ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 22, 2020

MONGELLA ACHOMEKEA HILI WAKATI MKAPA AKITAMBULISHA KITABU CHAKE MWANZA..



 Hiki ndicho alichozungumza Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kushoto) wakati Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa akitambulisha kitabu chake "My Life, My Purpose" ndani ya jiji hilo.
 Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kushoto) kitabu cha "My Life, My Purpose".

















MY LIFE MY PURPOSE.


SEHEMU KALI JIJINI MWANZA VICTORIA PALACE MOTEL


About Victoria Palace Motel Located in Capri-point, Mwanza, with superb views of Lake Victoria, Victoria Palace Motel combines contemporary elegance and warm African hospitality. Victoria Palace Motel offers affordable accommodation in Mwanza.. The fact that it is located only 10kms from the Airport, 1 kms from the city centre, makes Victoria Palace Motel one of the most preferred hotels by both corporate and leisure travellers. The hotel offers attractive rates for over night accommodation to leisure travellers before or after safaris to the famous Serengeti National Park, Ngorongoro Crater, Lake Manyara, Sealous Game Reserve and Zanzibar.All rooms are built around beautiful, All rooms are tastefully decorated and are equipped with all modern amenities.

Thursday, February 20, 2020

#LIVE: MAADHIMISHO YA SIKU YA MADKTARI TANZANIA . JNICC JIJINI DSM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 20, Febuari, 2020 anazungumza na Madaktari pamoja na watumishi wa Sekta ya Afya katika Hafla Maadhimisho ya Siku ya Madaktari Nchini inayofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dsm.

Wednesday, February 19, 2020

MWANZA LUTHERAN SECONDARY SCHOOL YAJA NA MKAKATI WA KUANDAA VIONGOZI


ILI kujikwamua toka lindi la ujinga na umasikini wazazi mkoani Mwanza wameaswa kuwapeleka vijana wao shule sanjari na kuwasimamia kikamiifu kupata elimu bora ya kuwafaa katika kuzikabili changamoto zao na taifa kwa ujumla. Akizungumza kwa kutumia mifano na hadithi mbalimbali katika hafla ya ufunguzi wa Shule mpya ya Mwanza Lutheran Secondary School (MLSS) iliyofanyika hii leo Februari 18, 2020, na kuhudhuriwa na wananchi, wanafunzi, waumini, viongozi wa Serikali na Dini, Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Andrew Gulle amesema Mtu ambaye hategemei kuelekezwa na kufundishwa hupotea, utii wa maelekezo mema , utii wa walimu, wachungaji, wainjilisti, wazazi, viongozi na kadhalika ni jambo muhimu. Kisha akaongeza "Kijana akikaidi na kuyapuuza maagizo ya wakubwa zake waliomtangulia mtu huyo hawezi kupata baraka, kwani elimu ndani yake kuna unyenyekevu na kusikiliza mafundisho ambapo hapo ndipo tunachota hekima na tisipo kubali kusikiliza na kujifunza tutabaki kama tulivyokuwa juzi yaani masikini" . Shule ya MLSS inayomilikiwa na Kanisa la KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria iko Mtaa wa Majengo Mapya katika Kata ya Mabatini jijini Mwanza ambapo makumi ya wanafunzi tayari wamesajiliwa kuanza masomo yao katika Shule hiyo.

Tuesday, February 18, 2020

Monday, February 17, 2020

#LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, 2020 anazindua Jengo la Manispaa ya Kigamboni na Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni katika Eneo la Gezaulole Kigamboni Jijini Dsm.

Sunday, February 16, 2020

Kili Canvas yawa kivutio kwa wakimbiaji Dar


Dar es Salaam Februari 15, 2020: Kili Canvas iliyozinduliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager hivi karibuni jijini Dar es Salaam, imekuwa kivutio kikubwa kwa wakimbiaji mbalimbali wa jiji hilo.

