ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 4, 2011

KAMA VIPI BADAE NDANI THE STONE


BaAda yA kaZi nA pILIkA pILIkA zA wIkI nZIMA, mWILi wAhITAji tUlIzO.

TUKUTANE PARE-PARE STONE CLUB MWANZA.

MALAWI KUPIGA MARUFUKU 'KUJAMBA'?

Mzozo umezuka nchini Malawi kufuatia mapendekezo kutaka kufikishwa bungeni kuhusu kujamba, kuwa ni kosa.

Waziri wa sheria wa Malawi, George Chaponda amesema muswada huo utakaojadiliwa kuwa sheria ndani ya bunge wiki ijayo, utapiga marufuku kabisa kwa mtu kufanya haja hiyo hadharani. Waziri huyo amekiambia kituo kimoja cha radio nchini humo- kwa maneno yake - "nenda chooni kama unajisikia kujamba".


Hata hivyo mkuu wa wanasheria nchini Malawi Anthony Karanga amesema kufanya haja hiyo hakufikii kuharibu hali ya hewa kiasi cha kuwa kosa la jinai.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema wananchi wa Malawi wanajiuliza mapendekezo ya sheria hiyo, iwapo itapitishwa, itatekelezwaje?

IMETOKEA SASA HIVI.....

Dereva tax wa gari lenye namba za usajili T 164 AVR akiwa mafuta mbaya amepitiliza hadi eneo la bustani ya kipita shoto cha katikati ya jiji la miamba na kugonga hata kuling'oa moja ya bango la biashara eneo hilo.

Dereva huyo alikuwa na abiria wawili wa kike na mtoto mdogo, wote hawakudhurika, chanzo: kwa mujibu wa dreva- kufeli kwa breki.

MMECHISHO - ASANTE NONINO!!..!!

Pichani ni wanahabari Henry Kavirondo wa chanel 10 (kulia) na Nashon Kennedy wa Mtanzania Daima wakikimbiana mara baada ya kukutana mjengoni wakiwa wametupia mapigozzz aina moja. HIVI ni kwanini?

MAJONZI YATAWALA MSIBA WA MAMA MZAZI WA MCHEZAJI WA ZAMANI WA TIMU YA PAMBA NA TAIFA STARS (FUMO FELICIAN).

Marehemu mama Teresa Felician Minde (1943-2011) aliyeaga dunia tarehe 1/2/2011.

Mume wa marehemu mzee Felician akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu mkewe.

Huzuni ilitawala ilipofika zamu ya Watoto wa marehemu kutoa heshima zao za mwisho.

Diwani wa kata ya Nyamagana mh. Kotecha akiwafariji wafiwa.

Watoto wa marehemu katika picha hii ni mchezaji wa zamani wa timu ya Pamba ya Mwanza, Fumo Felician (kulia)na kaka yake Felix Felician anayefuata.

Fumo alizimia wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu mama yake. Pichani akipata msaada toka kamati husika.

Sehemu ya wanandugu.

Jana jioni mara baada ya heshima za mwisho kutolewa mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwaajili ya mazishi yanayotaraji kufanyika siku ya jumapili tarehe 6.feb.2011.

Thursday, February 3, 2011

Mbowe na Kikwete USO KWA USO.

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe jana alikutana uso kwa uso na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni mara ya kwanza tangu chama hicho kilipotangaza kutotambua ushindi wa Kikwete uliompa fursa ya kuwa rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana.Tukio hilo la aina yake kutokea tangu kuanza kwa mwaka huu, liliwakutanisha Mbowe na Rais Kikwete katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono.

Mbowe na Kikwete walikutana uso kwa uso ikiwa ni siku 85 tangu Mbowe alipowaongoza wabunge wa chama chake kususia hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 10, Novemba 18 mwaka 2010 kutokana na msimamo wa chama chake kutotambua matokeo ya urais.

