ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 9, 2019

“Dkt. Gwajima, Urudi kutukatia hii Shule Mwanza”- Kiomoni.

 Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali nchini Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba akiwasilisha maombi ya Darasa kwa Naibu Katibu Mkuu (Picha Atley Kuni)
 Naibu katibu Mkuu akikagua majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Itilima mkoani Simuyu
 Naibu Katibu Mkuu akiongea na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Festo Dugange akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wakati wa Ziara hiyo.
 Diwani viti Maalum Chausiku Hassan Salumu Diwani Viti maalum Halmashauri ya Shinyanga vijijini akipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Nne kwakutekeleza ahadi za Ilani ya Chama cha mapinduzi ya mwaka 2015-2020 kwa vitendo


Wadau naomba mpokee habari hii.
“Dkt. Gwajima, Urudi kutukatia hii Shule Mwanza”- Kiomoni.
Na Atley Kuni- OR-TAMISEMI, Mwanza
Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, Wakili Kiomoni Kibamba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, amewakilisha maombi maalum kwa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima akimsihi kumpatia darasa maalum kwa ajili yakutoa somo kwa watumishi wa Halmashauri hiyo namna bora yakuweza kupangilia rasilimali watu katika sekta ya Afya kwenye Jiji hilo.
Wakili Kibamba ametoa ombi hilo muda mfupi mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, kutembelea Kituo cha Afya Igoma na kukagua miundominu kisha kuzungumza na watumishi wa kituo hicho sambamba na timu ya Afya ya Halmashauri, ambapo katika maongezi yake  Naibu Katibu Mkuu alihimiza suala la uwajibikaji lakini pia matumizi sahihi ya rasimali pamoja na huduma bora kwa mteja.
Akizungumza na watumishi hao, Dkt. Gwajima alisema inashangaza unakuta kituo kimoja cha afya kinaelemewa na wagonjwa ili hali kituo kingine kilichopo karibu hakina mgonjwa na chanzo kikuu ikiwa ni huduma mbovu na kutokumjali mgonjwa. Lakini pia suala la mtu mmoja kung’ang’ania eneo alilopangiwa ilihali uapande wa pili unaelemewa.
“Ndani ya kituo kimoja unakuta Muuguzi anasema mimi nimepangiwa wodi ya Mama na Mtoto kwaajili yakuzalisha, lakini ndani ya kituo hicho hicho upande mwingine mathalani wa wagonjwa wa nje wagonjwa wamejaa na ukitazama unakuta mtoa huduma huyo amezidiwa na hana msaada wakati yule wa wodi ya wazazi yeye yupo tu anasubiri mama aje ajifungue hili halina afya hata kidogo na ni matumizi mabaya ya rasimali watu” alisema Dkt. Gwajima.
Mara baada ya darasa hilo Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza hakuficha furaha yake na badala yake akaomba somo kama hilo angependa lifundishwe kwa watumishi wote wa afya wa Halmashauri hiyo kwa muda maalumu na ndipo alipo wasilisha maombi yake.
“Mhe. Naibu Katibu Mkuu, tumekuelewa sana, sasa mimi naomba niwasilishe maombi maalumu, nikuandalie darasa japo uje wewe na jopo lako unifundishie watu wa Halmashauri hii kwakweli naomba sana sana” alisihi Wakili Kibamba.
Kufuatia maombi hayo Naibu Katibu Mkuu alimkubalia ombi hilo na kuahidi kurudi katika Jiji hilo kwaajili yakwenda kutoa somo kwa watumishi hao.
Kituo cha Afya Igoma  kituo kilicha anzishwa mwaka 1982 na nimiongozi mwa vituo vilivyopo katika Jiji la Mwanza ambacho kinauwezo wa kuhudumia watu 41,293 na watumishi wapatao 62 na katika mwaka wa fedha 2017/18 kilipatiwa fedha na serikali milioni 400 kwaajili ya upanuzi kwa majengo ya upasuaji, wodi ya wazazi, jingo la maabara, jingo la mionzi, jingo lakufulia sambamba na jingo lakuhifadhia maiti, ambayo yote yamekamilika kwa kujali thamani ya fedha na hivyo kumfurahisha Naibu Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi kwenye mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza Shinyanga na Tabora ambapo katika ziara hiyo, amekuwa akitoa somo la matumizi bora ya rasimali watu na vitu lakini pia suala huduma bora kwa mteja.
 Mwisho.

