ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 4, 2024

WAZIRI JAFO ATEMA CHECHE UMUHIMU WA KUPAMBANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

 


NA VICTOR MASANGU,KISARAWE


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo amesema mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha mkaa mbadala katika eneo la Visegese Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani  kitakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuleta mapinduzi ya   kupunguza changamoto ya  uharibifu wa mazingira ambao ulikuwa unafanyika.

Jafoo alibainisha kwamba  mkaa utakaozalishwa katika kiwanda hicho utasaidia wananchi kuachana na kutumia kuni na mkaa unaotokana na kukatwa kwa miti ovyo  na kupelekea  uharibu  wa misitu na kupoteza uoto wa asili uliopo.

Dk.Jafo ameyasema hayo  wakati mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa ulipotembelea kiwanda hicho kukagua ujenzi na na kupanda miti katika eneo hilo ambapo alisema mradi huo ni muhimu kwani utakwenda kuokoa hekta zaidi ya 4,622,000 zinazopotea kutokana na vitendo vya kukata miti.

" Mradi huu katika upande mazingira utaleta heshima.kubwa, niwapongeze Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kwa kutekeleza maagizo ya viongozi wakuu katika mapambano ya kutokomeza uharibifu wa mazingira," amesema.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mzava akizungumza katika mradi huo amesema kwakua lengo la mradi ni kuzalisha nishati mbadala Stamico wanatakiwa kuongeza kasi na kusimamia mradi huo utekelezwe kwa viwango na kukamilika kwa muda uliopangwa.

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Kibaha, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Fatuma Nyangasa amesema Mwenge huo umembizwa km 125.7 na  kukagua, kuzindua, na kuweka mawe ya msingi miradi saba yenye thamani ya sh. Biln 3.4.

Pia Mwenge huo umeweka jiwe la Msingi katika mradi wa daraja Makurunge, umekagua maabara ya Ufundi umeme, ushonaji na mapishi pamoja na kuzindua klabu ya wapinga Rushwa.

Miradi mingine ni jengo la mama na mtoto, ambao ulizinduliwa, mradi wa darasa lenye watoto wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Sanze, mradi wa vijana uzalishaji wa  Kiwanda 

LINDI WAZINDUA MPANGO MKAKATI KUINUA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI

 

Mkuu wa mkoa wa Lindi mheshimiwa Zainab Telack akizindua mpango mkakati wa kuinua elimu ya msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi 
Mkuu wa mkoa wa Lindi mheshimiwa Zainab Telack akizindua mpango mkakati wa kuinua elimu ya msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi 

Mkuu wa mkoa wa Lindi mheshimiwa Zainab Telack akizindua mpango mkakati wa kuinua elimu ya msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi 

Fredy Mgunda, Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi umezindua mpango mkakati wa elimu ya msingi na Sekondari kwa mwaka 2024 kwa lengo la kuongeza ufaulu wa elimu kwa wanafunzi wanaosoma katika mkoa huo.

Akizungumza wakati wa sherehe za utoaji tuzo za elimu kwa wadau mbalimbali wa sekta ya elimu Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack alisema kuwa wamezindua mpango mkakati wa elimu kwa lengo la kutatua changamoto 15 zilizopo katika elimu ya msingi na sekondari katika mkoa huo.


Telack alisema kuwa baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na hali ya ikama ya walimu wa Shule za Msingi na Sekondari na hali ya msawazo wa walimu, kutathmini hali ya viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu, changamoto ya uwepo wa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kwa darasa la kwanza na la pili, zoezi la utoaji wa chakula katika shule za msingi na Sekondari.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na mpango wa utoaji wa motisha kwa walimu, wanafunzi, wasimamizi wengine wa walimu, mpango wa uandaaji mitihani ya majaribio kwa watahiniwa wa mitihani ya kitaifa.

