Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini dar leo. |
Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka
jana.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini
Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini
(NECTA),Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha
nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka kwa asilimia
12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab
,Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia
wavulana.
Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi
sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10
bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule
zingine.
Msonde amasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mpya
wa GPA kwa kuangalia masomo saba hivyo ufaulu umetokana na
mfumo huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.