ASIMULIA JINSI ALIVYOMWOKOA KIFUNGONI MTOTO WA MIAKA 6 ALIYEKUWA NA KESI YA KUBAKA MWANZA


Ni katika historia ya Chama cha Wandishi wa Habari Mwanza (MPC) kilipoanza, hadi sasa kilipofikia ambapo Mkurugenzi wa UTPC ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa MPC zamani Aboubakar Karsan anafunguka juu ya simulizi adhimu za chama hicho.

Pia ipo simulizi ya mwandishi aliyejinyonga.

RC MWANZA AFUNGUKA MKUTANO WA MARAFIKI WA HABARI.




Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amefungua mkutano wa wasaa wa marafiki wa Habari mkoani Mwanza ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi Habari Mkoa Mwanza (MPC).

Akifungua mkutano huo Novemba 09, 2019 jijini Mwanza, Mongella amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari hivyo itaendelea kushirikiana na wabahabari katika kuchochea maendeleo.

Aidha Mongella ameipongeza MPC kupitia Mwenyekiti wake Edwin Soko kwa kuandaa mkutano akisema utasaidia kujadili fursa mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo ukarabati na ujenzi meli mpya katika Ziwa Victoria pamoja na ujio wa reli ya kisasa (SGR) huku ukitoa picha halisi katika kuelekea kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Biashara mkoani Mwanza utakaofanyika mwaka ujao.

Naye Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amesema mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano baina ya vyombo vya habari na wadau katika kufanikisha ajenda ya maendeleo mkoani Mwanza huku akisisitiza wanahabari kufanya kazi kwa weledi ili kulinda mustakabali wa amani kwa Taifa.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akitoa salami za ufunguzi kwenye mkutano huo.
Wanahabari na marafiki wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Friday, November 8, 2019

AHUKUMIWA MAISHA JELA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8




Njombe

Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Njombe imemhukumu kifungo cha maisha jela mtuhumiwa Addo Aron Nziku baada ya kukutwa na hatia ya kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 katika kijiji cha kitulila halmashauri ya mji Njombe.
Shauri namba 31 la mwaka 2019, ni kesi iliyomkabili mtuhumiwa Addo Aron Nziku mwenye miaka 26 mbena na mkazi wa kijiji cha matola  halmashauri ya mji Njombe, dhidi ya jamhuri.
Shauri hili likiwa chini ya hakimu James na Mhanusi na Mwendesha mashataka wa serikali Nura Manja ambae ameieleza mahakama kuwa mtuhumiwa anadaiwa kumwingilia mwanafunzi huyo zaidi ya mara tatu kabla ya mtoto huyo kumweleza bibi yake juu ya maswahibu yanayompata.
Mtuhumiwa Addo Nziku anadaiwa kumwingilia kimwili mtoto huyo kwa zaidi ya mara tatu katika eneo la mabanzi yaliyoko nyuma ya nyumba ya wazazi wa mtoto huyo huku mara ya tatu akimuingilia katika eneo la kukata majani ya mifugo ambako mtoto huyo alitumwa kwenda kusaka majani ya simbilisi siku ya tarehe 26 mwezi wa kwanza.
Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya kujiridhisha na ushaidi uliotolewa kwa kumkuta na hatia ya kubaka kinyume na kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili E  sambamba na kifungu namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu namba 16 kama ilivyofanyiawa marejeo mwka 2002.

