ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 3, 2018

DIAMOND PLATNUMZ, RAYVANY WAFANYA VIDEO YAO YA KWANZA JIJINI MWANZA.

Mapema jana mwanamuziki mahiri barani Afrika anayetikisa dunia Diamond Platnumz ametua jijini Mwanza na kufanya video yake ya kwanza jijini hapa, akitumia lokesheni mbalimbali zinazo litangaza jiji hili la miamba.
Akiwa ameambatana na mkali mwingine kutoka WCB, aitwaye Rayvany, ambaye wameshirikiana katika ngoma mpya wanayoifanyia kichupa, siku za karibuni wanataraji kuwastua wengi kwa pishi waliloliandaa ambalo kwa mujibu wa vyanzo vyetu limelenga burudani zaidi na kuwarusha mashabiki.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akiwakaribisha Diamond Platnumz na Rayvany katika ofisi zake kwaajili ya mazungumzo mafupi.
Kwa kutambua na kuthamini mchango wa sanaa, hasa kazi nzuri ambayo inafanywa na wakali hao, makaribisho yamekuwa ya kipekee sana.
Utambulisho kwa wadau muhimu.












KILICHOTOKEA CHUO CHA UVUVI MWANZA.



GSENGOtV

Jana hali ya hewa ilibadilishwa na Dj mwenye kijiji chake, mitaa ilisimama !! Mbunge kutoka chuo cha Fisheries Mwanza @mustaphakinkulah Mita 500 kutoka kambi ya #JembekaCampusJam ilipo, historia inatengenezwa lakini tarehe 10/11/2018 ndio record zote hadharani.

Jeh inavunjwa au haivunjwi? Tukutane Jembe Beach Resort . 

BREAKING: WATU 7 WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI DODOMA.

Watu 7 wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ya serikali Mbande, mkoani Dodoma, usiku wa kuamkia leo. RPC Gilles Murotto amethibitisha.

Endelea kuwa nasi kwa taarifa kamili

Friday, November 2, 2018

MISHAHARA, KUPANDA KWA MADARAJA,UJENZI NYUMBA ZA WALIMU NI MOJA KATI YA MASUALA YALIYOCHOMOZA MWANZA.



ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

✍🏻.....Maadhimisho ya siku ya waalimu duniani, kitaifa yanafanyika jana jijini Mwanza, baada ya kuahirishwa  kama ilivyo ada kwa miaka yote kufanyika tarehe 05 Oct 2018 kwa maandalizi yake kuingiliwa tukio la ajali ya Mv Nyerere ambayo pia inatajwa kusababisha vifo vya waalimu kadhaa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe Seleman Jafo, amehutubia maelfu ya walimu wa mikoa mbalimbali waliojitokeza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.

Akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, waziri Jafo amefunguka mengi yaliyofanywa kwa walimu na Serikali ya awamu ya 5, chini ya Jemedari Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akisema kuwa siyo yote husemwa hadharani bali mengine kama stahiki za walimu hutendeka kimya kimya.

Suala la kupandishwa madaraja kwa walimu amelizungumzia.

"Hata hivyo nikiri wazi hatutomaliza shida hizi, mwaka huu peke yake, lakini mpango wa Serikali tutafanya kila liwezekanalo kwaajili ya kwenda kutatua matatizo ya walimu....."

BOFYA PLAY KUPATA ALICHOSEMA WAZIRI JAFO KUHUSU MISHAHARA YA WALIMU.....


GOR MAHIA YAPAA KUELEKEA NYUMBANI KWA EVERTON.


Mabingwa wapya wa ligi kuu soka nchini Kenya (KPL), Gor Mahia wameondoka asubuhi ya leo kuelekea nchini Uingereza kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Everton.

Gor Mahia inatarajia kukipiga na Everton usiku wa Jumanne ya wiki ijayo katika uwanja wa Goodson Park.

Pia inaelezwa kuwa moja ya ratiba ya Gor Mahia nchini humo ni kutazama mchezo wa ligi kuu (EPL) kati ya Everton na Brighton & Hove Albion, mchezo utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja huohuo wa Goodson Park.

Mchezo huo ni katika muendelezo wa mashindano ya Sporti Pesa yaliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Agosti yakihusisha vilabu kadhaa vya Afrika Mashariki ili kumpata mshindi mmoja atakayekutana na Everton.

Thursday, November 1, 2018

'KISIWA CHA JUMA WILAYANI UKEREWE CHAPATA UFUMBUZI'



ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Ukerewe ni kisiwa kikubwa kuliko vyote miongoni mwa visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria na pia ni kisiwa kikubwa kuliko vyote miongoni mwa visiwa vyote vilivyomo kwenye maziwa katika bara lote la Afrika. 

