ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 27, 2010

ST. AGUSTINO WATUNUKIWA NONDO ZAO LEO!!

MGENI RASMI ASKOFU MTEULE JIMBO KUU LA MWANZA, JUDE THADEUS RUWA'AINCHI AKIMTUNUKU SHAHADA MMOJA WA WANAFUNZI WALIOHITIMU LEO.
Jumla ya wanafunzi 1,735 wa ngazi mbalimbali wametunukiwa shahada ya kuhitimu mafunzo kwenye maafali ya chuo kikuu cha mtakatifu Agustino jijini Mwanza.


Maafali hayo ya kumi na mbili tangu chuo hicho kianzishwe mnamo mwaka 1998 yamefanyika katika viwanja vya Raila Odinga chuoni hapo huku yakihudhuriwa na Umati mkubwa wa ndugu jamaa, marafiki na wanavyuo waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.

Katika hotuba yake Dr. Kitima amewakemea baadhi ya viongozi wachache wenye ubinafsi na wasiojali watoto wa wakulima wanaoishauri serikali kupunguza mikopo kwa wanafunzi elimu ya juu ile hali wazazi wao wakiwa hawajiwezi na kumshukuru Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa kuanzisha mikopo kwa ajili ya elimu ya juu na Rais Kikwete kwa kuiendeleza.

Changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya maendeleo kwa Tanzania ni pamoja na wasomi kutokuwa na sauti katika kufanya maamuzi juu ya mwelekeo kwa uchumi wa nchi, wasomi wengi kuungana na wanasiasa katika kujenga ukuta wa kujitenga na wakulima wa vijijini kwa kuwapa mbinu za kupata mazao mengi ya kutosha bila kuwajengea uwezo wa kupata masoko ya uhakika nje ya nchi.

Sekta hii muhimu ya nyama choma, ndizi na viepe bila kusahau agudu-gudu (mambo ya drinks) yote yalikuwepo viwanjani hapo.

Chuo cha mtakatifu st. Agustino kilianza miaka 12 iliyopita kwa idadi ya wanafunzi 294, leo hii SAUTI pamoja na vyuo vyake vishiriki kina wanafunzi wapatao 20,700. Kikiw a chuo cha pili chenye idadi kubwa ya wanafunzi nchini.

Engo hii ya wahitimu ilingara kweli na rangi zake.

MIE NASEMA:- Hongereni SANA wahitimu wote wa chuo kikuu cha SAUTI Mwanza kwa kutunukiwa NONDO.
NAO WAHITIMU WAKISEMA:- "Shukurani kwa wahadhiri wetu kwa moyo wa kujituma, wafadhili kwa misaada mbalimbali".

BREKING NYUZzz!KAMANDA MUHIDIN MAALIM GURUMO ALAZWA MUHIMBILI.

Mwanamziki mkongwe wa muziki wa dansi Muhidin Maalimu Gurumo alimaarufu kama Anko,kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, amelazwa katika hosptali ya Muhimbili,ward ya Mwaisela namba 5 akiwa anasumbuliwa na matatizo ya mapafu kujaa maji.

Mzee Muhidin Gurumo ni baba mwanzilishi wa bendi ya Nuta Jazz ambayo sasa "Msondo Ngoma Music Band" aka Baba wa Mziki, aka Mambo hadharani.

Anko Muhidini Maalimu Gurumo amekuwa katika medani ya mziki kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950s rasmi mwaka 1960 na akiwa moja ya wanamziki wanzilishi wa Nuta jazz band 1964, kabla ya kubadili jina na kuitwa JUWATA JAZZ ikiwa chini ya chama cha wafanyakazi.

Anko Gurumo ni mwanamziki mtunzi,mwimbaji mkongwe na mbunifu wa mtindo mbali ya dansi kama vile Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae (alipokuwa Mlimani Park) na Ndekule (alipohamia kwa muda Orchestra Safari Sound wana OSS) n.k yeye akiwa ndie anayetoa majina haya.

Mzee Gurumo ni Baba wa mziki wa dansi nchini na pamoja kuwa amewahi kupigia bendi nyingi lakini "Msondo Ngoma Music Band" ndiyo ngome yake.

Ras Makunja na Globu ya Jamii inamwomba Mwenyezi Mungu ampe afueni Kamanda wetu Mzee Gurumo. Na pia wadau wa muziki tujitokeze kumsaidia.


HABARI KWA HISANI YA MICHUZI:

AJALI YA PIKIPIKI USIOMBEE!!!

