ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 27, 2010

ST. AGUSTINO WATUNUKIWA NONDO ZAO LEO!!

MGENI RASMI ASKOFU MTEULE JIMBO KUU LA MWANZA, JUDE THADEUS RUWA'AINCHI AKIMTUNUKU SHAHADA MMOJA WA WANAFUNZI WALIOHITIMU LEO.
Jumla ya wanafunzi 1,735 wa ngazi mbalimbali wametunukiwa shahada ya kuhitimu mafunzo kwenye maafali ya chuo kikuu cha mtakatifu Agustino jijini Mwanza.


Maafali hayo ya kumi na mbili tangu chuo hicho kianzishwe mnamo mwaka 1998 yamefanyika katika viwanja vya Raila Odinga chuoni hapo huku yakihudhuriwa na Umati mkubwa wa ndugu jamaa, marafiki na wanavyuo waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.

Katika hotuba yake Dr. Kitima amewakemea baadhi ya viongozi wachache wenye ubinafsi na wasiojali watoto wa wakulima wanaoishauri serikali kupunguza mikopo kwa wanafunzi elimu ya juu ile hali wazazi wao wakiwa hawajiwezi na kumshukuru Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa kuanzisha mikopo kwa ajili ya elimu ya juu na Rais Kikwete kwa kuiendeleza.

Changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya maendeleo kwa Tanzania ni pamoja na wasomi kutokuwa na sauti katika kufanya maamuzi juu ya mwelekeo kwa uchumi wa nchi, wasomi wengi kuungana na wanasiasa katika kujenga ukuta wa kujitenga na wakulima wa vijijini kwa kuwapa mbinu za kupata mazao mengi ya kutosha bila kuwajengea uwezo wa kupata masoko ya uhakika nje ya nchi.

Sekta hii muhimu ya nyama choma, ndizi na viepe bila kusahau agudu-gudu (mambo ya drinks) yote yalikuwepo viwanjani hapo.

Chuo cha mtakatifu st. Agustino kilianza miaka 12 iliyopita kwa idadi ya wanafunzi 294, leo hii SAUTI pamoja na vyuo vyake vishiriki kina wanafunzi wapatao 20,700. Kikiw a chuo cha pili chenye idadi kubwa ya wanafunzi nchini.

Engo hii ya wahitimu ilingara kweli na rangi zake.

MIE NASEMA:- Hongereni SANA wahitimu wote wa chuo kikuu cha SAUTI Mwanza kwa kutunukiwa NONDO.
NAO WAHITIMU WAKISEMA:- "Shukurani kwa wahadhiri wetu kwa moyo wa kujituma, wafadhili kwa misaada mbalimbali".

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.