ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 9, 2011

TANZANIA INVESTMENT FORUM 2011

Wizara ya Nishati na Madini ikishirikiana na ubalozi wa Tanzania Uk wameandaa kongamano la uwekezaji nchini. Hii ni katika kutekeleza sera za economic diplomacy pamoja na kuvutia mitaji ya kigeni. Mh Ngeleja.
Mada nyingi zilizungumziwa kuhusu nafasi na sheria za uwekezaji Tanzania ambapo Waziri Ngeleja kama mgeni rasmi na mwakilishi wa taifa aliwaweka wazi wawekezaji jinsi ya sheria mpya zilizotungwa na kuwahakikishia kuwa Tanzania na Watanzania wako tayari kupokea wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza ilimradi waje na njia ambazo hazitinyinya Watanzania na taifa lao.
Dr Abdelhelm Meru Mkurugenzi mkuu wa EPZA akitoa mada iliyosisimua kuliko zote

Balozi Peter Kallaghe akitafakari.
Eneo lililovutia sana washiriki lilikuwa eneo la nishati na madini pamoja na viwanda. Waekezaji ambao tayari wako nyumbani Tanzania wametoa sifa kwamba kwa sasa Tanzania inawezekana kuwa ndio nchi pekee Afrika yenye mazingira sawia kwa wawekezaji toka nje.
Mh ngeleja akibadilishana mawazo na Naibu Balozi chabaka na Moja ya wanakongamano

Waziri Ngeleja akiwa na Wajumbe wa JumuiyaTanzanian Uk
Mwanataaluma bi Barbara Njau alifafanua kwa ushahidi wa vielelezo kuwa uchumi Watanzania siku zijazo utakuwa haraka sana na kuwa Watanzania na nchi yao kwa ujumla kwa ujumla wako kwenye nafasi nzuri kabisa kimaendeleo kama watatumia rasilimali walizonazo kwa umakini na uangalifu.
Chanzo:Urban Pulse Creative.

HAPPY BIRTHDAY PRECIOUSMINZA


Familia ya Mr &Mrs. Daniel Mathias tunamshukuru Mungu kwa kuwa ni mwema kwa kutupatia mtoto wetu na kumpa afya njema, siku ya leo ametimiza mwaka mmoja, wakati tunaazimisha miaka 50 ya uhuru pia hapa nyumbani tunasherekea birthday ya kuzaliwa binti yetu,kwa niaba ya familia yangu tunakupongeza sana kwa umri uliofikia, Mungu akuongoze na kukupa afya njema. Tunakupenda, tunakujali na tunakuthamini.
HAPPY BIRTHDAY OUR LOVELY DAUGHTER PRECIOUSMINZA

TAMASHA LA KUWAENZI WAIMBAJI WA RWANDA WALIOFARIKI KUFANYIKA MWANZA JUMAPILI HII

Kwaya ya The Ambasador of Christ kutoka Kigali nchini Rwanda imewasili jijini Mwanza kwaajili ya tamasha la Kuimba na kushukuru linalotegemewa kufanyika siku ya jumapili jijini hapa.

The Ambasador of Christ wamewasili salama salmini.

Mmoja kati ya majeruhi wa ajali kwaya ya The Ambasador akisalimiana na wanakwaya wawakilishi Mwanza.

Salaam salaam...!!

The Ambasador wakisalimiana na kwaya wenyeji jijini Mwanza.

Kwaya wageni kutoka nchini Rwanda ya The Ambasadors of Christ almaarufu kwa jina la 'Kwetu Pazuri' imeshuka jijini Mwanza kutuliza kiu ya burudani ya muziki wa Injili kupitia zinduzi za album zake tano kwa mpigo ikiwemo singo 'kwetu pazuri' iliyo watambulisha na kuvuma kote Afrika Mashariki.

Lengo kuu la Tamasha hilo ni kutoa shukurani kwa watanzania kwa moyo wao wa upendo waliouonyesha kwao kuwasaidia pindi walipopata ajali iliyotokea mwaka jana hapa nchini huko wilayani Kahama na kundi hilo kupoteza waimbaji wake watatu.

Sehemu ya waimbaji kwaya ya The Ambasador of Christ.

Usikose siku ya jumapili ya tarehe 11mwezi huu katika dimba la CCM Kirumba, jijini Mwanza ambapo tutakutanishwa kwenye kusanyiko kubwa la Tamasha la muziki wa Injili lililo chini ya usimamizi wa Maua Music Centre ambapo kwaya na makundi mbalimbali kukusanyika na kutoa burudani ya nyimbo za sifa.VIDEO - 'Kwetu pazuri'

Thursday, December 8, 2011

MIAKA 50 YA UHURU MIUNDOMBINU KIGOMA mmH!