Mpango huu wa elimu kwa mwaka 2024 umezinduliwa na kukabidhiwa kwa viongozi wasimamizi wa elimu wa Mkoa na Wilaya ili kuhakikisha ufaulu unaendelea kuongezeka kwa ngazi zote za elimu sanjari na kuchochea maendeleo ya Sekta ya elimu kwa ujumla.

"Mpango Mkakati wa Elimu uliozinduliwa umejikita kutatua changamoto 15 ambazo ngazi ya elimu ya msingi na sekondari zinapaswa kuzisimamia kwa muda maalum uliopangwa" alisema Telack

Friday, May 3, 2024

ZAIDI YA BL5 ZA TOZO KODI NA USHURU WA MAEGESHO HAZIJALIPWA MKURUGENZI JIJI LA MWANZA AJA NA NYUNDO

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba ametoa siku tatu kuanzia Mei 2 hadi Jumapili Mei 5, mwaka huu kwa wafanyabiashara, wenye maegesho mahususi, wamiliki wa vibanda vya maduka kwenye masoko, makampuni ya kuzoa taka na wananchi waliojenga bila vibali kulipa ushuru, kodi na ada mbalimbali za halmashauri hiyo bila shuruti. Kibamba ametoa wito huo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini hapa akisisitiza kwamba amefikia hatua hiyo baada ya kufanya juhudi mbalimbali za kufuatilia ukusanyaji wa mapato kwa njia za kistaarabu lakini wafanyabiashara hao wamekuwa wazito kutii sheria kwa hiari. Amesema kodi zote na ushuru zitalipwa kwenye mfumo wa kielektroniki huku akiwataka wafanyabiashara hao kuepuka kulipa mikononi kwani atakayefanya hivyo malipo yake hayatakubalika na hayatatambulika, hivyo, ili kuepuka usumbufu amewataka kufika ofisini kwake kuchukua namba za malipo (control number). Amesema katika jitihada za kuhamasisha ukusanyaji huo wa kodi na ushuru waliwatumia watendaji wa mitaa kuwafikia wafanyabiashara na watu wote ambao wanafanya shughuli mbalimbali ambazo wanastahili kwa mujibu wa sheria kulipa kodi na ada mbalimbali kwa mujibu wa sheria za halmashauri ya jiji la Mwanza ili kuiwezesha kutoa huduma kwa wnaanchi kwa mujibu wa sheria. #samiasuluhuhassan #jembefm #mwanza

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AZINDUA RASMI UKUMBI WA KISASA KIBAHA MKOA WA PWANI.

 KIBAHA PWANI NA MWANDISHI VICTOR MASANGU

MSIMULIZI - ALBERT G.SENGO

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mzava, ameyasema hayo mjini Kibaha wakati akizindua mradi wa Ukumbi wa kisasa wa mikutano wa Destiny, uliogharimu sh. Milioni 500 huko Kwamatiisi mjini Kibaha na kusema ni vema taasisi hizo wezeshi zikaweka mazingira rafiki ili kuendelea kuwavutia wawekezaji wengine na kuongeza uchumi wa mkoa huo. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John, amesema Halmashauri ya Mji wa Kibaha ndio kitovu cha mkoa wa Pwani ambapo hupokea wengeni wengi hivyo uhitaji wa huduma hiyo ni mkubwa na wenye tija hivyo mradi wa ukumbi huo utaweza kukuza uchumi. #destiny #samiasuluhuhassan #kibaha #mkoawapwani

Thursday, May 2, 2024

CDF MKUNDA AELEZA UMUHIMU WA JKT KATIKA ULINZI WA TAIFA




MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba



MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba

MRADI WA RUWASA KUZINUFAISHA KAYA 164 ZA RUVU STESHENI KUPATA HUDUMA YA MAJI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Kaya zipatazo 164 zilizopo katika  eneo la  Ruvu station lililopo  Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wameondokana na changamoto ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita 11,820.

Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Debora Kanyika alisema kwamba kisima hicho kitakuwa na urefu wa mita 43.

Meneja Kanyika alibainisha kwamba mradi huo ambao utekelezaji wake ulianza tangu mwaka 2023 una uwezo wa kuhifadhi maji lita zipatazo elfu 50,000 juu ya mnara wa mita 12.

Kadhalika Meneja huyo alibainisha kuwa mradi huo wa kisima utakuwa na na vituo vipatavyo saba ambavyo ni kwa ajili ya kuweza kuchotea maji.

"Mradi huu una urefu wa mita zipatazo mita 43 na kwamba mnara wa mita 12 pamoja na vituo vipatavyo saba vya kuchotea maji kwa wananchi sambamba na mitambo ikiwa na mitambo ya kutandaza mabomba yenye kipenyo cha kuanzia inchi tatu hadi robo tatu,"alisema Meneja huyo.

Kadhalika alisema kwamba mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milion 328 kupitia mfuko wa Taifa wa maji wa (NWF).

Aidha Meneja huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi  umeongeza hali ya upatikanaji wa maji kwa asilimia moja kwa Wilaya ya Kibaha na sasa huduma hiyo imefikia asilimia 78.

Pia alifafanua kwamba mradi huo ni moja ya utekelezaji wa kampeni ya Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo mama kichwani.

Katika hatua nyingine Meneja alibainisha kwamba mradi huo umeweza kutoa fursa ya ajira kwa wananchi wapatao 63 ambao wanatoka katika maeneo mbali mbali ya Wilaya Kibaha.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Mzava ameridhishwa na meadi huo wa maji na kuwapongeza kwa dhati uongozi wa Ruwasa kwa kazi ambayo wanaifanya katika kuwahudumia wananchi.

Kadhalika aliwahimiiza viongozi wa Ruwasa kuhakikisha kwamba wanayafanyia marekebisho baadhi ya mambo katika mradi huo ikiwemo upatikanaji wa Jenereta.

CCM IRINGA WAWAPONGEZA WALIMU WAZALENDO

 

Katibu Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Iringa, Joseph Ryata akiongea na walimu wazalendo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa

Na Fredy Mgunda, Iringa 

CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimewpongeza walimu wazalendo kufundisha kwa juhudi na kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kutekeleza ila ya CCM ya 2020/2025 kwa vitendo.


Akizungumza na walimu wazalendo Katibu Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Iringa, Joseph Ryata alisema kuwa walimu wamekuwa na mchango mkubwa wa kimaendeleo kutokana na kutoa elimu kwa wote na mara nyingine kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu.


Ryata alisema kuwa walimu wanaaminiwa na jamii kutokana na elimu,burasa na maarifa wanayotumia kwa jamii wanayoishi nayo kwa kuwaelimisha mambo mbalimbali ya kimaisha na kimaendeleo.


Alitumia wasaa huo kuwataka walimu kusaidia serikali kuyaelezea mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kutoka ushauri wenye hoja za kujenga kwa viongozi wa Chama na Serikali katika maeneo wanayoishi ili kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezwa ipasavyo kwa maslahi ya wananchi.


Ryata amewapongeza walimu hao kwa umoja na uamuzi wao mzuri wa kuunda na kujiunga katika jukwaa la Walimu Wazalendo huku akisema Mwanachama au Kada wa CCM asipokuwa Mzalendo hawezi kuwa na tija ndani ya CCM na hawezi kufaidika vyema na fursa mbalimbali ndani ya Chama hicho na nchi kiujumla. 


Sambamba na hilo, Ryata amewataka walimu hao kuendelea kuielimisha jamii na kusimamia maadili, misingi ya utoaji Elimu Bora na Malezi kwa watoto ambao ndio wanafunzi wao wanapokuwa shuleni.

