ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 29, 2022

BREAKING: SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA YA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
 Tangazo kwa ajili ya Kazi ya muda ya Sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe 23/08/2022. 

Kazi zitatangazwa rasmi tarehe 01/05/2022 katika tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambayo ni www.nbs.go.tz

Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 14 Mei 2022.

255744996048_status_21aa2ab030b54e56a393d13d80300db8

255744996048_status_f8cc7916c7b8482da9860843364ea81c

255744996048_status_6cb08f58f3cc44f785114e3f1858ccfe

255744996048_status_58cb565fd2c2423b8a8e310e1c91bc7e

255744996048_status_713a4f51ca9349bbbb0b188b723c411c

Thursday, April 28, 2022

JUMLA YA WAHAMIAJI HARAMU 34 WAKATWA IRINGA.

 

kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa habari juu ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia

Wahamiaji haramu wakiwa chini ya ulinzi mara baada ya kukamatwa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linawashikiria jumla ya wahamiaji haramu 34 kutoka nchini Ethiopia wakisafirishwa kuelekea nchini Afrika ya Kusini baada ya kuwakamata katika eneo la Kitonga wilaya ya Kilolo.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema kuwa wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu hao kwa ushirikiano na idara ya uhamiaji mkoa wa Iringa. 

ACP Bukumbi Alisema kando ya kukamatwa Kwa raia hao wa kigeni Jeshi la polisi linamshikiria dereva wa Lori Maulid Chinunga miaka 37 mkazi wa Dar es salaam aliyehusika kuwasafirisha raia hao wakigeni kinyume Cha sheria.

Alisema kuwa  tarehe 27/04/2022 majira ya Saa 10:00 jioni, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Iringa eneo la Comfort-Kitonga Kata na Tarafa ya Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, tulifanikiwa kumkamata dereva MAULID CHINUNGA miaka 37, Muislam Mmakua na Mkazi wa Dar es salaam akiwa anasafirisha Raia wa kigeni wapatao 34 kutoka Nchini Ethiopia wakitokea Mkoani Pwani kuelekea Tunduma mkoani Mbeya kwenye gari aina ya FAW yenye namba za usajili T 529 DXF na tela  T 826 DXP mali ya kampuni MIGHTY LOGISTICS LTD, watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.   

Akitoa taarifa za matukio ya uhalifu mkoani Iringa Kamanda Bukumbi amelitaja pia tukio la kukatwa Mtu mmoja mkazi wa Kalenga Wilayani Iringa aliyekamatwa na meno ya tembo aliyoyaficha katika korongo.

Alisema kuwa Mnamo tarehe 16/04/2022 majira ya Saa 10:20 jioni maeneo ya Bumila Kata ya Nzihi Tarafa ya Kalenga Mkoa wa Iringa, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi dhidi ya ujangiri (KDU) tulifanikiwa kumkamata ROMANUS MUTUTURI  miaka 45, mhehe na mkristo, akiwa na vipande 02 vya Meno ya Tembo yenye thamani ya Tsh 35,189,122/= aliyokuwa ameyaficha kwenye korongo baada ya kupokea taarifa fiche kutoka mwananchi zilizowezesha kukamatwa kwake. 

"Mwisho nitoe rai kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa kuwa na utii wa sheria katika kipindi hiki tunapoelekea Sikukuu ya EID EL-FITR, wasiache nyumba zao bila uangalizi muda wote, watumiaji wa vyombo vya moto (magari, bajaji na pikipiki) njia kuu na maeneo mengine wawe na utii, pia wananchi waache kujihusisha na vitendo vya uhalifuna badala yake washirikiane na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kwa wakati ili ziweze kushughulikiwa" alisema ACP Bukumbi.

