ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 12, 2017

SERIKALI YAOMBWA KUTAFUTA NJIA MBADALA YA USAFIRI KWA WANAFUNZI.


BAADHI ya wazazi na wanafunzi wanaosoma shule za msingi za serikali katika kata za Upanga na Kivukoni jijini Dar es S alaam wameiomba serikali kutafuta njia mbadala ya usafiri kwa wanafunzi hao kufuatia katazo la kuzuia huduma ya usafiri iliyokuwa ikitolewa na kikundi cha KIWAKIDA.

TADB YAOMBWA KUSAIDIA SEKTA YA MIFUGO MKOANI ARUSHA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo mkoani Arusha kuhusu fursa za mikopo ya TADB. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akizungumza kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.

Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi (aliyesimama) akizungumzia changamoto zinazoikabilia sekta ya mifugo mkoani humo katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo mkoani Arusha.

Meneja wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (wa pili kulia aliyesimama) akitoa takwimu za mahitaji ya mikopo ya mkoa wa Arusha. Kulia  ni Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. George Nyamrunda.

Baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha waliohdhuria kikao cha pamoja na TADB wakitoa maoni yao kuhusiana hali ya hupatikanaji wa mikopo katika kusaidia sekta ya mifugo mkoani humo

Baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha waliohdhuria kikao cha pamoja na TADB wakitoa maoni yao kuhusiana hali ya hupatikanaji wa mikopo katika kusaidia sekta ya mifugo mkoani humo

Baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha waliohdhuria kikao cha pamoja na TADB wakitoa maoni yao kuhusiana hali ya hupatikanaji wa mikopo katika kusaidia sekta ya mifugo mkoani humo

Baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha waliohdhuria kikao cha pamoja na TADB wakitoa maoni yao kuhusiana hali ya hupatikanaji wa mikopo katika kusaidia sekta ya mifugo mkoani humo

Ugeni kutoka TADB wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha  mara baada ya katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.

Na mwandishi wetu, Arusha
Wadau wa sekta ya mifugo mkoani Arusha wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza sekta hiyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa nyama na maziwa.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, kwa niaba ya wafugaji wa mkoa wa Arusha, Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi amesema ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika sekta ya mifugo inawapa changamoto katika uendelezaji wa sekta ya mifugo nchini.
Bw. Kissiagi ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika inarudisha nyuma ukuaji wa sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.

“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.

Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa nchini.

Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa.

“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga.  

Naye, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)). 

“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.

Mkoa wa Arusha unashika nafasi ya tatu kati ya mikoa yenye mifugo mingi nchini ambapo inakadiriwa kuwa na zaidi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo milioni tatu.

JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI NI TANGAZO LA VITA.


Korea Kaskazini imelaani tena jaribio la kutaka kumuua kiongozi wake ambalo limetekelezwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Korea Kusini na kulitaja jaribio hilo kuwa sawa na tangazo la vita.
 Ubalozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kusema nchi hiyo itaanza oparesheni dhidi ya magaidi ambao walihusika na njama ya kutaka kumuua kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Taarifa hiyo imesema Pyongyang ina azma imara ya kuwasaka bila huruma na kuwaangamiza magaidi wote wa shirika kuu la kijasusi la Marekani CIA na shirika la kijasusi la Korea Kusini waliohusika na njama hiyo.

Taarifa hiyo imetoa wito kwa nchi za Umoja wa Mataifa kuunga mkono jitahada za Korea Kaskazini katika kukabiliana na magaidi hao waliotumwa na CIA.
Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitoa taarifa na kusema kuwa, CIA na Idara ya Intelijensia ya Korea Kusini zinapanga kutumia silaha ya kemikali kumuua kiongozi wa nchi hiyo.

Haya yanajiri katika hali ambayo, hali ya taharuki ingali imetanda katika Peninsula ya Korea haswa baada ya Marekani kufanyia majaribio kombora lake la "Minuteman III" lenye uwezo wa kupiga umbali wa karibu kilomita elfu sita na 760.

MAGAZETI YA LEO

Mambo 11 ya kuinufaisha Tanzania kwa Afrika Kusini, Vigogo wa Halotel wapanda kizimbani, Chadeama na CCM waumizana.

Rais Magufuli amkuna Zuma, Wafanyakazi 260 wakimbia uhakiki wav yeti, Mbowe ambana Waziri mkuu Bungeni, Simba kupindua tena? Pata kwa undani yaliyojiri katika magazeti ya leo hapa.