Mwaka jana, Mbowe alitangaza chama chake kutotambua matokeo ya rais huku akitoa madai mbalimbali kuhusu taratibu zilizotumika kumwingiza kiongozi huyo madarakani.

Katika tukio la kupiga picha za pamoja ndipo Mbowe alikutana uso kwa uso na Rais Kikwete ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono na kupiga picha pamoja huku wote wakiwa na tabasamu pana.

Alipotafutwa na gazeti la Mwananchi (wanyetishaji wa inshu hii) ili kuzungumzia tukio hilo, saa kadhaa baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Mbowe alisema alikwenda katika sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa ni za mahakama na kwamba hata kungekuwa na tofauti gani kusingemzuia yeye kusalimiana na Kikwete.

"Sherehe zile si zangu wala Rais Kikwete hivyo siwezi kuwa na chuki na mahakama, ni 'Birthday' ya Mahakama yenyewe ni mhimili wa dola," alisema Mbowe.

Mbowe alisema kuwa katika maadhimisho hayo alialikwa kama mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Mbowe alisema kuwa madai waliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana haikuwa na maana kwamba hawaitambui Serikali wala kutaka Rais Kikwete ang’oke madarakani.

Alisema kuwa mambo mawili kati ya matatu yaliyokuwemo katika dai lao yameshaanza kupatiwa ufumbuzi kwa namba moja au nyingine ambayo ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.


RAIS AZUNGUMZIA IMANI YA WANANCHI KWAKE:
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Rais Kikwete alisema kuwa baadhi ya wananchi wamekosa imani naye kutokana na msimamo wake wa kukataa kuingilia uhuru wa Mahakama wanapomtaka atengue maamuzi mbalimbali ya korti.
Kikwete alikuwa akizungumzia uwelewa wa wananchi juu ya sheria mbalimbali na nafasi ya Mahakama ambapo alisema kuwa wananchi hawana budi kufahamu jinsi Mahakama inavyofanya kazi.

Rais alitoa wito kwa Mahakama kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwamo vyombo vya habari katika kutoa elimu kuhusu sheria.

GHASIA ZACHUKUWA SURA MPYA MISRI.

Wafuasi wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak wamekabiliana na waandamanaji wanaomtaka kiongozi huyo aondoke madarakani katikati mwa mji wa Cairo.Maelfu ya wafuasi wa Bw Mubarak walimiminika kwenye eneo la Tahrir na kuondoa vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na waandamanaji.

Pande hizo mbili zilirushiana maneno kabla ya kuanza kurushiana mawe. Kuna Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia walikuwa miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa Bw Mubarak waliojitokeza katika eneo la Tahrir.

Athari za vurugu hizo.

Waandamanaji wanataka Rais Hosni Mubarak aondoke madarakani baada ya kutawala kwa muda wa miaka 30.

Mjini Cairo kwenyewe helikopta za kijeshi zimeendelea kuzunguka angani karibu na bustani ambapo maelfu ya watu walikusanyika licha ya amri ya kutotoka nje usiku iliyotangazwa na serikali.

Polisi waliagizwa kurejea kwenye barabara za mji wa Cairo walizoziacha siku ya Ijumaa, wakati yalipofanyika mandamanao makubwa ya kuipinga serikali. Mapambano mengine yameripotiwa kwenye mji wa Alexandria.

Wednesday, February 2, 2011

KARIBU KWENYE MAKUMBUSHO YA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE.

Hili ni jumba la Makumbusho ya Mwalimu J.K.Nyerere, Butiama mkoani Mara. Ushawahi kutembelea hapa?

Mchezo wa Bao huchezwa na makabila mengi hapanchini Mwalimu J.K Nyerere amekuwa akicheza na kuupenda mchezo huo hata baadhi ya vyama miaka ya sasa kumuenzi kwa kufanya mashindano mbalimbali nchini. Bao hili alipewa na wananchi wa Ndanda.

Joho la Uhitimu.

Hivi ni baadhi ya viatu alivyokuwa akivaa Hayati Mwalimu J.K.Nyerere. Mwalimu alipenda zaidi viatu vya kutumbukiza, pembeni kama mkoba ni redio yake. Itizame kwa uzuri katika picha inayofuata.NI Redio aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kusikiliza habari mbalimbali alipenda pia kuitumia katika baadhi ya ziara zake za ndani na nje ya nchi. Redio hii alipewa zawadi huko Ujerumani mwaka 1969.

A gift of traditional stool given to Mwl. Nyerere by the residents of Dar-es-Salaam after the victory of Kagera war in 1978 - 1979.

Jiwe la kusagia nafaka huitwa 'Ombwe' na dogo huitwa Esyo, kwa kawaida kazi ya kusaga hufanywa na wanawake. Chakula kikuu cha wazanaki ni ugali, huliwa kwa nyama, samaki na mboga za majani.

Picha nazo zipo.

Urithi wa asili wab Tamaduni za kizanaki silaha za jadi, vifaa vya nyumbani, ala za muziki, mapambo ya asili, lugha, mila, desturi - nk. Vyte utavikuta kwenye nyumba hii ya makumbusho ya Mwalimu.

MDAU PETER FABIAN.

NANI KAKWAMBIA MWAKA MPYA ULIKARIBISHWA KWA AMANI NA UTULIVU? ALAMBWA RISASI NA POLISI WAKATI AKIUKARIBISHA MWAKA.

Usiku wa kuukaribisha mwaka mpya 2011 kwa wengi huwa ni wa furaha, lakini kwa dada huyu kwake ulimwendea kombo kwa kukutana na balaa la kupata kilema cha maisha mara baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi mguu wake wa kulia na mtu inayesemekana kuwa ni askari wa jeshi la polisi ambaye mpaka sasa jina lake halijatajwa.Usiku wa saa sita na dakika zake, dada Lilian James akiwa na mpenzi wake wakielekea nyumbani kwao Mabatini, wakitokea stand ya zamani ya mabasi Mwanza walipofika eneo la 'Kileluu Mabatini' wakakutana na kundi kubwa la watu wakikimbia ambao walikuwa wakitawanywa na polisi kutokana na vurugu zilitokea usiku huo ambazo zimekuwa kama jadi kwa kila nyakati za kuukaribisha mwaka kwa baadhi ya watu kufanya uharibifu wa kuvunja vioo vya baadhi ya magari na kupora mali hasa eneo hilo la barabara ya mabatini-igoma. Wasielewe kinachoendelea na kujitenga na wakimbiao, mlio wa risasi ukasikika-'TPBUUU!!' Mwanaume akatimua mbio, mwanamke akashindwa kukimbia hata kusogeza mguu kwani risasi moja ilikuwa tayari imetandika mguu wake wa kulia.

Kesi bado iko polisi ikizungushwa isijulikane nini mstakabari wake na hata maafisa wa jeshi la polisi Mwanza hawajazungumza lolote kwa kilichotokea zaidi ya kupinga kwa kusema kuwa haikuwa risasi bali ni bomu la machozi.

Na kwa mujibu wa mwanaume wa Lilian James amesema kuwa kulipo pambazuka walikwenda polisi na vithibitisho vya maganda ya risasi ambavyo walipigwa mkwara na askari kisha kunyang'anywa kwa nguvu.


INAENDELEA......

Tuesday, February 1, 2011

LEO TENA!..!

Habari za asubuhi mdau! Hii ni Barabara ya Makongoro Mwanza.

TORRES AKIMWAGA WINO CHELSEA: LIVERPOOL WALAMBA DUME NDANI YA TRANSFER DEADLINE DAY.