Tuesday, April 26, 2022

DC MOYO ATAKA VIONGOZI WA DINI NA KIMILA KUSHIRIKISHWA KAMPENI YA CHANJO YA POLIO

 

Mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wajumbe wa chanjo ya polio Manispaa ya Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa kupitia idara ya afya Inatarajia kutoa chanjo ya Ugonjwa wa polio kwa watoto 25 elfu walio chini ya umri wa miaka mitano (5) ili kuwakinga na hatari ya kuambukizwa virusi vya maradhi hayo

Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr. Baraka alisema kuwa Halmashauri hiyo tayari imepokea dozi 27 elfu za kinga ya Polio na kwamba zoezi la chanjo litaanza kutekelezwa kuanzia April 28 hadi mei mosi mwaka huu.

Wakati wa mafunzo kwa kamati ya msingi ya huduma za afya kwa jamii Mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amehimiza viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo hiyo kwa watoto.

Dr. Chaula alisema kuwa lengo la kutoa mafunzo hayo ni kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya umuhimu wa wazazi na jamii kwa ujumla juu ya kuwapatia chanjo ya polio watoto wao.

Alisema kuwa ugonjwa wa polio unataja kuathiri watoto wenye umri wa miaka chini ya kumi na nne lakini kwa mujibu wa wataalam wa afya ugonjwa huo uathiri zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka mitano

Dr. Chaula alisema kuwa tayari chanjo zimekuwishapokelewa katika manispaa ya Iringa kilichosalioa ni utekelezwaji wa zoezi lakutoa chanjo kwa wahusika

Mganga mkuu wa Manispaaya Iringa ameyasema haya wakatiwa akimkaribisha mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo katika uzinduzi wa kampeni hiyo yaChanjo.

Kwa upande wake mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ni lazima kuwashilikisha viongozi wa mitaa ili waone umuhimu wa jambo hilo.

Alisema kuwa kuwashirikisha viongozi wa ngazi ya mtaa hadi kata kutasaidia kufanikisha zoezi hilo la chanjo ya polio kwa watoto wadogo na jamii kulijua swala hilo la polio.

Moyo aliwaomba viongozi wa dini wilaya ya Iringa kulichukua swala la polio kama la kwao kwa kuwaelimisha jamii juu ya chanjo ya polio kuwa ni chanjo salama ambayo inawakinga woto wao.

Aliwaomba wananchi kushiriki katika kampeni ya chanjo ya polio kwa watoto wadogo ambao ndio waathirika wakubwa na chanjo hizo zipo kwa ajili ya kuwakinga watoto wao.

Mkuu huyo wa wilaya alimazia kwa kumuagiza mganga mkuu wa manispaa ya Iringa kuhakikisha anaishirikisha jamii na viongozi wa dini na viongozi wa kimila ili waweze kusaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi husika.

 

Monday, April 25, 2022

FAMILIA YA MLINZI ANAYEDAIWA KUUAWA NA MFANYABIASHARA YATAKA UCHUNGUZI.

 


Familia ya mlinzi anayedaiwa kuuawa na mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Pendael Molllel imeliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua za kisheria kwa wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

Imesema kuwa imepanga kufanya maziko ya ndugu yao Jimmy Mollel (43), Aprili 26, Ngaramtoni wilayani Arumeru, baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mjomba wa marehemu, Ernest Julias alisema licha ya kuridhia kumzika ndugu yao wanaliomba jeshi hilo kufanya uchunguzi na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

“Nilimpigia RCO ameniambia majibu ya postmoterm (uchunguzi) ni kwa ajili ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi na sisi tumeridhika na tunatarajia kumzika nduyu yetu Jumanne ijayo eneo la Ngaramtoni, wilayani Arumeru,” alisema.

Alisema taarifa waliyoipata kutoka kwa daktari ilionyesha kuwa chanzo cha kifo ni maumivu makali yaliyosababishwa na jeraha alilonalo marehemu kwenye kisogo ambapo inaonekana alipigwa au kuchomwa na kitu chenye ncha kali.

