ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 18, 2010

UKISTAAJABU YA WENJE HUJAONA YA MASHA!!! LEO JIONI NDANI YA MILONGO ATOA MAJIBU SAHIHI KWA MASWALI YALIYO ULIZWA NA CHADEMA.

MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA L. KEGO MASHA JIONI YA LEO AMEZINDUA RASMI KAMPENI YAKE KTK JIMBO HILO. SERA ZILIWAINGIA WANANCHI HALI ILIYOPELEKEA KUBEBWA JUU.

KATIBU WA CCM MWANZA AL HADJI KUNDYA YEYE ALISISITIZA JUU YA SERA ZINAZOTEKELEZEKA (ZA CCM). ALIKOSHA NA MIFANO YAKE, ALIWATAHADHARISHA WANANCHI KUEPUKA SERA ZA MAZINGAOMBWE, ALIULIZA NI MTANZANIA GANI HII LEO AMBAYE ATAWEKEWA TOFALI JUU YA MEZA NAKUAMBIWA KULA NDUGU HUU NI MKATE?


PAMOJA NA BURUDANI NYINGINE AY ALITOA BURUDANI SAFI KABLA YA ZOEZI LA UMWAGAJI WA SERA. UNASHANGAA NINI? HATA WANA WA ISRAEL WAKATI WAKIVUKA BAHARI YA SHAMU WALIKUWA WAKIVUKA HUKU WAKIIMBA NA MUNGU AKAWASIKIA.

WADAU WA NGOMA YA ASILI TOKA KABILA LA WASUKUMA NAO WALIKUWEPO KUTIA NAKSH NA KUCHOMBEZAzz!.

MADIWANI WA KATA MBALIMBALI ZA WILAYA YA NYAMAGANA WALITAMBULISHWA KWA WANANCHI NA KUPEWA FURSA YA KUOMBA KURA.

BRASS BAND.

MZUKA WA WANACHAMA UKIPANDA NI BARRRAA!!

NI SEHEMU TU YA WANA NYAMAGANA WALIOHUDHURIA MKUTANO WA KAMPENI ZA MASHA VIWANJA VZA SHULE YA MSINGI MIRONGO NYAMAGANA JIJINI MWANZA.

TUKIO HILI LIMETOKEA HUKO MKOANI SINGIDA.

KIBAKA mmoja ambaye hajafahamika jna lake wala makazi ameuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali na kisha kuchomwa moto baada ya kufanya jaribio la kuvunja duka na kuiba bidhaa mbalimbali. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi majira ya saa 10 alfajiri katika eneo la Mwenge Manispaa ya singida ambapo kibaka huyo alikuwa na wenzake watano.

Hata hivyo wananchi wa maeneo ya jirani wamesema kuwa hiyo ni mara ya tatu kwa duka hilo kuvamiwa na vibaka na kisha mali kuchuliwa ambapo mwenye duka hiloa akiamka asubuhi anakuta duka jeupe na hivyo kumpunguzia nguvu kazi ya kujiletea maendeleo yake pamoja na familia yake. "Jamani sisi tumechoshwa na hawa wezi kila mara wanamwibia huyo kijana wa hili duka hebu angalieni mali yote imetolewa nje na kama sio kushiuka si angekuta hana kitu, tunasema tukikamata kibaka safai hii aaangalie mfano wa huyu mwenzao hatuna msaliamtume, polisi watakuja kuchukua majivu tu."Alissisistiza mama mmoja jirani na eneo hilo la tukio.


PICHA NA HABARI KWA HISANI YA BLOG YA FULL SHANGWE.

Blog hii inaungana na wadau wote wa habari kulaani matukio kama haya ya sehemu ya kundi la watu kujichukulia sheria mkononi na kusabisha madhara kwa wengine ikiwemo na kupoteza uhai wa muhisika, hali hii inapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote.

Friday, September 17, 2010

HAPA NYUMBA MBELE JARARAAA.... MBELE PEMBENI BIASHARAA.......

NI ENEO LA KILIMA CHA SAHARA, BUGANDO JIJINI MWANZA, TAKA ZIKITUPWA HAPA ENEO AMBALO NI MAKAZI YA WATU, WATOTO WAKIFANYA ENEO HILO KAMA SEHEMU YA KUJIVINJARI KWA MICHEZO YAO, VILEVILE SEHEMU YA BIASHARA KAMA UONAVYO.