Andy Carroll has become the most expensive English player in the history of football after joining Liverpool from Newcastle in a £35 million deal.LETE JEZI YETU"""!!!...
Carroll, 22, was targeted by Liverpool as a replacement for Fernando Torres, who has joined Chelsea in a deal worth up to £50 million. Liverpool failed with an offer for the Newcastle striker earlier on Monday but persisted with their interest and convinced the Magpies to sell their No. 9, who had drawn favourable comparisons with his predecessor Alan Shearer after taking the shirt at the start of the season.

A Liverpool statement read: "Andy Carroll has tonight completed his transfer from Newcastle United to Liverpool FC and signed a five-and-a-half-year deal that will keep him at Anfield until 2016. "The club agreed a record transfer fee with Newcastle earlier in the day for the transfer of the England international striker. The deal was subject to the completion of a medical, which the player has now passed. Andy Carroll will wear the No. 9 shirt for Liverpool."


FERNANDO TORRES AKIWA AMEPOZI NA UZI WA CLUB YA CHELSEA BAADA YA KUMALIZA KUSAINI MKATABA WAKE MPYA WA £50m KUTOKA LIVERPOOL.
Carroll amefunga jumla ya magoli 11 katika mechi 19 za ligi msimu huu, na kwa mara ya kwanza alishiriki katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa timu ya taifa ya England mwezi Novemba mwaka jana, wakati England iliposhindwa na Ufaransa magoli 2-1 katika uwanja wa Wembley. Following Torres' exit from Anfield, Carroll will play alongside Luis Suarez, who completed his £22.7 million move from Ajax to Liverpool earlier on Monday night. Torres' move to Chelsea also means that Carroll's transfer is the eighth most lucrative of all time.

Meanwhile, on a day when they signed Stephen Ireland on loan from Aston Villa and attempted to bing Wigan winger Charles N'Zogbia back to the club, Newcastle also loaned striker Xisco to Deportivo La Coruna. Xisco said on the Depor website: "I'm returning to my home. Deportivo have given me everything and I've come here focused on helping the team reach their objectives."

Monday, January 31, 2011

D-CHANGE FESTIVAL IN MWANZA ILIVYOKUWA.

Umoja wa makanisa jijini mwanza jana jioni umefunga rasmi mkutano wake mkubwa wa injili uliojulikana kwa jina 'D-Change Festival'. Kusanyiko hilo lilihusisha wanamuziki wa injiri akiwemo Solomoni Mukubwa, Anastazia Mukabwa, kundi la The Fielder-Marshals pamoja na Mhubiri na Muimbaji mkongwe Askofu Ben Bahati.Solomon Mukubwa akiwaimbisha wananchi waliofurika kwa wingi viwanja vya Furahisha, moja ya nyimbo zake.

Askofu Ben Bahati akiwaongoza watu walijitokeza kwa wingi kwenye viwanja hivyo vinavyopatikana kirumba jijini Mwanza, katika sala ya toba kama ishara ya kumpokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao.

Anastazia Mukabwa akiimba wimbo wa KIATU KIVUE mbele ya umati wa wakazi wa Mwanza,na kisha akaimba wimbo wake wa "Anayekudharau siku moja atakusalimia kwa Heshima" uliionekana kuwasisimua wengi uwanjani hapo.

Umati wa watu ulijitokeza kusikiliza habari njema za Kristo katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Kundi la The Field-marshals toka Kenya likimsifu MUNGU katika siku husika.

UPAKO zaidi TEMBELEA www.hosannainc.blogspot.com

Sunday, January 30, 2011

WAMACHINGA WAFANYA VURUGU MWANZA.

JIJI la Mwanza jana lilikumbwa na machafuko baada ya machinga kufanya vurugu na kuandamana wakipinga kuondolewa kufanya biashara katika maeneo ya mjini kati. Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa maduka katika maeneo mbalimbali mjini hapa, kuvunjwa vioo vya magari, maduka na baadhi ya barabara kutopitika kwa muda huku kituo kidogo cha Polisi Pamba, kikinusurika kuvamiwa na kuchomwa moto.MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS KANDORO AKIZUNGUMZA NA WAANDAMANAJI HAO KUPITIA GARI LA FFU, KULIA MWENYE SHATI YA BLUE NI MWENYEKITI WA WAMACHINGA MZ.
Pamoja na vurugu hizo, serikali mkoani Mwanza imewataka wafanyabiashara hao kuheshimu sheria na kanuni za mipango miji zilizowekwa pia maafikiano yaliyofikiwa baina ya viongozi wao, uongozi wa mkoa na halmashauri ya jiji hilo .