Thursday, May 11, 2017

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

KUFUATIA
uwepo wa baadhi za shule zisizokuwa na sifa, Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule Kanda ya Ziwa, Michael Cheyo, ameifunga moja kwa moja Shule ya Elite English Medium iliyopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza kutokana na kujiendesha bila kibali kutoka serikalini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Cheyo amesema kwamba amechukua hatua hiyo baada ya kukagua na kuthibitisha kuwa shule hiyo haina vigezo vya kuihalalisha kutoa huduma ya elimu kwa
watoto.

Kwa mujibu wa amri hiyo iliyotolewa kwa maandishi Aprili 6, mwaka huu, uongozi wa shule hiyo yenye wanafunzi 139 wa chekechea hadi darasa la pili, umetakiwa kuwahamishia wanafunzi hao kwenye shule zenye usajili kutoka mamlaka husika serikalini.

Licha ya shule hiyo kutokuwa na kibali cha kutoa huduma hiyo kutoka kwa Kamishina wa Elimu nchini, ukaguzi ulibaini kutokuwepo na walimu wenye sifa na kwamba  wanafunzi waliokuwepo wamekuwa wakitumia choo ambacho hakijaezekwa.

Cheyo ameeleza kwamba baada ya kufanya ucunguzi wamebaini shule hiyo ilianza kutoa huduma ya elimu mwaka 2012 bila kufuata taratibu za kiserikali huku mmiliki wake Dismas Mandela, amepata kuonywa na mamlaka husika mara kadhaa akitakiwa kuisajili lakini aliendelea kukaidi.

Aidha kwa upande wake Naibu Mthibiti wa Ubora wa Shule katika Wilaya ya Nyamagana, Mwalimu Winfrida Mwombeki, amesema mmiliki huyo amekuwa akikaidi maagizo ya kumzuia kuendesha shule hiyo kinyemela.

“Baada ya kugundua kwamba ameanzisha na kuendesha shule hiyo bila vibali vinavyotakiwa, mwaka 2013 tulimwita tukamuamuru aifunge na tukamuelekeza utaratibu anaopaswa kuufuata ikiwa ni pamoja na kuomba kibali serikalini, lakini hakufanya hivyo.

“Machi 20, 2016 tulifuatilia na kubaini kwamba Shule ya Elite English Medium bado ilikuwa inaendelea kutoa huduma ya elimu bila kurekebisha kasoro zilizopo, hivyo tulichukua hatua ya kumwandikia mmiliki wake barua ya maelekezo lakini alipuuza.

Mwombeki amesema Kabla ya hapo, walimuandikia barua  kwa nyakati tofauti tofauti, yaani Januari 2, 2013 na Oktoba 22, 2013 kumzuia kutoendelelea kutoa huduma ya elimu bila kibali lakini aliendelea kukaidi.

Akifafanua zaidi kuhusu uamuzi wa kuifunga shule hiyo, Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule Kanda ya Ziwa, Cheyo, amesema ukaguzi ulibaini kwamba hata walimu watano waliokuwa wakifundisha shuleni hapo; kati yao, watatu hawana vyeti vya taaluma hiyo.

“Tumemuamuru mmiliki husika aifunge shule hiyo na tumemwagiza asambaze wanafunzi kwenye shule mbalimbali zinazojiendesha kisheria. Tumechukua hatua hiyo kwa kuwa huyo mmiliki inaonekana ni mjeuri,” amesisitiza Cheyo.

Kutokana na hali hiyo, Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule Kanda ya Ziwa, Cheyo, ametoa wito kwa wazazi na walezi kujenga dhana ya kuhakiki uhalali wa shule kabla ya kuwapeleka watoto wao ili kuepuka matatizo yasiyo ya lazima.

BENKI YA KILIMO YAOMBWA KUTOA MIKOPO ARUSHA



Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega akihimiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (hayupo pichani) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha.
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kulia) akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki wakati akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga.
Meneja wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (kulia) akitoa takwimu za mahitaji ya mikopo ya mkoa wa Arusha. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. George Nyamrunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkabidhi muhtasari wa maeneo ya uwekezaji Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia).
Na Mwandishi wetu,           
Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuchangamkia fursa za uwekezaji katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo wakulima wanaojishughulisha katika sekta hizo mkoani Arusha ili kuchagiza sekta ya kilimo mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na ufugaji.
Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.
Bw. Assenga mkoa wa Arusha utaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.

MONGELLA ACHARUKA FEDHA ZA ELIMU

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amekiagiza chama cha Walimu Mkoa wa Mwanza (CWT) kuleta matokeo ya Wakuu wa Shule 28 waliosemekena kutumia fedha ya Elimu bila malipo kinyume cha utaratibu.

