ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
✍🏻.....Maadhimisho ya siku ya waalimu duniani, kitaifa yanafanyika jana jijini Mwanza, baada ya kuahirishwa kama ilivyo ada kwa miaka yote kufanyika tarehe 05 Oct 2018 kwa maandalizi yake kuingiliwa tukio la ajali ya Mv Nyerere ambayo pia inatajwa kusababisha vifo vya waalimu kadhaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe Seleman Jafo, amehutubia maelfu ya walimu wa mikoa mbalimbali waliojitokeza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, waziri Jafo amefunguka mengi yaliyofanywa kwa walimu na Serikali ya awamu ya 5, chini ya Jemedari Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akisema kuwa siyo yote husemwa hadharani bali mengine kama stahiki za walimu hutendeka kimya kimya.
Suala la kupandishwa madaraja kwa walimu amelizungumzia.
"Hata hivyo nikiri wazi hatutomaliza shida hizi, mwaka huu peke yake, lakini mpango wa Serikali tutafanya kila liwezekanalo kwaajili ya kwenda kutatua matatizo ya walimu....."
BOFYA PLAY KUPATA ALICHOSEMA WAZIRI JAFO KUHUSU MISHAHARA YA WALIMU.....
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.