ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 20, 2014

MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA WATAJA SABABU ZA KUVUTIWA NA KATIBA PENDEKEZWA

Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Dk. Ave Maria Semakafu akizungumza katika mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari. Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Dk. Ave Maria Semakafu akizungumza katika mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari.Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mtandao wa Wanawake na Katiba pamoja na TAMWA wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mtandao wa Wanawake na Katiba pamoja na TAMWA wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka akiwasilisha mada katika mkutano huo wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na TAMWA. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka akiwasilisha mada katika mkutano huo wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na TAMWA.Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji mada. Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji mada.Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji mada. Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji mada.

MTANDAO Wanawake na Katiba nchini pamoja na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) wamesema wanaunga mkono Katiba iliyopendekezwa na kujivunia hatua waliopiga katika kudai haki mbalimbali za mwanamke kwenye Katiba hiyo ukilinganisha na ile ya Mwaka 1977. Mtandao huo umetoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuzungumzia hatua ambayo mtandao huo unaoshirikisha zaidi ya hasasi 50 zinazopigania haki anuai katika jamii.

Akizungumza katika mkutano huo na wahariri wa habari, Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave Maria Semakafu alisema harakati za kutetea haki za binadamu na hususani za wanawake na watoto zilipata mwanya katika mchakato wa Katiba uliyomalizika jambo ambalo alisema ni hatua kubwa ya safari ya kumkomboa mwanamke. Dk. Maria Semakafu alisema kwa kuona mwanya nahatua waliopiga wanaharakati katika masuala hayo, kwa kupitia Mtandao wa Wanawake na Katiba pamoja na TAMWA wanaiunga mkono Katiba Pendekezwa kwa kile kuwa na utofauti mkubwa kimaboresho ukilinganisha na ile ya mwaka 2014.

 Alibainisha kuwa licha ya mapungufu kidogo yaliopo lakini umoja huo umefanikiwa. "..Mtandao unatambua kuwa kuna mapungufu yaliopo lakini kubwa zaidi ni kwamba ukilinganisha naKatiba ya Mwaka 1977, Katiba Pendekezwa imemtambua Mwanamke na imempa nafasi stahiki kushiriki katika kujenga, kulinda, kuilinda na kuitetea demokrasia inayozingatia haki za usawa," alisema Dk. Maria Semakafu.

Akitolea mfano alisema madai ya msingi 12 ambayo mtandao ulipaza sauti kutaka kuingizwa ni pamoja na haki za Wanawake kuainishwa kwenye Katiba Mpya, sheria Kandamizi kubatilishwa, kulindwa kwa utu wa mwanamke, utekelezwaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu haki za wanawake na haki sawa katika nafasi za uongozi.

Aliongeza kuwa mambo mengine ni haki za watoto wa kike, haki za kufikia, kutumia, kunufaika na kumiliki rasilimali, haki za uzazi salama, haki za wanawake wenye ulemavu, haki za kufikia na kufaidi huduma za msingi, kuwepo kwa tume ya usawa wa kijinsia na kuwa na mahakama ya familia katika katiba mpya. "...Kwa kiasi kikubwa katiba iliyopendekezwa imezingatia masuala mengi yaliodaiwa na mtandao.

Tunatambua juhudi kubwa zilizofanywa na wanawake na wanaume wote wa Bunge Maalum la Katiba, na kuwapongeza kwa yale yote waliyoyatetea kwa nguvu zote na hatimaye kuzingatiwa katika Katiba," alisema Dk. Maria Semakafu. Akizungumza awali kabla ya kumkaribisha Dk. Maria Semakafu, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka alivipongeza vyombo vya habari kwa kukubali kupaza sauti juu ya madai anuai ambayo yalitolewa na wanawake ili kuingizwa kwenye mchakato. "...Tunatambua pia mchango wa vyombo vya habari katika kujenga ufahamu kuhusu mchakato wa katiba na hasa kuhusu kwanini katiba mpya izingatie usawa wa kijinsia." alisema Msoka. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

BONDIA MAOKOLA AMDUNDA MKALAKALA KWA K,O YA RAUNDI YA 7 NA KUTETEA MKANDA WAKE

Mabondia Antony Peter kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamidu Mussa wakati wa mpambano wao Mussa alishinda kwa point mpambano huo. 
 Mabondia Ibrahimu Maokola kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Selemani Mkalakala wakati wa kugombania ubingwa wa Taifa unaotambuliwa na chama cha TPBC Maokola alishinda kwa k,o ya raundi ya saba. 
Bondia Selemani Mkalakala akiwa chini kwa konde zito alilotupiwa na Ibrahimu Maokola wakati wa mpasmbano wao wa ubingwa.
IBRAHIMU MAOKOLA