Kuna maeneo hapa nchini yamesahaulika kabisa hasa linapokuja suala la miundombinu, Mkoa wa Kigoma ni moja ya mifano.. siyo reli tu ambayo sasa imekuwa manati kusafiriwa bali hata barabara ni cheche, hapa ni basi lilikwama wilayani Kasulu mkoani Kigoma karibu na mto Malagalasi.

Kutokana na ubovu wa barabara eti' lori likagota katikati ya barabara na kuzuia njia hivyo dereva wa basi la abiria toka kampuni ya Allys aliamua kupita pembezoni mwa barabara hali iliyosababisha basi nalo' kuzama kwenye tope na kukwama kwa muda mrefu.

Utekaji nao umechukuwa kasi kwa kiwango kikubwa hivyo kwa ajili ya usalama kuna vituo mbalimbali vya ulinzi ambavyo hutoa askari wake kulinda usalama wa abiria dhidi ya maharamia.

UHABA WA FEDHA WASABABISHA MWANZA KUIONDOA TIMU YA BASKETBALL WANAWAKE MICHUANO YA TAIFA CUP

Kutokana na uhaba wa fedha mkoa wa Mwanza umeiondoa timu yake ya Basketbal wanawake kwenye ushiriki wa michuano ya TAIFA CUP yanayotaraji kuanza kutimua vumbi jijini Dar kuanzia tarehe 11 - 17 December 2011. Walio katikati ni Ben Mwangi(L) na Georgios Paterantonakis(R) wakikabidhi msaada wa jezi kwa Timu ya Basketbal wanaume Mkoa wa Mwanza.
Hayo yamebainishwa naye Kaimu M/kiti wa chama cha basketball mkoa wa Mwanza Sosho Kizito, wakati akipokea msaada wa seti moja ya jezi toka kwa uongozi wa Klabu ya Burudani ya Rock Bottom ya jijini Mwanza.

Sosho amesema kuwa kutokana na timu hizo kuwa na mahitaji mbalimbali kama vile gharama za kambi, usafiri, chakula na malazi, huku kukiwa hakuna dalili yoyote kwa timu zake kupata mafungu ya uwezeshwaji Chama cha mpira wa kikapu Mkoa wa Mwanza kimeamua kupeleka timu moja tu kwenye mashindano hayo ili angalau kuweza kuepuka aibu ya kukosa kushiriki kabisa.


Ben Mwangi.
Kwa upande wake Consolting Manager wa Gold Crest Hotel Ben Mwangi amesema kuwa Club yake imetoa msaada huo mara baada ya kuona hali ngumu inayoikabili timu hiyo, hivyo anaamini kabisa kuwa msaada huo utatumika kutia hamasa kwa Wanamwanza kujitokeza katika kufanikisha ushiriki wa timu yao.

Taarifa zinasema kuwa bado milango ya kupokea ufadhili iko wazi kwa wale wote wenye mapenzi mema na mafanikio ya Mwanza katika michezo.

Ili timu ya mkoa wa Mwanza wanaume kwa wanawake ziweze kushiriki vyema kwenye mashindano hayo kiasi cha shilingi milioni 10 kinahitajika.

Timu ya wanaume inaundwa na wachezaji wafuatao:- John Sapa Pastory, Eric John, Paschal Imanyi Magabe, Innocent, Ernest Masanja (Bugando Worrious), Victor Zacharia, Amran sufian, Bundala Charles, Simon Chelu, Timothy Ngalula (Bugando Heat), Evordius Henga, Vincent Shinda, Enock Charles, Samwel Mujanja, Ally Issa (Butimba Spider), Ahmed Said, Amri Mohamed (Dolphins Pasiansi), Amon Semberya, Francis Shilinde, Wilson Masanja na Kiziti Sosho Bahati (Bugando Planet), wachezaji walio nje ya mkoa wa mwanza ni pamoja na Adam Jegame, Juma kissoky na Mohamed Ally Dibo. Timu hiyo ipo chini ya kocha Robert John Mwita.

Wednesday, December 7, 2011

MVUA NA MAPITO YETU.

Mazingira ya barabara ya Libert iliyo katikati ya jiji la Mwanza kwenye kona inayounga barabara hiyo na barabara ya Nterere.

Kamera yako kwa chini zaidi.

Maji yanatabia ya kufura na hata kufunika Kijidaraja hiki cha eneo la Uhuru kwenye mto Mirongo.

Taswira ya Mto Mirongo kupandisha kuelekea Lango lango.

