ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 30, 2018

SASA NI KOMBE LA DUNIA BILA MESSI WALA RONALDO.


.....Ulimwengu hii leo umeshuhudia tukio kubwa la simulizi dunia, kwa mastaa wa Modern football Messi na Ronaldo kuiaga #Urusi .
FT #France 4-3 #Argentina
FT #Uruguay 2-1 #Portugal .
.
Wakali wa mambo wanasema huenda ikawa mwisho wa utawala wao Jeh nawe unamaoni gani? #SportsRipoti @elikanamathias & @danyajr_219

UFARANSA V ARGENTINA
Ufaransa imetua robo fainali ya Kombe la Dunia mara ya pili mfululizo na kubadili historia kufuatia ushindi kwenye mchuano wa kuvutia uwanjani Kazan dhidi ya Argentina.

Argentina, iliyokuwa na baadhi ya wachezaji bora duniani, Lionel Messi na Diego Maradona ugani Kazan, mmoja akicheza mwingine akiwashangilia, wameliaga Kombe la Dunia Urusi 2018.

Mabao ya haraka ya Kijana chipukizi Kylian Mbappe kipindi cha pili yameipa Les Bleus tiketi ya robo fainali Urusi 2018.

Ufaransa inamsubiri mshindi kati ya Uruguay na Ureno watakaokwatuana baadaye.

Ufaransa iliingia mechini vyema kwa kuchukua uongozi baada ya mlinzi Marcos Rojo kumuangusha Mbappe.

Griezmann alitandika Penalti hiyo na kujaa kimiani (dakika ya 13).

Hata hivyo, dakika chache kabla ya kipindi cha pili, Angel Di Maria aliisawazishia Argentina kwa shuti la ajabu kutoka yadi 30 na kumaliza kipindi cha pili kwa sare 1-1.

Punde tu pande hizo ziliporejea kutoka mapumziko, beki Gabriel Mercado aliinyakulia Argentina uongozi (Dakika ya 48) baada ya kuulekeza mkwaju wa Messi langoni.

Sherehe za Albiceleste zilikatizwa baadaye kwani uzembe wa ngome yake ilimruhusu beki Benjamin Pavard, aliyekuwa akishiriki mechi yake ya tisa kwa timu ya taifa, kuisawazishia Ufaransa. Pavard alifunga Dakika ya 58.

Ngoma ilionekana kumalizika sare kabla ya nyota wa PSG Mbappe kuidunisha Argentina kwa mabao ya haraka dakika za (64) na (68) na kuwainua mashabiki wa Ufaransa kutoka viti vyao.

Lionel Messi alijaribu kupunguza madeni ya Argentina kufuatia mabao hayo lakini mbio zake kwenye sanduku ziliandamwa na shuti lake dhaifu hadi kwa viganja vya mdakaji wa Ufaransa Lloris.

Argentina bao la tatu

Hata hivyo dakika chache baadaye Messi hakuchelea kumlisha Aguero naye nguvu huyo mpya, Kun Aguero alipiga kichwa safi dakika ya 92 na kukaribia kufufua matumaini ya Argentina.

Muda haukuwa na huruma kwa Argentina na kipute kilikamilika ushindi ukienda kwa Ufaransa.


Mjadala wa ni nani bora kati ya Messi na Ronaldo benchi kwa sasa.

Argentina na Ureno wameliaga Kombe la Dunia.

Ukurasa mpya umefunguliwa kwa mashabiki wa soka duniani kuhusu ubora wa wachezaji maarufu wa soka.
Ingawa kila mwamba ngoma, ngozi huivutia kwake, ukweli ni kuwa, wachezaji wapya wametumia vyema jukwaa lililopatikana Kombe la Dunia Urusi 2018.
Baada ya kutawala vinywa vya wengi ndani ya zaidi ya kipindi cha miaka 10, kuondoka kwa Argentina na Ureno Urusi hatua za mchujo, imewanyima Messi na Ronaldo muda zaidi wa kujadiliwa.
Kurunzi za soka sasa zimeelekezwa kwa Neymar wa Brazil, Paul Pogba, Kylian Mbappe na Antoine Griezmann wa Ufaransa, Edison Cavani na Luis Suarez wa Uruguay, Harry Kane wa Uingereza na Romelu Lukaku wa Ubelgiji.
Orodha ni ndefu, lakini yote yataamuliwa kulingana na mchango wa wachezaji hawa kwa ufanisi wa timu zao.

"SERA YA SERIKALI YA VIWANDA ISITUMIKE KAMA MWANYA WA UANZISHWAJI VIWANDA BUBU' - WASEMA WADAU



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Kakika juhudi za kumuunga mkono RAIS MAGUFULI kuelekea tanzania ya viwanda, Serikali imeombwa kuwajengea uwezo wajasiriamali na kuondoa bidhaa feki kwenye soko pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wanaonakili nembo na uzalishaji wa bidhaa zao  kinyume cha sheria.

Kilio hicho kimetolewa na wafanyabishara wa jijini Mwanza wanaozalisha vinywaji aina ya Wine zinazotokana na matunda pamoja na mtama.

Aidha meneja wa (TFDA) kanda ya ziwa MOSES MBAMBE,amewataka wananchi  kutoa ushirikiano pale wanapoona bidhaa ambayo wanaitilia sahaka nakuwataka wajasilia mali kurasimisha bidhaazao ili zitambulike na (TFDA) pia mbambe amesema kwa sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wajasiliamali wa kanda ya ziwa.

Mkurugenzi wa kiwanda cha Mwanza quality wine Leonald Lema amesema kuwa   mamlaka zinazohusika zinapashwa kuingilia kati kwani bidhaa feki zinawaathiri wao pia maptao kodi ya serikali.

Aidha LEMA amebainisha kuwa kiwanda chake hakina tatizo la vifungashio tatizo ambalo limekuwa likipigiwa kelele kuwa bidhaa nyingi hapa nchini zinakosa ubora katika ushindani kwenye soko ukilinganisha na bidhaa toka nje.

Naye Mkurugenzi wa FARU WINES Japhet Daniel amesema kuwa serikali kwa kutumia mihili yake inaweza kuwatambua wajasiriamali wasio sajiliwa kutumia vifungashio vya bidhaa za FARU BANANA.

RC MAKONDA ATANGAZA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA WALIOMALIZA MAFUNZO YA JKT NA MGAMBO*.


NA ZEPHANIA MANDIA GSENGOtV

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda* amewataka Vijana waliomaliza mafunzo ya JKT na Mgambo na hawana *kazi* kufika ofisini kwake Ijumaa ya July 06 kwaajili ya kupatiwa ajira ya kusimamia usafi na kuwatoza faini* vinara wa uchafuzi wa mazingira.

RC Makonda amesema katika fedha itakayotozwa kwa wachafuzi wa mazingia 50% itaenda kwenye Halmashauri na 50% kwa vijana wa JKT na Mgambo ambapo kabla Vijana hao hawajakabidhiwa jukumu hilo watapewa*mafunzo ya Sheria ya Usafi.

Huu ni Ubunifu Mkubwa aliofanya RC Makonda katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana sambamba na kuufanya mji kuwa katika hali ya usafi baada ya mbinu nyingi zilizokuwa zikitumiwa  kuhamasisha usafi kutokuwa na matokeo mazuri lakini kwa hii RC Makonda tunaenda kuona Dar es salaam ikiwa Safi. 
Aidha RC Makonda ameagiza makampuni yote yaliyopewa tenda ya usafi Dar es salaam kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata na Halmashauri kufika ofisini kwake Jumatano ya July 04 wakiwa na mikataba yao kwaajili ya kujiridhisha uwezo wao wa kufanya kazi baada ya uchunguzi aliofanya kubaini uwepo wa kampuni zilizopewa tenda Kubwa wakati hawana vifaa vya kutosha.

