ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 7, 2015

SERIKALI YA JAPAN YAIPATIA MSAADA WA DOLA LAKI 1.4 HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati alipowasili nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki Jijini Dar es salaam,kulikofanyika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) akionyesha kitu kwenye karatasi kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine,wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga akitoa hotuba yake mbele ya Ujumbe wa Wilaya ya Monduli pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakisaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Monduli.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.Wengine pichani ni Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine (katikati),Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Idara ya Miradi wa Ubalozi wa Japan nchini,Takashi Higuchi.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakibadilishana mikataba mara baada ya kuisaini,wakati wa hafla ya fupi iliyofanyika leo nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki jijini Dar.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri ya Monduli dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi miwili ya wilaya hiyo.Wengine pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine akitoa akizungumza machache mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga mara baada ya hafla hiyo.

Friday, March 6, 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA STUDIO MPYA ZA AZAM TV JIJINI DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa Studio mpya za Azam Tv zilizoko Tabata jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa Studio mpya za Azam Tv zilizoko Tabata jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Azam Tv Said Salim Bakhresa.
Mazungumzo.
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando.
Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza Kampuni za vyombo vya habari zikiwemo idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Mwananchi Communications Limited (MCL) amesema kuwa studio hizo zina ubora kuliko nyingine zote nchini.

Jumla ya dola za Kimarekani milioni 31 (zaidi ya sh. Bilioni 56 za Tanzania) zimetumika kutengeneza studio mpya za kisasa za Azam Tv, zilizopo eneo la Tabata jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Tv Rhys Torrington.
Mc wa uzinduzi ni Taji Liundi.
Jicho la kamera.
Mwanamuziki Barnaba akiburudisha.
Wageni waalikwa.
Eneo la tukio meza kuu na wageni waalikwa.
Sehemu ya studio mpya za Azam Tv zilizoko Tabata jijini Dar es salaam.

CHAMELEONE AJA NA ONLY YOU AKIMSHIRIKISHA PATO RANKING


Baada ya kuliteka na kulikamata vyema soko la muziki wa jana na hata leo, Mwanamuziki mwenye mafanikio kutoka nchini Uganda Jose Chameleone ameachia hewani mkwaju wake mpya na safari hii akivuka mipaka hadi nchini Nigeria, na sasa ana mshirikisha msanii toka pale anaitwa Pato Ranking.

Mkwaju unaitwa 'ONLY YOU' BOFYA PLAY KUUSIKILIZA.  

WANAKIJIJI CHA OLOLOSOKWAN WAIPA AIRTEL HEKO/SHUKRANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro (kutoka kulia), Diwani wa kata hiyo, Yannick Ndoinyo, Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali.
Diwani wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, Yannick Ndoinyo, (kulia), akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), wakati baadhi ya viongozi wa kata hiyo, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali. Wa (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali. Wa (pili kushoto) ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa UNESCO, Al-Amin Yusuph (wa pili kulia), aliyeongozana na baadhi ya viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali. 

Wengine ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi (wa tatu kulia) na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa

SADIFA VIPAJI VYA WASANII WA SARAKASI VIMULIKWE NA TAASISI ZA MAJESHI NA KUPEWA AJIRA IKIWEMO KUVIENDELEZA

Kijana Hamis Juma (20), mkazi wa kijiji cha Songiwe Kata ya Misasi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambaye ni msanii wa mchezo wa sarakasi, akionyesha umahili wake wa kipaji cha kutembea juu ya kamba huku akicheza muziki wa nyimbo za Injili za msanii Rose Mhando wakati alipotoa burudani kwenye sherehe za kuapishwa kwa Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Charles Kitwanga, wilayani humo hivi karibuni. 
 
NA PETER FABIAN, MISUNGWI.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Sadifa Juma Hamis, amezitaka taasisi za majeshi na Wizara ya Utamaduni Vijana na Michezo kuzipa kupaumbele vipaji vya sanaa zingine ili kuvipatia ajira na kuviendeleza badala ya kuegemea kwenye vipaji vya soka pekee.

Sadifa Hamis ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Donge Unguja Zanzibar, alitoa kauli hiyo hivi karibuni wilayani Misungwi wakati wa sherehe za kuapishwa Kamanda mpya wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Charles Kitwanga “Mawe matatu” ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini.

Mwenyekiti huyo alimtaja kijana Hamis Juma (20) mkazi wa kijiji cha Songiwe Kata Misasi wilayani humo ambaye ni msanii wa michezo ya sarakasi aliyekosa mtu wa kumsimamia na kumsaidia kuendelea kipaji chake katika vyuo vya sanaa ikiwemo elimu ili kunufaika na kuweza kujiajili au kuajiliwa na taasisi hizo badala ya kung’ania kumlika vipaji vya soka pekee.

“Msanii huyu wa fani ya sarakasi ni mahili kweli, nimedokezwa kuwa anatoka kijijini na amekuwa akitoa burudani ya hamasa sehemu mbalimbali anapoalikwa, lakini mchezo anaoucheza kuwaburudisha ni hatari kwa maisha yake kutokana na kutembea juu ya kamba kwa miguu yake huku akichezea chupa na akiruka na kujikunja kama jongoo,”alisema.

Sadifa, alisema kwamba kutokana na kijana Juma kuonyesha kipaji chake na umahili wa kutembea juu ya kamba , amekusudia kumualika jimboni kwake ili kuhakikisha wananchi wake wanamuona na kupata burudani ikizingatiwa fani hiyo ni miongoni mwa michezo aliyokuwa akiicheza na kuipenda kabla ya kuwa kiongozi.

