ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 29, 2018

BREAKING NEWS:- SIKU YA 9 MV NYERERE YASIMAMA WIMA ASILIMIA 100, WAMEKUTA NINI NDANI?NA. GSENGOtV
UKARA

Siku tisa zinakamilika hii leo tangu taifa la Tanzania kupoteza zaidi ya watu 220 kwenye ajali ya kupinduka majini kwa kivuko cha #MvNyerere. Gari ya mizigo aina ya Canter tani 1 na nusu, Pikipiki 1 yenye namba za usajili DFPA 2313 na baiskeli ambayo bila shaka ilikuwa ya mkulima.

Vyote hivyo vimeokotwa ndani ya maji na wazamiaji maalum wakishirikiana na wazawa eneo lilelile la ajali. 

Katika hatua nyingine ya kufunga zoezi la upokeaji michango, Kamati ya Maafa iliyochini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe, hii leo kabla ya saa 7 mchana (muda wa kuhitimisha zoezi la uokoaji na upokeaji michango) imepokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 50 toka Kampuni ya Uzalishaji Umeme Tanzania (SONGAS)  pamoja na hundi nyingine ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni 80 kutoka kwa ACACIA, fedha ambazo zote tayari zimeingizwa benki.

 Kwa sasa kivuko kiko wima kwa asilimia 100% pembezoni mwa ufukwe wa ziwa Victoria kijiji cha Bwisya, Ukara, wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. 

Tangu walipoanza kazi hiyo asubuhi leo Septemba 29, 2018, wazamiaji tayari wameopoa pikipiki moja na baiskeli, jana walifanikiwa kutoa gari aina ya Toyota Canter.
Mikoba ya mikononi, mifuko yenye bidhaa za aina mbalimbali za viatu vya watu wazima na watoto ni miongoni mwa mali zinayoopolewa kutoka chini ya maji.
Vitu vingine vinatolewa katika kivuko hicho ambacho tayari kimevutwa hadi pwani ya mwalo la kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Kivuko cha Mv Nyerere kilipopinduka Septemba 20 na kusababisha vifo vya watu 230 huku watu 41 wakiokolewa.


Thursday, September 27, 2018

DR. REGINALD MENGI AGUSWA NA MKAKATI WA RC MAKONDA KUSAIDIA WALEMAVU, AMUAHIDI BILIONI 5 KWAAJILI YA UJENZI KIWANDA CHA KUAJIRI WALEMAVU DAR

.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika mkakati wake wa kuwapa tumaini jipya watu wenye ulemavu leo ameahidiwa Kiasi cha Shilingi Billion 5 na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi kwaajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachowaajiri watu wenye ulemavu ambao wana ujuzi wa aina mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi.

 Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kueleza mpango wa kuwasiliana na wizara ya ardhi ombi la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda cha kuajiri watu wenye ulemavu jambo lililomgusa Dr. Mengi na kuahidi kutoa shilingi billion 5 kuunga mkono mpango huo.

 Hayo yote yamejiri leo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya kusaidia walemavu ya Dr. Reginald Mengi persons with disabilities Foundation iliyozinduliwa na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia amemsifu RC Makonda kwa agizo alilotoa kwa wenye viwanda kuwapa ajira walemavu kwa mujibu wa sheria na pia kampeni ya miguu bandia inayoendelea kuwasaidia walemavu. 

 Aidha RC Makonda pia ameeleza Mkakati wa kukutana na wamiliki wa shule binafsi kwaajili ya kuwaomba kusomesha watoto wawili wenye ulemavu bure kwa kila shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari ili kuwawezesha walemavu kupata elimu bora. 

 Kwa upande wake Naibu waziri Wizara ya Ajira, Wazee, watoto na watu wenye ulemavu Mhe. Anton Mavunde, Mbunge wa viti maalumu Mhe. Amina Molel na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyopambana kuwakwamua watu wenye ulemavu. 

 HUU SIO WAKATI KWA WALEMAVU KULIA WALA KUJUTA, NI WAKATI WA KUINUKA.

CHELSEA YAIBAMIZA LIVERPOOL KWENYE KOMBE LA MBUZI.ʟɪᴠᴇʀᴘᴏᴏʟ ᴠѕ ᴄʜᴇʟѕᴇᴀ ـ ʜɪɢʜʟɪɢʜᴛѕ

Wednesday, September 26, 2018

SHINDA BAJAJ NA SPORTS PESA ILIPOTINGA MWANZA


NA GSENGOtV
Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa tayari imezindua rasmi kampeni ya SHINDA NA SPORTPESA itakayodumu kwa siku 100 (SIKU 100 BAJAJ 100) ambapo mshindi mmoja ataweza kujishindia TVS KING mpya kila siku.