AKILIA KWA MAUMIVU MAKALI SIKU YA JANA NILIMKUTA JAMAA HUYU KITUO CHA KATI CHA POLISI MWANZA AKICHUKUWA SICK SHEET MARA BAADA YA KUUMIA KATIKA AJALI YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA.
Kasi ya ununuzi wa pikipiki kwa ajili ya kuzikodisha na matumizi binafsi, inazidi kuongezeka huku kukiwa hakuna tahadhari ya kutosha kuhakikisha wanaoendesha vyombo hivyo vya moto, wamepata mafunzo stahiki.
AMEVUNJIKA KABISA MGUU WA KULIA NA KUKIFANYA KIPANDE CHA CHINI KIKINING'INIA KUMAANISHA KUPOTEZA USHIRIKIANO.
TAARIFA kwamba katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, zaidi ya watu 181 wamefariki kwa ajali ya pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda, ni taarifa za mshtuko na si za kubeza. Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abass Kandoro nakumbuka alipata kuzungumza katika wiki ya nenda kwa usalama iliyomalizika mwezi wa nane 2010 alisema vifo vya watu hao vimesababishwa na ajali za pikipiki zaidi ya 1,414 zilizoripotiwa.

Zaidi ya asilimia 80 ya madereva wa daladala, pikipiki, magari binafsi na mabasi yaendayo mikoani, hawana sifa za udereva na mamlaka husika zimefumbia macho tatizo hilo.

Friday, November 26, 2010

STONE CLUB UKIKOSA WIKI HII BASI UMEPISHANA NA RAHA!!


WIKIENDI JAMANI IMEWADIA!!!
RAHA ZIKO STONE CLUB IJUMAA NA JUMAMOSI NI MWENDO WAaaaaaaaaaaa....RAHAaaaaaa!!
HASA UKIZINGATIA KESHO JUMAMOSI WANACHUO WA ST. AGUSTIN WANATUNUKIWA! HA-HAA-HAaaaaa!!
USPITWE NA HII MZEYAA!!

FILAMUCENTRAL BORA ZA 2010


Ikiwa tunaelekea mwisho wa mwaka 2010.kama wadau wa tasnia ya filamu tumeandaa mchakato wa kuchagua FILAMUCENTRAL BORA ZA 2010. Wadau watapata kuchagua filamu na wasanii waliofanya vizuri mwaka huu.Mchakato utaanza tarehe 1/12/2010 hadi 24/12/2010 hadi 24/12/2010.
Kura zitapigwa kupitia www.filamucentral.co.tz na zawadi kem kem zitatolewa kila siku kwa wapiga kura.

Bofya www.filamucentral.co.tz kwa maelezo zaidi

TOP TEN WA UNIQUE MODEL 2010 HII HAPA........

Na hii ndiyo drem team ya Giraffe Unique Model 2010, ambapo jumla ya washiriki kumi wamepita katika mchujo na kuingia kwenye mtanange wa tarehe 24/12/2010.
Majina ya wanamitindo waliopita ni kama ifuatavyo:- Dorah Mhando, Purity Walele, Asia Dachicalorine Mwakasaka, Diana Mainason, Mariam Rabii, Ritah Samwel, Carina Suleiman na Bilkis Suleiman.

Thursday, November 25, 2010

ROBERT CUP LAKE ZONE BASKETBALL LEAGUE YAMALIZIKA.

KUSHOTO NI BUTIMBA SPIDERS, KULIA MWEMBENI TOKA MUSOMA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI.
Fainali za ROBERT CUP LAKE ZONE BASKETBALL LEAGUE zimefanyika jana katika uwanja wa chuo cha ualimu butimba, game hizi zimefanyika baada ya ligi ya mpira wa kikapu ya Robert cup mkoa kumalizika wiki iliyopita na kupata timu 4 kutoka Mwanza zilizoingia hatua ya ligi ya kanda ya ziwa kuungana na bingwa mtetezi wa mwaka jana na timu zingine tatu kutoka mikoa ya shinyanga, Mara na Kagera.
MGENI RASMI WAZIRI MTEULE WA KAZI NA AJIRA MH. GAUDENCIA MUGOZI KABAKA.
Ligi hiyo ilijumuisha jumla ya timu 9 hapa mwanza na timu ya bugando warrious kufanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa ikifuatiwa na bugando heat na tatu ilikuwa butimba spiders, zingine zilikuwa ni st. francis, dolphin pasiansi, SAUT, young saut, young spiders,
Timu nne za juu, warrious, heat, spiders, saut ziliingia hatua ya kanda pamoja na bingwa mtetezi bugando planet, risasi toka shy, kagera combine n a mwembeni musoma.
mgini rasmi alikuwa mlezi wa chama mh. Gaudencia mugosi Kabaka mlezi wa chama cha mpira wa kikapu mkoa.


