ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 21, 2022

RAO PWANI AKEMEA VITENDO VYA WAZAZI KUWABAGUA WALEMAVU KATIKA KUPATA ELIMU

 

Afisa elimu Mkoa wa Pwani Sara Mlaki akizungumza wakati wa kufunga rasmi mafunzo hayo ya siku Tano kwa walimu wa MJM .


 Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja wakionyesha kile walichofundishwa kwa muda wa siku tano.

Na Victor Masangu,Bagamoyo.

Afisa elimu Mkoa wa Pwani  Sara Mlaki amewataka wazazi na walezi kuachana na tabia ya kuwaficha na kuwafungia ndani watoto wao wenye ulemavu na badala yake watumie vituo vya utayari 36 ambavyo vimeanzishwa kwa ajili ya kwenda kuwaandikisha kupata elimu ya awali ili kuwaandaa na kujiunga na darasa la kwanza mwaka 2023.


Aidha afisa elimu huyo amewaasa walimu Jamiii Wasaidizi (MJM) ambao wemepatiwa mafunzo kwenda kuwaangalia kwa namna ya kipekee  watoto wenye ulemavu wasibaguliwe na kupatiwa haki yao ya msingi katika kupata elimu kama wengine.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kufunga Mafunzo ya siku Tano Kwa Walimu Jamiii Wasaidizi(MJM) wapatao 38 kutoka halmashauri zote tisa zilizopo katika Mkoa wa Pwani yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufundisha watoto  wenye umri wa kuanzia miaka 5 hadi 9.

Alisema kwamba watoto wote ambao ni walemavu na wamefikia umri wa kuanza shule ya awali  katika Mkoa wa Pwani wanapaswa kupatiwa haki zao zote za msingi kama ilivyokuwa kwa watoto wengine kupatiwa elimu  bila ya kuwa na ubaguzi wowote.

Pia alisema kwamba walimu hao waliohitumu mafunzo kwa kushirikiana na jamii husika wanatakiwa kuhakikisha wanaweka mipango mizuri katika vituo hivyo vya utayari ili kusiwe na upendeleo wowote na kila mtoto aweze kupata elimu hiyo ya awali.

"Walimu wa MJM ambao mmepatiwa mafunzo haya ni lazima mkayafanyie kazi kwa vitendo katika vituo vya utayari ambavyo vimeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto kupata elimu ya awali,"

 "Ninawaomba wazazi na walezi kuachana kabisa na vitendo vya kuwaficha na kuwafungia ndani  watoto ambao ni walemavu na badala yake wawape fursa ya kuwapeleka kupata elimu ,"alifafanua Mlaki

Kadhalika aliwakumbusha walimu hao waliohitumu mafunzo ya MJM kutekeleza majukumu yao ipasavyo kama walivyofundishwa na kwamba watoe ushirikiano wa kutosha kwa wazazi pamoja na jamii katika suala zima la kuwaandikisha watoto wao katika vituo hivyo vya utayari.

Naye mmoja wa  wawezeshaji katika  mafunzo akiwamo Hellen Kulwa alisema kuwa  kupitia Mafunzo waliyoyatoa Kwa MJM  hao Katika kuzingatia mahitaji maalumu ya wanafunzi Wenye Ulemavu Wana hakika watayafanyia kazi ipasavyo hasa Katika kutumia mbinu walizofundishwa.

Nao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo walisema kwamba watakwenda kuyatumia vizuri mafunzo ambayo wameyapata na kuahidi kuyafanyia kazi bila ubaguzi wowote yale yote ambayo yameelekezwa kwa kipindi cha muda wa siku tano.

 Mafunzo hayo ya siku Tano walimu wa MJM wameweza kufundishwa kutengeneza dhana  za Darasani  Ikiwamo mipira ,Vikombe Kwa kutumia karatasi Kuandika herufi kwa kutumia Mbegu na kuandaa Kona za Hesabu,Michezo ,Mazingira na Kona za Nyumbani.

Wednesday, October 19, 2022

UVCCM IRINGA VIJIJINI KUANZISHA MIRADI YA KIMAENDELEO KILA KATA

 

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini Elia Kidavile akizungumzia umuhimuwa vijanawa  chama chama  mapinduzi kujitengemea kiuchumi
 kaimu afisa Tarafa ya Pawaga Emmanuel Ngabuji aliwapongeza vijana  kumuunganga mkono Rais Samia

Na Fredy Mgunda, Iringa.


Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa Vijijini inakusudia kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ngazi za kata ili kujiimarisha kiuchumi na kuwa sehemu ya wachangia wakuu wa maendeleo

Akizungumza na vijana wa kata ya Ilolo Mpya,Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini Elia Kidavile, alisema kuwa jumuiya hiyo inapaswa kuwa na miradi yake kila kata ili kuondoa ombaomba ya kila mara kwa wadau walewale kila siku.

Kidavile alisema kuwa ndoto ya uongozi wake ni kuifanya jumuiya hiyo kuinuka kiuchumi kila kata na kuwa na miradi ambayo inaweza kutelezwa kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.

"Natamani jumuiya hii ya Iringa vijijini tuweze kujitegemea kwenye matukio mbalimbali ya chama na umoja huo ili kuondokana na ombaomba anayo kila mara tunaenda kwa wadau walile"alisema kidavile


Alisema kwa kuanza watapokea maoni ya vijana katika maeneo husika ili waweze kupendekeza aina ya miradin wanayoihitaji kulingana na jiografia ya maeneo hayo.

 
Lakini pia mwenyekiti huyo wa UVCCM Iringa vijijini aliwapongeza vijana wa kata ya Ilolo Mpya kwa kujitolea kuchangia kokoto mchanga na nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya sekondari William Lukuvi ikiwa ni sehemu kuunga utekelezwaji wa ilani ya CCM katika kuboresha elimu nchini 


Kwa upande wake kaimu afisa Tarafa ya Pawaga Emmanuel Ngabuji alisema kuwa Umoja wa Vijana Kata ya Ilolo mpya umewasilisha kwa vitendo shukrani zao kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo hayo

Ngabuji alisema kuwa zaidi ya Milioni mia sita (600,000,000) zimetolewa kwenye tarafa ya Pawaga kwa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali za sekondari ambapo imewapunguzia wananchi kuchangia kwenye ujenzi wa madarasa hayo.


Alisema kuwa vijana wanatakiwa kuipenda nchi yao na viongozi wanaowaongoza kwa kuwa wamekuwa wakionyesha njia ya kuleta maendeleo kwa wananchi wote.

Ngabuji alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa watanzania na kuomba watanzania waendelee kumuunga mkono.
 
Aloice Mkongo na anord masagari ni vijana wa jumuiya hiyo ya  UVCCM wilaya ya Iringa vijijini wameamua kujitolea kuchangia shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari William Lukuvi  kutoka na kazi nzuri ya kimaendeleo ambayo imekuwa unafanywa na Rais Samia.


Akitoa neno la shukrani kwa vijana hao waliojitolea katika  kuchangia ujenzi wa madarasa na Ofisi Kaimu mkuu wa shule ya Sekondari Wiliam lukuvi Abisai Ugi amesema hatua hiyo imesaidia pakubwa kufanikisha mradi huo


Ruwasa kibaha yawafuta machozi kwa maji safi na salama wananchi wa Kijiji cha kimara misale

 


Na Victor Masangu,Kibaha 


Wananchi wa Kijiji cha Kimara Misale kata ya Dutumi Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wameondokana na kero ya siku nyingi ya ukosefu wa 
 ya maji Safi na salama waliyokuwa nayo kwa muda mrefu baada ya kukamilika kwa mradi wa maji uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini  (RUWASA).

Wakazi hao kwa muda mrefu walikuwa wakitumia maji ya mto Ngerengere na Ruvu jambo ambalo wanaeleza kuwa lilikua kero kwao kutokana na baadhi yao kuliwa na mamba na wengine kupata ulemavu waliosababishiwa na mamba katika mto Ruvu.

Wakizungumza  muda mfupi baada ya kukabidhiwa mradi wa maji na RUWASA walisema awali walikuwa wakitembea umbali wa kilometa mbili hadi tano kufuata huduma hiyo.

Nasra Jafari ameshukuru Serikali kwa hatua hiyo ambayo inawezesha sasa kufanya kazi zao za nyumbani kwa wakati tofauti na zamani ambapo walikua wanachelewa kutekeleza majukumu yao kwa kukosa maji.

Naye Diha Kunga (70) amesema kitendo cha Serikali kuwafikishia maji katika kijiji chao kimewasaidia wazee ambao kwasasa wanapata maji karibu na wanapoishi bila malipo tofauti na awali ambapo walilazimika kutumia muda mwingi kwenda mtoni na kuomba msaada kwa ndugu.