Canvas hiyo ina lengo la kuhamasisha wakimbiaji wa vitongoji tofauti vya Jiji la Dar es Salaam na Mji wa Moshi katika kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi, 2020 mkoani Kilimanjaro

Kili Canvas ni picha maalumu iliyochorwa kwa ukubwa ambapo mkimbiaji yeyote akipita karibu yake anapigwa picha na picha hiyo yenye muunganisho wa teknolojia ya kisasa baadaye kumtumia picha hiyo kupitia simu yake ya mkononi. Hata hivyo mkimbiaji anatakiwa kujisajili na kupewa chip maalumu ambayo anatakiwa kuwanayo kwa maelekezo ya wahusika.

Mtangazaji wa Wasafi Redio Fm, Maulid Kitenge mmoja wa wakimbiaji wa Wasafi Jogging Club ambye amevutiwa na Canvas hiyo jijini Dar es Salaam, alisema, “Hii ni teknolojia nzuri ambayo inakupatia picha yako tena nzuri pasipo kupata taabu yoyote. 

Binafsi napendelea sana kufanya mazoezi nikishirikiana na Wasafi Jogging kwani mazoezi ni afya lakini mazoezi humfanya mtu kuonekana mpya kila wakati na zaidi mazoezi ni sehemu ya michezo ambao umenifanya kufahamiana na marafiki wengi.
Kitenge alisema mwaka jana nilikimbia Kili Marathoni lanini mwaka huu pia lazima nishiriki pia kwa kuvuna record yangu yam waka jana.Si mimi tu bali wanafamilia wote wa Wasafi Jogging tunatarajia kushiriki Kili Marathon 2020.

Wito kwako wewe Mtanzania ambapo mashindano haya hufanyika Nchini kwako kila mwako na haushiriki,”Tuungane 2020 kama Watanzania tukashiriki kilele cha mbio za Kili Marathon pale Mkoani Kilimanjaro kwani ni takribani nchi 52 Duniani hushiriki mashindano hayo.

Nae Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli alisema kuwa, mtu yeyote anayependa mchezo wa kukimbia anaweza kupata fursa ya kupita katika Canvas hiyo na kufaidi teknolojia hiyo ya kisasa ya kupigwa picha na kasha kutumiwa katika simu yake.

“Hii ni fursa kwa kila mtu anayependelea mchezo wa kukimbia, na si lazima awe ni mshiriki wa Kili Marathon, ndiyo maana tukasema yeyote anaweza kujisajili na kupata chip hiyo kwa kipindi hiki cha kuhamasishana kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon,” alisema Kikuli. 

Kwa mujibu wa Kikuli, Canvas hiyo ilikuwa katika Ufukwe wa Coco Beach Masaki, lakini kwa siku tatu yaani Februari 17-19,2020 itakuwa Uwanja wanje wa Taifa Temeke na Februari 20 – 21,2020 Canvas itakuwa Viwanja vya Leaders na baadae kuelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 “Ili uweze kupigwa picha na kutumiwa kwenye simu yako kwa wale wakimbiaji ni lazima ujisajili na kupewa Chip maalumu ambayo utaelekezwa wapi pa kuiweka wakati unakimbia. Mara tu utakapopita karibu na Canvas kamera zetu zitakutambua na kukupiga picha kwa teknolojia maalumu na kutumiwa papo hapo kwenye simu yako” Kikuli alisema

Kwa mujibu wa Meneja huyo, usajili bado unaendelea kwaajili ya kujipatia Chip unafanyika Mlimani City na Uwanja wa Taifa Temeke pale njea jijini Dar es Salaam.

MASAUNI ATEMBELEA KIWANDA CHA VIATU CHA KARANGA MKOANI KILIMANJARO,AWATAKA KUONGEZA UFANISI KATIKA BIDHAA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia kiatu kinachotengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga mkoani Kilimanjaro,mwishoni mwa wiki  wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa shughuli zinazofanywa kiwandani hapo ambapo aliwataka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa hizo za ngozi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya viwanda nchini.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia kiatu kinachotengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga mkoani Kilimanjaro,mwishoni mwa wiki wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa shughuli zinazofanywa kiwandani hapo ambapo aliwataka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa hizo za ngozi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya viwanda nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea  kiatu kinachotengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga mkoani Kilimanjaro,mwishoni mwa wiki wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa shughuli zinazofanywa kiwandani hapo ambapo aliwataka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa hizo za ngozi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya viwanda nchini