Mgani rasmi katika mpambano huo Joseph Vitalis kulia akimvisha mkanda wa ubingwa unaotambulika na chama cha TPBC bondia Ibrahimu Maokola baada ya kumdunda Seleman Mkalakala kwa k,o ya raundi ya 7 kushoto ni promota wa mpambano huo Shabani Adiosi Picha na  SUPER D BOXING NEWES

Friday, December 19, 2014

KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAZALISHA ZAIDI

Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana akiwakaribisha wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo nchini. Anayesalimiana naye ni Prof. Longinus Rutasitara (Naibu Katibu Mtendaji Uchumi Jumla). Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua mitambo ya kuzalishia sukari katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye kofia ya bluu) akionja sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Kushoto ni Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Nyuma ni shehena ya sukari iliyo tayari kuingia sokoni.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa mashine ya kumwagilia maji miwa ijulikanayo kwa kitaalamu kama Centre Pivot System.
Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana (Kulia) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine mpya zinazotumika kuvutia maji kwa ajili ya kumwagilia miwa.

Msimamizi Mkuu wa Mtambo wa maji wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mhandisi Abdul Adinani (Kulia) akitoa maelekezo ya namna ya maji yanavyochujwa kabla ya kutumika kwa ajili ya umwagiliaji wa miwa. Wanaomsikiliza ni Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mtaalamu wa uchongaji na usawazishaji wa ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa, Mhandisi Ali Khamis (Kulia) akitoa maelezo ya namna matrekta yanayotumia setalaiti (hayapo pichani) yanavyofanya kazi. Wanaomskiliza ni Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughilikia masuala ya Uchumi Jumla na  Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa kwa vitendo matrekta yanayotumia setalaiti kusawazisha shamba kwa ajili ya uzalishaji miwa.

KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAZALISHA ZAIDI
Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Kiwanja cha Sukari cha Kagera kimeanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika katika soko la sukari nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo la upatikanaji wa sukari Tanzania na nchi za jirani zinazotumia sukari kutoka kiwandani hapo.

Hayo yamewekwa wazi na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bw. Ashwin Rana, wakati alipokuwa akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

“Kwa sasa tumeweza kuongeza mauzo katika kanda kufikia tani 40,000, pamoja na kuongeza ununuzi kutoka kwa wakulima wa miwa wa nje zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka,” alisema.

Bw. Rana  aliongeza kuwa Kiwanda chake kimewekeza zaidi katika upanuzi wa eneo la shamba la miwa la umwagiliaji la hekta 3600 pamoja na kuwekeza zaidi katika teknolojia ya kisasa katika kilimo.

“Kampuni yetu imewekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na vifaa vya kisasa ikiwemo matrekta yanayotumia setalaiti katika ufanyaji kazi wake katika kuandaa mashamba,” aliongeza.

Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amekipongeza Kiwanda hicho kwa  kuwekeza kwenye uzalishaji wa kisasa wa miwa hali inayoongeza uzalishaji wa sukari kuwa mkubwa kiwandani hapo.

Bibi Mwanri ameongeza kuwa Kiwanda hicho kinastahili pongezi za kipekee kwa kuweza kuongeza ajira zaidi ya watu 6000 waliopo kiwandani.
“Kwa kweli munastahili sifa kwa kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania pamoja na kuuza umeme kwenye gridi ya Taifa,” alisema.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanda hicho, kwa sasa kinakabiliwa na na changamoto za uuzaji haramu wa sukari zinazoingia kimagendo nchini ambao umechangiwa kushindwa kwa kiwanda kuuza sukari ili kurudisha gharama za uzalishaji kutokana bei za sukari zinazoagiwa kutoka nje kuwa bei ya chini sana.

“Bei ya Sukari Duniani imeshuka sana kutokana na Nchi kubwa duniani kusaidia wakulima katika uzalishaji na pembejeo (subsidies) na hivyo sukari kuuzwa katika soko la dunia kwa bei ya chini (Dumping) na kufanya kuwa bei kuwa ndogo kuliko gharama halisi ya uzalishaji,” aliongeza.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni pamoja na kiwanda kushindwa kulipa mikopo iliyochokuwa benki kutokana na kuwepo sokoni kwa sukari ambayo ni ya magendo na bei ya chini hivyo kiwanda kushindwa kufikia malengo hata ya kiundeshaji na mipango mikakati.