Kwenye promosheni hiyo ambayo tayari washindi wamekwishaanza kujinyakulia Bajaj zao, lakini pia kutakuwa na zawadi nyingine zinazoshindaniwa ambazo ni pamoja na tiketi tatu kwenda nchini Uingereza kutazama mechi ya EPL, tiketi moja ikitolewa kila mwezi sambamba na jezi orijino zitakazotolewa kila wiki.

Kwa ufupi sana Mwanza ilikuwaje....
WATU WAWILI WAUAWA NA KUTOLEWA VIUNGO GEITA.

Wakazi wawili wa Kijiji cha Lubanga mkoani Geita wameuwawa kwa kukatwa mapanga na kunyofolewa viungo mbalimbali vya mwili, tukio linalodaiwa kufanywa na watu wasiojulikana na kutoweka na viungo hivyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani humo wakati akizungumza na www.eatv.tv , Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki na waliouawa ni mtu na shangazi yake suala ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.

Kamanda Mponjoli amewataja waliouawa kuwa ni Kija Lushanga (70) na Pendo Bukelebe (48) ambapo amesema kuwa imani potofu za kishirikina imekuwa jambo la kawaida kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa na ni changamoto kwa Jeshi la Polisi katika majukumu yake kwani matukio mengi yanafanywa na wanafamilia.

“Kufuatia mauaji hayo jeshi la polisi tumekamata watu wanne kwa mahojiano na uchunguzi bado unaendelea na hatuwezi wataja kutokana na sababu za kiusalama, lakini Kanda ya Ziwa hakuna uelewa wa wananchi kutoamini kuwa imani za kishirikina ni matatizo na wao kujichukulia sheria mkononi”, amesema Mponjoli

Ameongeza kuwa, “Jamii inayozunguka eneo hili inahusisha mauaji haya na imani za kishirikina lakini sisi kama Jeshi la Polisi kwa sasa tunachukulia kuwa ni mauaji isipokuwa tutakapokamilisha uchunguzi ndio tutajua nini kiini cha mauaji na watu kuondoka na viungo hivyo”.

Mkoa wa Geita ni miongoni mwa mikoa yenye matukio ya mauaji ya wanawake kukatwa mapanga kutokana na kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo Mei 17, 2018 Sophia Sitta mkazi wa kijiji cha Mwabasabhi wilayani Chato aliuawa na mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

April 05, 2018 wanawake wanne wilayani Nyang’hwale waliuawa kwa kunyongwa kisha miili yao kutupwa porini. Juni 06 ,2018 polisi walimuua kwa kumpiga risasi Panda Kinasa (36) ambaye alikua akiteka watu kudai fedha kisha kuwaua.

Takwimu za polisi za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa watu 32 walipoteza maisha mkoani Geita kwa kipindi cha miezi mitatu Oktoba Disemba 2015 kutokana na mauji ya kutumia mapanga yanayodaiwa kusababishwa na imani za kishirikina.

Tuesday, September 25, 2018

MBUNGE WA JIMBO LA KWIMBA SHANIF MANSOOR,AFUNGUA BARABARA ZA VIJIJI AMBAZO ZILIKUWA HAZIPITIKI JIMBONI KWAKE.NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

MBUNGE wa jimbo la Kwimba Shanif Mansoor amefungua barabara za vijiji jimboni kwake ambazo kwa kipindi kirefu zilikuwa hazitumiki kwa kuwa zilikuwa hazipitiki kutokana na ubovu kwa barabara hizo.

Aidha Mhe. Mansoor ametembelea pia kukagua upanuzi wa Kituo cha Afya Mwamashimba ambacho kipo katika hatua ya mwanzo ya ujenzi.

Moja ya adha kubwa wanayoipata wananchi Jimbo la Kwimba kwa kipindi kirefu imekuwa uhaba wa kupatikana huduma za afya, hivyo upanuzi huo utasaidia kuwa na hakika ya usalama wa afya kwa wananchi hasa wanawake na watoto.
ELIMU YA MASAFA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI.

 Dkt. Peter Kilima kutoka Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta za umma PS3, akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya Elimu kwa Masafa kwa Madiwani.
 Dkt. Adephonce Fuka, kutoka Chuo kikuu Huria akitoa mada kuhusu mwenendo wa Elimu ya Masafa kwa Madiwani katika Mkutano wa 34 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa ALAT jijini Dodoma.


