Rais DKT.JOHN MAGUFULI amesema kuwa Serikali imedhamiria kujenga jengo la kisasa la abiria pamoja na uzio katika uwanja wa ndege wa mwanza ili kuufanya uwanja huo kuwa na hadhi ya kimataifa.
DK.MAGUFULI ameyasema hayo jijini Mwanza mara baada ya kurejea nchini akitokea UGANDA kuhudhuria mkutano wa wakuu wa jumuiya ya afrika mashariki ambapo wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Mwanza wamemuomba afanikishe ujenzi wa jengo la abiria ili kuondoa adha iliyopo kutokana na upanuzi wa uwanja huo unaoendelea hivi sasa kutohusisha ujenzi wa jengo hilo
Baada ya Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kukamatwa na Polisi na kuwekwa ndani wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata ambazo Chama hicho kinaongoza. Jembe Fm kupitia kipindi chake KAZI NA NGOMA kimemtafuta kwa njia ya simu Katibu Mwenezi wa chama hicho, ADO SHAIBU naye amezungumza kile kilichomtokea Mhe. Zitto, huku akijinadi kwa kusema, kwa hatua hiyo hawatorudishwa nyuma. BAADA YA KUTOKA ZITTO AZUNGUMZA HAYA. Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuwataka watu wasirudishwe nyuma kwa vitisho na usumbufu wa sheria kandamizi zinazopelekea baadhi ya viongozi kukamatwa na kuwekwa ndani. Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23, 2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo.
"Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo" alisema Zitto Kabwe
Aidha Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambapo diwani wa CHADEMA ameauwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali katika mwili wake
"Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia" alisema Zitto Kabwe
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari(hawapo pichani), ambapo alitangaza kuanza rasmi kwa zoezi la ukaguzi wa magari binafsi mwanzoni mwa mwezi ujao.Wengine ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Fortunatus Musilimu na Mjumbe wa baraza hilo,Henry Bantu(kushoto).Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu,akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambapo ilitangazwa operesheni ya ukaguzi wa magari binafsi unaotarajiwa kuanza mwezi machi mwanzoni.Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Henry Bantu, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambapo ilitangazwa operesheni ya ukaguzi wa magari binafsi unaotarajiwa kuanza mwezi machi mwanzoni.Katikatini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu(kulia).Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
Mjumbe waBaraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),Geoffrey Silanda, akijibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwake wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari(hawapo pichani).Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Waandishi wa Habari akiuliza swali kuhusu magari mabovu yanayobeba wanafunzi kwaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi uliofanyika leo katika ukumbi wa wizara jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabili liyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando hadi February 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).
Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU), Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea Tido maelezo ya awali.
Hata hivyo, Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta ameieleza Mahakama kuwa amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya (Ph), hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 28,2018 kwa ajili ya Tido kusomewa (Ph).
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Tido anakabiliwa na makosa matano ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
Inadaiwa alilitenda kosa hilo June 16,2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa TBC alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya uendeshaji wa vipindi kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BVI) bila kutangaza zabuni na kuisababishia channel hiyo kunufaika.
Inadaiwa kati ya June 16 na November 16,2008 akiwa Falme za Kiarabu, kama muajiriwa wa TBC kwa cheo cha Mkurugenzi Mkuu kwa mamlaka yake alilisababishia shirika la TBC hasara ya Sh.Mil 887.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Angelina Mabula amesema ni marufuku halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa fidia.
Mhe. Mabula amesema hayo Wilayani Butiama mkoa Mara wakati wa ziara yake yenye nia ya kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi.
Amesema wakati wa mchakato wa kuchukua maeneo ya mwananchi ni vyema wahusika wakashirikishwa kuanzia hatua ya awali sambambana na kuelimishwa juu ya zoezi hilo ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea.