Hata hivyo RC Makonda ameziagiza Manispaa zote za jiji hilo kuhakikisha kila mfanyabiashara na vituo vya daladala vinakuwa na Sehemu ya kuweka taka (dustbin).

Pamoja na hayo RC Makonda ametangaza fursa kwa wadau wenye vyoo vya kuhama (mobile toilet) kufika ofisini kwake ili wakutanishwe na halmashauri ili waweke makubaliano ya ushirikiano ili kuondoa tabia ya watu kujisaidia kwenye kuta na vichochoro.

Miongoni mwa majukumu ya Vijana hao ni kuhakiki makampuni kwenye mitaa kama yapo na yanafanya kazi kweli, kujua wananchi wanapeleka wapi takataka, kukamata watupaji wa taka na kuwatoza faini ambapo Kama huna pesa utapewa adhabu ya kufanya usafi wiki nzima chini ya usimamizi mkali.

MMILIKI WA MABASI YA ZACHARIA AKAMATWA BAADA YA KUSHAMBULIA MAAFISA USALAMA KWA RISASI



NEWS: Mmiliki wa Mabasi ya Zacharia, Peter Zacharia amekamatwa baada ya kuwashambulia kwa riasi maofisa Usalama walikwenda kumkamata.

Mkuu wa Mkoa wa Mara amethibitisha (Tizama video).

DRC YAADHIMISHA MIAKA 58 YA UHURU,CENCO IKITILIA SHAKA UCHAGUZI.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 58 ya uhuru wake ilioupata kutoka kwa waliokuwa wakoloni wa taifa hilo nchi ya Ubelgiji, June 30, 1960.
Maadhimisho haya yanafanyika wakati huu Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki CENCO likielezea wasiwasi wake kuhusu mchakato wa Uchaguzi unaopangwa kufanyika mwezi desemba mwaka huu.
Akihutubia taifa kupitia televisheni inayomilikiwa na serikali , rais Joseph Kabila amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ilivyopangwa na CENI huku akiwataka kujitokeza kuunga mkono na kushiriki zoezi la uchaguzi.
Aidha Gavana wa jimbo la kivu kaskazini Julien Paluku amethibitisha kuachwa huru kwa wafungwa 60 kutoka gereza kuu la Goma munzenze,kufuatia msamaha wa raisi katika maadhimisho haya.
Drc inafanya maadhimisho hayo huku ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo umasikini,ukosefu wa usalama katika eneo la mashariki mwa nchi na hofu ya ikiwa uchaguzi mkuu utafanyika kama ilivyopangwa kufanyika Desemba mwaka huu.

RC MAKONDA APOKEA SHEHENA YA VIFAA VYA MATIBABU KUTOKA KOREA KUSINI.

 NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo amepokea *shehena ya Vifaa vya matibabu* vyenye thamani ya shilingi *milioni 100* kutoka serikali ya *Korea Kusini* kupitia shirika la *KOICA*.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na *Digital X-ray 3, Ultrasound 1, Kabati la usalama wa viumbe* (safety cabinet) 1, *Mashine 3 za kupima mkojo, mashine ya kuwapa joto watoto njiti* (baby warmer) pamoja na *mashine ya utakitshaji.*
 Baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa *Balozi wa Korea kusini Bwana Geum Young Song RC Makonda* amekabidhi vifaa hivyo kwenye *vituo vya Afya vya Sinza, Mnazi Mmoja na Mbagala* ambako kuna uhaba wa vifaa. 

 Kabla ya kupokea vifaa hivyo *RC Makonda* alifanya *mazungumzo* na *Balozi* huyo wa Korea kusini na kuwasilisha *ombi la kujengwa kwa Chuo cha kisasa cha mafunzo ya udaktari na uuguzi* ambapo *Balozi Geum Young Song amepokea kwa mikono miwili ombi hilo.*
 *RC Makonda* pia amemueleza Balozi ombi la kujengwa kwa *kituo kikubwa cha upimaji wa magonjwa mbalimbali* kwa wananchi kwenye *eneo moja* ambapo pia Balozi *amepokea* ombi hilo na kumsifu *RC Makonda* kwa moyo wake wa kujali wananchi. 