BINGWA WA MKOA
1. bugando warious - kikombe, medali na sh. laki moja
2. bugando heat - kikombe, medali na 75000
3. butimba spiders- kikombe na 50000
4. mfungaji bora - victor zacharia(heat) - trouphy
5. mchezaji bora(mvp) - eric john (warious) - troughy


BINGWA WA KANDA
1. bugando heat - kikombe, medali, na sh. laki 2
2. bugando warious - kikombe, medali na 1500000
3. bukoba combine - kikombe na 100000
4. mfungaji bora - victor zacharia
5. mvp - ernest shija richard (warious)
Mashindandano yalidhaminiwa na kampuni ya MOIL na familia ya Mama G. kabaka.

HEPI BAZDEI TU YU' ISABELA!!

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA..... MTOTO MZURI MUSOMA NZIMA (WADAU-NATANIAaaaa!!)
NIMEPOKEA SMS TOKA KWAKE ESTER KHERI KUTOKA MUSOMA MKOANI MARA NAYE ANASEMA
"mambo vipi broo,leo ni birthday ya ma luv friend isabela nshama"

PPF KUTOA SEMINA KWA WAAJIRI KANDA YA ZIWA VICTORIA.

Katika kumkwamua mfanyakazina adha aipatayo ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha kutokana na kutokuwa na kipato cha kutosha kuweza kujikimu na maisha mara baada ya kuondoka kwenye ajira, Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF kanda ya ziwa umeamua kukutana na waajiri kwania ya kuwapatia semina ili watambue umuhimu na wajibu wao kisheria wa kuandikisha wafanyakazi wao.
Meneja wa PPF kanda ya ziwa bw.Meshark Bandawe amesema kuwa moja ya changamoto kubwa inayoikabili sekta nzima ya hifadhi ya mfuko huo wa jamii ni waajiri wengi kutofikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Sambamba na kutoa darasa kwa waajiri hao bw. Bandawe amesema kuwa semina hiyo itatoa maelezo kwa kina juu ya huduma mpya zitolewazo na mfuko huo, kuvielezea vitega uchumi vilivyopo sambamba na kupokea ushauri na mapendekezo juu ya utoaji wa huduma za PPF kanda ya ziwa kwa nia ya kuziboresha hivyo kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.

SEMINA HIYO YA KANDA YA ZIWA KATI YA PPF NA WAAJIRI INATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 29NOVEMBER 2010 LAKAIRO HOTEL JIJINI MWANZA.

Wednesday, November 24, 2010

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI TANZANIA.

Rais Kikwete amewaacha mawaziri kadhaa wa zamani na kuteua sura mpya kama vile Profesa Anna Tibaijuka.

1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe

Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira

2.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia

3. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano) Samia Suluhu

2. Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa

4. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi

2. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu

5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika

- Naibu: Aggrey Mwanri

- Naibu: Kassim Majaliwa

6. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo

- Naibu: Gregory Teu

- Naibu: Pereira Ame Silima

7. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha

- Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki

8. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani

9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi

10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi

11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo

- Naibu: Benedict Ole Nangoro

12. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

- Naibu: Charles Kitwanga

13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye

14. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige

15. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima

16. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli

- Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe

17. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu

- Naibu: Athumani Mfutakamba

18. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami

- Naibu: Lazaro Nyalandu

19. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa

- Naibu: Philipo Mulugo

20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda

- Naibu: Dr. Lucy Nkya

21. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga

22. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba Umi Ali Mwalimu

23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi

- Naibu:Dr. Fenella Mukangara

24. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta

- Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah

25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe

- Naibu: Christopher Chiza

26. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya

- Naibu: Eng. Gerson Lwinge

Tuesday, November 23, 2010

BAYLOR YATOA MSAADA KWA HOSPITALI ZA MWANZA.

SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI BAYLOR LA TEXAS NCHINI MAREKANI LEO ASUBUHI LIMETOA VIFAA MBALIMBALI VYA HOSPITALI KWA VITUO 9 VYA AFYA MKOANI MWANZA VITAKAVYOTUMIKA KUTOA MATIBABU KWA WATOTO WALIOATHIRIKA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI ILI WAWEZE KUENDELEA KUISHI WAKIWA NA AFYA NJEMA.

MD WA BAYLOR MR.MAGIMBA AKIELEKEZA MATUMIZI KWA 1 YA VIFAA HIVYO.

MKURUGENZI WA SHIRIKA HILO BW. AYOUB MAGIMBA AMEVITAJA VITUO VYA AFYA VILIVYOKABIDHIWA VIFAA HIVYO KUWA NI HOSPITALI YA MWANANCHI, HOSP. YA WILAYA YA NYAMAGANA, HOSP. YA WILAYA YA MISUNGWI, HOSP. YA BUKUMBI, HOSP. YA WILAYA YA MAGU, HOSPITALI YA JESHI, HOSP. YA WILAYA YA KWIMBA, KITUO CHA AFYA KISESA PAMOJA NA KABILA.

VIFAA HIVYO VILIVYOKABIDHIWA LEO INAKADIRIWA KUWA VIMEGHARIMU KIASI CHA ZAIDI YA SHILINGI MILLIONI 18 ZA KITANZANIA.