PATASHIKA MITAA YA MIRONGO.
Vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa sita, zilianza saa tatu asubuhi baada ya mgambo wa jiji na askari wa kutuliza ghasia kuwatawanya wafanyabiashara hao katika maeneo ya Makoroboi, Mission na Soko Kuu.

WAMACHINGA WAKIKUSANYA BIDHAA ZAO.
Kutokana na hali hiyo, machinga walijikusanya na kuanza kuvamia maduka, magari kabla ya kuandamana saa 4:38 asubuhi hadi katika jengo la ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza wakishinikiza kutoondolewa katika maeneo hayo.

Nje ya jengo hilo , waliweka vizuizi vya mawe katika barabara zote zinazoingia jiji na kulazimisha pikipiki na magari yaliyokuwa yakipita kurudi yalikotoka huku wakiwa na chupa za maji ya kunawa kwa ajili ya kujikinga na moshi wa mabomu iwapo polisi wangewafyatulia mabomu ya machozi.

Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia na makachero kuweka ulinzi mkali katika lango kuu la kuingilia jiji hadi viongozi akiwemo Mkurugenzi wa jiji Wilson Kabwe na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro walipofika na kufanya mazungumzo na viongozi wa machinga hao.

Baada ya mazungumzo hayo, Kandoro aliwaambia machinga kuwa hapingani na sheria na kanuni za mipango miji kwa kuruhusu machinga wafanye biashara katika maeneo waliyoruhusiwa, isipokuwa wafuate masharti waliyopewa katika maeneo ya Makoroboi, Mirongo, Vitunguu Soko Kuu na Mlango Mmoja.

AJALI KATIKA PILIKA ZA KUNUSURU BIASHARA.
Baada ya kuondoka katika ofisi za halmashauri hiyo, machinga waliingia mitaani tena na kuanza vurugu wakivamia maduka na kuvunja vioo kwa madai kwa wafanyabishara wengine, hawatafanya biashara.

Sambamba na kuvamia maduka, walijiandaa kwenda kuvamia Kituo cha Polisi Pamba kwa lengo la kukichoma moto kwa kutumia matairi ya gari kabla ya polisi waliokuwa doria kuwawahi na kuwadhibiti, ambapo walitupa matairi ya moto katika barabara ya Pamba jirani na kituo hicho.


Awali, katika vurugu hizo magari T. 541 BHN aina ya Toyota Carina, T. 352 ALF, T.234 ASA na lori aina ya FIAT lenye namba T. 988 AGM, yalipigwa mawe na kulazimishwa kutopita jijini ambapo gari hilo lilivunjwa kioo cha pembeni mbele. Gari lingine lililovunjwa kioo cha nyuma katika eneo la Rwagasore ni T. 400 AHT aina ya Toyota Land Cruiser mali ya mfanyabishara maarufu Mkeshi Vunjabei ambaye baadaye saa 7:52 mchana walivamia duka lake, lakini waliwahiwa na polisi.

Barabara zilizokumbwa na vurugu hizo na kutopitika kwa muda huku wafanyabiashara wengine wakifunga maduka yao kuepuka vurugu hizo ni Nyerere, Rwagasore, Rumumba, Uhuru, Makoroboi na Liberty. Hadi jana jioni, vurugu zilikuwa zikiendelea katika baadhi ya maeneo na kufanya mji wa Mwanza kuwa kimya kutokana na shughuli kusimama, hata hivyo vurugu hizo hazikuwa kubwa.