"Hawa RUWASA wametufanyia jambo kubwa tangu kijiji hiki kuanzishwa mwaka huu ndio tunapatiwa maji tena sisi wazee tumepata msamaha kila siku tunachota bure hili ni jambo la faraja kwetu" amesema Diha.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi huo Meneja wa RUWASA Mhandisi Debora Kanyika  amesema  mradi huo umetekelezwa na Mkandarasi kampuni ya Buildall Constractors kwa gharama ya sh. 498,709,539.89 fedha za UVIKO-19  na kwamba wananchi 1,700 watanufaika.

Mhandisi Kanyika amesema mradi huo umehusisha ujenzi wa tanki la juu la lita 50,000 kwenye mnara wa mita 12, vituo nane vyenye vichotea maji viwili viwili, uchimbaji wa visima viwili katika vitongoji vya Kimara na Kigogo, nyumba ya mashine, ufungaji wa umeme wa jua na uchimbaji ulazaji wa mabomba na ufukiaji wa mtandao wa maji upatao kilomita 8.4.

Meneja huyo amesema kwasasa mradi huo umefikia asilimia 98 ambapo wananchi wanapata maji kwa usimamizi wa Jumuiya ya Watumia maji kijiji cha Kimara Misale wakati mkandarasi akiwa katika hatua za mwisho.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimara Misale Salum Mtego amesema upatikanaji wa mradi huo unawaondoa wananchi kwenye adha ya kutembea umbali mrefu na kuchota maji mto Ruvu.

Mtego amesema sasa wananchi wataondokana na adha ya kuliwa na mamba kwani wapo watu wanne ndani ya miaka zaidi ya miwili wameliwa na mamba wakiwa wanachota maji kwenye mto Ruvu.

Naye  Mwenyekiti wa bodi ya Maji  kimara Misale Sudi Omari amesema wametoa msamaha kwa wazee zaidi ya 40 kupata maji bure ndoo nne kila siku pamoja na walemavu wawili huku wananchi wengine wakipata huduma hiyo kwa sh 100 kwa ndoo tatu.  

KARIBU KWENYE MATEMBEZI YA MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI YA MATITI

 TAREHE 22 October 2022, saa 12 asubuhi tukutane Jengo la CCM Mkoa wa Mwanza.

Baada ya matembezi kutakuwa na huduma ya upimaji na uchunguzi wa saratani ya matiti bure katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Imepewa nguvu na Jembe Development Group, Jembe ni Jembe na Jembe Fm 93.7 #mwanza

WASAIDIZI JAMII WA MWALIMU 38 PWANI WAPATIWA MAFUNZO KABAMBE UFUNDISHAJI WATOTO WADOGO.


Na Victor MasanguBagamoyo 

Katika kukabiliana na changamoto iliyopo kwa baadhi ya watoto kusahaulika kupata fursa ya elimu ya awali Ofisi ya elimu Mkoa wa Pwani kupitia mradi wa shule bora imeamua kutoa mafunzo ya siku tano kwa wasaidizi jamii wa walimu (MJM) lengo ikiwa ni kuwaandaa kwenda kuwafundisha watoto wadogo katika vituo vya utayari 36 vilivyoanzishwa.

Hayo yamebainishwa na Afisa elimu vifaa na takwimu katika halmashauri ya Chalinze  Harord Chungu ambayo pia alikuwa mwezeshaji katika mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo na mbinu ya kufundisha ambayo yamefanyika katika shule ya Sekondari Bagamoyo na kuhudhuliwa na maafisa elimu mbali mbali.

Aidha alisema kwamba mafunzo hayo yameweza kuwashirikisha wasaidizi jamii wa mwalimu kutoka katika halmashauri zote za Mkoa wa Pwani na kwamba wataweza kujifunza mambo mbali mbali yanayohusiana na jinsi ya kuwafundisha watoto hao wadogo.

"Hawa washiriki wanapatiwa mafunzo ya jinsi ya kuwajengea uwezo zaidi namna ya kuwafundisha watoto hao wadogo ambao watakuwa katika vituo vya utayari kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo kwa njia ya vitabu na njia nyinginezo,"alisema 

Kwa upande wake Afisa elimu ya watu wazima Wilaya ya Kisarawe  Ester Senkoro alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga zaidi kwenda kuimarisha watoto hao kupata elimu kabla ya kujiunga na darasa la kwanza msimu wa mwaka 2023.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya MJM  akiwemo Joyce Thobias na Abdulkadilia  wamesema kwamba kupitia mpango huo wa shule bora utaweza kuwapa fursa ya   kwenda kuyafanyia kazi ya ufundishaji katika vituo hivyo vya utayari kwa lengo la kuboresha elimu kuanzia ngazi ya awali. 