‘’Cha msingi ni kuanza kuzungumza na mwananchi kabla ya kuchukua eneo lake na kumueleza eneo ambalo ataachiwa na halmashauri zihakikishe mwananchi huyo anapimiwa pamoja na kupatiwa hati yake’’ alisema Mabula
Aidha, mhe. Mabula amesema eneo litakalochukuliwa na halmashauri viwanja vyake kuuzwa fedha itakayopatikana halmashauri ihakikishe inatumika katika kutengeneza miundo mbinu na huduma nyingine za jamii na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo migogoro haiwezi kutokea.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ameziagiza halmashauri kuhakikisha zinapanga miji kulingana na ‘master plan’ ili kuwa miji bora iliyopangika.
Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu juhudi za mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo kutokana na uwajibikaji mkubwa katika kuwasemea wananchi wa jimbo hilo hususani katika kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta ya Madini.
Mhe Biteko ametoa pongezi hizo kwa mbunge huyo wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Songwe.
Naibu waziri huyo alisema kuwa mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea wananchi wake hususani katika kuchochea shughuli za maendeleo ili kuongeza ufanisi wa maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.
Pongezi hizo zinajili wakati ambapo mbunge Mulugo amefanikiwa kutatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya kikundi cha TUJIKOMBE na Kampuni ya Bafex kwenye eneo la uchimbaji dhahabu la mlima Elizabeth.
Katika kumaliza mgogoro huo kampuni ya Bafex imekubali kugharamia mradi utakaochaguliwa na kikundi hicho kama fidia ya gharama walizozitumia wachimbaji hao kuendeleza eneo hilo.
"Mheshimiwa Mulugo wewe ni hazina ya Songwe, namuomba Mungu aendelee kukutunza kwaajili ya watu hawa. Mimi nipo Bungeni muda wote wewe ajenda yako ni watu wako na unafanya hivyo bila kuchoka. Kwakweli wewe ni NOMA" Alisema Mhe. Biteko huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Sambamba na hayo pia amempongeza Mbunge huyo kwa ushirikiano mzuri baina yake na serikali ya Wilaya pamoja na Chama Cha Mapinduzi jambo ambapo linaakisi uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema kuwa kilio hicho cha wananchi kimedumu kwa muda mrefu hivyo jukumu la serikali ni kutatua kero za wananchi sio kuchochea migogoro.
Dar es Salaam. Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, amejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam, usiku huu baada ya gari dogo alilokuwa akiliendesha lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT. Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, amejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam, usiku huu baada ya gari dogo alilokuwa akiliendesha lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT.
Kwa mujibu wa dereva wa lori la mafuta lililohusika katika ajali, William Colonel, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupanda kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta na gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda.
Lori la mafuta na gari dogo yote yalikuwa upande wa kushoto wa barabara. Imeelezwa lori hilo baada ya kuanguka lililibana gari dogo lililokuwa katikati. Shuhuda wa ajali hiyo, Adeodatus Sylivester Charles "Nilimtambua majeruhi kwani namfahamu tangu akiwa mtoto na sasa ni mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru" amesema shuhuda Huyo.
Anasema baada ya ajali kutokea alikuta wasamaria wema tayari wanamtoa majeruhi kwenye gari akiwa ameumia sana. “Nilikuta ametolewa kwenye gari yake akiwa ameumia sana, nikamsaidia kuvitoa vitu vyake kama simu na pochi na kumpelekea maana alikua analalamika simu yangu simu yangu, na watu walikua tayari wameshasogea eneo la ajali wanagombania vitu hivyo.
Madereva wote wa malori walitoka salama bila majeraha ya aina yoyote.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (watatu kushoto) alipowapeleka Kasesera na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma Abdallah katika eneo la biashara za Machinga katika Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupata uzoefu wa namna Wilaya ya Ilala ilivyofanikiwa katika kuboresha mazingira na kuwaweka pamoja machinga hao katika shughuli zao. Wapili kushoto ni Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo.
Baadhi ya kinamama wakimweleza kero Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipokuwa na ugeni huo.
Kasesera akiwa na Mwenyekiti wa Machinga wa kariakoo katika ziara hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesera akitazama bidhaa za machinga ambazo alisema hadhi ya bidhaa hizo inaonekana ni zaidi na za machinga
Kasesera akitazama sampuli ya baadhi ya vifaa vya jikoni vinavyofanya kazi ambavyo anauza Machinga.
Machinga ambaye ni mtaalamu wa programu za kompyuta namoyo Yusuf, akimpa maelezo Kasesera ya namna ambavyo Umoja wa Machinga unavyohifadhi kumbukumbu zote za machinga katika komyupta. Kulia ni Mbunge wa Kilolo Asia Juma akifuatilia kwa karibu
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma akimweleza jambo Ofisa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya walipokuwa kwenye ofisi hiyo ya Machinga Kariakoo
Kasesera na ujumbe wake wakitoka katika Ofisi ya Machinga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera na Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Juma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Machinga wakati wa ziara hiyo
Kasesera akimfurahia Ustadhi ambaye ni mmoja wa machinga Kariakoo
Kasesera akifurahia jezi la Timu ya Machinga baada ya kuzawadiwa katika ziara hiyo
Kasesera na Amina wakichagua nguo kwenye vitalu vya biashara za Machinga wakati wa ziara hiyo
Kasesera akilipa fedha baada ya kuchagua nguo alizopenda.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Vilio, simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.
Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.
Wanafunzi zaidi ya wanne aliokuwa akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama hawaamini baada ya kushuhudia jeneza lenye mwili wake, huku wengine wakipoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Viongozi waliofika mpaka sasa katika viwanja vya NIT ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi; Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika.
Mkuu wa wilaya ya kwimba Mtemi safiri,amewakabidhi Bendera ya Taifa wanakwaya ya AICT Ngudu mjini wakijiandaa kwenda nchini Rwanda kuitangaza amani kupitia neno la Mungu kwa njia ya injili.
Ni wakati huo huo ambapo, Umoja wa makanisa ya kikristo(CCT)kata ya Ngudu wilayani Kwimba mkoani Mwanza ukitumia hafla hiyo kulaani hatua ya baadhi ya wananchi wachache wa kata hiyo, kuusimamisha msafara wa waziri mkuu KASIMU MAJALIWA kushinikiza kuondolewa kwa mkuu wa wilaya hiyo mhandisi MTEMI SEMEON.
Mwenyekiti wa umoja huo Mchungaji SAIMON CHEM amesema kuwa madai ya baadhi ya wananchi kuwa mkuu wa wilaya hiyo amekuwa akiwaamrisha polisi kuwakamata kwa kisingizio cha uzururaji na kisha kuwalimisha kwenye shamba lake si ya kweli.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara,wakulima na wenye viwanda(TCCIA)wilayani kwimba RENATUS MAGENI akabainisha kiini cha sintofahamu iliyojitokeza.
Sakata hilo pia limemwibua mwenyekiti wa chama cha ACT-WAZALENDO wilayani kwimba GASTUS LUSIMBYA.
Viongozi hao wametoa tamko hilo wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya taifa kwa wanakwaya wa kanisa la AICT la mjini ngudu wanaokwenda kuliwakilisha taifa katika uimbaji nchini Rwanda.
Akikabidhi bendera hiyo, mkuu wa wilaya Kwimba MTEMI SEMEON amewataka waimbaji hao kuwa mabalozi wazuri na kuwa kielelezo halisi cha Taifa linalosifika kwa amani duniani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na mmoja wa kiongozi wa Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amekerwa na usiri wa mapato na matumizi ya muwekezaji wa mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Mhe Biteko ameonyesha masikitiko makubwa wakati akizungumza na uongozi wa mgodi huo mara baada ya uongozi wa mgodi huo kushindwa kumpatia taarifa ya mapato na matumizi wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani humo kukagua shughuli za uchimbaji Madini.