 

Kwa upande wao walimu wazalendo wamekipongeza chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa kuendelea kuwapa ushirikiano na kutambua mchango wao katika jamii huku wakiomba Uongozi  uzidi kuwapambania na kuzisema kero na changamoto zinazowakabili walimu katika utumishi.

WATUMISHI WA TAWIRI WAUNGANA NA WAFANYAKAZI DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YAO ADHIMU

 

WATUMISHI wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)  Mei Mosi 2024 wameungana na Wafanyakazi Duniani kote kuadhimisha Siku yao adhimu ambapo kitaifa maadhimisho yanaendelea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijinu Arusha na Mgeni Rasmi wa Sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango

TAWIRI tunajivuni mchango mkubwa wa watumishi katika kusimamia, kuratibu na kufanya tafiti za wanyamapori nchini kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza utalii nchini. 

Aidha, Kauli mbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu ni *"Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha"*




 Kauli mbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu ni *"Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha"*

KIBAHA DC WAPITISHIWA MIRADI YAO YOTE 13 NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA


 NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imeweza kupata baraka baada ya kiongozi wa  mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 Godfrey Msava kuridhishwa na kupitisha miradi yote 13 ya mandeleo.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa amepitisha miradi yote  hiyo 13 ambayo  imepitiwa na mwenge wa uhuru na kuwapongeza viongozi mbali mbali ambao wameweza kuhakikisha wanaisimamia vema na kutumia fedha vizuri ambazo zimetolewa  na serikali kwa kuzingatia mfumo wa kidigitali.










Alisema kwamba licha ya kuridhishwa na miradi hiyo mbali mbali ya maendeleo lakini ameagiza baadhi ya miradi ambayo imeonekana kuna na dosari  kadhaa wahakikishe wanazifanyia kazi na kuzirekebisha.

"Nawapongeza viongozi wote wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kuweza kutekeleza miradi yenu kwa vitendo na kitu kikubwa fedha ambazo zinatolewa na serikali zitumike vizuri katika kutekeleza miradi ya maendeleo "alisema Mzava

Kadhalika aliongeza kuwa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan anatenga fedha kwa ajili ya miradi mbali mbali ili kuwasogezea huduma wananchi hivyo viongozi na watendaji wanapaswa kusimamia miradi hiyo kwa maslahi ya wananchi.

Mwenge wa uhuru umepita katika miradi mbali mbali ya maendeleo ambapo umekagua mradi mkubwa wa kongani ya viwanda 
ya  SINOTAN, uliopo Kata ya Kwala ambao  utagharimu kiasi cha shilingi  trilioni 8.4. mpaka kukamilika kwake.

Pia Mwenge huo wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika  mradi wa ujenzi wa barabara kutoka barabara ya Morogoro kwenda ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha yenye urefu wa mita  zipatazo 300  ikiwa katika kiwango cha lami.

Aidha mwenge wa uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha pia umepitia miradi mingine ya maendeleo ikiwemo uzinduzi wa  zahanati ya Vikuruti ambayo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Kadhali iliweza kuzindua mradi mkubwa wa maji ambao unatekelezwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(RUWASA) ambao umegharimu kiasi cha shilingi 328.

Sambamba na hilo mbio za Mwenge wa uhuru umeweza kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika sekta mbali mbali ikiwemo,afya,elimu,maji miundombinu ya barabara mapambano ya rushwa ukimwi,lishe pamoja na miradi mingine ya maendeleo.

Awali akiupokea Mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon alibainisha kwamba Mwenge huo katika Halmashauri mbili za Kibaha mji na Wilaya ya Kibaha utazindua jumla ya miradi 28 yenye thamani ya shilingi trilioni 8.5.

Nao baadhi ya wananchi ambao waliweza kupata fursa ya kushiriki katika mbio hizo wameshukuru Mwenge wa uhuru kwa kuweza kuzindua baadhi ya miradi na mingine kuweka mawe ya msingi ambayo kwa upande wao ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia huduma muhimu za kijamii.

