Thursday, January 13, 2011
HABARI
Halmashauri ya Jiji la Mwanza limetoa siku tano kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga na mama lishe kuondoka katika maeneo ya katikaki ya jiji kwa vile wamekuwa wakivunja sheria ndongo ya mazingira na usafi namba 312 ya mwaka 2010 na sheria ya Mipango miji na Ujenzi Mijini.Tamko hilo limetolewa juzi na Meya wa Jiji la Mwanza Bw.Josephat Manyerere (Diwani wa Kata ya Nyakato Wilayani Ilemela) kwamba Halmashauri ya Jiji kwa kushirikiana na wakuu wa vilaya za Nyamagana na Ilemela, kikosi cha polisi na vyombo vingine Dola vitaendesha oporesheni kabambe ya kuwaondoa wamachinga hao waliotapakaa kila kona ya jiji wakifanya biashara holela.
Tamko hilo linaonekana kukinzana na lile la ruksa ya kuendelea kufanya biashara toka kwa Mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje (Chadema) alilolitoa siku chache zilizopita wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kulaani tukio la polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa Chadema Arusha katika mkutano uliofanyika viwanja vya Ngoko’s vilivyopo Kata ya Milongo jijini mwanza.
Meya Manyerere amefafanua kuwa kutokana na hadhi ya Jiji la Mwanza na kusifika kushika nafasi ya kwanza ya usafi kwa miaka mitano mfululizo, likitembelewa na wageni mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ili kuilinda hadhi hiyo uongozi hawana budi kuwaondoa wamachinga na mama ntilie ambao wamekuwa kero na kusababisha kuziba barabara za watembea kwa miguu sambamba na kuacha uchafu kila maeneo.
Meya Amewataka wabunge na madiwani wa Jiji la Mwanza kuacha tabia ya kuwapotosha wananchi na badala yake wawe mstari wa mbele kuwaeleza ukweli na kuwaweka tayari kufuata taratibu na sheria zilizopo ili jiji la mwanza liendelee kuwa kioo katika suala la usafi na utunzaji mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza bw. Wilson Kabwe amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia kanuni na sheria kwa kuondoka maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara na kuelekea kwenye maeneo waliyopangiwa toka awali.
Maeneo yaliyotengwa kwaajili ya wafanyabiashara hao ni Kiloleli, Buzuruga, Kitangili, Nyegezi, Mlango mmoja, Mabatini na kwenye magulio katika maeneo ya Mkuyuni, Igombe, Sabasaba, Nyakato National, Kayenze, Kitangiri, Buhongwa, Mkolani, Igogo, Magomeni Kirumba na Igoma hii ni kwa kufuata siku kama ilivyopangwa na si vinginevyo.
Hi Sengo
hongera sana kwa kutufanya hata sisi tulio mbali na tanzania hususani mwanza kuelewa nini kinaendelea, nilikuwa na maombi yafuatayo nikiwa kama mfuatiliaji wa blog yako kila siku hata kama sicommet chochote lakini huwa lazima nifungue mara nyingi huwa najulikana kama bm.
1. kuna habari huwa unazianzisha lakini baadaye unatuacha kwenye mataa, mfano uliwahi kuandika bustani ya eden ndani ya mwanza lakini mpaka leo hatujui kama inaendelea kujengwa au mradi ulikuwa feki umekufa? uliwahi kusema machinga wataondolewa makoroboi kupisha kikwangua anga cjui ujenzi umeshaanza au vipi na ni hoteli, ofisi au shopping malls au vyote kwa mpigo na linamilikiwa na nani? ulisema ppf kuendelea kupendezesha mwanza kwa majengo, je kuna ujenzi wowote unaoendelea hapo mwanza ukiwa kama mradi wa ppf au nssf kwa sasa? ulitoa ramani ya soko mwanza je litaanza au limeshaanza kujengwa lini? rumours imevunjwa kunajengwa nini........ pamoja na mangine mengi. nafikiri ukiwa kama mwandishi wa habari unaweza hata kuongea na viongozi wa jiji wakakupa undani wa mambo yalivyo au ni wakali?