Taka zilizojikita kwenye mfereji wa mto Mirongo ni kichocheo kikubwa cha mafuriko kwa wakazi wa maeneo ya karibu na mto.

SELEBRESHENI YA MY WIFE WANGU LAST NIGHT ..!!

Hepibazdei tu yuuuu... Hepibazdei tu yuuuu pppuuu kwa mshumaaa.

Cake.

Toka Star Tv Mc wa shughuli hiyo Fatma Shemweta.

ChiazZz!!

Mie na mtoto mzaliwa.

Richie One akikabidhisha zawadi kwa 'mtoto mzaliwa' huku akishuhudiwa na Mariam (kati).

Safu ya Frends' tukioni, Kutoka kushoto Ze-Man, mfanyabiashara maarufu Jack Fick, Dj Eddie Grand naye mfanyabiashara Sele Fish wa Mwanza.

Toka shoto ni Chepe, Richie One na wengineo wakimsikilizia JB Mkuu wa Majaji toka kundi la Mabaga Fresh ambapo walikuwa ni sehemu ya wageni waalikwa.

Tuesday, December 6, 2011

KABILA AONGOZA KWENYE UCHAGUZI DRC

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anaongoza kwa asilimia 46 ya kura zote, matokeo yanavyoonyesha.

Ikiwa zaidi ya robo tatu ya kura zikiwa zishahesabiwa mpinzani wake mkuu, Etienne Tshisekedi, ana aslimia 36, tume ya uchaguzi imesema.

Malori yaliyobeba polisi wa kuzuia ghasia wanapiga doria katika miji mikuu iwapo patatatokea vurugu, matokeo yote yakitarajiwa kutolewa siku ya Jumanne, huku kukiwa na madai ya kuwepo udanganyifu.

Takriban watu 3,000 walikimbia mji mkuu, Kinshasa, mwishoni mwa juma.

Uchaguzi wa Jumatatu iliyopita ni wa pili kufanyika tangu vita vya mwaka 1998-2003 kumalizika rasmi, ambapo takriban watu milioni nne walifariki dunia.

Makundi yenye silaha yanaendelea kufanya shughuli zao mashariki mwa nchi hiyo, yenye ukubwa wa theluthi mbili ya Ulaya ya Magharibi.

Mwandishi wa BBC Thomas Fessy mjini Kinshasa alisema wafuasi wa Bw Tshisekedi wanasisistiza kashinda na kuna uwezekano mkubwa hawatokubali kushindwa katika uchaguzi uliogubikwa na madai ya wizi wa kura.

Wakongo wapinga nje ya nchi
Hata hivyo, mkuu wa tume ya uchaguzi alisema siku ya mwisho iliyowekwa ya Jumanne kutangaza matokeo yote huenda isifikiwe.

Daniel Ngoy Mulunda, alisema, "Kwanza tutahakikisha makaratasi yote ya matokeo yamefika na tuna taarifa zote. Kama sivyo, hatutoweza kuwapa zaidi ya matokeo machache tu."

Afisa mwandamizi aliye karibu na Bw Kabila ameonya kuwa jeshi linaweza kusambazwa iwapo "hali itakuwa na vurugu sana ya kuwazidi polisi".

"Hatuwezi kuacha ghasia ziendelee," Kikaya Bin Karubi, balozi wa Kongo nchini Uingereza amenukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Polisi walirusha mabomu ya machozi kwa wafuasi wa upinzani kwenye mji mkuu siku ya Jumatatu, na milio ya risasi ilisikika kwenye jimbo la Kasai Magharibi, maeneo yote yakiwa ngome za upinzani, baada ya serikali kufunga kituo cha televisheni na redio, shirika la Reuters lilisema.


Kulikua na ghasia zaidi Jumatatu usiku nje ya nyumba ya Bw Tshisekedi mjini Kinshasa na kwenye makao makuu ya chama chake cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), mwandishi wetu alisema.

Wanaomwuunga mkono Bw Tshisekedi walifanya maandamano Afrika Kusini, na Ubelgiji, nchi iliyokuwa koloni lake, siku ya Jumatatu wakitaka atanagzwe kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

Waanadamanji hao walijaribu kuuvamia ubalozi wa Kongo mjini Pretoria, na kuwalazimu polisi kurusha mabomu ya kutoa machozi, shirika la AFP limeripoti.

Waandamanaji wamemshutumu rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kwa kusaidia kuandaa uchaguzi uliojaa udanganyifu huko Kongo na kutaka asijihusishe na masuala ya nchi hiyo.