Kisiwa hiki kina ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 530. Kisiwa hiki kinaunda wilaya ya Ukerewe ambayo ni moja wapo kati ya wilaya saba za mkoa wa Mwanza. na kipo kilomita 45 kaskazini mwa jiji la Mwanza kikimiliki visiwa vidogo zaidi ya 30. 

Baada ya kumaliza siku tatu za maonesho ya makampuni mbalimbali ya kimataifa yenye kuunda ndege zisizokuwa na rubani, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ambaye ni mmoja ya wadau wakubwa wa mradi huo anasema haya......

 "Kijiografia Mwanza ni kubwa na sifa hiyo inanogeshwa na uwepo wa visiwa zaidi ya 30 vinavyomilikiwa na mkoa wetu, pamoja na juhudi kubwa za Serikali katika kuboresha huduma za mawasiliano ya miundombinu ya barabara na safari ya njia ya maji hivyo kurahisisha huduma nyingine kama biashara na uchumi lakini bado miundo mbinu hiyo haijawa suluhu linapokuja suala la afya ambalo linahitaji dharula ya haraka"


"Baada ya kuumiza kichwa kwa kufikiri tukihangaika kusaka suluhisho la kudumu litakalo harakisha huduma kwenye vituo ili kuepusha vifo vya akinamama na watoto wanaokosa huduma za haraka, tofauti na helkopta na ndege kubwa ambazo zinahitaji gharama kubwa, ndipo likaja wazo hili la kutumia ndege zisizokuwa na rubani yaani drone" ZAIDI BOFYA PLAYA 

KEMI GOES NEXT LEVEL IN THE ART OF DESIGN

 Models shows the fashion work of Kemi
 Models shows the fashion work of Kemi
Models shows the fashion work of Kemi


TANZANIA’s fashion designer, Kemi Kalikawe, has gone next level in fashion designing showbiz after her brilliant performance in many world class events.

The just ended  International Young Fashion Designers Tour at Hyatt Kilimanjaro Hotel in the city proved the designer is now a force to reckon as she parades her designs on the global arena.

The feat earned the designer a huge international appeal, especially in Panama where her rare designs applied to the mixed Central American audience and has drawn a huge number of fans.

The Tanzanian rose high above the huge names in designing during the International Young Fashion Designers Showcase Tour of Dar es Salaam that attracted many internationally acclaimed designers.

Kalikawe, who showcased her designs under Naledi Tanzania  banner, has also participated in the previous fashion shows of Iceland and Panama prior to the Dar es Salaam fashion gala and will go to China for the last show. Her 2 central designs are made from Barkcloth also called 'The Cloth of Kings' a sustainable cloth made from a tree in her home town Bukoba. These center pieces of her collection have stood out in their architectural and yet feminine cuts, inspired by her interior design background.

Others who paraded their designs alongside Kalikawe included Tony Vergara and Veronica Angel from Panama, Hildur Yeoman from Iceland.

Others were Junne Liu and Jarel Zhang from China, Lina Yingzi and Yuzhu from Kanoe while  Mary Yu, Kenny Li, Singchin Lo and Mountain Yam were from Hong Kong.

Also attended  the International Young Fashion Designers Showcase Tour of Dar es Salaam had government officials with the guest of honour being Hon. Mizengo P. Pinda, former Prime Minister of Tanzania. Other officials were Ambassador Ramadhani M. Mwinyi, Mr. Xu Chen, Charge d'affaires ad interim of the Embassy of China in Tanzania, Mr Godfrey Lebejo Mngerza, director of BASATA, Hon Rtd Judge Thomas Mihayo, Chairman of Tanzania Tourists Board (TTB), Mr Joseph Kahama, Secretary General of Tanzania China Friendship Promotion Association and various stakeholder of designing and modeling sectors from in and outside the country.

Kalikawe used this rear international platform to give a chance to   upcome designers to also showcase their work at the opening cocktail event. This opportunity helped to focus on talented youth who can later be promoted to the international level as well.

Delighted with early success, Kalikawe said the international events have promoted her and her works very much and given her a confidence in her career.

“The international level events have opened doors to showcase my designs to the world. I am getting calls from people in Hong Kong interested in buying my work. I feel honoured since I will be able to shine a light on the talent of Tanzania in the design sector. More over each trip has been a journey of sight seeing, cross culture friendship building with fellow designers and wonderful memories. One distinct memory of wander was attending a special dinner in celebration of us designers hosted by at the First Lady of Panama, at the presidential residents, what an honer is was. I look forward to the last stop in China coming soon,” she joyfully said.

This series of the shows have been initiated by Dr. Annie Wu and supervised by an institution called Belt and Road International Young Artist Development Centre and organised by PR Network Hong Kong. The  series of fashion  designing events have been already staged in Reykjavik, Iceland ,Panama City and now in Dar es Salaam. The next event will be in Zhuhai (China).

KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI

Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali akizungumza jambo mbele ya waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda,ikiwemo na kuwapokea wageni wa uwekezaji wa viwanda kutoka nchini China na wenyeji wao kutoka kampuni ya Kiluwa Group Ltd.


MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa (pichani kushoto) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo alipokwenda kuwatambulisha Wadau wake wa Uwekezaji katika masuala ya Viwanda kutoka nchini China,kwa kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),na kueleza mikakati yao mbalimbali waliyonayo kuhusiana na uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania,kulia ni Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali. 
Wawekezaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology kutoka nchini China,wakiwa wameambatana na Mkurugenzi wao Mayi Hong wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo,uliofanyika katika kituo cha Uwekezaji (TIC),jijini Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akisalimia na Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Group,Naima Mohamed Kiluwa,walipokwenda kwenye ofisi za kituo hicho kuwatambulisha wadau wao wa uwekezaji katika mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,anaeshuhudia pichani kati Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na mambo ya uwekezaji wa viwanda hapa nchini Tanzania,maara aada kuzungumza na waandishi wa habara katika ofisi za kituo hicho .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe walipowasili leo kwenda kutambulishwa na Mdau wake Mkubwa kwenye mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.

Wakiwa katika picha ya pamoja

*Dola za Marekani milioni 100 kutumika katika ujenzi 
*Ahimiza Watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yao


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa amesema katika kuhakikisha anaunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za ujenzi wa Tanzania ya viwanda amefanikiwa kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini China kuja kujenga viwanda kuwekeza nchini.

Kiluwa amesema kupitia ushawishi wake na kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wawekezaji hao kutoka China wamekubali kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya bidhaa za ngozi, Kiwanda cha Saa pamoja na Kiwanda cha Simu na kwamba awamu ya kwanza ya uwekezaji huo jumla ya dola za Marekani milioni 100 zitatumika.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa wawekezaji hao Kiluwa amesema viwanda hivyo vitajengwa Mlandizi mkoani Pwani na wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo za vibali ujenzi wa viwanda hivyo utaanza mara moja.Pia amesema mbali ya kujengwa kwa viwanda hivyo wawakezaji hao wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha kubangua korosho mkoani 

Mtwara na kinachoendelea sasa ni mazungumzo ambayo yanakwenda vizuri na hakuna kitakachoshindikana."Wawekezaji hawa wameonesha nia kujenga kiwanda cha korosho na walikuwa tayari kwenda mkoani Mtwara kuona mazingira." 

Kiluwa amefafanua kwenye mazungumzo yake na wawekezaji hao aliwagusia kuhusu zao la korosho nchini na hivyo wamekubali kujenga kiwanda cha korosho.Amezungmzia umuhimu wa wananchi kuwa na uzalendo kwa nchi yao katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa uchumi wa nchi na hasa kuelekea ujenzi waTanzania ya viwanda.

"Tuwe wazalendo kwa nchi yetu kwa kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kujenga Tanzania yenye uchumi imara kupitia viwanda.Ni jukumu letu Watanzania kusimama imara kufanikisha dhamira ya Rais wetu mpendwa,"amesema Kiluwa na kuongeza kwa kutambua malengo ya Rais ameamua kushiriki kwa vitendo kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

"Kushawishi wawekezaji ni kazi ngumu lakini naifanya kwa moyo wangu wote huku nikitanguliza uzalendo kwa taifa langu.Nitoe rai kwa wanaohusika na utoaji wa vibali kuhakikisha wanatoa kwa wakati ili wawekezaji ambao wanakuja kuwekeza waanze shughuli za uwekezaji nchi kwetu,"amesema Kiluwa na kuongeza kuwa anafurahishwa pia na ushirikiano uliopo kati yake na TIC.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka TIC John Mnali amesema moja ya mikakati yao ni kuendelea kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania ambako kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.Pia amefafanua pamoja na kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji nchini wamekuwa wakisaidia kuhakikisha wawakezaji wanapata vibali vyote muhimu vinavyotakiwa katika uwekezaji."Moja ya jukumu letu ni kuwasaidia wawekezaji waweze kupata vibali kwa haraka ili waendelee na uwekezaji."

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong ambaye amesema wamefurashiwa na mazingira mazuri ya uwekezaji ya nchini Tanzania na kutokana na 
mazingira mazuri yamewavutia kuwekeza kwa kujenga viwanda hivyo katika eneo la Mlandizi mkoani Pwani.

"Tutajenga kiwanda cha kuongeza thamani ya ngozi na kisha kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.Pia tutajenga kiwanda cha saa na kiwanda cha simu.Tumetenga Dola za Marekani milioni 100 kwa ajili ya viwanda hivyo.Pia katika mazungumzo yetu na Kiluwa tumejadiliana kuhusu ujenzi wa kiwanda cha korosho na tunaamini tutajenga,"amesema Hong.