Copa Kolo, Gosso, Souleman, Tiene Gradel, Bony, Tiote, Yaya Drogba, Gervinho COTE D'IVOIRE |
Kaseja Cholo, Morris, Maftah, Nyomi Kazimoto, Salum, Nurdin, Mkude Mbwana, Ulimwengu TANZANIA |
Mpira umeisha katika uwanja wa Felixs Houphouet Boigny mjini Abdijan nchini Ivory Coast kati ya timu ya taifa la Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya taifa hilo. Ivory Coast walijipatia bao la kwanza kwenye dakika ya 15 kipindi cha kwanza kupitia mchezaji Solomon Kalou, aliyetumia vyema makosa ya mabeki wa Taifa Stars waliojisahau na kucheza bila uelewano mara kadhaa, hivyo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Ivory Coast walikuwa wakiongoza kwa bao hilo.
Kipindi cha pili dakika ya 70 Taifa Stars inacheza pungufu mara baada ya mchezaji wake kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na hatimaye akazawadiwa kadi nyekundu, muda mfupi baadaye (dakika ya 80) Didier Drogba akapachika bao la pili.
Didier Drogba |
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Didier Drogba kuonekana katika dimba la nyumbani tangu kuisaidia klabu yake ya Chelsea kushinda kombe la Uefa Champions League mwezi uliopita kitu ambacho kilitarajiwa kuwa chachu kwa mashabiki wake wa nyumbani kumshangilia kwa nguvu shujaa wao na ndivyo ilivyokuwa leo.