Kwa upande wake *Balozi* wa Korea Kusini nchini Tanzania *Bwana Geum Young Song* amesema wametoa vifaa hivyo *kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Dar es salaam katika uboreshaji wa sekta ya Afya* na wataendelea kusaidiana na serikali.

MAMBO MUHIMU YANAYOPATIKANA KATIKA RIPOTI YA UTAFITI WA UHISANI NCHINI ILIYOANDALIWA NA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Mchambuzi na mwandishi wa ripoti ya utafiti wa Uhisania Tanzania Bw. Tom Were akiichambua ripoti hiyo mapema jana jiji Dar es salaam.

Watanzania wametakiwa kuwa na moyo wa kutoa kwa kusaidiana wenyewe ndani ya jamii na hata katika kuendeleza huduma mbalimbali za kijamii ili kuweza kusaidia taifa kusonga mbele.


Hayo yamesemwa mapema jana jijini Dar es salaam na Mwanachama wa Bodi ya wakurugenzi ya Foundation for Civil Society Bi. Nesia Mahenge wakati wa uzinduzi wa riporti ya utafiti maalum kuhusu uhisani na utamaduni wa kujitolea ndani ya Tanzania.

Ripoti hiyo iliyohusisha utafiti uliofanywa kati ya mwezi februari hadi mwezi aprili na kuhusisha mashirika ya Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na Jukwaa la Uhisani Tanzania (Tanzania Philanthropy Forum) kwa lengo la kupata taarifa muhimu kuhusu hali ya uhisani au hali ya kujitolea kwa jamii nchini Tanzania.
Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Foundation for Civil Society Nesia Mahenge akielezea kwa undani mambo yanayopatikana katika ripoti hiyo ya Utafiti wa Uhisani nchini Tanzania.

Mwanachama wa bodi huyo alisisitiza umuhimu wa mtu mmoja mmoja  pamoja na taasisi mbalimbali binafsi hususani zinazofanya kazi za kijamii kuendelea kujitolea katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kuacha tabia ya kuisubiri serikali kufanya kila kitu.

Aliendelea kusisitiza kuwa ni vema kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo ikiwa ni moja wapo ya njia nzuri ya kuisaidia serikali katika kuinua miradi kadhaa ikiwemo Elimu, Afya, Ujenzi na sio kwa kuwezesha kifedha tu lakini hata katika kusaidia kuleta wahisani watakao fanikisha zoezi hilo pia ni hatua kubwa.

“Lakini pia katika hali ya kujitolea kwa Tanzania uelekeo wake sio mbaya sana kwani watanzania wanaonyesha kuwa wana moyo wa kutoa kwa kusaidiana, lakini pia hata katika juhudi za kujiletea maendeleo kwa kusaidia huduma mbalimbali za kijamii hali inaonyesha bado tupo vizuri” alisema Nesia
Wachambuzi wakiichambua Ripoti ya Utafiti wa Uhisani Tanzania 

Aliongezea kwamba tatizo moja linalojitokeza katika nchi yetu ni kwamba kunakosekana takwimu/taarifa sahihi za watu wanaojitolea lakini zingekuwepo ingesaidia kujua kiwango husika cha watu wanaojitolea katika miradi ndani ya jamii yao na hii inatokana na sharia na mifumo iliyowekwa ndani ya nchi yetu.

Na mwisho alipenda kuwashauri wadau kutumia matokeo ya utafiti huu kama sehemu ya kubadilishana uzoefu katika tasnia nzima ya uhisani na kujitolea katika jamii na kuhamasisha umuhimu wa uhisani miongoni mwa jamii ya watoaji pia kuweka muongozo wa kuendeleza uhisani Tanzania.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini uchambuzi wa Ripoti ya uhisani Tanzania iliyozindiliwa na Foundation for Civil Society mapama jana jijini Dar es salaam.