2. naweza kupata picha za chuo cha saut pamoja na maeneo mengine yanayojengwa kisasa mwanza mfano. kiseke, nyakato bwiru isamilo, nyegezi, capripoint, ilemela nk si lazima sana ila nikipata nitashukuru haina haraka sana hata kama itapita miezi kadhaa maana najua na wewe uko busy na hii ya blog unajitolea tu. hizo picha ni wewe mwenyewe uzpost au unitumie kwenye email kwangu vyovyote poa tu.
pole kwa maelezo mengi na ahsante kwa kazi unayofanya Mungu akubariki wewe na familia yako.
"Mama nanihiii.... njoo umwone mwanao!" ile kufika tu!..anatupa macho, mtoto kajikandika mafuta usoni, viganjani, kichwani hadi kwenye nguo, kope za macho zinafunguka kwa mahesabu kutokana na wingi wa mafuta. !TOBA!
Upande wa nyuma wa kichwa nako...tu..tu-tu! Nibaraa! Naivuta picha kama bidhaa hii ingekuwa zile za kemikali ingekuwaje!? Ndomana bidhaa nyingi zilizo na kemikali au hata zisizo na kemikali, lebo zasema weka mbali na watoto.
KAMCHEZO KAPYA.
Mara zote michezo inawajengea watoto tunu njema kama umakini, utulivu, furaha, urafiki, ubunifu, kuchemsha bongo, kutulia nyumbani na mengine mengi.
TUWAPE NAFASI WATOTO KUCHEZA NA TUWE WAANGALIFU.
Tuesday, January 11, 2011
BANGO
Shirikisho la Soka duniani FIFA, limemtangaza mchezaji wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi kuwa mchezaji bora wa soka wa mwaka 2010.Messi scored more than any other player in Europe's top five leagues in 2010, with 42 goals in 36 La Liga games, as well as finishing top scorer in the Champions League in 2010 with 12 goals in 12 games. He totalled 60 goals for the year for club and country.
"To be honest, I didn't expect to win today, but it was already great to be here next to my two mates," Messi said as he accepted the award. "To win it makes it even more special.
"I want to share with all of my friends, my family, all the Barcelonistas and the Argentinians."
Xavi added: "This award is a triumph for the cantera and for the philosophy of the club. It is a moment to savour. We shall see what happens next season.
"My life wouldn't have changed with this award, and I will continue to play like I normally have. The Ballon d'Or remains in Barcelona and there is no problem with this."
Real Madrid coach Jose Mourinho had earlier been named FIFA World Coach of the Year for Men's Football. Mourinho won Serie A, the Champions League and Coppa Italia with Inter Milan in the 2009-10 season and has made an impressive start to life at the Bernabeu. "I'm the best coach in the world for 2010 because I was the coach of the best team in the world in 2010," he said. "We were a family and we continue to be a family. I continue to be part of it from afar. "I want Inter to win every game except those against my team."
:::::::MPANGO MZIMA WA TUZO NI KAMA IFUATAVYO:-
FIFA Men's World Player of the Year: Lionel Messi
FIFA Women's World Player of the Year: Marta
FIFA World Coach of the Year for Men's Football: Jose Mourinho
FIFA World Coach of the Year for Women's Football: Silvia Neid
FIFA FIFPro World XI of 2010: Iker Casillas; Maicon, Gerard Pique, Lucio, Carles Puyol; Xavi, Wesley Sneijder, Andres Iniesta; Cristiano Ronaldo, David Villa, Lionel Messi
FIFA Puskas Award: Hamit Altintop
FIFA Fair Play Award: Haiti Under-17 women's team
FIFA Presidential Award: Archbishop Desmond Tutu