Kiwanda cha Sukari cha Kagera kiko katika sehemu Kaskazini Magharibi ya Tanzania (karibu na mpaka wa Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na Serikali kwa sekta binafsi mwaka 2001. Malengo ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa masoko ya ndani na kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati na majengo ili kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.

KAJALA AKUNWA NA KUMWAGA MAHELA KWA WAIMBAJI WA SKYLIGHT BAND WANAOTOA BURUDANI KILA IJUMAA THAI VILLAGE

DSC_0028
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village huku akipewa sapoti na Digna Mbepera.
DSC_0030
Digna Mbepera na Bela Kombo wakimpa back up Aneth Kushaba AK47 kwenye show zao za kila Ijumaa ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0071
Majembe ya Skylight Band yakionyesha manjonjo yao jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.
DSC_0082
Aneth Kushaba na Sam Mapenzi wakiwapa raha mashabiki wao huku Digna Mbepera na Bella Kombo.
DSC_0092
Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakifanya yao jukwaani.
DSC_0147
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiserebuka mdogo mdogo.
DSC_0149
DSC_0158
Birthday girl nae hakubaki nyuma aliunga tela na kuburudika na Skylight Band.
DSC_0279
Msanii wa bongo movie Kajala akitembeza manoti ya wekundu wa msimbazi kwa waimbaji wa Skylight Band Ijumaa iliyopita alipokunwa na uimbaji wao.
DSC_0280
Kajala akizichomoa tu kwenye pochi lake.
DSC_0281
Joniko Flower akisubiria zamu yake.
DSC_0282
Joniko Flower akipokea manoti yake kutoka kwa Msanii wa bongo movie Kajala.
DSC_0283
Na kwa wale wasanii waliokuwa back stage pia walibahatika kujizolea manoti kutoka kwa Kajala.
DSC_0298
Wapenzi wa Skylight Band wakishuhudia tukio hilo.
DSC_0306
Twende kazi... na burudani iendeleeee..!
DSC_0326
Mashabiki nao wakajibu mapigo.
DSC_0340
Sam Mapenzi akitunzwa na shabiki wake.
DSC_0160
Sam Mapenzi akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band, Ijumaa iliyopita huku Joniko Flower na Sony Masamba wakimpa sapoti.
DSC_0164
Mashabiki wakiendelea kula raha..!
DSC_0170
Birthday girl na mabeste zake wakicheza mdogo mdogo.
DSC_0189
Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma...... mashabiki wakiondoka ma-style ya Skylight Band.
DSC_0115
Hashim Donode na Bela Kombo wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band huku wakipewa back up na Aneth Kushaba pamoja na Digna Mbepera.
DSC_0121
nakupenda pia pia aha...Nakupenda pia...You make me wanna say....Nakupenda pia pia ahaa.....Vijana wakiwa kwenye hisia kali jukwaani.
DSC_0198
Mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Joniko Flower akiwachezesha ligwaride la sebene majembe ya Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village .
DSC_0146
Mtaalamu wa kupiga kinanda Danny akifanya yake huku akipata Ukodak.
DSC_0044
Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki huku bendi hiyo ikimpa zawadi ya kumwimbia wimbo maalum wa sherehe hizo kumpongeza.
DSC_0045
Birthday girl akiendelea na zozezi la kulisha vipande vya cake shosti zake.
DSC_0048
DSC_0053
Birthday girl akiteta jambo na mchumba wake Lota Mollel.
DSC_0054
Mahaba niuweeeeeeee! Birthday girl akipata kiss kutoka kwa mchumba wake Lota Mollel.
DSC_0056
Birthday girl akiendelea kukata cake kwa ajili ya kuwalisha ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika naye.
DSC_0058
Birthday gilr na mchumba wake wakilishana cake kimahaba zaidi....!
DSC_0207
Emma Beyz na Danny Kinanda.
DSC_0223
Wadau wakipata Ukodak.
DSC_0356
Mdau Iddi Baka na Blogger King Kif wakishow love mbele ya camera yetu.
DSC_0226
Warembo wa ukweli na wenye viwango na ubora wanapatikana Skylight Band pekee hakunaga kwingine.
DSC_0239
DSC_0358
Nyomi la mashabiki wa Skylight Band likiwa limeshona Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village.