NDANI YA JIJI LINALOONGOZA KWA USAFI TUZO MFULULIZO KATIKA MIJI YA AFRIKA MASHARIKI. YAANI POA TU! MICHEZO INAENDELEA.

KWETU USWAZI HATUA CHACHE MBELE KIDUCHU NDANI YA ENEO HILO BIASHARA YA CHAKULA INAFANYIKA BILA HATA TAHADHARI.

MENGINEYO: VIATU MKOMBOZI.

WALE WA MASHUKAzz! MASHUKA LEO LEO!!

OFISI YA WAZIRI MKUU WA KENYA.


OFISI RASMI YA KISERIKALI YA WAZIRI MKUU WA KENYA RAILA ODINGA BAADA YA UKARABATI MKUBWA ULIOGHARIMU PESA YA KENYA SHILINGI MILLIONI 329 . EH BANA EEE!! Eeeh inapendeza kweri kweri kwakwerri..

Thursday, September 16, 2010

MTANGAZAJI WA RFA KID BWAY' AVAMIWA NA ALIYEJITAMBULISHA KUWA NI MSANII, APOTEZA FAHAMU, HAJITAMBUI HADI SASA.


MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRIKA AMBAYE VILEVILE YU PRODUCER WA KUREKODI MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NDANI YA TETEMESHA PRODUCTION SANDU GEORGE MPANDA MAARUFU KWA JINA LA KID BWAY AMELAZWA HOSPITALI YA BUGANDO MARA BAADA YA KUVAMIWA NA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA JAMAA ASIYEFAHAMIKA.

TAARIFA ZINASEMA KUWA KID BWAY AKIWA NYUMBANI KWAKE LUMALA JIJINI MWANZA, JAMAA ALIYEMVANIA ALIFIKA NYUMBANI HAPO MAJIRA YA SAA 2:30 USIKU NA KUJITAMBULISHA KAMA MSANII AKIHITAJI KUFANYA RECORDING, BAADA YA MAZUNGUMZO NA KUJITAMBULISHA ALIKARIBISHWA NDANI HADI CHUMBA CHA KUREKODIA STUDIO.

NYUMBANI KWA MTANGAZAJI HUYO ANAISHI NA JAMAA ZAKE WAWILI AMBAO WAKATI KID AKIMKARIBISHA MTENDA UHALIFU HUO NYUMBANI HAPO JAMAA HAO WALIMWONA KIJANA HUYO KISHA KILA MMOJA AKAINGIA CHUMBANI KWAKE. DAKIKA KADHAA WAKASIKIA KWA KIPINDI KIREFU SPIKA ZA STUDIO ZIKIKOROMA ISIVYO KAWAIDA NA KUANZA KUDADISI HUKU WAKIMWITA KID BWAY KUWA INAKUWAJE! WAKAITA NA KUITA NDIPO WALIPO AMUA KUINGIA STUDIO NA KUMKUTA SAKAFUNI KAANGUKA DABU ZIKIMTOKA MASIKIONI, PUANI NA KWENYE MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWA.

KWA HIVI SASA KID YUPO HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO AKIWA HOI HAJITAMBUI YAANI KAPOTEZA FAHAMU, ALITUNDIKIWA DRIPU YA MAJI IKIWA NI HUDUMA YA KWANZA AMBAYO AMEPATIWA JANA MARA BAADA YA KUFIKA HOSPITALINI HAPO AKISUBIRI KIPIMO CHA T SCAN KUONA KWA UNDANI ZAIDI SEHEMU ALIZODHURIKA. HAKUNA TAARIFA YOYOTE YA UPOTEVU WA MALI HALI INAYOPELEKEA WADADISI WA MAMBO KUDHANI KUWA YAWEZEKANA KULIKUWA NA VITA YA KICHINI CHINI AKA BIFU(AMBAYO HAIJAFAHAMIKA).

UCHUNGUZI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI UNAENDELEA KUFANYWA ILI KUJUA NINI SABABU ZA UVAMIZI HUO.

TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUKUJULISHA.

TWAMWOMBA MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU BROTHER UPATE PONA.

Tuesday, September 14, 2010

SEPTEMBER 11, CHADEMA ILIPOTINGA MIRONGO MWANZA. YASEMA HIZI NI RASHA RASHA MVUA KAMILI YAJA...

MGOMBEA WA URAISI KWA TIKETI YA CHADEMA DR WILLIBROD SLAA AKIMTAMBULISHA BW. WENJE MGOMBEA WA UBUNGE KWA TIKETI YA CHAMA HICHO WILAYA YA NYAMAGANA, KIUFUPI ZILIIPUKA SHANGWE ZA KUTOSHA WAKATI MGOMBEA HUYU AKIOMBEWA KURA.

DK SLAA ALISEMA WATANZANIA WASIFIKIRI KUWA MADINI NA RASLIMALI NYINGINE ZITAKAA MILELE BALI ZINAPUNGUA KWA SABABU ZINAVUNWA NA HAZIZAI NA ANASHANGAA KUONA KUWA WILAYA KAMA GEITA YENYE UTAJIRI WA MADINI INAKOSA MAJI SAFI INGAWA NCHI INA MIAKA TAKRIBANI 50 YA UHURU.

KATIKA HATUA NYINGINE MWANASHERIA MAARUFU MABERE MARANDO AMEAHIDI KURUSHA MABOMU ZAIDI KUFICHUA ALIOUTAJA KUWA NI UOZO (SABABU ZA KUKWAMA KIUCHUMI)ILI KUIHAKIKISHIA CHADEMA USHINDI.

MGOMBEA URAISI WA TANZANIA KUPITIA CHADEMA DR WILLBROD SLAA AKIHUTUBIA MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KATIKA MFULULIZO WA KAMPENI ZAKE KWENYE UWANJA WA SHULE YA MSINGI MIRONGO.

WANANCHI WAKILA KIAPO KUKIHAKIKISHIA USHINDI CHAMA HICHO NGAZI ZA UDIWANI, UBUNGE HADI URAISI, MARA BAADA YA KUSOMEWA VIPENGELE VYA ILANI YA CHAMA HICHO.

ILANI YA CHAMA HICHO IMEGUSIA ELIMU, AJIRA, ULINZI NA USALAMA, KILIMO, AFYA, MICHEZO, NJIA ZA KUKUZA UCHUMI, RASLIMALI ZA TAIFA NA MENGINE MENGI.

NIKIRIPOTI KUTOKA JUKWAANI LA ZIADA LIPO ENDELEA KUCHUNGULIA BLOGU HII KUKUPA NEWz BIN NEWz KIPINDI HIKI TUKIELEKEA OCT 31.

Monday, September 13, 2010

MTEMBEZI NAE.....

MUONEKANO WA SASA WA STENDI KUU YA ZAMANI YA MABASI MWANZA (TANGANYIKA BUS STAND).

KAMA ZILIVYO KLABU KUBWA NCHINI KUWA NA MAJENGO YAKE KAMA KITEGA UCHUMI NDIVYO ILIVYO KWA KLABU YA WANAKISHAMAPANDA - TOTO AFRICA MWANZA.

KONA YA KUPANDISHA KUELEKEA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO.

MSIKITI WA IBADHI NA MAJENGO YAKE KTK MAKUTANO YA BARABARA YA LIBERT NA NKOMO.


GENEVIEVE EMMANUEL NDIYE VODACOM MISS TANZANIA 2010.

VODACOM MISS TANZANIA 2010, GENEVIEVE EMMANUEL (KATI) AKIWA NA MSHINDI WA PILI GLORY MWANGA (KUSHOTO) NA CONSOLATA LUKOSI.

TANO BORA.

KAMA NI BURUDANI TANZANIA KWA HIVI SASA LEVO ZINAPANDA KWA KASI ILE MBAYA, MASHUHUDA WA KAZI YA MAVIJANA HAYA YA THT NDANI YA VODACOM MISS TANZANIA WATAUNGANA NAMI KUSAPOTI KAULI YANGU..

PICHA NA HABARI KWA HISANI YA OTHMAN MICHUZI.