Kumbukumbu hizo zimekosekana kufuatia viongozi wa ngazi ya juu ya mgodi kutokuwepo kwenye kikao hicho pamoja na kukiri kupokea taarifa ya ujio wake kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
Alisema kuwa viongozi hao kukosekana pamoja na kuwa na taarifa ya muda mrefu juu ya ziara hiyo ni utovu mkubwa na nidhamu kwa serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema kuwa pamoja na kutokuwepo kwao lakini taarifa zilitakiwa kuwepo ofisini kwani ni kosa kisheria kukosekana kwa taarifa za mgodi ilihali sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaeleza vyema kuwa mmiliki wa leseni ya Madini anatakiwa kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi kwa miaka mitano.
"Endapo atashindwa kufanya hivyo serikali itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo cha mwaka mmoja jela ama faini ya shilingi Milioni 50 mpaka milioni 150" Alisema Naibu Waziri huyo
Mhe Biteko akizungumza huku akionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi ambao walikuwepo katika eneo la ofisi ya mgodi huo huku wakishindwa kuhudhuria katika kikao hicho cha kazi alisisitiza kuwa muwekezaji wa mgodi huo anapaswa kuzingatia na kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi.
Sambamba na hayo pia Mhe Biteko aliutaka uongozi wa mgodi huo kutoa taarifa sahihi za uwepo wa mashapu katika mgodi waliyokuwa wakichimba au kama mashapu katika mgodi huo yameisha wafuate taratibu za kisheria za ufungaji wa mgodi ikiwemo kuyarudisha mazingira katika halo take ya kawaida.
DAKTARI
bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and
Immunology), Profesa John Shao, ameelezea uzoefu wakejuu ya mahangaiko waliyokumbana nayo
wafanyaakzi walioumia wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi inapofikia muda wa
kulipwa fidia.
Akitoa
uzoefu huo mbele ya madaktari wanaoshiriki mafunzo ya siku tano (5) ya tathmini
yaMfanyakazi aliyepataulemavu uliotokana
na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi
Februari 21, 2018, Profesa Shao ambaye kwa sasa amestafu kazi, alisema uwepo wa
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), utawezesha wafanyakazi walioumia kazini kwa
mazingira mbalimbali waweze kupata haki zao stahiki.
Ukosefu
wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya tathmini wakati huo, kulipelekea shida
nyingi kwa wafanyakazi waliopata madhara kazini.
Aidha
Profesa Shao ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye taasisi za tiba akiwa
kama Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC Moshi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Tumaini, na pia aliwahi kufanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwa ni
pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya
Karatu, aliushauri Mfuko katika kutekeleza majukumu yake ni lazima sasa ujikite
katika mambo ambayo aliyaona wakati huo yakiwa na mapungufu.
“Kuwe
na utaratibu katika ngazi ya vituo vya afya vya binafsi na vya serikali ambavyo
vitawapokea wagonjwa kama hawa na kuwapima kutokana na jinsi walivyoumia na
kuwapatia rufaa ya kwenda katika hospitali za wilaya, mkoa au hizi za madaktari
bingwa ili waweze kupata huduma hiyo na vile vile kutathminiwa kwa usahihi.”
Alisema.
Alishauri
kuwa kazi hii ya kufanya tathmini isiachiwe kwa Daktari mmoja au muuguzi mmoja
au afisa mmoja tu bali pawepo na kikundi (team work) ambacho kimepata mafunzo
mazuri kinachoweza kupima na kutoa muelekeo mzima na katika kufanikisha hili
lazima pawepo na mfumo mzuri endelevu wa mafunzo kama haya.
“Uwepo
mfumo wa wataalamu (madaktari) wanaopata mafunzo haya watoke kila kada ili wapatiwe
mafunzo stahiki ya kuwahudumia wagonjwa wanaopata madhara yatokanayo na kazi,
ili wawe na uwezo wa kutoa tathmini iliyo sahihi.
Pia
alishauri kuwepo na mfumo wa kuimarisha uanzishwaji viwanda walau kuwe na Minimum Standard ya viwanda vinavyoanzishwa
vikidhi mazingira salama ya kazi na hatua hiyo iende sambamba na mafunzo kwa
wafanyakazi walioajiriwa wawe na muda wa kupewa elimu ya madhara yanayoweza
kutokea kwenye mazingira yao ya kazi na jinsi gani wanaweza kujiepusha nayo.
Aidha
gwiji huyo wa uchunguzi wa vijidudu na madawa, aliwaasa madaktari hao kutoka
mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kufanya kazi kwa uadilifu
mkubwa, kuongeza uwajibikaji, moyo wa kujitolea na kutojiona kama vile mgonjwa
aliyeumia anatumiwa kama mojawapo ya kuongeza kipato kwa watendaji.
Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and
Immunology), Profesa John Shao, akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuhudumia wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na usalama mahala pa kazi wakati wa mafunzo ya madaktari wanaojifunza namna ya kufanya tathmini
yaMfanyakazi aliyepataulemavu uliotokana
na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi
Februari 21, 2018
Mshiriki akifuatilia kwa makini nasaha za Profesa Shao.
Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Assessment Manager), wakifuatilia nasaha za Profesa Shao.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akiongoza mafunzo hayo.
Profesa Shao, (kushoto), akiteta jambo na mmoja wa washiriki.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), akisalimiana na Profesa John Shao.
Profesa John Shao, akisalimiana na Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), Dkt. Ali Mtulia.
Sehemu ya washiriki.
Profesa John Shao.
MABINGWA WANAPOKUTANA:
Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina,(kulia) na Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and
Immunology), Profesa John Shao, wakisalimiana.
Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina, akifafanua jambo.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya kwimba mkoani Mwanza wamepinga madai kuwa mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Mtemi Simioni amekuwa akiwaamrisha Polisi kuwakamata baadhi ya wananchi wa kata ya Ngudu kwa kisingizio cha uzururaji na kisha kuwalimisha kwenye shamba lake. Ni Siku mbili baada ya baadhi ya wananchi wa kata ya Ngudu wilayani kwimba mkoani Mwanza kuzuia msafara wa waziri mkuu Kasimu Majaliwa wakitaka kuondolewa kwa mkuu wa wilaya hiyo mhandisi MTEMI SEMEON kwa madai kuwaamrisha polisi kuwakamata kwa kisingizio cha uzururaji na kisha kuwalimisha kwenye shamba lake. Kufuatia malalamiko hayo ya baadhi ya wananchi ,Madiwani wa halmashauri ya Kwimba mkoani Mwanza ambao wamekutana na vyombo vya habari wamesema kuwa madai hayo si ya kweli na kwamba wananchi wa ngudu waliosimamisha msafara wa waziri mkuu KASIMU MAJALIWA wanatumiwa na kikundi cha watu kisichotaka watu kufanya kazi pamoja na wale waliokuwa wakijipatia fedha za umma kwa njia za udanganyifu kabla ya mianya hiyo kuzibwa na mkuu huyo wa wilaya. Hawa ni baadhi ya Madiwani wa halmashauri hiyo ya Kwimba wakiongozwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Shija Malando ambao kwa pamoja wakatoa msimamo wao kuhusu kitendo cha diwani wa kata ya Gudu Juston Malifedha. Madiwani hao ambao wamejitokeza mbele ya vyombo vya habari wakaeleza kiini cha sintofahamu iliyojitokeza katika ziara ya ya mhe.kassim majaliwa kassim.
Arusha Yasimama Kwenye Maombi: Miaka 63 ya Uhuru
-
Viongozi wa dini ,mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda na wananchi
wakiendelea na maombi katika matembezi ya kuombea mkoa wa Arusha na
maathimisho ya mi...