Amesema atakayethibitika amekula fedha hizo mara baada ya uchunguzi hawana budi kuondolewa na kwamba hakutakuwa na muda wa kuwavumilia.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa Elimu Wilaya ya Nyamagana amesema hakuna  mtu  atakeonewa na atakaethibitika ataondolewa kwenye Ukuu wa shule.

“Jambo hili nimeamua kulisema hapa kwa sababu lina minong,ono mingi kwamba watu wanaonewa hakuna mtu atakaeonewa,kubebwa wala kupendelewa kila mtu apate haki yake inayostahili”amesema Mongella.

Ameeleza kuwa fedha hizo ni moja ya ahadi ya Rais Mgufuli wakati wa kampeni zake na kwamba ni jambo ambalo alilifanya mara baada ya kuingia ofisini ambapo amesema licha ya fedha hizo kufika mashuleni bado hakidhi mahitaji.

“Licha ya kwamba fedha haitoshi lakini tutawezaje kuongezewa nyingine wakati hiyo tulionayo tunakula, leo hii ndugu zangu kuna shule hapa , wakuu wa shule mpo fedha ya shule iliyokuja ya elimu bila malipo wengine mmeshaimaliza hamjakaa hata na kamati za shule, wala bodi ya shule haijui kitu watu tunatakiwa tusome alama ya nyakati”ameeleza Mongella.

SASA NI RASMI FAINALI YA UEFA:- JUVENTUS KUKIPUTA DHIDI YA REAL MADRID


Hakuna siri tena baada ya fumbo kufumbuliwa, ni wazi sasa tena rasmi fainali ya UEFA Champions League 2017 inakwenda kuwakutanisha Kibibi kizee cha Turin Juventus dhidi ya Real Madrid.

Juventus kwa mara ya pili imefuzu katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya baada ya kuishinda Monaco kwa jumla ya mabao 4-1

Juventus ambao hawajashinda kombe hilo tangu 1996 na waliopoteza katika fainali ya mwaka 2015 dhidi ya Barcelona watakabiliana na Real Madrid walioshinda leo kwa jumla ya mabao 2-4, katika uwanja wa Cardiff mnamo tarehe 3 mwezi Juni.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LASTUKA MAPEMA LAJA KAMPENI YA UKAGUZI WA MAGARI YA SHULE.


TAREHE 10.05.2017
NA ZEPHANIA MANDIA / GSENGO BLOG.

SIKU chache baada ya ya kutokea kwa tukio la ajali mkoani Arusha na kusababisha vifo vya watu 32 , Polisi mkoani Mwanza wameanzisha zoezi la ukaguzi wa magari ya shule.


Zoezi hilo limefanyika jana tarehe 10 Mwezi May 2017 katika viwanja vya polisi Mabatini na zaidi yamagari 30 yanayobeba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari jijini Mwanza kukaguliwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi ameagiza kila gari la shule linabeba wanafunzi likaguliwe.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Robert Husein BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

Wednesday, May 10, 2017

SALUM MWALIMU AMTUMIA RAIS JPM, MAJALIWA NA MBOWE KUJINADI UCHAGUZI EALA.

Mgombea wa uwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kwa upande wa Chadema, Salum Mwalimu ametumia jina la Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kujinadi.

Wakati akihitimisha maombi yake ya kura baada ya kuulizwa maswali matatu na wabunge, Mwalimu amesema atakapovuka mpaka wa Tanzania kuiwakilisha katika mataifa mengine kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki endapo atachaguliwa atakuwa mwakilishi wa Taifa na si chama.

Mwalimu amesema hata akivuka mpaka Rais ni (John) Magufuli, Waziri Mkuu ni(Kassim) Majaliwa na (Freeman) Mbowe atabaki kuwa mwenyekiti wa chama, hivyo kuwahimiza wabunge kumchagua bila kujali itikadi za chama.

Wagombea wengine wa nafasi hiyo kwa Chadema ni Profesa Abdallah Safari, Pamela Massay,  Ezekia Wenje, Lawrence Masha  na  Josephine Lemoyan

MAN UNITED NA UZI WAO MPYA KWA MSIMU UJAO.


Manchester United mapemaa imeamua kuuweka hadharani uzi wake mpya wa msimu wa 2017/18.
Uzi huo unaonekana kurudisha kumbukumbu ya Man United kuhusiana na jezi za enzo hizoo wakati wa kipindi cha Alex Ferguson na wachezaji kama Ryan Giggs walikuwa wakichipukia.



WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA 2017/2018

 Waziri wa Mambo ya  Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe  Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kushoto  ni  Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na makamanda wa Jeshi la Polisi muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge la Bajeti ambapo wizara yake iliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Waziri wa Mambo ya  Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akifurahia na baadhi ya wabunge mara baada ya kumaliza kuwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe  Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

ASKARI 4 WA KULINDA AMANI WA UN WAUAWA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI.