WAZIRI PROF. NDALICHAKO KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA WANASAYANSI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Andrea Pembe akizungumza na Waandishi wa habarai juu ya Kongamano lake la sita la Kisayansi tarehe 2 na 3 Julai 2018. Kongamano hili litafanyika katika ukumbi wa LAPF Millenium Tower, jijini Dar es Salaam.

Ofisa Uhusiano wa Muhas akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mkutano huo utakaoanza jumatatu.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako anataraji kuwa mgeni rasmi katika kongamano la sita la kisayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) litakalofanyka tarehe 2 na 3 Julai 2018 katika ukumbi wa LAPF Millenium Tower, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Andrea Pembe amesema jukumu mojawapo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MUHAS) ni kutoa mafunzo ili kujenga rasilimali watu ya fazi za afya, kufanya tafiti na kushiriki kikamilifu utoaji huduma za afya kwa umma.

Amesema ili matokeo ya tafiti zinazofanywa yaweze kutumiwa na watekelezaji, wadau, wafanyakazi wa huduma za afya na wengine wanaofanya kazi katika maeneo husika ya kitaalamu, matokeo ya tafiti hizi hayana budi yasambazwe kwa ufanisi. 

“Hivyo basi, madhumuni ya kongamano hili la sita ni kushirikiana, kuelezana, kujifunza na kubadilishana ujuzi unaotokana na matokeo ya tafiti kati ya watafiti mbali mbali, watoa huduma wa afya, watekelezaji wa mikakati na sera mbalimbali na wadau wengine wote ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kushirikisha jamii kwa ujumla kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Katika Kongamano hili, Chuo kitaeleza mafanikio ya tafiti na athari zake kwa upande wa kijamii na maendeleo ya uchumi wa nchi. Katika Kongamano la sita la kisayansi, Chuo kitaonyesha matokeo ya tafiti za hivi karibuni ya kisayansi kutoka miradi mbali mbali ya tafiti zinazotoka ndani na nje ya nchi katika kipindi cha miaka ya nyuma. 

Kitu cha muhimu zaidi katika jamii ya wanataaluma wa MUHAS ni kuwa watapata fursa ya kushiriki matokeo yao na kubadilishana mawazo na wataalamu pamoja na wadau kutoka sehemu mbalimbali za nchi na duniani kote ikiwa lengo kuu ni kuboresha afya kupitia tafiti” amesema Prof. Pembe.

Amesema kuwa kauli mbiu ya Kongamano hili ni “Uimarishaji wa Uchumi wa Viwanda kupitia Tafiti za Afya kwenye nchi zenye kipato cha chini”. Kauli mbiu hii imechaguliwa mahususi kusisitiza umuhimu wa matumizi ya matokeo ya tafiti za Kisayansi za afya katika kuchangia uimarishaji wa uchumi wa viwanda hapa Tanzania na chi nyingine zenye uchumi wa kipato cha chini. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ili kuimarisha uchumi wenye viwanda Taifa linatakiwa kuwa na majibu ya changamoto zinazokabili sekta ya Afya na kuboresha ukuaji wa uchumi.

Ametaja kuwa katika kongamano hili Makala za kisayansi 164 zitawasilishwa kwa njia ya maongezi (Oral Presentations). Makala zitakazo wakilishwa zimeangukia katika mada ndogo ndogo zifuatazo:

Tafiti za Afya ya Uzazi,Tafiti wa Magonjwa yasiyoambukiza, Tafiti wa Magonjwa yanayoambukiza,Utafiti wa Msingi katika Maswala ya Afya, Tafiti za Sera na Mifumo ya Afya, Tafiti za Teknolojia ya Habari mawasiliano pamoja na Afya, Tafiti za Afya ya Kinywa, Tafiti za Tiba Asili na Tiba Mbadala, Huduma za Dawa za Tiba,Tafiti za Maswala ya Jinsia na Afya.