 Baadhi ya Madiwani wakiwa katika Mkutano huo wa 34 wa Jumuiya ya ALAT, huku wakitazama na kuona jinsi watakavyokuwa wakinufaika na Elimu ya Masafa kupitia Simu zao za Adroidi. (Picha na Habari na Atley Kuni wa OR TAMISEMI)


Elimu ya Msafa kuwajengea uwezo MadiwaniNa. Atley Kuni- OR TAMISEMIMadiwani kote nchini wataanza kupata mafunzo ya uongozi kwanjia   ya   masafa   kupitia   mtandao   wa   kielektroniki,   yaani   kupitiamfumo   wa   intaneti,   hali   itakayowawezesha   kujiimarisha   katikautendaji wa majukumu yao ya kila siku na kuwatumikia wananchi.

Akitoa mada katika mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Serikaliza   Mitaa   nchini,   Mhadhiri   wa   chuo   Chuo   Kikuu   Huria,   Dkt.Adephonce   Fuka,   alisema   shabaha   ya   mafunzo   hayo   nikuwajengea uwezo Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchikatika maeneo yao.

 Akizungumza wakati wa mawasilisho, Dkt. Fuka alisema nia kuu nikuhakikisha Madiwani  wanatekeleza  majukumu   yao   kwa mujibuwa   sheria,   taratibu   na   kanuni   zinazoongoza   mabaraza   yamadiwani, na mafunzo hayo ni maboresho ya kitabu cha rejea yaMh.   Diwani   kilichotumika   kufundisha   Madiwani   kutoka  Mamlakaza Serikali za Mitaa 93 hapo awali.

Mafunzo   hayo   ambayo   yameandaliwa   kwa   mtindo   wa   Elimu-Masafa ili kuwezesha kujifunza mahali popote, yataendeshwa naChuo cha Serikali za Mitaa - Hombolo, na  ni marejeo ya mafunzoya awali ambayo yalitolewa kwa viongozi hao kwa Halmasahuri 93zilizopo chini ya mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma(PS3).

Akitoa maelezo ya awali kabla ya kutolewa kwa wasilisho la elimuhiyo ya masafa kwa njia ya kieletroniki, mwakilishi kutoka PS3,Dkt. Peter Kilima, alisema mradi huo unaofadhiliwa na Serikali yaMarekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani(USAID),   unafanya   kazi  katika  mikoa   13   na   Halmashauri   93   natayari umejipanga kutoa elimu kwa madiwani nchi nzima.

“Mradi   huu   ni   wa   miaka   mitano,   na   moja   ya   maeneotunayoimarisha ni mfumo ya Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Mfumo wa Kielektroniki.DKT ABBASI AKUNWA NA UTENDAJI, MAGEUZI YA RC GEITA


Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto mwenye kaunda suti ya blue) amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (katikati) kwa utendaji wake wa ubunifu na unaolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 25, 2018 akiambata na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) alipofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo katika ziara ya kufuatilia utendaji wa sekta ya habari.

Katika mazungumzo hayo Dkt. Abbasi amemueleza Mhandisi Gabriel kuwa mafanikio hayo ya Geita na mengine ambayo Serikali kwa ujumla inayatekeleza umuhimu yanapaswa kutangazwa na kutetewa kwa kuwa yana manufaa nakubwa kwa wananchi.

Katika mazungumzo RC Gabriel alisema mkoa wake umehakikisha mapato kutoka kwa makampuni ya madini yanatumika kuondoa adha za wananchi katika sekta muhimu kama afya, elimu na wajasiriamali.

Alisisitiza kuwa katika sekta ya Afya wamepanga kuwa kufikia Mei, 2019 zahanati zote mkoani Geita zitakuwa zimekamilika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO), Bw. Pascal Shelutete amemuhakikishia Mhandisi Gabriel ushirikiano wa kutosha katika eneo la mawasiliano lengo ni kuhakikisha taarifa za Serikali zinawafikia wananchi.

Aidha, Bw. Shelutete pia amempongeza RC huyo kwa utendaji wake makini na wa kimageuzi  unaowagusa na kuwafunza wengi nchini.

LUKA MODRIC AVUNJA UFALME WA MESSI NA RONALDO.

Nyota wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric ametangazwa mchezaji bora wa dunia wa FIFA mwaka 2018 kwenye tuzo zilizotolewa usiku wa jana jijini London Uingereza.

Modric aliisaidia Real Madrid kutwaa klabu bingwa Ulaya pamoja na timu yake ya taifa ya Croatia kufika fainali ya kombe la dunia 2018 ambapo ilipoteza dhidi ya Ufaransa.