Askari 12 wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa MINUSCA wameuawa na kujeruhiwa baada ya msafara wa magari yao kutekwa nyara na kushambuliwa na genge la waasi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Stephane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema wanajeshi wanne wa UN wameuawa huku wanane wakiachwa na majeraha mabaya, baada ya kuzuka makabiliano kati yao na kundi la waasi wa Kikristo la Anti-Balaka, karibu na eneo la Bangassou, yapata kilomita 474 mashariki mwa mji mkuu, Bangui Jumatatu usiku.

Amesema mbali na mauaji na majeraha hayo, askari mmoja wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoweka na hatima yake haijulikani hadi sasa.

Wapiganaji wa Kikristo wa Anti-Balaka huko CAR
Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres ametoa taarifa ya kulaani mashambulizi hayo dhidi ya maafisa wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, akisisitiza kuwa kuhujumiwa askari wa umoja huo ni sawa na jinai za kivita.
 Mapigano ya hivi karibuni katika miji ya Bambari, Ouaka, Mkoa wa Kati na Makoum, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mbali na kuua makumi ya raia, yamesasabisha maelfu ya raia wa nchi hiyo kukimbilia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya Rais François Bozizé.

MTI WAUA WATANO ARUSHA.

 Watu watano wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na mti wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Watu watano wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na mti wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao wilayani Arumeru mkoani Arusha.


Tuesday, May 9, 2017

KWA SASA MAFUTA YANASAKWA KAMA DHAHABU NCHINI BURUNDI.

Na nchini Burundi uhaba wa fuel kwa ajili ya vyombo vya usafiri umeendelea kushuhudiwa licha ya serikali ya Bujumbura kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kupitisha sharia mpya za ugavi wa nishati hiyo.


Kutokana na hali hiyo, bei za usafiri nayo imeonekana kupanda kinyume na ilivyozoeleka. Hayo yanajiri katika hali ambayo, machafuko ya kisiasa yanatajwa kupungua kwa kiasi, ikilinganishwa na kipindi cha miaka miwili iliyopita, hasa baada ya kuibuka mgogogro wa kisiasa uliosababishwa na hatua ya Rais Nkurunziza kugombea kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais uliopita.
Foleni zikiendelea kushuhudiwa katika vituo vya uuzaji mafuta Burundi.

WAKOREA WAFANYA MABADILIKO WAMCHAGUA MOON JAE KUWA RAIS WAO.



Wapiga kura nchini Korea Kusini wamemchagua Moon Jae-in kuwa rais mpya wa taifa hilo, utafiti wa baada ya uchaguzi unaonesha.

Makadirio yanaonesha Bw Moon alipata 41.4% ya kura, mpinzani wake wa karibu mhafidhina Hong Joon-Pyo, akiwa na 23.3%.

Bw Moon amekuwa akiunga mkono kufanyika kwa mazungumzo na Korea Kaskazini, jambo ambalo litabadilisha sera ya sasa ya Korea Kusini.

Uchaguzi huo wa mapema uliitishwa baada ya Park Geun-hye kuondolewa madarakani kutokana na tuhuma za ufisadi.

Bi Park alidaiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu kuitisha pesa kutoka kwa kampuni mbalimbali kwa kutumia jina lake, tuhuma ambazo amezikanusha.

Iwapo Bw Moon atathibitishwa kwua mshindi, huenda akaapishwa Jumatano.

Utafiti wa baada ya uchaguzi ulifanywa kwa pamoja na vituo vitatu vya runinga nchini humo.

Moon ni nani?
Ni mwana wa wakimbizi waliotoka Korea Kaskazini.

Bw Moon alifungwa jela alipokuwa mwanafunzi miaka ya 1970 kwa kuongoza maandamano dhidi ya kiongozi wa zamani wa kijeshi Park Chung-hee - babake Bi Park.

Baadaye alihudumu katika vikosi maalum vya wanajeshi wa Korea Kusini kabla ya kuwa wakili wa haki za kibinadamu.

Bw Moon, ambaye chama chake cha Democratic Party ni cha mrengo wa kati-kushoto, aliwania urais dhidi ya Bi Park mwaka 2012 lakini akashindwa.

Alijipigia debe kama mtu ambaye anaweza kusongeza taifa hilo mbele kutoka kipindi cha misukosuko na kashfa chini ya Bi Park.

"Nahisi kwamba sio mimi pekee na chama change bali pia watu wenyewe wanataka serikali ya mabadiliko," alisema alipokuwa anapiga kura.

