Saturday, October 25, 2014
KUELEKEA MECHI DHIDI YA MAN UNITED MOURINHO ASIFU UMAHIRI WA VAN GAAL.
Mkufunzi wa timu ya Manchester Louis van Gaal amesisitiza kuwa hakuchukuwa jukumu kubwa la kumfanya Jose Mourinho kuwa miongoni mwa wakufunzi waliofaulu duniani.
Mkufunzi huyo wa Chelsea aliyefanya kazi chini ya Van Gaal katika kilabu ya Barcelona amekuwa akimsifu Kocha Van Gaal kwa mafanikio yake pamoja na Bobby Robson.
''Amekuwa akizungumza kunihusu na namshukuru kwa hilo lakini amekuwa akijifanyia mwenyewe'' alisema Van Gaal.
Wawili hao watakutana katika uwanja wa Old Trafford siku ya jumapili wakati ambapo Manchester United itakutana na Chelsea.
Kwa mara ya kwanza walikutana miaka 17 iliopita wakati Van Gaal alipomkabidhi Mourinho kazi katika kamati ya kufunzi katika uwanja wa Barcelona.
CHANZO BBC SWAHILI.
MEYA WA JIJI LA MWANZA NI MMOJA KATI YA WATIMUA VUMBI KESHO ROCK CITY MARATHON CCM KIRUMBA
MWANZA.
Baada ya kuutangaza mwezi mzima wa usajili kwa washiriki, hatimaye leo dirisha la kusajiri washiriki wa mbio za Rock City Marathon kupitia mitandao na analojia, limefungwa rasmi ikiwa ni masaa machache kwa mashindano hayo kuanza kutimua vumbi.
Mathew Kasonta ambaye ni mratibu wa Rock City Marathon, amewataka washiriki waliojisajili kushiriki mbio hizo kufika mapema kesho Jumapili (26/10/2014) asubuhi katika uwanja wa CCM Kirumba ili kuweza kushiriki kikamilifu na kwa tija, kuufufua mchezo huo, kuvibaini vipaji ikiwa ni pamoja na kunyanyua hamasha ya wapenzi na mashabiki wa mchezo huo ambao katika zama za baadaye ndiyo walezi. BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Mstahiki meya wa jiji la Mwanza akionesha fomu yake ya usajili kushiriki mbio za Rock City Marathon. |
Zaidi ya shilingi milioni 9 zimetengwa kama sehemu ya zawadi kwa mbio za Rock City Marathon ambapo mbali na washiriki kutoka ndani ya nchi washiriki wengine ni kutoka nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na sehemu mbalimbali toka kwa mabara tofauti duniani ambapo vilevile Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula atakuwa ni mmoja wa washiriki wa mbio hizo.
Mabula alikuwa mtu wa kwanza kuchukuwa fomu ya ushiriki na kuijaza ikiwa ni kipindi cha takribani mwezi mmoja sasa.
Friday, October 24, 2014
CHIDI BENZ AKAMATWA AIRPORT NA MADAWA YA KULEVYA.
Kuna taarifa zilitoka on millardayo.com leo jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.
Ambapo hatimaye kupitia Amlifanya imefahamika ni kweli msanii huyu amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kwenye mahojiano kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema msanii huyu alipohojiwa amekiri kweli kuwa dawa hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa anatumia ila anashangaa ni kwa nini vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza kubaini ni dawa aina gani za kulevya’
Sauti ya Kamishna Hamis Sulemani akithibitisha tukio hilo unaweza kuusikiliza hapa. BOFYA PLAY KUISIKILIZA.
JE YANGA ITAPONA KESHO DHIDI YA STAND UNITED DIMBA LA KAMBARAGE SHINYANGA
Friday, October 24, 2014
No comments
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania Bara inataraji kuendelea tena kesho (jumamosi) kwa michezo kadhaa kutoka hapa mkoani Shinyanga, Yanga Afrika iliyo katika nafasi ya nne itacheza kwa mara ya pili ugenini, katika uwanja ambao timu hiyo ya Dar es Salaam hushangiliwa zaidi ya uwanja wa Taifa, itacheza na wenyeji Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage. Katika mgawanyo wa mashabiki katika Mikoa ya kanda ya Ziwa, Yanga ina idadi kubwa ya wapenzi katika Mkoa wa Shinyanga.