JOHN CENA AMPIGA SAPRAIZI' MWANAMUZIKI WA AFRIKA YA KUSINI ANAYEIMBA KISWAHILI.


John Cena Surprises Sho Madjozi While Performing 'John Cena'

South African singer Sho Madjozi performs her viral tune "John Cena" - right before finally meeting her idol in person for the first time! You don't want to miss her incredible reaction!

Thursday, November 7, 2019

TIMU NANE ZATINGA HATUA YA NANE BORA ASAS SUPER LEAGUE 2019

 Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) Cyprian Kuyava akisalimiana na moja ya timu ambayo imetinga hatua ya nane bora ligi ya ASAS SUPER LEAGUE mkoani Iringa


 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalah akiwa na viongozi wa chama cha soka mkoa wa Iringa wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Young Stars ambayo nayo imetinga hatua ya nane bora
NA FREDY MGUNDA, IRINGA

TIMU za 8 zilizokuwa zikishiriki ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa inayojulikana kwa jina la Asas Super league  2019 zimefanikiwa kuingia hatua ya nane bora katika kuelekea kumpata bingwa wa mkoa atakayeondoka na kitita cha milioni mbili.

Timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya nane bora ni,Mafinga Academy Fc, Mkimbizi Fc, Young Stars, Ismani Fc, Irole Fc,Kalinga Fc, Kidamali Fc timu moja kati ya Nzihi na Mbegamwekundu atajihakikishia kuingia katika nane bora za ligi hiyo mkoani hapa.

Wakati timu hizo zikiingia katika nane bora timu za Acosato fc, African Wanderas hizo zimeshuka daraja hadi la nne wakati timu za Mapanda Fc, Mshindo fc na Magulilwa zikicheza mchezo wa mtoano kuendelea kubaki ligi hiyo ama kuungana na walioshuka daraja. 

Katika ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Maziwa ya Asas mchezaji, Emmanuel Geka wa Kidamali Fc anaendelea kuongoza kwa ufungaji wa magoli baada ya kufikisha magoli 8 huku akifatiwa kwa karibu na wachezaji, Riziki Kelvin (Ismani Fc) na Luka Duma (Irole Fc) wenye mabao 7 kila mmoja.

Wachezaji wanaofatia katika mashindano hayo ni Baraka Athuman (Mafinga Academy) mwenye magoli 5 huku wachezaji Kelvin Msafiri (Kalinga Fc), Conrodgers Mhavile (Irole fc) na Mohamed Rashid (Ismani fc) wakiwa na magoli manne.

Na katika mechi zilizopigwa juzi Upendo Fc ilitoshana nguvu na timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Iringa kwa goli 1 – 1 yaliyofungwa na Elisha Chuma (Chuo cha Iringa) na Jemin Fred kwa upande wa Upendo Fc.

Wakati michezo mingine ilikuwa kati ya Ismani fc dhidi ya Acosato ambapo Isman waliibuka na ushindi wa magoli 4 -1 kwa magoli yaliyofungwa na Mohamed Rashid, Riziki Kelvin na Razack Kibuga huku goli la kufutia machozi kwa upande wa Acosato likifungwa na Mohamed Salufu.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya  Kidamali Fc dhidi ya Irole fc ambapo Kidamali walishindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani na kukubali kipigo cha mabao 3 -1 kwa magoli ya Luka Duma aliyefunga mawili, Conrodgers Mhavile .

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa, Cyprian Kuyava akizungumza na Tanzania Daima alivipongeza vilabu vyote vilivyofuzu hatua ya nane bora licha ya changamoto zilizojitokeza kutokana na ugumu wa mashindano hayo mwaka huu.

Kuyava alisema kwamba kuna baadhi ya timu zimecheza kwa nidhamu kubwa hali iliyosababisha kuweza kufuzu katika hatua hiyo kubwa kabisa na kuwapongeza waamuzi, makamishna na wasimamizi wa ligi kwa umakini na umahiri wanaoendelea kuonyesha katika ligi ya Asas.

Aidha alizipongeza timu zote zilizoshiriki ligi hiyo kwa nidhamu, ushindani weredi mkubwa wakati wote wa mashindano hayo yalipokuwa yakifanyika katika hatua za makundi na kuzitaka timu zilifuzu hatua ya nane bora kufanya maandalizi mazuri kuweza kuibuka na ubingwa.

Alisema kuwa changamoto zilizojitokeza katika hatua ya makundi zinatakiwa kufanyiwa kazi katika hatua ya nane bora ili kuweza kumpata bingwa mshindani katika ligi za mabingwa ya mikoa Tanzania Bara.

 Bingwa wa mashindano hayo atapata kombe na sh. 2,000,000,jezi seti moja,mipira mitatu, na nafasi ya kushiriki ligi ya mikoa.  Mshindi wa Pili shilingi 1,000,000, Mipira 2, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki huku Mshindi wa Tatu - Tsh 500,000/=, Jezi Seti 1

MWANZA YALAMBA TUZO TAMISEMI HAMASA YA KUANDIKISHA WAPIGA KURA


Mkoa wa Mwanza mshindi nafasi ya tatu katika uhamasishaji wapiga kura  Uchaguzi Serikali za Mitaa mwaka 2019, Beatrice Kimoleta ni Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa - TAMISEMI 

Wednesday, November 6, 2019

MAOFISA WA TIMU YA MKOA WA MWANZA WACHARAZWA VIBOKO NA MA-SHEIKH WA BAKWATA 2-1



Ulikuwa ni mchezo wa kulipa kisasi baada ya kunyanyaswa sana kwa kufungwa michezo miwili iliyopita lakini safari hii timu ya Ma-Sheikh wa Bakwata mkoa wa Mwanza wameikalisha chini timu ya Maofisa wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa kuilaza bao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliokuwa umejaa kila aina ya mbwembwe na vibweka toka pande zote mbili. 
Kikosi cha Maofisa wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
 Kikosi cha Ma-Sheikh wa Bakwata mkoa wa Mwanza.
 Golikipa wa zamani wa timu ya Soka ya Pamba Sc ya jijini Mwanza na Yanga ya jijini Dar es salaam, Juma Mhina (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza iliyoongozwa na nahodha wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (wanne kutoka kulia).
 Timu zote mbili kabla ya mchezo dimba la Nyamagana jijini Mwanza.
 Mongella.
 Kadio.
 Mapumziko.
Michezo ni Afya.

OFISI YA WAZIRI MKUU YATOA TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA HAPA NCHINI.



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, imetoa hali ya  dawa za kulevya hapa nchini kwa mwaka 2018, na kuiwakilisha kwa wabunge.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Waziri mwenye dhamana ya Ofisi hiyo, Mhe. Jenista Mhagama, amesema lengo la kutoa taarifa hiyo kwa jamii, ni kuwafahamisha wananchi hali ya dawa za kulevya hapa nchini na jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hilo.

"Aidha taarifa hii imewasiishwa kwa wabunge ili waweze kuwaelezea wananchi kwenye majimbo yao Hali halisi ya tatizo la dawa za kulevya hapa nchini na jitihada zinazofanywa na serikali katika kupambana na tatizo hilo" amesema Waziri Jenista.

Amesema vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi viliendelea kutekeleza agizo la Rais Dkt John Magufuli, katika kumuwezesha nchi yetu na kupata mafanikio katika kudhibiti dawa hizo, kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la kupambana na dawa za kulevya(UNODC) Tanzania umepungua uingizaji nchini wa dawa za kulevya aina ya heroin kwa asilimia 90.

Ameongeza kuwa "licha ya jitihada hizo lakini bangi bado ni tatizo kubwa hapa nchini, na mikoa ambayo imeonekana kuathirika zaidi na kilimo cha bangi ni pamoja Mara, Tanga, Morogoro, Arusha,Kagera na ruvuma" amesema.