Orodha kamili ya washindi

MCHEZAJI BORA WA KIUME 

Nyota wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA 'FIFA Best Men's Player'. Amewashinda Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah.

MCHEZAJI BORA WA KIKE
Nyota wa Brazil na klabu ya Orlando Pride, Marta Vieira da Silva ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike.

GOLI BORA
Mohamed Salah ameshinda tuzo ya goli bora la mwaka 'Fifa Puskas Award' kupitia goli lake alilofunga dhidi ya Everton.

KOCHA BORA SOKA LA WANAUME
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps ameshinda tuzo ya kocha bora wa FIFA. Deschamps aliiwezesha Ufaransa kutwaa kombe la dunia 2018.

KIPA BORA 
Kipa wa Real Madrid na Ubelgiji ambaye msimu uliopita aling'aa na Chelsea Thibaut Courtois, ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mwaka.

KOCHA BORA SOKA LA WANAWAKE
Kocha wa timu ya wanawake ya Olympique Lyon ya Ufaransa, Reynald Pedros, ameshinda tuzo ya kocha bora wa soka la wanawake.

MASHABIKI BORA
Mashabiki wa timu ya taifa ya Peru wameshinda tuzo ya mashabiki bora wa Fifa, 'The Fifa Fan Award'

TUZO YA FAIR PLAY 
Mchezaji Lennart Thy wa klabu ya VVV-Venlo ya Uholanzi ameshinda tuzo ya 'FIFA Fair Play'. Lennart alikosa mechi ya ligi kati ya timu yake dhidi ya PSV Eindhoven akiwa ameenda kujitolea msaada kwa mgonjwa wa kansa.

KIKOSI BORA CHA FIFA

1. David de Gea
2. Dani Alves
3. Marcelo
4. Raphael Varane
5. Sergio Ramos
6. N'Golo Kante
7. Lionel Messi
8. Luka Modric
9. Kylian Mbappe
10. Eden Hazard
11. Cristiano Ronaldo

"SEHEMU PEKEE YA VIJANA KUIMARISHA KIPATO NI KUPITIA SEKTA YA KILIMO" DKT TIZEBA

Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu ya kujitolea kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 25 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela wakikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza wakati walipotembelea kambi maalumu ya vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga walioamua kufanya ujenzi kwa kujitolea, wakati akiwa safarini kuelekea Wilayani Korogwe leo tarehe 25 Septemba 2018.

Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu wakijitolea katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 25 Septemba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Muheza-Tanga

Imeelezwa kuwa sehemu pekee ya kuimarisha kilimo cha mwananchi mmoja mmoja, wananchi katika makundi ya kijamii hususani vijana ni kupitia sekta ya kilimo kwani ndio sehemu pekee ya ukombozi wa mkulima katika jamii.

Imeelezwa kuwa kuna uwezekano wa kufanya biashara mbalimbali nchini ambazo zinaweza kuongeza kipato lakini sahemu sahihi isiyokuwa na jazba na dhoruba katika utendaji ni kufanya kilimo biashara ambacho kamwe hakiwezi kumtupa mkulima.

Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo, ameyasema hayo leo tarehe 25 Septemba 2018 wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.

Vijana hao ambao wameamua kutumia nguvu zao pasina malipo wameamua kwa umoja wao kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kauli yake inayohamasisha chachu na juhudi za kiutendaji kwa wananchi ya "Hapa Kazi Tu".

Aidha, katika kuhamasisha juhudi za kiutendaji Waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo ameunga mkono juhudi za vijana hao kwa kuchangia fedha ya chakula shilingi 1,100,000 sambamba na kushiriki ujenzi wa jengo maalumu la upasuaji.

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alitembelea ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza akiwa safarini kutembelea mashamba ya mkonge ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya kikazi Mkoani Tanga aliyoianza jana tarehe 25 Septemba 2018 ya kukutana na makundi mbalimbali ya wakulima wa zao la Mkonge ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima wa zao hilo.

PICHA ZIARA YA MDAU WA MAENDELEO KUFUTA SIFURI.

 
Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Iyela,Ndele Mwaselela akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne ambao wapo kambi kwa ajili ya kujiandaa na Mitihani ya kidato cha nne mwaka hu ikiw ani mpango wa kutokomeza sifuri katika shule. 

Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Iyela,Ndele Mwaselela, akikabidhi Chakula kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Sekondari ya Iyela  ambapo mdau huyo wa Maendeleo alikabidhi gunia mbili za mchele.  

WAKULIMA WADOGO WA MKONGE WAIPINGA KAMPUNI YA KATANI MBELE YA WAZIRI WA KILIMO WATAKA MFUMO WA SOKO HURIA

Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi katika Wilaya ya Korogwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK, Tanga)
Kikao kazi wakulima wa zao la Mkonge na Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba kilichofanyika katika kijiji na kata ya Makuyuni Wilaya ya Korogwe  wakati wa ziara ya waziri huyo ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga, jana tarehe 24 Septemba 2018. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akitoa maelezo mafupi Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba kuhusu zao la Mkonge mkoani humo mbele ya wakulima wakulima katika kijiji na kata ya Makuyuni, Wilayani Korogwe jana tarehe 24 Septemba 2018. 
Wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi wilaya ya Korogwe wakifatilia kwa makini mkutano wa Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba wakati wa mkutano wa pamoja kujadili zao la Mkonge Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi wilaya ya Korogwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. 

Na Mathias Canal-WK, Tanga

Wakulima wadogo wa zao la mkonge Wilayani Korogwe mkoa wa Tanga, wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuanzisha soko huria kwa ajili ya ununuzi wa zao hilo ili malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha tani 100,000 kwa mwaka yafikiwe.

Wakulima hao wameilalamikia Kampuni ya Katani Ltd. kwamba inachukuwa asilimia 54 na kumuachia mkulima asilimia 46 jambo walilodai ni unyonyaji unaofanywa na kampuni hiyo kinyume na utaratibu wa kiutendaji.

Wakulima hao wametoa malalamiko yao mbele ya waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza na wananchi katika maeneo tofauti wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili kutekeleza maagizo aliyopewa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ya kutembelea mashamba ya Mkonge mkoani humo na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.

Katika mkutano huo pia wakulima hao walijadili suala la bei na namna ambavyo sera iliyowekwa na serikali inayoelekeza kuwa kila mwaka mkonge uzalishwe tani 100,000 na kwamba sera hiyo haisimamiwi ipasavyo kwani endapo kama ikisimamiwa ipasavyo zao hilo litaingia kwenye zao kuu la kibiashara nchini.

Akizungumza katika mikutano hiyo Waziri wa Kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba alisema kuwa Tanzania ilikuwa ndiyo nchi pekee barani Afrika kupokea zao la mkonge kutoka Jimbo la Yucatan, nchini Mexico mwaka 1893. Mkoa wa Tanga ndio ulikuwa kinara wa kulima zao hilo kwa wingi kwa kuwa na mashamba makubwa ikifuatiwa na Morogoro.
Hadi kufikia mwaka 1964, uzalishaji wa mkonge nchini ulikuwa ni tani 235,000 kwa mwaka, hivyo kuifanya Tanzania kuwa ndiyo nchi pekee iliyokuwa ikifanya vizuri katika zao la mkonge barani Afrika.
Aliongeza kuwa Kutokana hali hiyo, sekta ya kilimo hicho ndiyo sekta ambayo ilikuwa imeajiri watu wengi hususani katika maeneo ya mashambani. Hivyo Mkoa wa Tanga ulikuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi kutokana na faida ya uwapo wa zao hilo ukitoa viwanda vilivyokuwepo enzi hizo.
Licha ya zao hilo kuwa na manufaa ya kiuchumi, ni bidhaa ya nyuzi pekee ndiyo ilikuwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuuzwa katika masoko ya dunia. Hata hivyo, ujio wa kamba mbadala za nailoni katika miaka ya 1970 uliweza kuua soko la mkonge kwa kiasi kikubwa hali iliyolazimu kushusha uzalishaji na kufikia tani 32,000 pekee kwa mwaka.
Dkt Tizeba alisisitiza kuwa zao la Mkonge ni miongoni mwa mazao muhimu ya kibiashara hivyo serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imejidhatiti kuhakikisha zao hilo linaendelea kukua na kuongeza uzalishaji maradufu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanufaikaji wakubwa ni wakulima na sio vinginevyo.

Akijibu malalamiko ya wananchi ambao ni wakulima wa mkonge katika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Dkt Tizeba alisema kuwa serikali haiwezi kuchukua hatua za haraka katika kutatua mgogoro huo badala yake inaendelea kujiridhisha ili kubaini ukweli kuhusu uendeshaji wa zao hilo kupitia kampuni ya Katani LTD na ndani ya wiki mbili itatoa maelekezo ya serikali.

Dkt Tizeba ameitaka kampuni ya Katani LTD pamoja na wakulima wa katani kutunza kumbukumbu zao zote ili ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itakapoanza kazi ya ukaguzi iweze kupata taarifa za uhakika.