ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 10, 2016

BREAKING NEWS: TETEMEKO KUBWA LIMEIKUMBA MWANZA, BUKOBA, CHATO NA MUSOMA

 Hali ya taharuki imelikumba leo jiji la Mwanza kwenye majira ya saa 9:40 alasili baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi ambalo liliweza kudumu kwa muda wa dakika kadhaa.

Hali ilikuwa tete kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali ambao either makazi yao au shughuli zao ziko kwenye majengo marefu mjini hapa kwani walilazimika kubanana kwenye milango ya kutokea al-muradi kila mmoja kutaka kuendoka kwenye majengo hayo na jitihada za kujinusuru. 

Mpaka sasa Jembe Fm inaendelea kukusanya taarifa kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza kubaini athari zilizoweza kujitokeza.
KUSIKILIZA KILICHOTOKEA BOFYA PLAY (SAUTI KUKUJIA HIVI PUNDE)


KUTOKA HUKO BUKOBA Nyumba kadhaa zimeanguka mjini manispaa na halmashauri ya Bukoba, baada ya kutokea tetemeko la ardhi ambayo kipimo chake akijaripotiwa, huku taarifa kutoka Misenyi zinasema taharuki imetanda na wakaazi wametoka nje ya nyumba ilhali taarifa za majeruhi na vifo hazijatolewa ingawa tumeshuudia watu wakikimbizwa hospitalini. Tutawaletea undani.
Pia inasemekana Tetemeko hilo limetokea CHATO NA MUSOMA..

VIGOGO 6 UKAWA WAKUTANA FARAGHA, FAO LA KUJITOA LAGEUKA MWIBA, LISSU KUWATETEA WATUHUMIWA WA KUIKASHIFU SERIKALI.

Vigogo 6 UKAWA wakutana faragha, Fao la kujitoa lageuka mwiba, Lissu kuwatetea watuhumiwa wa kuikashifu serikali. Pata undani wa dondoo hizi hapa; 

Bibi wa jumba la treni aondolewa, Sheria uhalali wa mtoto yaja, UKAWA na Dk. Tulia watifuana tena, CUF: Lipumba anaweza kurudi. Pata undani wa dondoo hizi hapa; 

PICHA: ILIVYOKUWA KWENYE USIKU WA OZONA MISS LAKE ZONE TALENT SEARCH.

Usiku wa Septemba katika kiwanja cha Jembe Beach Resort Warembo mbali mbali wameshindanishwa kwa ajili ya kuonesha  vipaji vyao tofauti tofauti ikiwemo kuimba na kuigiza pamoja na masuala ya urembo ambapo warembo wengi kanda ya ziwa waejitokeza kushiriki kaatika tukio hilo.Unaweza kucheki picha za matukio yote Kupitia Gsengo Blog.


Mwandaaji wa Tamasha hilo Frola akitoa neno.

Friday, September 9, 2016

PICHA ZA MATAYARISHO YA LEO AT JEMBE BEACH USIKU WA OZONA MISS LAKE ZONE TALENT SEARCH

Sound Cheki ikiendelea hapa Jembe Beach Resort Mwanza kuelekea Pre- Part ya Ozona Miss Lake Zone 2016 itakayopigwa usiku huu hapa, warembo wote watashindanishwa katika sekta ya kuonesha vipaji mbalimbali wakijiachia zaidi ili kuwa kielelezo cha fainali itakayoigwa kesho pale Rock City Mall Mwanza.

Wadhamini wote watakutana ikiwa ni wa mara ya kwanza, wafanyabiashara, wajanja wa town, marafiki, ndugu mashabiki wa Jembe Fm ndani kwaajili ya kupata picha nzuri za kumbukumbu.
Marekebisho ya mwisho.
Eneo la Bustani ya Jembe Beach Resort Malimbe Mwanza.
Engo ya wajanja wasiopenda kelele.
Bustani engo ya VIP one.
Mazingira na jiografia ya yanayoizunguka himaya ya Jembe Beach Resort Mwanza.
The angle kuelekea Club.
Mazingira dot Com.
Angle nyingine.
Mtangazaji wa kipindi cha Hot Stage ya Jembe FM Bonz Balaa akijinoma na mishkaki ya kuku + ugali na dagaa wakukaanga.
Hip Hop kwa chati...toka kilima cha Jembe ni Jembe Malimbe Mwanza Tanzania...yaaani full utalii.
Jiografia na picha toka kwa juu.
Karibu sana ukiku huu wa tarehe 9/sept/2016