Sera zake?
Bw Moon amekuwa akiunga mkono kufanyika kwa mazungumzo na Korea kaskazini lakini kuendelee kwua na shinikizo na vikwazo dhidi ya utawala wa taifa hilo.

Hili ni kinyume na serikali ya Bi Park aliyekatiza karibu uhusiano wote na Korea Kaskazini.

Amekuwa akikosoa serikali mbili za awali kwa kushindwa kuzuia mradi wa Korea Kaskazini kustawisha silaha.

Lakini ingawa wasiwasi katika rasi ya Korea ulifanya uchaguzi huo kufuatiliwa kwa karibu, walichoangazia zaidi raia wa Korea Kusini ni kukomesha ufisadi na kuimarisha uchumi. Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana umekithiri.

Bw Moon amezungumzia pia wazo la kufanyia mageuzi kampuni kubwa zinazomilikuwa na familia nchini humo, ambazo hutawala uzalishaji na uchumi.

YANGA IYOOOooo KILELENI.

VIDEO
Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans, wamerudi kileleni rasmi baada ya kuwachakaza wapinzani wao Kagera Sugar bao 2-1 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Timu ya Yanga iliweza kujiandikia bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Saimoni Msuva katika dakika 38 za mchezo katika kipindi cha kwanza na kuisababisha Kagera Sugar kuanza upya mashambulizi yake na hatimaye yaliweza kuzaa matunda kwa kuweza kusawazisha bao hilo ndani ya dakika  45 (+2) za nyongeza kabla kipindi cha kwanza kuisha kwa kupitia mchezaji wake Mbaraka Yusufu.





Mara tu timu hizo ziliporejea kutoka mapumziko, hali ya mchezo ilionekana ya tofauti kutokana timu zote zikishambuliana kwa nguvu nyingi ili kuhakikisha kupata ushindi lakini bahati ikaangukia kwa Yanga katika dakika 53 za mchezo waliweza kuona nyavu za wapinzani wao kwa mara ya pili kwa kupitia krosi matata kutoka kwa Haruna Niyonzima na kumaliziwa golini na Obrey Chirwa.

Kwa ushindi huo timu ya Yanga kwa sasa ndiyo imekuwa inaongoza ligi kuu kwa pointi 62

PRESS RELEASE: STELLA MWANGI’S “BIG GIRL” PICKED AS SOUNDTRACK FOR “ROUGH NIGHT” FEATURING SCARLET JOHANSSON


PRESS RELEASE: 

STELLA MWANGI’S “BIG GIRL” PICKED AS SOUNDTRACK FOR HOLLYWOOD FILM “ROUGH NIGHT” FEAT. SCARLET JOHANSSON

It’s the year of Stella Mwangi! Her smash hit - BIG GIRL off her self- titled EP has been picked as the official trailer soundtrack for Hollywood film Rough Night starring mega star Scarlet Johansson.  The movie is set to premier in theatres (16th June 2017). This is a major milestone for the multi-talented Kenyan – Norwegian artiste who has been making Hollywood headlines with her EP since its release in 2016. Stella is the first Kenyan to have her music featured in several Hollywood projects. From BET’s Being Mary Jane to FOX’s Rosewood, Stella continues to receive Hollywood certification and this move has guaranteed more recognition for Stella Mwangi in terms of the Hollywood film community and key placements.

Here’s the Rough Night Trailer featuring BIG GIRLhttps://www.youtube.com/watch? v=b4ae1928XTY

An elated Stella announced the news via her Facebook profile on Monday 8th May: "I am excited to confirm that 'Big Girl' off my latest EP Album #StellaMwangi is soundtrack to Hollywood movie #RoughtNightMovie starring Scarlet Johansson, Kate McKinnon, Zoe Kravitz, Jillian Bell and Ilana Glazer," adding "Check outroughnightmovie.com for ticket details."


BIG GIRL, the first single off the EP is a certified club hit with Stella’s distinct and authentic hip hop flow.  In 2016, the song was leased to Donut Media – an American production that specializes in producing TV and YouTube content on the freshest car, motorsports, supercars, auto news and car and prank videos every week.

EDITORS’ NOTES:
Stella Mwangi’s EP is a fusion of songs with high energy and her distinct Hip Hop flow that unites her fans across the globe. The EP has been breaking ground in Europe. The fifth single off her super successful self-titled EP WORK was recently ranked at number 18 on the Italian Top 100 Radio charts and beat David Guetta and Sean Paul in Italy (DJ Damasco) radio chart in April.

STELLA MWANGI EP LINKS:

FOR MORE: