Wanahistoria wawili wadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk Maxilian Chuhila na James Zotto katika picha ya pamoja baada ya kukipeleka kitacho chao kuhusu Utengamano wa Africa, mgogoro wa Sahara nchini Africa Kusini.
Dk Maxilian Chuhila akizungumza na wanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Johannesburg kuhusu kitabu cha utangamano wa Afrika baada ya kukifikisha kitabu hicho nchini Africa Kusini
BAADA ya kuzindua kitabu kinachohusu Utengamano wa Afrika; Mgogoro wa Sahara nchini Tanzania na baadae Kenya, Watanzania wawili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanikiwa kukifikisha kitabu chao nchini Afrika Kusini.
Wanahistoria hao Dk Maximilian Chuhila na James Zotto wamefanikiwa kukipeleka kitabu chao nchini Afrika Kusini wakilenga kitumike kufundishia elimu ya juu katika nchi za Afrika.
Awali, Dk Chuhila na Zotto walifanya uzinduzi wa kitabu hicho kilicho chapishwa na APE Network Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) mkoani Iringa na baadae wakakipeleka Chuo Kikuu cha Kennyata, Nchini Kenya.
Jana Juni 11, 2024 wahadhiri hao walifanikiwa kufikisha maudhui ya kitabu hicho katika Chuo Kikuu cha Johannesburg huku wakipata nafasi ya kuzungumza na wanahistoria mbalimbali kutoka nchini humo wakiwamo wanafunzi na wahadhiri.
Dk Chuhila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Historia nchini amesema kitabu hicho ni miongoni mwa vitabu vilivyo onyesha kwa undani masuala ya utengamano wa Afrika hasa kuhusu mgogoro wa Sahara.
Kabla ya kuandika, Wanahistoria hao wawili walifanya utafiti nchini Morroco kisha kuja na kitabu wanacho amini kama kikitumika vyuo vikuu kitaongeza uelewa kuhusu utnganao wa Afrika hasa, mgogoro huo wa Sahara.
Awali, Zotto alisema utengamano wa Afrika ni silaha laini inayoweza kumaliza mzozo wa Sahara uliodumu kwa zaidi ya miongo miwili sasa.
Morroco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi Polisario zimekuwa zikilumbana kwa zaidi ya miongo miwili kuhusiana na udhibiti wa eneo hilo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa, Jimson Sanga amesema jitihada za wanahistoria hao zinapaswa kuigwa na wahadhiri wengine kwamba, badala ya kuandaa maudhui yanayoishia ndani ya nchi, wanaweza kusambaza duniani kote.
“Binafsi nimeona kumbe inawezekana, kama tunaweza kufanya tafiti za ndani ya nchi basi tunaweza kufanya tafiti nche na maandiko yetu yakatumika katika kutoa elimu vyuo vikuu mbalimbali,” amesema Sanga.
Amesema badala ya kuwa wanapokea maandiko na vitabu kutoka mataifa mengine, wanaweza pia kusambaza maudhuo hayo nje ya nchi.
Mwisho.