ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 19, 2020

MWANZA LUTHERAN SECONDARY SCHOOL YAJA NA MKAKATI WA KUANDAA VIONGOZI


ILI kujikwamua toka lindi la ujinga na umasikini wazazi mkoani Mwanza wameaswa kuwapeleka vijana wao shule sanjari na kuwasimamia kikamiifu kupata elimu bora ya kuwafaa katika kuzikabili changamoto zao na taifa kwa ujumla. Akizungumza kwa kutumia mifano na hadithi mbalimbali katika hafla ya ufunguzi wa Shule mpya ya Mwanza Lutheran Secondary School (MLSS) iliyofanyika hii leo Februari 18, 2020, na kuhudhuriwa na wananchi, wanafunzi, waumini, viongozi wa Serikali na Dini, Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Andrew Gulle amesema Mtu ambaye hategemei kuelekezwa na kufundishwa hupotea, utii wa maelekezo mema , utii wa walimu, wachungaji, wainjilisti, wazazi, viongozi na kadhalika ni jambo muhimu. Kisha akaongeza "Kijana akikaidi na kuyapuuza maagizo ya wakubwa zake waliomtangulia mtu huyo hawezi kupata baraka, kwani elimu ndani yake kuna unyenyekevu na kusikiliza mafundisho ambapo hapo ndipo tunachota hekima na tisipo kubali kusikiliza na kujifunza tutabaki kama tulivyokuwa juzi yaani masikini" . Shule ya MLSS inayomilikiwa na Kanisa la KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria iko Mtaa wa Majengo Mapya katika Kata ya Mabatini jijini Mwanza ambapo makumi ya wanafunzi tayari wamesajiliwa kuanza masomo yao katika Shule hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.