Kamanda Polisi mkoani Arusha, Justine Masejo, amethibitisha kukamatwa kwa Mollel na wenzake watatu Mjini Moshi walikokimbilia kwenda kujificha, wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

DC MOYO AWATAKA UVCCM IRINGA KUULINDA MUUNGANO WA TANZANIA


Mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa (CCM) Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM mkoa wa Iringa

Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM mkoa wa Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM mkoa wa IringaNa Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa (CCM) Mohamed Hassan Moyo aliwataka vijana wa chama cha mapinduzi kuendelea kuelezea mafanikio ya muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo serikali kwa kipindi chote ilivyofanya kazi kuleta maendeleo.


Akizungumza kwenye kongamano maalumu la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa (UVCCM),Moyo alisema kuwa kumeibuka wimbi la watu ambao wanataka kuuvunja muungano kwa maslai yao.


Alisema wapo watu hawataki kuona muungano huo ukiendelea kuimarika hivyo jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wanapaswa kuendelea kuulinda muungano ili usivunjike.


Moyo alisema kuwa vijana wanawajibu wa kuwapinga watu wote ambao wanampango wa kuuvunja muungano kwa nia ovu zao hivyo vijana ndio wanajukumu la kuulinda muungano.


Aidha Moyo aliwataka vijana wa chama hicho wanaoenda kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenda kushiriki uchaguzi kwa uadilifu ili kupata viongozi walio imara na bora kukiongoza chama hicho.


Alisema kuwa vijana wanaoenda kugombea wanatakiwa kuwa wanaccm kweli na sio mamluki wanaopandikizwa kwa lengo la kuja kukivuruga chama hicho hivyo wanatakiwa kuwa makini kwenye chaguzi za chama.

Moyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Iringa hautakubari kuona wagombea wanashinda kwa kutoa rushwa hivyo TAKUKURU itakuwa macho muda wote.


Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi safi ambao watakiongoza chama hicho kwa mafanikio ya kukivusha chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali ambazo chama hicho kitashiriki kutafuta mamlaka ya kuunda serikali.


kwa upande wake katibu mkuu wa umoja wa Vijana
(UVCCM) taifa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,Kenani Kihongosi alisema kuwa katiba ya chama cha mapinduzi inamtaka mwanachama yeyote anahaki ya kugombea nafasi yoyote bila ya kuwa na uwoga wowote ule.


Kihongosi aliwata vijana wa UVCCM kuacha tabia ya kulalamika kuwa wananyimwa nafasi za uongozi lakini kipindi cha uchaguzi vijana hao hawajitokezi kugombea.

Kihongosi alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anawaamini  vijana ndio maana kwenye teuzi mbalimbali za serikali,ameteua Zaidi ya asilimia 75 hadi themanini za vijana kwenye kuongoza serikali ya awamu ya sita.


Aliagiza kwa makatibu wote wa UVCCM Tanzania kuacha mara moja kuwabeba wagombea,waache wanachama waamue nani anastahili kuwa kiongozi wa chama hicho ambaye anauwezo wa kuongoza jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.Kihongosi alisema kuwa hataki kusikia fomu za wagombea zinapotelea ofisini bali fomu zote zinatakiwa kufika sehemu husika ili vikao husika viweze kutoa maamuzi kwa mjibu wa katiba ya chama.Alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu atasimamia kanuni na sheria za chama hicho ili kupata viongozi bora ambao wataweza kukiongoza chama hicho na wanachama chake kwa kuwa rushwa haina nafasi mwaka huu.

Aidha Kihongosi aliwataka vijana wa umoja huo kucha tabia ya kuwapiga majungu vijana wenzao ili kila mmoja apate nafasi anayostahili kulingana na nafasi anayoishika naanayoigombea.

“Ni marufuku kwa viongozi kupanga safu katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa kufanya hivyo kutapekea chama kupata viongozi wabovu ambao hawastahili kuwa viongozi” alisema KihongosiKihongosi amewataka vijana wa umoja huo kwenda kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kulingana na uwezo wako.

