ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 9, 2023

"MUME ALIRUDI SAA SABA USIKU MWANAMKE AUA WATOTO WAKE WAWILI, KUMCHOMA VISU MUME WAKE MARA TATU KISHA KUJARIBU KUJIUA


Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja anadaiwa kuua watoto wake wawili, Kumchoma visu mume wake mara tatu kabla ya kujaribu kujiua eneo la Ongata Rongai.

Mwanamke huyo ambaye amelazwa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta na akiwa hali mahututi, anasemekana kumchoma visu  mume wake kufuatia ugomvi katika nyumba yao kwenye barabara ya Maasai Lodge.

Ugomvi huo ulielekea pabaya baada ya mwanamke huyo kumdunga mume wake mara tatu – kichwani,shingoni - baada yake kurejea nyumbani saa saba usiku, polisi wanasema.

Mwanamume huyo alinusurika kifo baada ya kukimbia kutoka kwa nyumba hiyo akibubujikwa na damu na kuomba msaada kutoka kwa majirani ambao walimkimbiza kwenye kituo cha afya kilicho karibu

Kwa mujibu wa polisi, mama huyo wa watoto wawili ambaye alibaki nyumbani, anasemekana kufunga milango kabla ya kuua wanawe wawili - miaka sita na miwili – kuwachoma visu.

Polisi wanasema kuwa alijaribu kujiua kwa kisu hicho lakini juhudi zake ziliambulia patupu.

 Alisalia na vidonda kwenye tumbo na kifua.

Polisi waliitwa eneo la tukio na kupeleka miili hiyo kwenye hifadhi ya maiti.

Wanandao hao wamelazwa hospitalini chini ya ulinzi mkali. Kamanda wa Polisi wa Kajiado Kaskazini Hussein Gura alisema kuwa polisi walipata silaha iliyoyumiwa kutekeleza mauaji hayo na wameanzisha uchunguzi.

MKOA WA PWANI WASHUSHA KIKOSI CHA WACHEZAJI 120 MICHUANO YA UMISETA TAIFA

 


Na Victor Masangu,Pwani 


Jumla ya wachezaji wapatao 120 wamechaguliwa kwa ajili ya kuunda kikosi cha timu ya Mkoa wa Pwani kitakachoshiriki katika mashindano ya Umoja wa michezo na sanaa kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya Taifa itakayoanza kutimua vumbi Juni 15 hadi 25 mwaka huu  mkoani Tabora.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta amesema kwamba wachezaji hao wamechaguliwa kutokana na uwezo na vipaji walivyonavyo  katika fani ya michezo mbali mbali.

Buleta alitasema hayo wakati wa halfa ya kutangzwa kwa kikosi cha wachezaji iliyofanyika katika viwanja vya shirikika la elimu Kibaha na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo walimu,Wanafunzi pamoja na wadau wa michezo.

Afisa michezo huyo alisema kwamba wachezaji hao wataingia kambini kwa kipindi cha muda wa siku tano kwa ajili ya kujiandaa na kujinoa vilivyo kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mashindano ya Kitaifa mkoani Tabora tarehe 14 mwezi huu.


"Tunashukuru tulikuwa na wachezaji wapatao 700 hapo awali lakini baada ya kufanya mchujo tumefanikiwa kupata wachezaji wapatao 120 ambao ndio watakaouwakilisha Mkoa wa Pwani katika mashindano ya  Taifa mkoani Tabora,"alisema Buleta.

Kadhalika aliongeza kuwa katika mashindano ya mwaka huu wachezaji wamejipanga vilivyo kuweza  kuibuka na ubingwa  wa Kitaifa kutoka na kujiandaa vizuri katika michezo mbali mbali watakayoshiriki.

Amebainisha michezo ambayo watashiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Netiboli,mpira wa miguu,kikapu,wavu,mpira wa mikono,riadha,fani za ndani,ngoma,kwaya sambamba na mziki wa kizazi kipya.

Katika hatua nyingine alimshukuru kwa dhati mdau wa michezo ambaye pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Mussa Mansoor kwa kuchangia vifaa mbali mbali vya michezo kwa timu ya Mkoa ili iweze kufanya vizuri.

Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mussa Mansoor alisema lengo lake kubwa ni kusaidia kukuza sekta ya michezo kuanzia ngazi za chini kwani michezo kwa sasa ni fursa za ajira.


Pia aliongeza kuwa ametoa vifaa mbali mbali vya michezo kwa lengo la kuwasaidia vijana waweze kupata fursa ya kuonyesha na kuibua vipaji vyao walivyonavyo.

 Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo amewataka wanamichezo ambao wamechaguliwa kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ili waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ngazi ya Taifa.

Thursday, June 8, 2023

'YANGA KESHO NI FUNGA KAZI'

 


𝗣𝗥𝗘𝗦𝗦💬


"Kesho ni mchezo wa mwisho wa ligi na ni sikukuu na siku kubwa kwetu ni siku ambayo tunaenda kusherekea mafanikio yetu kwa msimu huu na siku nzuri kuwa na mashabiki wetu"


"Tumekuwa na Safari nyingi na mechi nyingi zenye huzuni na zenye furaha kwetu. Uchovu bado ni mkubwa kutokana na ratiba hii ngumu lakini mara zote tumekuwa tayari kupambana"


"Mazingira ya michezo tunayocheza sasahivi naweza kusema ni mazingira ambayo hayapo kwenye ulimwengu wa mpira wa miguu lakini inabidi kujituma na ninaamini kesho tutakuwa na mchezo tofauti kutokana na mapumziko ya siku hizi mbili"


©Cedric Kaze 


#timuyawananchi 

#daimambelenyumamwiko 🟢🟡

Tuesday, June 6, 2023

VODACOM MWANZA YASHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUFANYA USAFI MAENEO SUGU NA KOROFI

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Siku ya Mazingira Duniani  inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi wa Juni, huleta pamoja mamilioni ya watu kote duniani na kuwashirikisha kwenye jitihada za kutunza na kuboresha Dunia. Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 ya Siku ya Mazingira Duniani. Siku ya Mazingira Duniani ni jukwaa la kimataifa la kuchochea mabadiliko chanya. Watu kutoka kwa zaidi ya nchi 150 hushiriki katika siku hii ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa, ambayo inasherehekea hatua za kushughulikia mazingira na uwezo wa serikali, mashirika ya biashara na watu binafsi kuunda ulimwengu endelevu zaidi. Hafla hii imekuwa likisimamiwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) tangu kuanzishwa kwake katika mwaka 1973. HISTORIA Siku ya Mazingira Duniani huangazia changamoto kuu za mazingira tunazokumbana nazo kwa sasa duniani. Siku hii ya kimataifa ya umoja wa mataifa imepanuka na kuwa jukwaa kuu la kimataifa la kuhamasisha kuhusu mazingira huku mamilioni ya watu wakishiriki ili kutunza mazingira. Kutoka jijini Mwanza Vodacom imeshiriki shughuli za usafi kwenye maeneo sugu na korofi katikati ya jiji la hilo

Monday, June 5, 2023

MAMA MARIAM MWINYI AZINDUA MSIMU WA NNE WA CRDB Bank MARATHON, SHILINGI BILIONI 1 KUKUSANYWA KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO

 

Benki ya CRDB kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation, leo imezindua rasmi msimu wa nne wa mbio za CRDB Bank Marathon ikwa na lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia kuboresha afya ya mama na mtoto nchini. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa mahojiano ya wanahabari na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mheshimiwa Mariam Mwinyi, yaliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.

