LIGI kuu ya Vodacom Tanzania Bara inataraji kuendelea tena kesho (jumamosi) kwa michezo kadhaa kutoka hapa mkoani Shinyanga, Yanga Afrika iliyo katika nafasi ya nne itacheza kwa mara ya pili ugenini, katika uwanja ambao timu hiyo ya Dar es Salaam hushangiliwa zaidi ya uwanja wa Taifa, itacheza na wenyeji Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage. Katika mgawanyo wa mashabiki katika Mikoa ya kanda ya Ziwa, Yanga ina idadi kubwa ya wapenzi katika Mkoa wa Shinyanga. Stand United wao watajivumia mtaji wake wa awali wa kuwa na mashabiki toka Kanda ya Ziwa waliona na kiu ya kuendelea kuona mechi mbalimbali za ligi kuu zikiendelea kuwa karibu na ukanda wao na wakati huo huo wale mahasimu wa Yanga, Simba SC ni dhahiri kuwa mashabiki wake wataiunga mkono Stand ili imuadhiri mtani wao Yanga. Zaidi BOFYA PLAY KUSIKILIZA
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.