Stand United wao watajivumia mtaji wake wa awali wa kuwa na mashabiki toka Kanda ya Ziwa waliona na kiu ya kuendelea kuona mechi mbalimbali za ligi kuu zikiendelea kuwa karibu na ukanda wao na wakati huo huo wale mahasimu wa Yanga, Simba SC ni dhahiri kuwa mashabiki wake wataiunga mkono Stand ili imuadhiri mtani wao Yanga. Zaidi BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Stand United wao watajivumia mtaji wake wa awali wa kuwa na mashabiki toka Kanda ya Ziwa waliona na kiu ya kuendelea kuona mechi mbalimbali za ligi kuu zikiendelea kuwa karibu na ukanda wao na wakati huo huo wale mahasimu wa Yanga, Simba SC ni dhahiri kuwa mashabiki wake wataiunga mkono Stand ili imuadhiri mtani wao Yanga. Zaidi BOFYA PLAY KUSIKILIZA
NGUMI KUPIGWA KESHO OKTOBER 25 FRENDS CORNER MANZESE
Bondia Ally Bugingo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Amani Bariki 'Manny Chuga' mpambano utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends corner Manzese Dar es salaam katikati ni Antony Rutta. |
Bondia Sadiki Nuru akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho jumamosi |
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika kesho oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese ambapo anapambana na George Dimoso mpambano wa raundi nane. |
Bondia Fadhili Boika kushoto akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba 25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam picha naSUPER D BLOG |
Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika
Jumamosi ya October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
Pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
COSTAL UNION WAKIFANYA MAZOEZI UWANJA WA KAITABA LEO TAYARI KWA MCHEZO WAO NA KAGERA SUGAR KESHO KAITABA
Kocha Mpya wa Coasta Union kutoka Nchini Kenya Yusuph Chippo akiwacheki Vijana wake kwenye Uwanja wa Kaitaba leo. Costal Union watacheza mchezo wao na Wenyeji Kagera Sugar kesho kwenye Mchezo wa Ligi kuu Vodacom. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.com |
KOCHA wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Yusuf Chipo akiteta jambo na Wachezaji wake leo kwenye Uwanja wa Kagera Sugar. |
KOCHA wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Yusuf Chipo amesema ameridhika na kiwango cha vijana wake na wako tayari kuwavaa Kagera Sugar kesho Jumamosi. |
Kagera Sugar wako nafasi ya tano wakiwa na pointi 5 sawa na Mbeya City baada ya kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Mjini Shinyanga Stand United, Huku Costal Union wakiwa nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa Ligi kuu wakiwa na pointi 7. |
Wachezaji wa Costal Union wakiwa makini kumsikiliza Mwalimu wao na kupanga mipango ya kutoka na Alama tatu muhimu kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.com |
Wakati wa mapumziko kidogo |
Nyoosha nyonga. |
Sawazisha. |
Vuta pumzi. |
Kipa Shaaban Hassan Kado(wa pili kulia) wa Coastal Union nae aliambatana na kikosi |
Wachezaji wa Costal union wakitoka Uwanjani baada ya Mazoezi yao kumalizika kwa siku ya leo Ijumaa kabla ya kukutana na Kagera Sugar kesho jumamosi Kaitaba |
Baada ya Kumaliza Mazoezi. |
Wakiteta jambo! |
Mchezaji wa Costal Union Razack Alphan |
SKYLIGHT BAND WAZIDI KULITIKISA JIJI LA DAR, USIKOSE LEO THAI VILLAGE NA KESHO NDANI YA JEMBE BEACH JIJINI MWANZA TAMASHA LA NYAMA CHOMA
Digna Mbepera akiimba kwa ustadi mkubwa kabisa kutoa Burudani kwa mashabiki wake. |
Kifaaa kipya machachari na moto mtoto mzuriiiiii Bela Kombo akizipiga zile vocal kaliiiii ndani ya Thai Village. |
Aneth Kushaba AK47 Le Meneja Her Self akichunguliaaaaaa huku akizipiga zile vocal kaliiii ndani Thai village. |
Majembe ya Skylight Band Hashim Donode wa kwanza kulia, Bela Kombo (katikati), Aneth Kushaba na Digna Mbepera(Wa kwanza kushoto) wakishirikiana kutoa Burudani kaliiii ndani ya Thai Village Masaki |
Shabiki Huyu akashindwa kujizuia na kuamua kumpa Sapoti Aneth Kushaba baada ya kuguswa na zile vokaliii nzuriiii |
Bana Ba Congo wakiongozwa na Sam Mapenzi(wa kwanza kulia) wakiyarudi mauno vilivyoooo kuwapa raha mashabiki wao. |
Sony Masamba(Katikati) akizipia Vokali nzuriiii za Congo huku akipewa sapoti ya mauno nyorotiiii na Joniko Flower(wa kwanza kushoto) na Sam Mapenzi kulia |
Rahaaa kweliiii kweliiii Bana Ba Congo wakiendelea kutoa Burudaniii safiiiii ndani ya Thai Village Ijumaa Iliyopita. |
Weweeeee hapana chezea kabisaaa mguu juu juuuu |
Aneth Kushaba akiyarudi maunooo vilivyoooo akipewa Sapoti na Donode (katikati). |
Safiii kabisa Majembe kazini Digna Mbepera (mwenye Top Nyeupe) akiwa na Donode (katikati) na Aneth Kushaba wa Kwanza kulia wakiendelea kutoa burudani kaliii ndani ya Thai Village Masaki Ijumaa iliyopita. |
Aneth Kushaba(Wa kwanza kulia)akiimba kwa rahaaaa kabisa huku akipewa sapoti na Hashimu Donode |
Joniko Flower akiwaimbisha mashabiki hawapo piachani ndani ya Kiota cha maraha Thai Village Ijumaa iliyopita |
Mashabiki wakicheza mastailiii kibaoooo waliyokuwa wakielekezwa na Joniko Flower, Njooo na wewe leo ujifunze kucheza kikuku na nyingine kiba0. |
Imma Bass akimpa baraka nyingiiiiii mpiga Bass Mwenzake Tophy huku wakiwa na furaha kubwaaa kabisa.Usikoseeee Leo ndani ya Thai Village itakuwa Balaaa ............ |
Subscribe to:
Posts (Atom)