“Ntapeleka taarifa za kijana huyu kwa viongozi wa taasisi za majeshi, Waziri wa Vijana Utamaduni na Michezo hata kumsemea Bungeni ili kuweza kumtafuta na kukiona kipaji chake na wakiendeleze zaidi na kuwa mwanamichezo wa kimataifa, huku vijijini nimegundua vipaji vipo ila havijulikani kutokana na kutojitangaza na kupata watu wa kuwachukua,”alisisitiza.

Kwa upande  kijana Juma alisema ujuzi na kipaji hicho ni cha kuzaliwa nacho na hakuwahi kujifunza katika Chuo chochote zaidi ya kucheza kwa ubunifu na tahadhari kubwa ikizingatiwa maeneo anayoishi na kutoka hayana huduma nzuri ya Hospitali endapo ataumia na kupata majeruhi, pia sanaa hiyo ndo ajira yake ya kujipatia mkate wa kila siku.

Naye Kamanda Kitwanga, alisema amekunwa na kijana huyo atajitahidi kumtafutia Chuo cha kupata ujuzi zaidi na kujiendeleza kama vile Chuo cha sanaa Bagamoyo ili kumuwezesha kuwa mkali zaidi wa sanaa hiyo na ikiwezekana aweze kumulikwa na kuchukuliwa na taasisi za majeshi kusaidia kulinda kipaji chake na kukiendeleza.

SKYLIGHT BAND YAENDELEA KUPIGA JALAMBA, NI KILA IJUMAA NDANI YA KIOTA CHA THAI VILLAGE, SIYO YA KUKOSA LEO.

DSC_0155
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa na mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower (kushoto) kutoa burudani kwa mashabiki wake Ijumaa iliyopita ndani ukumbi wa maraha Thai Village Masaki jijini Dar... Ni Ijumaa hii tena watatoa burudani ya aina yake kutoka kwa waimbaji mahiri na wabunifu... Kutoka kulia ni Sam Mapenzi, Ashura Kitenge na Sony Masamba.
DSC_0075
Binti mrembo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti na Meneja wa Band, Aneth Kushaba AK47 katika show yao ya Ijumaa iliyopita ndani ya koita cha Thai Village-Masaki.
DSC_0117
Sam Mapenzi akisikilizia Back Vocal kutoka kwa Mkali wa R&B John Music wakati akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa maraha Thai Village Masaki.
DSC_0136
Mashabiki wa Skylight Band wakijinafasi kwenye dancing floor Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Thai Village uliopo Masaki jijini Dar.
DSC_0104
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiwapa burudani mashabiki wa bendi hiyo huku akisindikizwa Ashura Kitenge.
DSC_0152
Mashabiki wa Skylight Band wakifanya yao.
DSC_0108
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani.
DSC_0160
Mashabiki nao wakajibu mapigo.
DSC_0162
I’m looking for my Johnny……I’m looking for my honey…ya ya ya….you telling me this, you telling me that….I say this is not for me….Johnny do me corny….Johnny do me corny... 
DSC_0171
DSC_0181
Number one fans wa Skylight Band...hawa jamaa mpaka Mwanza watia maguu ni jinsi gani Band hii ilivyokuwa kwenye damu zao.
DSC_0183
Customer care katika pozi matata sana....
DSC_0190
Mdau wa Skylight Band, Gerald Kilimo (kushoto), Aneth Kushaba AK47 pamoja na @eddievied wakipata Ukodak.
DSC_0193
Mdau Mulle na mratibu wa Skylight Band, Lubea wakiibia Ukodak.
DSC_0201
Aneth Kushaba AK47 akipata ukodak na shabiki wake.

Thursday, March 5, 2015

ALBINO WAZUSHA VURUGU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania wakiwasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyewakaribisha ili kuwasikiliaza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​. Hata hivyo mkutano huo baadaye uliingia dosari. 
CHANZO:BBC SWAHILI
Vurugu zilizofanywa na baadhi ya walemavu wa ngozi Albino katika Ikulu ya Tanzania zimesababisha kuahirishwa kwa kikao kati ya viongozi wao na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete alikuwa akitarajiwa kufanya mkutano na viongozi wa Albino Tanzania TAS aliowaalika kuzungumzia hoja zao kutokana na mauaji ya walemavu hao yanayoendelea nchini humo.
Lakini heka heka iliyotokea katika eneo la mapokezi iliwalazimu maafisa wa Ikulu kuwatawanya walemavu hao.
Ni muda mfupi baada ya ukaguzi kuanza kufanyika katika moja ya lango la kuingilia Ikulu,kundi moja la walemavu hao waliokuwa katika moja ya chumba wakaanzisha malalamiko kwa sauti huku viongozi wao wakiwa wanajiandaa kuruhusiwa na kuingia ndani.
Kelele hizo na mabishano hayo miongoni mwa walemavu hao kwa mbali ikaanza kuonekana ni dosari namba moja hasa baada ya kupandisha mori na kila mtu kuanza kusema lake kupinga ushiriki wa viongozi hao
Kutokana na vurugu hizo maafisa wa Ikulu waliwatawanya Walemavu hao kutoka nje ya Geti , na hapo ikawa mwanzo wa sakata jipya baada ya kuanza kulumbana na viongozi wao na hatimaye kuanza kupigana na mambo yakawa hivi.Baada ya kutulizwa ugomvi kilichofuata ni nyimbo za kupinga uhalali wa viongozi wao
Hata hivyi vurugu hizi zinatazamwa tofauti na baadhi ya walemavu hao,ambao wanasema ni vurugu hizo zimepoteza fursa ya kuwasilisha matatizo yao kwa Rais.
RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA ALBINO TANZANIA
 IKULU JIJINI DAR 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo. Walioketi kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akiongea na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania baad ya kukutana nao pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU