Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto mwenye kaunda suti ya blue) amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (katikati) kwa utendaji wake wa ubunifu na unaolenga kuboresha maisha ya Watanzania.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 25, 2018 akiambata na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) alipofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo katika ziara ya kufuatilia utendaji wa sekta ya habari.
Katika mazungumzo hayo Dkt. Abbasi amemueleza Mhandisi Gabriel kuwa mafanikio hayo ya Geita na mengine ambayo Serikali kwa ujumla inayatekeleza umuhimu yanapaswa kutangazwa na kutetewa kwa kuwa yana manufaa nakubwa kwa wananchi.
Katika mazungumzo RC Gabriel alisema mkoa wake umehakikisha mapato kutoka kwa makampuni ya madini yanatumika kuondoa adha za wananchi katika sekta muhimu kama afya, elimu na wajasiriamali.
Alisisitiza kuwa katika sekta ya Afya wamepanga kuwa kufikia Mei, 2019 zahanati zote mkoani Geita zitakuwa zimekamilika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO), Bw. Pascal Shelutete amemuhakikishia Mhandisi Gabriel ushirikiano wa kutosha katika eneo la mawasiliano lengo ni kuhakikisha taarifa za Serikali zinawafikia wananchi.
Aidha, Bw. Shelutete pia amempongeza RC huyo kwa utendaji wake makini na wa kimageuzi unaowagusa na kuwafunza wengi nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.