindwa kupata kauli ya viongozi hao juu ya tukio hilo ambalo kwa linadaiwa kuwa la kumi nne kutokea kwa muda wa kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu.
 
Huku baadhi ya wananchi wakiomba serikali ya Mkoa kupitia kwa RC Mongella kuubana Uongozi wa Polisi Mkoa na Wilaya zake kuhakikisha wanawasaka watu hao wanaoendesha uporaji wa mali, fedha na kuuwa pamoja na kuwajeruhi kwa risasi watu wengine ili kukomesha mitandao hiyo mkoani Mwanza ambayo imeshika kasi kwa sasa.
 
Imedaiwa kwa yapo makundi ya mitandao mitano kati ya saba ambayo kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (Mbunge-Misungwi) kueleza hivi karibuni katika matukio ya ujambazi jijini Mwanza Polisi ilibai kuwepo mtandao wa makundi saba ya uhalifu ambapo mawili kati yao yalikuwa tayari yamesambaratishwa huku Polisi ikihangaika kuyasaka makundi matano ya uhalifu.
 
Baadhi ya wananchi wamedai kuwa pengine kuendelea kwa matukio ya uhalifu wa kutumia silaha ni dalili tosha kuwa makundi matano bado hayajabainika, huku wakitaka juhudi zaidi ziongezwe na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi watakaoweza kutoa taarifa za siri ili kuwezesha kukamatwa watu walio ndani ya makundi hayo wakiwemo wamiliki wake na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, na wengine wakitaka Jeshi hilo kuwafatilia nyendo za watu walioachiwa huru kutoka katika Magereza mbalimbali hivi karibuni kwa msamaha wa Rais Dk John Magufuli, alioutoa kuazimisha sherehe za Muungano wa tanzania na Zanzibar.

WACHA NIKUSOGEZEE YALIYOJIRI HII LEO BUNGENI.


Hotuba ya bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji kwa mwaka 2016/2017 yawasilishwa mezani kwa ajili ya majadiliano.     


Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mhe. Vedasto ahoji mpango wa serikali wa kutengeneza barabara ya kiwango cha lami katika eneo la kihistoria la vita vya maji maji.     


Je kwa nini serikali inachukua muda mrefu kurekebisha mishahara ya walimu baada ya kupandishwa vyeo? Mhe. Angela kairuki afafanua.       


Haya hapa majibu ya serikali juu ya ushirikiano wa ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali katika ukaguzi wa taasisi za muungano.    

Mhe. Charles Mwijage atoa ufafanuzi juu ya mpango wa serikali kujenga viwanda katika mkoa wa Katavi na kutoa mafunzo ya ujasiliamli kwa vijana.

Mbunge wa viti maalum Mhe.Upendo Peneza aitaka serikali kutekeleza ahadi yake ya kupunguza misamaha ya kodi hadi asilimia 1 ya GDP.

MUME AMUUWA MKE WAKE PAMOJA NA MTOTO KWA KUWACHINJA NA KISU WILAYANI BAGAMOYO MKOA WA PWANI

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Frowin Mbale (26) ambaye ni mkazi wa kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kikatili ya  mke  pamoja na mtoto  wake kwa kuwachinja  shingoni na kisu kasha kuwatupa vichakani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushongi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kudai kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 10:30 jioni katika kijiji cha zinga  kata ya Dunda Wilayani Bagamoyo.

Kamanda Mushongi amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mwenzake  mmoja  aliyejulikana kwa jina la Rajabu Juma (20) na walifanikiwa kuwakamata juzi usiku majira ya saa 2:30 katika maeneo ya  kijiji cha zinga.

Pia Kamanda Mushongi amewataja marehemu hao kuwa ni Oliver Erasto (200 pamoja na mwanae Emmanuel Frowin (3) ambao miili yao ilikutwa imetupwa katika vichaka vya kaole kata ya dunda

 “Kutokana na tukio hili watuhumiwa wote kwa sasa tumewashikiria baada ya kutaka kutoroka ila kwa bahati nzuri wananchi waliweza kutoa taarifa mapema kwa vyombo vinavyohusika na ndipo walipofanikiwa kuwakamata,”aisema Kamanda Mushongi.

Aidha alifafafnua kuwa mtuhumiwa huyo akiwa na rafiki yake walimlaghai mkewe waongozane pamoja wakiwa na mototo wao kwenda kuangalia ujenzi wa nyumba yao unaoendelea katika eneo la kaole lakini walipofika huko ndipo walipoamua kufanya tukio la mauaji hayo ya kikatili.

Mushongi akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo amesema uchunguzi walioufanya umebaini mauji hayo yametokana  na wivu wa mapenzi, ambapo mume  huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mtu mwingine aliyejulikaana na kwa jina la moja la Hamza mkazi wa kawe.

Katika hatua nyingine Mushongi amelaani vikali tabia kama hiyo na kuwataka wazazi na walezi Mkoani Pwani kutovunja sheria kwa kujichukulia sheria mikononi kwani  kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu na sheri za nchi.

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI RUFAA ILIYOLETWA NA MWENDESHA MASHTAKA WA SERIKALI (DPP) KESI YA ALIYEKUWA KAMISHNA MKUU WA TRA NA WENZAKE.

 Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania ambaye pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare wamefika Mahakama kuu leo May 06 2016 ili kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.

Rufani hiyo imesikilizwa leo ambapo mahakama kuu imefuta pingamizi hilo kutokana na kuwa na dosari hivyo shauri linarudi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuendelea pale lilipokuwa limeishia na upande wa Jamhuri wanaweza kuandaa tena rufani na kufungua tena.

Serikali ilikuwa imekata Rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia washitakiwa shitaka  la kutakatisha pesa ambalo liliwafanya wanyimwe dhamana.

Baada ya shitaka hilo kufutwa, watuhumiwa sasa wanaweza kuomba dhamana.