 

 

KATIBU MKUU UVCCM AONYA RUSHWA UCHAGUZI WA CCM

 

Katibu mkuu wa umoja wa Vijana (UVCCM) taifa Kenani Kihongosi akiongea na vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi

Baadhi ya wananchama wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa wakimsikiliza katibu mkuu wa UVCCM taifa Kenani Kihongosi

Na Fredy Mgunda,Iringa.

KATIBU mkuu wa umoja wa Vijana (UVCCM) taifa Kenani Kihongosi amewataka vijana wa umoja huo kwenda kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kulingana na uwezo wako.

Kihongosi alisema kuwa katiba ya chama cha mapinduzi inamtaka mwanachama yeyote anahaki ya kugombea nafasi yoyote bila ya kuwa na uwoga wowote ule.

Akizungumza wakati wa kongamano maalum la umoja wa vijana mkoa wa Iringa(UVCCM) kuacha tabia ya kulalamika kuwa wananyimwa nafasi za uongozi lakini kipindi cha uchaguzi vijana hao hawajitokezi kugombea.

Kihongosi alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anawaamini vijana ndio maana kwenye teuzi mbalimbali za serikali,ameteua Zaidi ya asilimia 75 hadi themanini za vijana kwenye kuongoza serikali ya awamu ya sita.

Aliagiza kwa makatibu wote wa UVCCM Tanzania kuacha mara moja kuwabeba wagombea,waache wanachama waamue nani anastahili kuwa kiongozi wa chama hicho ambaye anauwezo wa kuongoza jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.

Kihongosi alisema kuwa hataki kusikia fomu za wagombea zinapotelea ofisini bali fomu zote zinatakiwa kufika sehemu husika ili vikao husika viweze kutoa maamuzi kwa mjibu wa katiba ya chama.

Alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu atasimamia kanuni na sheria za chama hicho ili kupata viongozi bora ambao wataweza kukiongoza chama hicho na wanachama chake kwa kuwa rushwa haina nafasi mwaka huu.

Aidha Kihongosi aliwataka vijana wa umoja huo kucha tabia ya kuwapiga majungu vijana wenzao ili kila mmoja apate nafasi anayostahili kulingana na nafasi anayoishika naanayoigombea.

“Ni marufuku kwa viongozi kupanga safu katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa kufanya hivyo kutapekea chama kupata viongozi wabovu ambao hawastahili kuwa viongozi” alisema Kihongosi

Alisema kuwa mwaka huu ni mwaka wa zoezi la SENSA hivyo wananchi wote wanatakiwa kujitokeza,kuhimizana na kujitokeza kuhesabiwa wakati ukifika ili serikali iweze kujua namna ya kupanga bajeti na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Kihongosi alisema kuwa vijana wanawajibu wa kujitokeza kuhesabiwa na kuhamasisha wananchi wengine kujitokeza kuhesabiwa wakati wa zoezi la SENSA.

Kwa upande wake Katibu wa ccm mkoa wa Iringa Rukia Mkindu amewataka vijana wa umoja wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa (UVCCM) kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kuanzia ngazi ya shina hadi taifa kwa lengo la kuongeza chama hicho.

Mkindu aliwaomba vijana hao kuwa wanapoenda kugombea kuacha tabia ya kupokea na kutoa rushwa kwa kufanya hivyo kutatoa viongozi ambao sio bora kukiongoza chama hicho hapo baadae.

Aidha katibu wa Iringa Mkindu alitumia muda huo kumpongeza katibu mkuu wa umoja wa vijana taifa Kenani Kihongosi kwa kuchaguliwa kuwa katibu mkuu na kufanya kazi kubwa katika umoja huo kwa muda mfupi alipochaguliwa kuwa kiongozi.

Mkindu alimazia kwa kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.