 Afisa Elimu Wilaya ya Bagamoyo  Wema Kajigili pamoja na   Mkuu wa Shule ya Bagamoyo Sekondari Ombeni Ally wamesema kwamba mafunzo hayo ni umuhimu Sana na yataweza kuleta tija zaidi ya kuwasaidia watoto wadogo.

Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa na Ofisi ya elimu Mkoa wa Pwani kwa ufadhili wa uingereza Ukaid kupitia mradi wa shule bora nchini ili kuwawezesha watoto kupata elimu ya awali kabla ya kujiunga na darasa la kwanza mwaka 2023.

Mradi huo wa shule bora unatekelezwa katika mikoa tisa ambayo ni Simiyu, Tanga, Dodoma, Pwani, Mara, Katavi, Kigoma,Singida, pamoja na Mkoa wa Rukwa.

Tuesday, October 18, 2022

ST CLARE HOSPITAL MWANZA WAJA NA SULUHISHO TIBA YA MIONZI KUNUSURU UHAI KWA WANANCHI KANDA YA ZIWA.

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

"Umegusia suala la Tezi dume hapo, wengi wanaume ukileta mjadala wa changamoto hiyo, fikra zao huelekea kwenye kile kipimo cha kidole ambacho wengi hukikwepa wakisema si rafiki, unatoa rai gani kwa wanaume?" Ungana na kamera ya Jembe Fm kujua vipimo mbalimbali vinavyofanyika toka katika kitengo cha MIONZI Hospitali ya St. Clare iliyopo Nyahinji, mkolani jijini Mwanza.

Monday, October 17, 2022

MWANAUME ALIA BAADA YA MPENZIWE KUWA NA UHUSIANO NA MTU ALIYEDAI KUWA BINAMUYE.

Mwanamume huyo alisema walitengana na mpenzi wake baada ya miaka miwili.
Picha: @kinyuaWaMuthoni. Chanzo: Twitter 

Mwanamume aliyetambulika kama Kinyua Wa Muthoni, amewasisimua wanamitandao kwenye Twitter, baada ya uhusiano wa miaka miwili na mpenzi wake kufika kikomo ghafla. 

Kwenye misururu ya jumbe za Twitter zilizoonekana mwanamume huyo aliyevunjika moyo alisema alisitisha uhusiano baada ya kugundua mpenzi wake alikuwa akimchezea akili. 

Kwa mujibu wa Kinyua, mwanamke huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume aliyemfahamu na aliyetambulishwa kwake kama binamu wa mpenzi wake mnamo Januari. 

"Leo nimesitisha uhusiano na mpenzi wangu. Amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine kisiri. Tumechumbiana na msichana huyo kwa miaka miwili. Alinitambulisha kwa jamaa zake na nilikuwa nasubiria kujuana na wazazi wake, ila ninasikitika sasa," Kinyua aliandika. 

Kinyua alichukua fursa hiyo kumfurahisha mpenzi wake na "cousin" yake ndipo aweze kumkubali ila alipigwa na butwaa. Kinyua alishangaa wakati rafikiye alipomuitia kazi ya kuweka kamera za CCTV kwenye nyumba fulani eneo la Ruaka. 

Wakati alipoendelea kufanya kazi aliona gari la binamu ya mpenzi wake na kusema analijua. 

Kinyua alisema walielekezwa kwenye nyumba moja na keyateka wa jengo hilo, na alipofika mlangoni mwa nyumba ya 'cousin' ya mpenzi wake alikutana na viatu alivyokuwa amemnunulia.

 "Keateka alitunong'onezea kuwa, 'Nafikiri yuko na girlfriend yake'. Roho ilianza kuenda mbio kwa kuona viatu vilivyofanana na vile nilivyomnunulia. Nilipobisha yeye ndiye aliyefungua mlango ila alikuwa amelewa chakari kiasi kwamba hakuweza kunitambua. 

"Nilihisi ni kama nilikuwa nanyongwa, baada ya yeye kumuarifu mwanamume huyo kwamba 'babe una wageni'.

 Nilimuita kwa mutumia majina yake yote kama yalivyokuwa kwenye kitambulishoi ndipo akapata fahamu," Kinyua alisimulia. 

MIILI MIWILI YAPATIKANA IKINING'INIA KARIBU NA SHULE KAUNTI YA KISII.

 


Miili ya wanaume hao imepatikana ikining'inia karibu na shule. 

 Mikono ya wanaume hao wawili ilikuwa imefungwa pamoja kwa nyuma, kaptura zao kuteremshwa hadi katikati na walionekana kama waliopigwa kabla ya kunyongwa. 

Kamanda wa polisi wa Kisii Kusini Charles Machinji amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wawili hao ni Erick Ogega na Canvas Magembe wenye umri wa miaka 25 na 22 mtawalia.

 Kulingana na Machinji, kulikuwa na ishara tosha kuwa wawili hao waliuawa asubuhi ya mapema, Jumatatu, Oktoba 17.

RAIS SAMIA AMEONDOA MFUMO DUME, WANAWAKE MJIAMINI - WAZIRI MABULA.

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Dkt. Angeline Mabula amewataka wanawake kujiamini na kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka ili kujiimarisha kiuchumi badala ya kuendelea kulalamika kukwamishwa na mfumo dume.

Waziri Dkt. Mabula aliyasema hayo Oktoba 16, 2022 jijini Mwanza wakati akifungua kongamano la Jukwaa la Wanawake Viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kuongeza kuwa suala la mfumo dume nchini si changamoto kwani tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameliondoa.

“Hamtakiwi kuwa wanyonge tena, mjiamini kwani hakuna mfumo dume kwa sasa, wanawake tunaweza na hilo limedhihirishwa na Rais wetu Mhe. Rais Samia, ndiyo maana baada ya kuingia madarakani amepata tuzo mbalimbali kutokana na uchapaji kazi wake” alisisitiza Waziri Dkt. Mabula.

Aidha alisema Rais Samia ameendelea kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, akitolea mfano jijini Mwanza ambapo alisema soko kuu la Mwanza na Kirumba yatachochea fursa za kiuchumi kwa wananchi hususani wanawake ambao ni wengi masokoni.

Pia Dkt. Mabula aliwahimiza wanawake hao viongozi kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo za uzalishaji mali na kimafunzo na kisha kuwashirikisha wanawake wenzao kupitia vyama vya ushirika ili kusonga mbele kwa pamoja huku akiwahimiza kuwa tayari kuipokea sheria mpya ya bima ya afya kwa wote itakayorahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya.

“Mkawe mabalozi wazuri wa kuelimisha wenzenu kuhusu bima ya afya kwa wote kwani kama huna uhakika wa afya yako, hutaweza kunufaika na fursa mbalimbali za uzalishaji mali. Kumbuka mlio hapa ni viongozi, mmeaminiwa na waliowachagua hivyo usifurahie tu kuwa kiongozi, bali kipindi chako kikiisha uwe umeacha alama” alidokeza Waziri Dkt. Mabula.

Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Antony Mavunde alitumia kongamano hilo kuwahimiza wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali akisema kwa sasa mpango uliopo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 nchi ijitosheleze kwa uzalishaji wa sukari na mafuta ya kula hivyo angetamani kuona wanawake wanachangamka kwa kuanzisha viwanda vidogo.

Naye Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege alisema changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakumba wanawake ni mitaji ya uhakika kwa ajili ya kuanzisha miradi ya uzalishaji mali na hivyo kuwahimiza kutumia kongamano hilo kuweka mikakati ya pamoja ya kusonga mbele na kwamba Serikali kupitia Wizara ya Kilimo iko tayari kuwasimamia.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Viongozi wa SACCOS, Monica Komba alisema awali wanawake waliathiriwa na kutojiamini kutokana na mfumo dume uliokuwa ukiwanyima fursa mbalimbali za kiuchumi lakini kupitia jukwaa hilo kumekuwa na mabadiliko makubwa ambapo kwa sasa wanashiriki shughuli mbalimbali na hivyo kuondokana na utegemezi.