Akizindua msimu wa nne wa CRDB Marathon 2023, Mama Mariam Mwinyi aliipongeza Benki ya CRDB kwa msaada wake usioyumba kwa afya ya mama na mtoto kupitia mbio hizo. Katika hotuba yake, alitoa wito kwa Watanzania kutoka nyanja mbalimbali, pamoja na wakimbiaji kutoka nje ya Tanzania, kujiandikisha kwa wingi katika mbio za CRDB Bank Marathon 2023.
Mama Mariam Mwinyi alisisitiza kuwa juhudi za pamoja za washirika na wakimbiaji ni muhimu katika kufikia lengo la kuchangisha fedha kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii ziilizoanishwa katika malengo ya mbio hizi ikiwamo afaya ya mama na mtoto. Aliongezea kuwa kumsaidia mama ni kusaidia jamii nzima na akawataka watu binafsi kuunga mkono jitihada hizo na kuchangia katika mbio hizo.

Katika mahojiano hayo Mama Mariam Mwinyi alizungumzia wito wake binafsi katika kusaidia jamii uliopelekea kuanzisha taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation yenye lengo la kuboresha maisha ya Wazanzibari kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia zaidi afya ya mama na mtoto. Alitoa shukurani zake kwa benki hiyo kwa kuchagua kujikita katika sekta ya afya Zanzibar, eneo ambalo linamgusa sana na ambapo pia ni mdau mkubwa.
“Ustawi wa jamii yetu unahitaji kila mmoja wetu kuwa na wito wa kujitoa katika masuala mbalimbali ya kijamii,” alisema Mama Mariam Mwinyi. “Kupitia Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation tunalenga kuinua maisha ya Wazanzibari kiuchumi na kijamii kwa kutilia mkazo zaidi afya ya mama na mtoto, naipongeza Benki ya CRDB na washirika wake kwa kuungana nasi katika kuleta mabadiliko katika sekta ya afya Zanzibar kupitia CRDB Bank Marathon."

Mheshimiwa alitumia fursa hiyo pia kutangaza kuwa Mheshimiwa Dk Hussein Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, amekubali kuwa Mgeni Rasmi katika msimu wa nnne wa CRDB Marathon 2023. Mbio hizo zimepangwa kufanyika Agosti 13 katika viwanja vya The Green maarufu kama viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya CRDB Bank Foundation, alieleza kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha msimu wa nne unakuwa wa kipekee na uzoefu uliobora zaidi kwa wakimbiaji na washiriki wote. Tully anibainisha kuwa mbio za mwaka huu wamejipanga kuhakikisha usalama zaidi kwa wakimbiaji, na kusema kuwa katika upande wa burudani pia wamejipanga vilivyo na kuhimiza washiriki kujisajili wao pamoja na familia zao kwani mbio hizo pia zimezingatia burudani kwa watoto.

Mwambapa alibainisha kuwa msimu wa nne wa CRDB Bank Marathon unalenga kufikia malengo matatu muhimu. Kwanza, ujenzi wa kituo cha afya cha mama na watoto katika visiwa vya Zanzibar ni kipaumbele kikubwa. Mpango huo unaoendana na malengo ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, inayoongozwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi, unaimarisha zaidi dhamira ya Benki ya CRDB katika kusaidia afya ya mama na mtoto nchini.
Pili, kupitia mbio hizo  Benki ya CRDB imejipanga kuendeleza jitihada za kusaidia matibabu ya akina mama walio na mimba hatarishi na kutatua changamoto ya fistula katika hospitali ya CCBRT. Mwambapa alisisitiza umuhimu wamsaada huo sio tu kutoa matibabu bali pia kuwawezesha akina mama hao kiuchumi ili kusaidia familia na jamii zao ipasavyo.

Aidha, CRDB Bank Marathon 2023 inalenga kuendeleza msaada wake kwa matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Mwambapa amesema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita bado ipo ya haja ya kuendelea kushughulikia changamoto hiyo ya kiafya inayowaathiri watoto nchini.
Tullo Mafuru, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Sanlam ambao ni washirika wakubwa wa CRDB Bank Marathon amesema taasisi yao inajivunia kuwa sehemu ya mbio hizo kwa misimu minne mfululizo. Tullo alisema Sanlam ikiwa kampuni inayoongoza katika sekta ya bima nchini afya ya wateja imekuwa kipaumbele kikibwa kwao, sababu ambayo imepelekea kusaidia kufanikisha malengo ya mbio hizo husasani katika kusaidia afya ya mama na mtoto.