Amesema jumla ya washiriki na wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchini na nje ya nchi kutoka nchi za Rwanda, Uingreza, Japan, Uturuki, Italy na Marekani.

DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA

6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
*****************
Na Emmanuel J. Shilatu

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote.
...
*Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa.

Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1.

*Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro.

*Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo ajira nyingi za Waalimu na Madaktari zitazalishwa.

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa amewasili nchini Tanzania Alhamis Juni 28, 2018 kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Hayo ndio matunda ya Tanzania kuimarika kwenye mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo, matunda ya ziara ya Rais wa Zimbabwe nchini Tanzania.

Pongezi kwa Rais Magufuli na Rais Mnangagwa kwa kujenga historia mpya.

*Shilatu E.J*
0767488622

Friday, June 29, 2018

KUANZIA TAREHE 2-6 JULY 2018 MBUNGE WA ILEMELA AJA NA ZOEZI LA KUPIMA AFYA BURE


TANGAZO

Mhe. Dkt Angelina Mabula Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilemela na Timu ya Madaktari toka Chuo Kikuu cha Tiba Cha California Marekani anawatangazoia wananchi wote wa Manispaa ya Ilemela kuwa kutakuwa na Upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa wanawake wote na Upimaji wa VVU kwa hiari kuanzia Tarehe 02 – 06/07/2018 kuanzia saa 2 asubuhi HADI saa 10 jioni.

Huduma hii itatolewa katika Vituo vya Afya vya Sangabuye na Buzuruga.

Hakuna Gharama wala Malipo yoyote.

TANGAZO LIMETOLEWA NA

MKURUGENZI WA MANISPAA
ILEMELA.

MADADA POA SASA WANAMIMINIKA VIJIJINI KUVUNA KWENYE MIFUKO YA WAKULIMA



GSENGOtV
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana la KIVULINI Yasini Ally amesema haiingii akilini kwa mkulima aliyeuza mazao yake na kupata mamilioni ya fedha ashindwe kununua hata godoro, zaidi ya kukimbilia kununua magodoro yaliyotengenezwa kienyeji kwa kutumia mifuko ya magunia ya saflet iliyoshindiliwa makapi ya majani ya mpunga.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliurd Mwiteleke  amesema kuwa Halmashauri yake inatarajia kuanza kampeni maalum inayolenga kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, wanawake na wazee ambayo itakayodumu kwa kipindi cha miezi miwili.

Kauli hiyo inatoka ndani ya kongamano la mafunzo ya jinsi ya kubaini na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii lililoandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI shughuli ikifanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Misungwi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kitaifa wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia.
 Wadau mbalimbali hapa wanapata fursa ya kuchangia.
 Sehemu ya kusanyiko mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Idara, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani, Mahakama, Polisi pamoja na Sungusungu.
 Kwa umakini elimu inapenya kwa wadau.
 Kusanyiko na tafakari.
 Kwa umakini elimu inapenya kwa wadau.
 Kwa umakini elimu inapenya kwa wadau.
 Wadau wa mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliurd Mwiteleke, wakati akiwasilisha mada kwenye darasa.
Wadau waliketi kulingana na vitengo vyao ni wasaa wa kuainisha changamoto, kujenga hoja na kuweka mikakati.

Thursday, June 28, 2018

HUWENDA HUU UKAWA MWAROBAINI KWA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO WAFANYAO KAZI ZA MAJUMBANI


NA ZEPHANIA MANDIA / G.SENGO TV.

SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA TDWC, LIMETOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA KUWAJENGEA UWEZO WA JINSI YA KURIPOTI TAARIFA NA UFUATILIAJI WAKE HATUA KWA HATUA IKIWA NI PAMOJA NA JINSI YA KUZIBAINI CHANGAMOTO WALIZONAZO WATOTO WAFANYAO KAZI ZA MAJUMBANI.