Pia milungi imeendelea kutumiwa na watu wa rika mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2018, juhudi za za vyombo vya dola vimefanikiwa ukamataji wa tani 24.3 za bangi na watuhumiwa 10,061, na tani nane 8.97 za mirungi na watuhumiwa 1,186.

Aidha amebainisha kuwa serikali imeendelea kutoa huduma za tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya na jumla ya vituo sita vilivyopo katika mikoa ya Dar es saalam, Mwanza, Mbeya na Dodoma viliendelea kupatiwa huduma za methadone.

SHIRIKA LA NDEGE LA LUFTHANSA LAFUTA SAFARI ZA NDEGE1,300 KWA SABABU YA MGOMO.

Shirika la Ndege la Ujerumani Lufthansa limefuta karibu safari 1,300 hapo kesho na Ijumaa kwa sababu ya mgomo uliopangwa na chama kinachowawakilisha wahudumu wa ndege nchini Ujerumani.

Chama cha UFO kimewataka wanachama wake kuanza mgomo wa saa 48 kuanzia leo usiku wa manane.

Ni sehemu ya mgogoro mkali na shirika kubwa kabisa la ndege Ujerumani kuhusu mishahara na hadhi ya kisheria ya chama hicho.

Lufthansa imesema leo kuwa inatengeneza mpango maalum wa safari za ndege na abiria watahitajika kuangalia taarifa kuhusu safari zao kwenye tovuti yao.

Shirika hilo limesema litaweza kuwa na safari 2,300 kati ya 3,000 zilizopangwa kesho Alhamisi na 2,400 ya zilizopangwa Ijumaa. Karibu abiria 180,000 wataathirika na kufutwa kwa safari hizo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA NA KATIBU MKUU CCM BASHIRU ALLY WAKABIDHI NG'OMBE 5 NA SARUJI MIFUKO 100 MAULID MWANZA


"Mhe. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dr. Bashiru Ally alifana ziara mkoani petu na alipita ofisi za BAKWATA za mkoa zilizopo kata ya Mbugani akakuta ujenzi wa msikiti unaendelea naye akaahidi kutoa mifuko 100 ya saruji, na ndiyo ambayo nimekuja kukabidhi leo" Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella na kisha akaongeza ....
"Suala la pili ambalo limenileta ni kuwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa naye ameniagiza nilete ng'ombe watano kwaajili ya kitoweo cha sikukuu ya Maulid ambayo kitaifa yanafanyika hapa Mwanza, hivyo nimekuja kukabidhi naomba kuwasilisha"
 Sheikh Mkuu Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke akitoa neno la shukurani kwenye makabidhiano hayo yaliyofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
 Mifuko ya Saruji.
  Mbele ya Ma-Sheikh wa mikoa na nchi mbalimbali hususani Kenya na Uganda wameshuhudia makabidhiano hayo.
 Ng'ombe walionona.
Heri ya Maulid Mwanza.

UJENZI WA CHELEZO KWAAJILI YA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAWASISIMUA MA-SHEIKH - WASHUSHA DUA KWA JPM


Wakati zoezi la kuandaa uso wa kazi tayari kwa kuanza ujenzi wa Chelezo kitakachotumika kujengea Meli mpya katika Ziwa Victoria likiendelea kwa kasi katika eneo la Bandari ya Mwanza Kusini, Ma-Sheikh na waumini wa dini ya Kiislamu kutoka ndani na nje ya nchi waliofurika jijini Mwanza kushiriki Maulid inayofanyika kitaifa mkoani hapa wanapata nafasi kutembelea kujionea uwekezaji huo.

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke Baada ya kutembelea eneo hilo na kushuhudia hatua mbalimbali za uwekezaji wa ujenzi wa kisasa unaoendelea na kubadili kabisa taswira ya eneo la bandari, anaamua kuwasilisha mawazo na minong'ono iliyokuwa ikitawala kwenye vinywa vya waumini wenzake wakati wakiendelea na ziara na kuamua kuwasilisha hisia zao mbele ya Wandishi wa Habari.