Tuesday, April 30, 2024

'HAYA NDIYO NILIYOYAKUTA NDANI YA HIFADHI YA MAKUMBUSHO YA AZIMIO YA ARUSHA'

 NA ALBERT G. SENGO/ ARUSHA

Napata fursa ya kutembelea Makumbusho ya Azimio la Arusha yaliyoko eneo la Kaloleni, karibu na Mnara wa Uhuru (Mnara wa Mwenge). Hadi mwaka 1967, jengo hili lilitumika kama ukumbi wa ustawi wa jamii kwa jamii ya Kaloleni jijini Arusha. Mnamo Januari 1967, jengo hilo lilikuwa na mkutano wa kihistoria ambao Sera ya Kisiasa na Kiuchumi ya Tanzania ya Ujamaa na Kujitegemea ilitolewa. Mnamo Februari 1977 jengo hilo lilibadilishwa kuwa jumba la kumbukumbu ndogo la kisiasa na uchumi. Jeh ni yapi yaliyomo ndani ya Makumbusho haya? Ungana nami msimulizi wako Albert G. Sengo nikupitishe hatua kwa hatua katika eneo hili ambalo ni nyenzo muhimu ya kufundishia kwa historia, kiraia, masomo ya jumla na masomo ya sayansi ya siasa.

ZEE LA NYETI AJILAUMU KIFO CHA GADNA - "UKISIKIA MTU ANAUMWA USIAHIRISHE NENDA KAMSABAHI"

 NA ALBERT G. SENGO/ ROMBO, KILIMANJARO

Mwandishi wa Habari za Burudani na Michezo wa Gazeti la Mwananchi ambaye pia ni Mtangazaji na Mjasiliamali, Henry Mdimu 'Zee la Nyeti' amezungumza na Jembe Fm wakati wa mazishi ya mwanahabari nguli wa Clouds Fm, Gadna G. Habash, jinsi alivyoguswa na msiba wa marehemu huyo aliyefariki asubuhi ya Jumamosi ya tarehe 20 April 2024 baada ya kuugua na kulazwa katika Hospitali ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam. Mdimu ameiasa jamii kutopuuzia suala la kwenda kwa wakati kuwajulia hali wapendwa wao wanapougua kwani yeye aliahirisha mara kadhaa kwenda kumtembelea hospitalini marehemu Gadna wakati alipopata taarifa za kulazwa kwake. "Nimejuta Gadna wiki moja kabla ya kifo chake nilikuwa nafanya show Morogoro kwahiyo tuklikuwa tumeshaelewana, tumeshalipana hela ya tangazo lakini kesho yake nikasikia jamaa amelazwa, nikawaambia stuff wangu msimsumbue huyu jamaa kwasababu nimetoka naye mbali, tutakuja kufanya naye tangazo siku nyingine na nikirudi Dae es salaam nitakuja kumwona" "Nimeenda Dar es salaam nimekaa siku tatu, sikupata nafasi ya kwenda hospitali lakini nilikuwa napiga simu kwa marafiki, jamani kuna mtu amekwenda kumwona Gadna?'" Jibu - "Yes" Swali - "Anaendeleaje?" Jibu - "Yuko Powa" "Basi nikasema niende tena Morogoro nikirudi nitamkuta, nafika tu Morogoro nasikia Gadna amefariki"............ #samiasuluhuhassan #mwanza #rombo #gadna

MKE WA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI ATIMIZA AHADI YAKE KWA VITENDO VIJANA WA HAMASA

 


NA VICTOR MASANGU KIBAHA 


Jumuiya ya Umoja wa vijana ya Chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kibaha mji umempongeza kwa dhati mke wa Mbunge wa  Jimbo la Kibaha mji Selina Koka kwa kuona umuhimu wa kuwasapoti vijana kwa kutoa  msaada wa  mahitaji na vitu  mbali mbali ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa  kwa vijana.


Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kibaha mjini Gamalu Makona wakati wa halfa fupi ya kukabidhiwa baadhi ya mahitaji na vitu mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia vijana wa hamasa ambao wapo katika mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na  kuupokea Mwenge wa uhuru.
Aidha Katibu huyo alisema kwamba Mama Koka amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mambo mbali mbali katika jumuiya ya vijana katika Jimbo la Kibaha mji.

Aliongeza kwamba Mama Koka amewashika mkono na kuwapatia msaada wa vyakula mbali mbali,sambamba na mabati viti meza kwa ajili ya ujenzi wa banda ambalo litakuwa linatumika kukutana vijana wa uvccm pamoja na kupumzikia ili kujadili mambo ya jumuiya na maendeleo.

"Kwa kweli tunamshukuru na kumpongeza Mama Koka kwa kuwa na upendo wa kipekee maana hivi karibuni alikuja kututembelea umoja wetu na kile ambacho alituahidi kiukweli amekitekeleza na Mungu aweze kumbariki yeye pamoja na Mbunge kwa kuwa na moyo wa kujitolea,"alisema Katibu.

Akikabidhi msaada huo wa vitu mbali mbali kwa niaba ya Mama Koka Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Method Mselewa alisema kwamba msaada huo ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya mke wa Mbunge kwa vijana hao ambayo aliitoa alipokwenda kuwatembelea hivi karibu.

Katibu Method alisema Mama Koka anatambua mchango mkubwa ambao unafanywa na jumuiya ya vijana hivyo akaamua kutoa mahitaji mbali mbali ambayo yatawasaidia vijana pindi wanapokuwa wakiendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na Mwenge wa uhuru.

Mselewa alibainisha kwamba vijana hao ni Taifa la kesho hivyo wanapaswa kupendana na kuwa na maadili mazuri pamoja na  uzalendo kwani ndio viongozi watarajiwa katika siku za usoni.

"Hapa nimekuja kwa niaba na mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Koka na nimekuja na vitu mbambali kwa ajili ya chakula pamoja na redio ambayo mtakuwa mkiitumia katika burudani na mambo mengine,"alifafanua Katibu huyo.

Aliwahimiza vijana kuendelea kufanya mazoezi pamoja na kushiriki kikamilifu katika kuupokea Mwenge wa uhuru ambao utatembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon ambaye naye alifika kuwajulia hali vijana hao wa hamasa amewahimza kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika ujio wa mapokezi ya mbio za Mwenge wa uhuru na kwamba serikali ipo pamoja nao.

Katika hatua nyingine aliwaahidi katika mkesha wa mwenge kutakuwa na burudani mbali mbali za wasanii wakubwa pamoja na wasani wa kibaha na kwamba siku hiyo wategemee kuona burudani ya aina yake hivyo wajitokeze kwa wingi.

MWENGE WA UHURU WATOA BARAKA KWA RUWASA MRADI WA MAJI FUKAYOSI UENDELEE

 


NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO


Wananchi wapatao elfu 3666 katika kijiji cha Kidomole  pamoja na vitongoji vyake mbali mbali vilivyopo katika  kata ya Fukayosi  Wilayani Bgamoyo Mkoa wa Pwani wanatarajia kuondokana na changamoto ya usumbufu wa majii fikapo mwezi Mei mwaka huu baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji ambao utakuwa ni mkomboz mkubwa kwa wananchi hao.

Hayo yamebainishwa na  Meneja wa wakala wa Usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Bagamoyo  James kionaumela wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge  wa Uhuru  kitaifa ndugu  Godfrey Mnzava kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo ambapo alisema kwa sasa upo katika hatua za mwisho kwa ajili ya upanuzi.


Meneja huyo alibainisha kwamba unatekelzwa chini ya mkandarasi mzawa AM&Partiner Limeted na Building Contractors kutoka jijini Dar es Salaam na kwamba kwa mujibu wa mkataba huo mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 11 mwaka huu.

Alifafanua kwamba katika upanuzi wa mradi huo pia unakwenda sambamba na ujenzi wa  tibio la maji katika eneo la Saadan na kwamba mradi huo umegharimu kiasi cha   zaidi ya  shilingi milioni 603 ambazo ni fedha kutoka katika mfuko wa maji( NWF)





Meneja huyo alibainiha kwamba utekelezaji wa mradi huo ulianza rasmi mnamo tangu Mei 11 mwaka 2023 na pia utaweza kuzinufaisha kaya zipatazo 796 kutoka kata ya Fykayosi pamoja na vitongoji vyake wananchi wataweza kuondokana na changamoto ya maji na hatimaye kupata huduma ya maji safi na salama.

Pia alisema kuwa katika kutekeleza mradi huo umeweza kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana wa lika mbali mbali  wapatao 50 ambao kwa sasa wameweza kujipatia kipato halali na kujikwamua kiuchumi.

Meneja huyo alibainisha kwamba katika eneo la kijiji cha Kidomole utekelezaji wa mradi huo umefikia kwa kiwango cha asilimia 90% ikiwa ni pamoja na ujenzi wa tanki kubwa lenye ujazo wa lita elfu 50,000 kwenye mnara wa mita 12.

Katika hatua nyingine Meneja huyo alitoa shukrani za dhati kwa Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anatenga fedha katika kuboresha sekta ya maji kwa vitendo lengo ikiwa ni kuwapatia huduma wananchi ya maji safi na salama.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava pamoja na wakimbiza mwenge wenzake wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kukubaliana kwa pamoja kuupitisha pamoja na kuwapongeza Ruwasa kwa kazi nzuri ambazo wanazifanya katika kuwapelekea huduma ya maji wananchi.

Alisema kwamba huduma ya maji ni muhimu sana kwa wananchi hivyo Ruwasa waendelee kuchapa kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatekeleza miradi ya maji kwa kiwango ambacho kinastahili kulingana na fedha ambazo zinatolewa na Rais.

Monday, April 29, 2024

MIRADI YA TRILIONI 8.5 KUTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU MKOA WA PWANI.

 

VICTOR MASANGU,CHALINZE


Mbio za Mwenge wa Uhuru umewasili leo rasmi mkoani Pwani ukitokea Mkoani Morogoro ambapo umekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo utembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo.

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge alisema kwamba katika mbio hizo mwenge huo utatembelea jumla ya miradi ipatayo 126.


Kunenge alibainisha kwamba mbio za Mwenge huo wa uhuru kwa mwaka huu  utakimbizwa katika Halmashauri tisa zilizopo katika Wilaya saba  ambapo jumla ya kilometa 1,225.3 zitakimbizwa katika maeneo mbali mbali.

Kunenge alifafanua kwamba kati ya miradi hiyo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi,miradi 22 itazinduliwa na miradi ipatayo 86 itakaguliwa.

Aidha Kunenge alisema kuwa miradi hiyo itagharimu  kiasi cha shilingi Trilioni 8.536  ambapo serikali kuu imechangia bilioni 13.6,Halmashauri za wilaya shilingi bilioni 2.3 nguvu za wananchi na wawekezaji trilioni 8.5 na wadau wa maendeleo bilioni 14.6.

Pia alimshukuru Rais wa awamu ya sita kwa kuweka mazingira bora kwa ustawi na ufanisi zaidi katika sekta binafsi nchini.


Pia Kunenge katika hatua nyingine alisema kwamba katika kupambana na janga la ukimwi wameendelea kupambana kwa kutoa elimu ya upimaji wa wenza.

Kadhalika aliongeza katika kupambana na dawa za kulevya wameendelea kuimarisha mapambano kwa kubadilisha fikra,hisia na tabia.

Awali kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mnzava alizitaka halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaandaa nyaraka zote za miradi ya maendeleo.8