MKURUGENZI WA SHIRIKA HILO BW. AYOUB MAGIMBA AMEVITAJA VITUO VYA AFYA VILIVYOKABIDHIWA VIFAA HIVYO KUWA NI HOSPITALI YA MWANANCHI, NA HOSP. YA WILAYA YA NYAMAGANA.

VITUO VINGINE NI HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI, HOSP. YA BUKUMBI, HOSP. YA WILAYA YA MAGU, HOSPITALI YA JESHI, HOSP. YA WILAYA YA KWIMBA, KITUO CHA AFYA KISESA PAMOJA NA KABILA.

MKURUGENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO DK. CHARLES MAJINGE AMESEMA KUWA MBALI NA IDARA ZAKE KUJIPANGA VYEMA KUHAKIKISHA KUWA MISAADA YOYE INATUMIKA KAMA ILIVYODHAMIRIWA PIA HOSPITALI HIYO HIVI KARIBUNI INATARAJIA KUZINDUA KITUO CHA KUHUDUMIA WATOTO KANDA YA ZIWA KILICHOPO KARIBU NA HOSPITALI HIYO.

BAYLOR COLLEGE OF MEDICINE CHILDREN'S FOUNDATION-TANZANIA IS REGISTED, TANZANIA NON-GOVERNMENT ORGANISATION (NGO) SUPPORT THE ENHENCED SCALE-PU OF PEDIATRIC AND ADOLESCENT HIV/AIDS PREVENTATION, CARE AND TREATMENT SERVICES IN TANZANIA SPECIFICALLY IN THE SOUTHERN HIGHLANDS AND LAKE ZONES.

Monday, November 22, 2010

AIR JETLINK EXPRESS YAZINDULIWA MWANZA.

WAZIRI MKUU WA KENYA BW.RAILA ODINGA LEO AMEFANYA ZIARA FUPI MKOANI MWANZA NCHINI TANZANIA KWA NIA YA KUZINDUA HUDUMA YA USAFIRI WA ANGA KUPITIA SHIRIKA LA NDEGE ZA JETLINK YA NCHINI KENYA.

UZINDUZI HUO UMEHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SEKTA YA ANGA TOKA NCHI YA KENYA IKIWA NI PAMOJA NA WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI KENYA BW.AMOS KIMUNYI.

MSAFARA WA WAZIRI ODINGA ULIPOKELEWA NA NGOMA ASILI TOKA VIKUNDI MBALIMBALI MAARUFU JIJINI MWANZA.

NGOMA HII YA DOGOLI TOKA UKEREWE ILIMVUTIA SANA MH.RAILA, HALI ILIYOPELEKEA KUKAWIA KUONA ZAIDI MAUFUNDI YA UCHEZAJI.

WAZIRI MKUU WA KENYA BW.ODINGA AKISALIMIANA NA MBUNGE WA ROLYA (CCM), MH.LAMECK AIRO.

MAPOKEZI NA TUNUKU YA MAUA.

BW.ODINGA AMESEMA KUWA HUDUMA HIYO SIYO KWAMBA ITASAIDIA KUSUKUMA TU SEKTA YA BIASHARA NA WAWEKEZAJI BALI PIA ITAKUWA NYONGEZA KTK KURAHISISHA KUTAMBULISHA SEKTA YA UTALII WA TANZANIA HUSUSANI MKOA WA MWANZA, KWA WATALII KUFIKA KWA URAHISI MBUGA ZA SERENGETI KUJIONEA MALIASILI ZA UTALII NA HIVYO KUKUZA UCHUMI NA PATO LA NCHI.

NDANI YA TABASAMU AIR JETLINK DADAz.

MKUU WA MKOA WA MWANZA BW.ABASS KANDORO KWA PAMOJA NA WAZIRI MKUU WA KENYA BW.RAILA ODINGA WAKIKATA KEKI YA AIR JETLINK EXPRESS.

WADAU WA SEKTA YA ANGA MWANZA.

NDANI YA HAFLA HIYO WAFANYABIASHARA WA JIJI LA MWANZA NAO WALIPATA FURSA YA KUMZAWADIA ZAWADI WAZIRI MKUU WA KENYA.

WAKIPIGA CHIAAAAZzzz! KUASHIRIA MAKUBALIANO YA PAMOJA.

CAPTAIN MAREMO.


MPANGO HUO WA HUDUMA NI FARAJA KWA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA KUPANUKA HIVYO KULETA TIJA KUFANIKISHA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI. AIR JETLINK EXPRESS NDEGE YA PILI KWA UTOAJI HUDUMA YA USAFIRI WA ANGA NCHINI KENYA ITAKUWA IKITOA HUDUMA ZAKE MWANZA, KISUMU NA NAIROBI.