"Wakati mwingine wakisema hawa (huku akimnyooshea kidole Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella) tunaweza kusema kuwa wanajitetea, lakini wakati mwingine tuseme sisi juu ya haya makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli kwani tuna haki kama Watanzania" Alisema Sheikh Kabeke na kisha kuongeza "Nitoe wito kwa Watanzania wakipata fursa watembelee miradi hii ya Serikali ili iwatoe upofu"

"Sasa kwa heshima na taadhima tunamuweka kati Mkuu wa Mkoa Bwana Mongella amwakilishe Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli, kwa niaba yake kuzipokea dua zetu Waislamu tuliofika hapa tukaona kwa jicho hili la nyama yale yanayofanywa na Serikali yake"

SAMATA AWEKA HISTORIA NYINGINE UEFA KWA KUFUNGA NYUMBANI KWA LIVERPOOL




HISTORIA imeonekana Leo Kwa MBWANA ALLY SAMATTA ndani Ya Anflied. Amekuwa Mchezaji wa kwanza kutoka TANZANIA Hlf kufunga GOAL katka uwanja wa LIVERPOOL

MAMLAKA YA MAJI ARUSHA YATAKIWA KUPELEKA MAJI NAMANGA

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony (mbele) akikagua chanzo cha maji cha mradi wa Longido katika Mto Simba uliopo wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ili kutazama uwezekano wa kutoa maji kwenye chanzo hicho na kupeleka Namanga.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony (katikati) akitoa maelekezo kwa wataalam kutoka Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA) wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji wa Longido. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA, Mhandisi Justine Rujomba

 Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony (kushoto) akitoa maelekezo kwa wataalam kutoka Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA) wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji wa Longido.

Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA) imetakiwa kuharakisha zoezi la tathmini ya kupeleka huduma ya maji katika Mji wa Namanga ili kusaidia wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Agizo hilo limetolewa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara yake kwenye chanzo cha mradi wa maji wa Longido katika Mto Simba uliopo wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Novemba 4, 2019 kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wake.

Mhandisi Sanga alisema ameridhika na hatua aliyoishuhudia ya ujenzi wa mradi wa Longido hata hivyo aliitaka AUWSA kuhakikisha inatazama namna ya haraka ya kufikisha huduma ya maji kwenye mji wa Namanga kutoka kwenye chanzo cha mradi huo hasa ikizingatiwa kwamba mji huo unasumbuliwa na kero ya upatikanaji wa huduma ya maji.

“Ninawapongeza AUWSA kwa usimamizi mzuri wa mradi lakini nataka kuona mnafanya tathmini haraka ya namna ya kufikisha maji kwenye mji wa Namanga kwani kuna changamoto kubwa sana kwenye mji huo,” alisema Mhandisi Sanga.

Akizungumzia uwezekano wa kutumia chanzo hicho cha Mto Simba kupelekea maji Namanga, Mhandisi Sanga alisema maji yaliyopo yanaonekana kuwa mengi na yanaweza kutosheleza kuhudumia maeneo yote mawili sambamba na maeneo mengine ya jirani.

“Tumekuja hapa kuona uwezekano wa kutoa maji kwenye eneo hili ili kufikisha Namanga, na nilichoshuhudia ni kwamba chanzo hiki kinaonekana kuwa na maji ya kutosha kwa maeneo yote mawili yani Longido na Namanga,” alisema.

Aliwataka kufanya mawasiliano ya haraka na Bonde la Pangani ili kuharakisha zoezi la tathmini ya kuona kiasi cha maji kinachoweza kuongezwa ili kuwezesha kupeleka maji kwenye mji wa Namanga kutoka kwenye chanzo hicho bila kuathiri matumizi ya asili ya chanzo hicho.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa AUWSA, Mhandisi Justine Rujomba alisema mradi wa Lingido umelenga kuongeza upatikanaji wa maji katika mji mdogo wa Longido kutoka asilimia 15 za sasa ambazo ni sawa na wananchi 2,510 hadi kufikia asilimia mia moja ambayo ni sawa na wananchi 16, 712.