JOSEPHAT MWANZI,NI MWALIMU WA MAFUNZO HAYO AMESEMA TATIZO LA UNYANYASAJI WATOTO WAFANYAO KAZI ZA NDANI BADO NI KUBWA,TAKWIMU ZINAONYESHA TANZANIA BARA NA VISIWANI IDADI NI KUBWA KWA ZAIDI YA WATOTO 12OO WANAFANYAKAZI ZA NDANI KUISHI KATIKA BWIWI LA MANYANYASO NA KUNYIMWA HAKI ZAO STAHIKI.

MRATIBU WA MAFUNZO HAYO BWANA GEOGE LEONARD, WA SHIRIKA LISILOKUA LA KISEREKALI LA TDWC, AMESEMA KWA SASA WANASAPOTI MASHIRIKA ZAIDI YA 50 YALIYOKO KANDA YA ZIWA ILI WAAJIRI NA WATOTO WAFANYAKAZI WA NDANI KUPATIWA ELIMU YA KUTOSHA. 

HALI NI SHWARI SASA KATIKA ENEO AMBALO ABIRIA WALIKUWA WAKIVAMIA MAJIRA YA ASUBUHI NA KUFANYIWA VITENDO VYA UNYAMA



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Baada ya kupitia kipindi kigumu cha hali ya sintofahamu katika usalama kwa takribani miezi mitatu toka mwishoni mwa mwaka jana 2017 mwezi wa 12 na mwanzoni mwa mwaka 2018 kwa mwezi wa kwanza na wa pili, hatimaye sasa hali ya amani imerejea katika eneo la Nyegezi lililopo ndani ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Jeshi la Wananchi mkoani hapa mkono kwa mkono kwa kushirikiana na wananchi wamefanikisha kujenga kituo cha polisi kwa ajili ya ulinzi na kutoa usaidizi.

Hili ni eneo ambalo wananchi waliokuwa wakiamka alfajiri kwenda kwenye vituo vya mabasi walikuwa wakivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa nondo, huku kukiripotiwa vifo na baadhi yao kupata vilema vya maisha.

DKT TIZEBA AZINDUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA KILIMO JIJINI DODOMA

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Katikati) na Katibu wa Baraza la wafanyakazi Wizara ya kilimo Bi Agnes Hugo wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa mkutano na uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.

Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba leo 28 Juni 2018 amefungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo, mkutano utakaotuama kwa siku mbili kuanzia leo mpaka kesho 29 Juni 2018 katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo Dkt Tizeba aliwasisitiza wajumbe wa baraza hilo kwa umoja wao kujadili kwa muktadha wa kutatua changamoto na kuboresha sekta ya kilimo kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa ikiwa ni pamoja na kuhusu elimu ya majukumu ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi, Elimu juu ya watumishi wa Umma na hoja kutoka vyama vya wafanyakazi sambamba na wajumbe kupitishwa katika bajeti ya wizara kwa mwaka 2018/2019.

Alisema kuwa Baraza la wafanyakazi ni chombo muhimu ambacho kimepewa nguvu kisheria ili kuwapa watumishi nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusu utendaji na ufanisi wa Taasisi ili kuongeza tija mahali pa kazi hivyo wajumbe hao wanapaswa kujadili mada hizo kwa ufanisi na tija.

Alisisitiza kuwa Baraza hilo linapaswa kuzaa matokeo mazuri ikiwemo uboreshaji wa mazingira ya kazi huku akisema kuwa serikali imekuwa ikisisitiza kila taasisi ya umma kuunda mabaraza ya wafanyakazi ili kuongeza ufanisi na tija katika mchango wa mapinduzi ya uchumi wa viwanda.

Alisema, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli inatambua ushirikiano wa pande hizo mbili katika maamuzi hivyo ni vigumu kutekeleza majukumu endapo pande moja haitashirikishwa kwani umuhimu huo umetiliwa mkazo na kupitia sera, sheria na kanuni zinazosimamia uendeshaji wa taasisi za umma.