Usajili wa mbio za CRDB Bank Marathon 2023 umefunguliwa rasmi kupitia tovuti rasmi ya mbio hizo www.crdbbankmarathon.com. Watanzania na washiriki wa kimataifa wanakaribishwa kujisajili na kushiriki mbio hizi za kizalendo zenye nia ya kuboresha ustawi wa jamii nchini ikiwamo afya ya mama na mtoto nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa, mwaka huu malengo ni kupata washiriki 7,000.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita mbio za CRDB Bank Marathon zimekua kwa kiasi kikubwa kwa, shukrani kwa washirika na wakimbiaji kutoka Tanzania na kutoka duniani kote. Kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, mbio hizo zimeweza kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 kusaidia changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

“Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kusaidia upasuaji wa watoto zaidi ya 300 wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, kusaidia ujenzi wa Kituo cha kisasa cha Mawasiliano katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, kusaidia matibabu ya akina mama walio katika mazingira hatarishi.
wajawazito katika Hospitali ya CCBRT,” alisema Mwambapa huku akiongeza kuwa fedha hizo pia zilisaidia uhifadhi wa mazingira kupitia kampeni ya Benki ya CRDB ya Pendezesha Tanzania, na Resi za Ngalawa wakati wa tamasha la Kizimkazi.

Mbio za CRDB Bank Marathon zimepata heshima kubwa kupelekea kupata usajili wa kimataifa kutoka kwa kutoka Chama cha Usajili na Upimaji wa Mbio za Kimataifa (AIMS) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa Riadha (World Athletics).


MBUNGE MAFIA AUNGANA NA RAIS SAMIA KUWAPA KONGOLE WACHEZAJI WA YANGA


 Na Victor Masangu,Pwani


Naibu Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh.Omary Kipanga amekipongeza kwa dhati kikosi cha timu ya yanga kwa kuweza kuingia fainali na kufanikiwa kushika nafasi ya pili katika kivumbi cha michuano ya kombe la shirikisho.


Kipanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mafia alisema kwamba licha ya timu ya yanga kutopata fursa ya kuutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu lakini wameweza kupambana kwa hali na mali katika fainali hizo na kufanikiwa kupata bao la ugenini dhidi ya timu ya USM Alger.

"Kimsingi mimi nikiwa kama naibu Waziri pia ni mdau mkubwa wa mambo ya michezo na kiukweli vijana wetu walikuwa wanaipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano hayo ya kombe la shirikisho hakika nawapongeza sana wachezaji pamoja na jopo zima la viongozi kwa kupambana vizuri.,"alibainisha Kipanga.

Aidha Naibu waziri huyo alitoa pongezi zake kwa Rais wa awamu ya sita Dkt.kwa kuendelea kuboresha sekta ya michezo ikiwa sambamba na kuwapa motisha zaidi wachezaji wa yanga hadi wameweza kupambana kuanzia mwanzo hadi kufikia katika hatua ya mwisho ya kucheza fainali.


"Yanga wameweza kutuheshimisha Kama Taifa katika michuano hiyo ya shirikisho na ndio maana na Mimi naungana na Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kuwapongeza kwa kazi nzuri ambayo wameifanya katika medani ya mchezo wa soka,"aliongeza Kipanga.

Katika hatua nyingine aliwataka wachezaji wasife moyo kwani hatua anbayo wameifikia ni heshima kubwa kwa Taifa na kwamba wajipange vizuri na kujiandaa katika michuano mingine ya kimataifa katika msimu ujao kwani pia michezo kwa sasa ni fursa za ajira.

Sunday, June 4, 2023

RAIS WA YANGA AMPA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MEDALI YAKE

 NA ALBERT G. SENGO

Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amesema kuwa atamkabidhi medali yake ya nafasi ya pili Kombe la Shirikisho barani Afrika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kutunukiwa jana usiku. #samiasuluhuhassan #yanga #yanganasimba