Naye Mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliwataka vijana wa chama cha mapinduzi kuendelea kuelezea mafanikio ya muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo serikali kwa kipindi chote ilivyofanya kazi kuleta maendeleo.

Moyo alisema kuwa vijana wanawajibu wa kuwapinga watu wote ambao wanampango wa kuuvunja muungano kwa nia ovu zao hivyo vijana ndio wanajukumu la kuulinda muungano.

Alisema kuwa vijana wanaoenda kugombea wanatakiwa kuwa wanaccm kweli na sio mamluki wanaopandikizwa kwa lengo la kuja kukivuruga chama hicho hivyo wanatakiwa kuwa makini kwenye chaguzi za chama.

Moyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Iringa hautakubari kuona wagombea wanashinda kwa kutoa rushwa hivyo TAKUKURU itakuwa macho muda wote.

Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi safi ambao watakiongoza chama hicho kwa mafanikio ya kukivusha chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali ambazo chama hicho kitashiriki kutafuta mamlaka ya kuunda serikali.

 

Sunday, April 24, 2022

SABABU ZA MIMBA KUTOKA, VIPODOZI NA KEMIKALI VYATAJWA


KUTOKA Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya Jijini Mwanza, Jembe fm inakukutanisha na Dr. Richard Rumanyika, huyu ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Uzazi na Kizazi ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Tiba Cha Katoliki (CUHAS)

UNYAMA:- MAMA AMZIKA MWANAYE KIMYAKIMYA USIKU BAADA YA KUFA NJAA.

 

mtotopic

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa

Mtoto Salah Jackson (5) mwenye ulemavu wa viungo, mkazi wa kijiji cha Makiwaru, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kutokana na njaa na kisha mama yake mzazi kumzika kimya kimya usiku wa manane.

Mtoto huyo anadaiwa kuzikwa na mama yake mzazi aitwaye Rebecca Siowi (30) usiku wa kuamkia Aprili 22, 2022 nyumbani kwa bibi yake walikokuwa wakiishi yeye pamoja na mama yake baada ya mume kumtelekeza na watoto watano.

Tukio hilo liligundulika baada ya mtoto huyo kutoonekana jioni ya Aprili 21 nyumbani alikokuwa akiishi kwa bibi yake, ambapo bibi yake huyo alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake huyo bila mafanikio ndipo Aprili 22 alipobainika kuwa amezikwa.

Akizungumzia tukio hilo leo Aprili 23, 2022 Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amekiri kuwepo kwa tukio hilo, akisema baada ya kupata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa wananchi walifika eneo la tukio kuona sehemu alipozikwa mtoto huyo.

Kamanda Maigwa amesema walipofika eneo la tukio walilazimika kuomba kibali cha kuufukua mwili wa mtoto huyo ili kujua sasababu hasa za kifo cha mtoto huyo kutokana na maneneo ambayo yalikuwa yakisemwa mtaani.

"Hili tukio kweli lipo na baada ya Jeshi la polisi kupata taarifa juu ya tukio hilo tulienda kuomba kibali cha kufukua mwili wa mtoto ili kujiridhisha sababu za kifo cha mtoto huyo ni nini kutokana na maneno mengi yaliyokuwepo mtaani.


"Tulifukua mwili jana na kuupeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na majibu ya daktari yalipotoka yalionyesha kwamba huyu mtoto alikufa kutokana na njaa,” amesema Kamanda Maigwa

Akizungumzia tukio hilo, jirani wa familia hiyo, Maria Nko amesema hata kama mtoto huyo alikufa kwa njaa mama yake huyo hakupaswa kumzika mwanaye kama mbwa tena usiku wa manane.

"Kwa kweli hili tukio linaumiza na inaonekana huyu mama alikuwa akimtesa huyu mtoto kutokana na ulemavu aliokuwa nao, inakuwaje hao watoto wake wengine hawajafa na njaa na kwa nini amzike mwenyewe tena?” amehoji.