HAPPY BIRTHDAY TO MY WIFE.....'

yOu aRE tHE 1 mY ONLY.
says albert g. sengo

Monday, December 5, 2011

HATIMAYE MR EBBO AZIKWA NYUMBANI KWAO

Askofu Thomas Laizer akiongoza sala katika safari ya mwisho ya Mr. Ebbo mjini Arusha.

Dada wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mr. Ebbo.

Familia ya Mr.Eboo.

Maelfu ya wananchi wamejitokeza kwa wingi leo mjini Arusha katika safari ya mwisho ya msanii wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava)Abeili Motika almaarufu kwa jina la Mr.Eboo ambaye amezikwa kwenye makaburi ya ukoo nyumbani kwa mzee Lotiko.

Wananchi hao ambao walikuwa na shauku ya kuuaga mwili wa marehemu huyo walijitokeza kwa wingi huku wakionekana kuwa na nyuso za majonzi, kila mmoja akihuzunika na wengi wakidai kuwa mwimbaji huyo wa bongo flava ameacha pigo kubwa kwa jamii ya kimasai na Taifa kwa ujumla kwani muziki wake sambamba na kuburudisha ulikuwa unaelimisha kwa kiwango kikubwa.

Akiongea katika mazishi hayo askofu mkuu wa jimbo la kaskazini Thomas Laizer alisema kuwa wao kama kanisa wameupokea msiba huo kwa masikitikio makubwa kwani msanii huyo alikuwa anaelimisha jamii kupitia nyimbo zake pia aliweza kuutangaza mkoa wa Arusha pamoja na thaminisha asili ya kabila la kimasai kupitia nyimbo zake.

ZAIDI YA AKINAMAMA 30 WAPEWA ELIMU YA USINDIKAJI SABUNI

Jumla ya akina mama wawakilishi kutoka vikundi mbalimbali wapatao 30 wa Kata ya Mbugani wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamenufaika na mafunzo ya ujasiliamali ya kutengeneza sabuni kwaajili ya kuanzisha viwanda vidogovidogo vitakavyo wasaidia kuongeza kipato na kujikwamua kiuchumi. Diwani wa viti maalum jimbo la Nyamagana Bi Neema Mafuma akitoa maelezo kwa washiriki namna ya kusindika sabuni.

Mafunzo hayo ya siku tatu yametolewa na wawezeshaji kutoka Mfuko wa Mbunge wa Wilaya ya Nyamagana mh. Ezekiel Wenje , chini ya usimamizi wa diwani wa viti maalum jimbo la Nyamagana kata ya Mahina bi. Neema Mafuma kwa lengo la kuwafundisha mbinu zaidi za ujasiliamali kwaajili ya kujipanua kwenye soko la uzalishaji mali hasa kwa bidhaa zinazohitajika sokoni.

Mpango huo umetoa elimu kwa akina mama hao ili kukabiliana na mfumuko wa bei unao likabili taifa hasa kwa bidhaa za matumizi ya kila siku ambapo nyingine zinaweza kutengenezwa na vikundi vidogo vidogo hivyo kupunguza makali ya maisha kwa kuuzwa kwa bei nafuu kwa jamii.





Sunday, December 4, 2011

ROCK BOTTOM YAZINDULIWA MWANZA

Consolting Manager wa Gold Crest Hotl inayomiliki Rock Bottom Club Mr. Ben Mwangi akikaribisha wadau wa burudani waliotinga shimoni humo kwa mara ya kwanza kula raha.

Mkurugenzi wa uendeshaji Gold Crest Mr. akitambulisha safu ya wafanyabiashara ambao ni wadau wa wa Rock Bottom Club iliyopo eneo la chini ndani ya Hoteli ya kitalii ya Gold Crest jijini Mwanza.

Dj Denis (L) na Mr. Joseph Mangapi, utambulishoni.

Miss Tz Genevive na warembo wenzake nao walikuwepo...

'Its ON'

Waweza ng'amua ni nani huyu?

Kutoka kulia Dj Maliz, Mc. Stoper, G, Meneja wa Burudani Villa Park Rama na Mashkaji.

Wadau namba moko wa blogu hii nao walichoma ndani.

Kutoka Left Philly Kabago toka Passion Fm, Nzali toka Afya Radio na 'flowers wake' wakipata Flash.

Dj Denis mtamboni akikisanukisha.

Friendz'''

"Umesema ya baridi?" mambo ya kaunta.

Yes we are!

Mfanyabiashara maarufu nchini Papaa King (With Light Blue Shirt) na wageni wake.

Mwonekano wa Rock Bottom.

You are most welcome to Rock Bottom Club Mwanza.