Kongamano hilo limeambatana na kauli mbiu ya siku ya kimataifa ya ushirika inayoadhimishwa Oktoba 17, 2022 isemayo “Imarisha uwezo wako wa kifedha kwa siku zijazo kupitia ushirika wa akiba na mikopo”.
Na George Binagi, Mwanza
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Dkt. Angeline Mabula akizungumza kwenye kongamano la jukwaa la wanawake viongozi wa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo (SACCOS) lililofanyika jijini Mwanza.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Dkt. Angeline Mabula akizungumza kwenye kongamano hilo. Waliokaa kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Antony Mavunde, Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SCCULT) Dkt. Cuthbert Msuya.
Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Antony Mavunde akitoa salamu zake kwenye kongamano hilo ambapo alisema bajeti ya Wizara hiyo imeongezeka kutoka Bilioni 294 kwa mwaka hadi kufikia Bilioni 954 mwaka 2022/23 na hivyo kutoa fursa kubwa ya kukuza sekta ya kilimo.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza,  Emil Kasagala akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mawanza, Adam Malima wakati wa kongamano hilo ambapo aliwahimiza wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo jijini Mwanza ikiwemo za kiutalii.
Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wanawake Viongozi wa SACCOS, Monica Komba akizungumza kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wanawake Viongozi wa SACCOS, Monica Komba. Waliokaa kutoka kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Dkt. Angeline Mabula, Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Antony Mavunde, Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SCCULT) Dkt. Cuthbert Msuya.
Wanawake viongozi wa SACCOS wakifuatilia kongamano hilo.
Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akitoa salamu kwenye kongamano hilo.
Picha ya pamoja.

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA "BENKI BORA TANZANIA" KUTOKA JARIDA LA GLOBAL FINANCE

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akipokea cheti cha tuzo ya "Benki Bora Tanzania" kutoka kwa Mwanzili na Mhariri Mtendaji wa Global Finance, Joseph Giarraputo, katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa Benki Bora Duniani iliyofanyika kwenye ukumbi wa ‘National Press Club’, Washington, nchini Marekeni, Oktoba 15, 2022. Hii ni mara ya nne mfulululizo kwa Benki ya CRDB kutunikiwa tuzo ya Benki Bora nchini na jarida hilo maarufu duniani la biashara na fedha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu kushoto), na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa wakionyesha cheti cha tuzo ya "Benki Bora Tanzania" walichokabidhiwa na Mwanzili na Mhariri Mtendaji wa Global Finance, Joseph Giarraputo (wapili kushoto) katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa Benki Bora Duniani iliyofanyika kwenye ukumbi wa The National Press Club, Washington, nchini Marekeni, Oktoba 15, 2022. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mali, Joseph Maji (wapili kulia), Meneja Mwanadamizi wa Programu Endelevu, Kenneth Kasigila (wakwanza kulia), na Masele Msita, Meneja Biashara na Mahusiano ya Kimkakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifuatia utoaji wa tuzo kwa Benki Bora Duniani uliyofanyika kwenye ukumbi wa The National Press Club, Washington, nchini Marekeni, Oktoba 15, 2022, ambapo kwa mara ya nne mfulululizo sasa Benki ya CRDB imekuwa ikitunikiwa tuzo ya Benki Bora nchini na jarida hilo maarufu duniani la biashara na fedha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kakatiki) akiwa pamoja na Meneja Biashara na Mahusiano ya Kimkakati wa Benki hiyo, Masele Msita wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa Benki Bora Duniani uliyofanyika kwenye ukumbi wa The National Press Club, Washington, nchini Marekeni, Oktoba 15, 2022, ambapo kwa mara ya nne mfulululizo sasa Benki ya CRDB imekuwa ikitunikiwa tuzo ya Benki Bora nchini na jarida hilo maarufu duniani la biashara na fedha.

 ==========   ========   =========

Washington DC, Marekani - Benki ya CRDB imetunikiwa  tuzo ya Benki Bora ya Tanzania kwa mwaka wa nne mfululizo, ikidhihirisha namna ambavyo benki hiyo imekuwa kiongozi katika huduma bora na utendaji sekta ya fedha nchini. Tuzo hiyo imetolewa na jarida maarufu duniani la biashara na fedha la Global Finance lenye makao yake mjini New York, Marekani.

Benki ya CRDB ilikabidhiwa tuzo hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari, Washighton, Marekani ambayo ilihudhuriwa na viongozi zaidi ya 900 wa sekta ya fedha kutoka kote ulimwenguni.

Tuzo hiyo inatambua ukuaji endelevu wa Benki ya CRDB, ambao umekuwa ukinufaisha wateja, wawekezaji na uchumi wa nchi kwa ujumla. Tuzo hiyo pia inatambua mafanikio ya mkakati wa benki hiyo wa mabadiliko ya kidijitali, ambao umechochea ubunifu wa huduma za kidijitali hivyo kuongeza ujumuishaji wa kifedha nchini.