Mhandisi Rujomba aliongeza kuwa malengo hayo ni hadi kufikia mwaka 2025 na kwamba hadi kukamilika kwake utakuwa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 15.8. Aidha aliongeza kuwa wamepokea maagizo ya Naibu Katibu Mkuu na wanaanza kufanyia kazi maramoja.

Mhandisi Sanga yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa mkoani humo kwa lengo la kujionea hali halisi ya utekelezaji sambamba na kuelewa changamoto zilizopo ili kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Monday, November 4, 2019

MAULID KITAIFA MWANZA YADHIHIRISHA KUWA TANZANIA NCHI PEKEE DUNIANI ISIYOTIKISWA NA UDINI.



 Pengine hili likawa mfano wa kuigwa duniani nalo linatokea katika nchi moja barani Afrika nayo ni Tanzania, nchi inayotajwa kuwa kisiwa cha amani, pale unapokuta viongozi wa dini kubwa ambazo zinapishana katika imani, zinashirikiana pamoja tena hatua kwa hatua kufanikisha sehemu ya mapokeo ya imani.

Ni katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki kuelekea sikukuu ya Mtume Muhammad ambapo maandalizi ya sherehe hizo zinafanyika kitaifa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza yamefanywa na Kamati ya Amani inayoundwa na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo nao kwenye uzinduzi licha ya kutajwa waziwazi kama sehemu ya kamati vilevile viongozi hao wa dini ya Kikristo wametunukiwa zawadi kama kumbukumbu ya ushiriki wao.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa wiki ya Maulid ambayo maana yake ni "Mazazi" au Birthday kwa kiingereza..

Maulid ilianziashwa miaka 600 baada ya kifo cha Mtume (Swalla Allahu alayh wasalam) yaani karne 6 baada ya Mtume kuondoka duniani huko misri.
Watu wa kwanza kuanzisha kusherekea mazazi (Maulid) ya Mtume (Swalla Allaahu alayh wasalam) katika historia ya Uislam ni utawala wa Banu Ubaid ambao walijulikana kama Faatwimiyuun ambao ni Mashia waliokuwa wamejimegua kutoka kwenye kijikundi kingine cha shia (Ismailiya)
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa wiki ya Maulid akihutubia umma uliofika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini humo.
 Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Issa Othman Issa akitoa neno kumkaribisha mgeni rasmi. 
 Sheikh Mkuu mkoa wa Mwanza Hassan kabeke akifafanua jambo kwenye kusanyiko hilo la ufunguzi wa wiki ya Maulid katika viwanja vya Furahisha vilivyopo katika kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini humo.

 Meza kuu na umakini wake.
 Sehemu ya waumini waliojitokeza. 
 Pia kulikuwa na mabanda ya uelimishaji na utoaji mafunzo.
 Bidhaa mbalimbali za miongozo ya dini zitapatikana kwa kipindi chote cha maadhimisho.
 Inatokea Tanzania pekee.
 Kauli mbiu ya Maulid 2019.
 "Ndugu wakutanapo" mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akifurahia jambo na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mama Amina Masenza (kushoto) 
 Katika taarifa iliyotolewa miezi kadhaa iliyopita na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mohammed Khamis Said, kwa vyombo vya habari, iliainisha Maulid ya kitaifa kuadhimishwa usiku wa Jumamosi, mwezi 11 RABIUL AWWAL 1441H sawa na Novemba 9, 2019 katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na Baraza la Maulid litafanyika Jumapili Novemba 10, ambayo ndiyo itakuwa siku ya mapumziko kitaifa. 

Baraza litaanza saa 9:00 Alasiri katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT), Kapripoint, Mwanza.