Katika hatua nyingine Mhe tizeba aliwakumbusha wajumbe hao kuwa miongoni mwa majukumu muhimu ya sekta ya kilimo ni pamoja na kutambua kuwa katika maendeleo ya nchi asilimi 66.5 ya watanzania wanategemea sekta ya kilimo pamoja na kuhakikisha usalama wa chakula nchini hivyo ni vyema katika mkutano huo kujadili mada hizo na kuwa na mategemeo ya kuwanufaisha zaidi wakulima kote nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza kabla ya kumkaribisha waziri wa kalimo kufungua kikao hicho cha Baraza la wafanyakazi alisema kuwa Baraza hilo jipya limeundwa kufuatia Baraza la awali kufikia muda wa ukomo wake baada ya maridhiano baina ya Menejimenti ya wizara ya kilimo na vyama vya wafanyakazi vya TUGHE na RAAWU kufikiwa.

Mhandisi Mtigumwe aliongeza kuwa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya ajira na mahusiano kazini Na 6 ya mwaka 2004 na sheria ya majadiliano ya pamoja katika utumishi wa umma Na 19 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2005. Ambapo kwa mujibu wa sheria hizo lengo la kuanzishwa mabaraza ya wafanyakazi ni kuwa na chombo cha ushauri na majadiliano ya pamoja kati ya wafanyakazi na waajiri ili kuwa na ushirikishwaji mpana wa wafanyakazi mahala pa kazi.

Alisema, kufuatia mabadiliko ya muundo wa Wizara ya kilimo hususani baada ya idara ya utafiti kuwa Taasisi inayojitegemea imelazimu muundo wa Baraza hilo kufanyiwa mabadiliko na kupelekea kupungua kwa idadi ya wajumbe kutoka 98 hadi kufikia 57, Aidha, mkataba mpya wa kuunda Baraza la wafanyakazi umezingatia mabadiliko hayo.

MAPEMA LEO ASUBUHI MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA ZIMBABWE


Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa amewasili leo Alhamisi Juni 28, 2018 saa 5:30 asubuhi katika uwanja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli.
Baada ya kuwasili amepigiwa mizinga 21, kukagua gwaride la heshima.
Mbali na Rais Magufuli, viongozi wengine waliofika kumpokea rais huyo wa Zimbabwe ni Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi;  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba;  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Baada ya mapokezi ya uwanjani, marais  hao wameelekea Ikulu kwa mazungumzo zaidi.
JEH ZIARA YA RAIS WA ZIMBABWE INA MANUFAA GANI KWA TANZANIA?
Katika taarifa kutoka ikulu Tanzania, Rais Magufuli amesema wamekubaliana tume ya pamoja ya ushirikiano, iliyokutana mwisho mnamo 1998, ikutane mara baada ya uchaguzi mkuu wa Zimbabwe mwezi ujao ili kujadili vikwazo na kutafuta majawabu ya kukuza biashara na uwekezaji baina ya Mataifa haya mawili.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Tanzania, Said Msonga anaamini huenda Rais Mnangagwa anatumia ziara hii kama mbinu ya kutaka kuibua hisia za wanamchi na kutaka kuonekana mzalendo na kumtengenezea mazingira ya kushinda uchaguzi.

HAPPY BIRTHDAY BOY //CUTHBERT A. SENGO//



Mwezi wa majembe yangu, mwingine huyoooOooo June 27th second born  ana 👊🏻+👊🏻 years old. .
.
You may have given me some trouble when you were growing up, but that’s because the apple doesn’t fall too far from the tree. .
.
When I look at you now though I see a version of me that also happens to be more kind, honest, and hardworking. .
.
I am overjoyed that you have turned into the kind of man I am proud to call my son. #HappyBirthday Cuthbert A. Sengo.

Cuthbert
Cuthbert and his Mom
Chilling..
Who got the power.
Me at the middle ni mwendo wa majotro.
Sisi.
















Mwanza.