"Tunajivunia kutambuliwa kama Benki Bora ya Tanzania na Global Finance kwa mara nyingine tena. Hii inaonyesha kwamba tuko kwenye njia sahihi ya kutoa huduma bora kwa wateja wetu na kujenga thamani kwa wanahisa wetu sambamba na kuleta mabadiliko katika sekta ya fedha nchini," alisema Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.

Kwa miaka minne iliyopita, Benki ya CRDB imekuwa ikiboresha mifumo yake ya utoaji huduma ili kuwapa wateja huduma za kiwango cha kimataifa. Benki hiyo pia imekuwa ikupanua wigo wa bidhaa zake, na kuimarisha mtandao wake kwa kuwekeza kwenye njia za kidijitali za utoaji huduma.

Nsekela aliwashukuru wateja, wanahisa na wawekezaji wa Benki hiyo kwa mafanikio ya tuzo hiyo. Kwa sasa Benki ya CRDB ndiyo benki kubwa zaidi nchini Tanzania, ikiwa na mali ya zaidi ya TZS 10 Trilioni. Benki pia inaongoza kwa amana za wateja (Shilingi Trilioni 7) na mikopo ya awali (Shilingi Trilioni 6).

Jopo la majaji wa tuzo za Global Finance limeichagua Benki ya CRDB mahususi kwa ajili ya mafanikio yake katika viashiria vyote vya biashara. “Katika kipindi cha mwaka jana, tumeshuhudia Benki ya CRDB ikifanya maboresho makubwa katika huduma kwa wateja, hususan huduma za kidijitali,” alisema Joseph Giarraputo, Mwanzilishi na Mhariri Mtendaji wa Global Finance.

Giarraputo pia alitaja kuwa tuzo hiyo inatambua kazi ya kupongezwa iliyofanywa na Benki ya CRDB katika kusaidia sekta za biashara na wajasiriamali wadogo na wa kati katika kuondokana na changamoto zilizosababishwa na janga la UVIKO-19. "Juhudi zote hizi zimeendelea kuimarisha benki hii, na kupelekea utendaji mzuri," aliongeza.

Benki ya CRDB imeendelea kupata matokeo mazuri ya kifedha mwaka hadi mwaka, katika mwaka wa fedha uliopita ilipata faida ya Shilingi bilioni 268.2, sawa na ongezeko la asilimia 62.3 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 165.2 mwaka 2020. Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2022, ilipata faida Shilingi bilioni 174 bilioni, kulinganisha na Shilingi bilioni 88 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Nsekela amesema matokeo mazuri ya kifedha ya Benki ya CRDB kwa kiasi kikubwa yanachangaiwa na mazingira mazuri ya biashara nchini. Aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Hii ni tuzo ya pili ya Benki ya CRDB ya 'Benki Bora Tanzania' mwaka huu, kufuatia tuzo kama hiyo kutoka kwa jarida maarufu la fedha na uchumi la Uingereza la Euromoney mwezi Julai.

 

WAZIRI MKUU AZINDUA JENGO LA KITENGO CHA HUDUMA YA MACHO BUGANDO.

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua jengo la Idara ya Macho katika Hospitali ya Kanda Bugando ambalo limekuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za kibingwa za macho.

“Ujenzi wa mradi huu unakwenda kupunguza usumbufu kwa wagonjwa waliokuwa wakisafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 1,000 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda hospitali ya KCMC au Muhimbili kwa ajili ya kupata huduma bora za macho.”
Waziri Mkuu amezindua jengo hilo jana Jumapili, Oktoba 16, 2022 katika Hospitali ya Kanda Bugando jijini Mwanza akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu kukagua shughuli za maendeleo zinazotekeleza na Serikali mkoani hapa. Mradi huo umegharimu shilingi bilioni 3.7. Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua mradi huo unaolenga Kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma bora za kibingwa na zinazokidhi matakwa na matarajio ya wagonjwa, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini likiwemo Kanisa Katoliki katika kuboresha huduma za jamii yakiwemo matibabu.






Mheshimiwa Majaliwa amesema katika Hospitali ya Bugando Serikali imekuwa na ubia na kanisa kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kugharamia mishahara kwa watumishi 1,191 sawa na asilimia 66 ya watumishi wote wa hospitali ambapo kila mwezi jumla ya shilingi bilioni 1.7 hulipwa na Serikali.

WADAU WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 20 SHULE YA SEKONDARI LUPILA.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa Mahafali ya 31 ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Lupila.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akikata utepe kuashiria kufungua rasmi kwa Mahafali ya 31 ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Lupila.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wenzake wa maendeleo Kata ya Lupila wakati wa Mahafali ya 31 ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Lupila.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga  (wa pili kulia) alipotembelea bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Lupila.
Mzee Yohana Sanga ambaye ni mdau wa maendeleo Lupila na mwanzilishi wa Shule ya Sekondari Lupila (kushoto) akikabidhi kwa niaba ya wadau wa maendeleo kiasi cha shilingi 2,600,000 kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Abkasa Ngwale ikiwa ni motisha kwa walimu.


 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Lupila, Yohana Madope (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi 50,000 kwa mhitimu wa kidato cha sita aliyepata daraja la kwanza (1.7).

Wadau wachangia zaidi ya Milioni 20 Shule ya Sekondari Lupila

Na Mohamed Saif

Wazawa na Wadau wa maendeleo ya Kata ya Lupila Wilayani Makete Mkoani Njombe wamechangia kiasi cha shilingi milioni 20.8 kwa ajili ya maendeleo ya Shule ya Sekondari ya Lupila.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 31 ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Lupila amebainisha hayo Oktoba 15, 2022 kwa niaba ya wadau hao.

“Wadau kwa umoja wetu, tumechanga kiasi cha shilingi milioni 20,810,000 na tumezitolea maelekezo makhsusi fedha hizi ambapo kiasi cha shilingi 17,700,000 kipelekwe kwenye kuboresha miundombinu ya shule ikiwa ni pamoja na vitanda na madawati kwa ajili ya wanafunzi wetu,” alisema Mhandisi Sanga.

Aidha, kiasi cha fedha kilichobaki kilikabidhiwa kwa wanafunzi waliofanya vizuri (wahitimu kidato cha sita waliopata daraja la kwanza kwa alama saba hadi tisa) sambamba na walimu ikiwa ni motisha kwa kazi nzuri waliyoifanya. 

Amesema wanafanya hayo ili kuwapunguzia mzigo wazazi lakini pia kusaidiana na Serikali hasa ikizingatiwa kuwa Serikali inalo jukumu hilo kwa nchi nzima.

“Tunaamini Serikali hili ni jukumu lake la msingi na inafanya hivi nchi nzima lakini pale ambapo wadau tunaona tunaweza kuchangia basi hapa ndipo nasi tunapoweka mkono wetu,” alifafanua Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga alipongeza jitihada za walimu na wanafunzi wa Sekondari ya Lupila ambazo alisema zinawahamasisha wadau kuendelea kuichangia shule hiyo ili ifike mbali zaidi.

Amesema matokeo ya Kidato cha Sita yamekuwa ya kivutio cha kipekee hasa ikizingatiwa kuwa licha ya shule hiyo kutoa watahiniwa wa kidato cha sita kwa mara ya kwanza hapo mwaka jana, lakini walifanikiwa kuongoza kimkoa kwa kushika nafasi ya kwanza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Lupila, Yohana Madope ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki wa mahafali hayo alipongeza jitihada binafsi za Mhandisi Anthony Sanga katika kushirikiana na wananchi wake kwenye shughuli za kimaendeleo na kijamii.

“Mhandisi Sanga wananchi wa Lupila tunakushukuru sana, matendo yako ni ya kipekee haijawahi kutokea, tunaendelea kukuombea unafanya mambo makubwa nyumbani kwako usichoke, ninakuomba wewe na wadau wengine muendelee kutusaidia kuijenga Lupila yetu na tunawasihi muendelee kuhamasisha na wengine,” alisema Madope

Naye Diwani wa Kata ya Lupila, Ernesta Lwila alipongeza jitihada za wadau hao kwenye kuinua suala la elimu hata hivyo aliwasihi wajikite pia kwenye masuala mengine ili kuinua uchumi wa Lupila.

Akizungumzia kwa ujumla uratibu, dhamira na umoja wa wadau hao, Katibu wa wadau Aliten Ntullo ambaye pia ni mwalimu wa Sekondari ya Njombe alisema wameunda kundi sogozi ambalo linashirikisha wazawa wa Lupila waliopo nje na ndani lengo likiwa ni kujadili na kuhamasisha maendeleo.