ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 21, 2013

BASI LA ALLYS LAFYEKA 9 LAJERUHI 15, NALO BUNDA BASI LAUA MWENDESHA BAISKELI.

Daladala iliyogongwa na basi la Ally's.
WATU kumi wamekufa, wanane kati yao papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizohusisha mabasi ya kampuni ya Bunda na Ally, mkoani Mwanza.

Ajali hizo zilitokea jana usiku katika barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga katika maeneo ya Mitindo wilayani Misungwi na eneo la Buhongwa Dampo wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.

Ajali mbaya zaidi iliyosisimua na kusababisha vilio kuugubika mji wa Usagara wilayani Misungwi, ilitokea majira ya saa 1:40 Buhongwa, ambapo Basi la Allys lenye namba za usajiri T.691 AGP liligonga Daladala (Toyota Hiace)na kusabaisha vifo vya watu tisa ambao kati yao, saba walikufa palepale. 
Mwonekano wa dalaldala kwa nyuma. 
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Valentine Mulowola akithibitisha ajali hiyo, alisema basi hilo lililokuwa na hitilafu ya taa za mbele, lilikuwa likitoka Arusha kwenda jijini Mwanza wakati daladala hiyo ikitoka Buhongwa kwenda Usagara wilayani Misungwi.

Baadhi ya abiria waliokuwa katika ajali hiyo akiwemo Shija Francisco ambaye alijeruhiwa mkono wa kulia, basi hilo liliwagonga sehemu ya ubavu wa kulia na kusabisha Hiace hiyo ipinduke na kuviringika mara tatu nje ya barabara, wakati likijaribu kulipita roli moja lililokuwa mbele yake, kwenye kona.

“Ilikuwa ghafla mno tulipojikuta uso kwa uso na basi hilo ambalo halikuwa na taa, dereva akajaribu kulikwepa lakini hakufanikiwa, lilitugonga na kufanya gari letu lipinduke na kuviringika mara tatu.” Alieleza Franchisco mkazi wa Usagara huku akimlilia mkazi mwenzake Juma Basu (27) aliyekufa papo hapo.

Usiku huo wa ajali ilishuhudiwa miili ya watu hao ambayo baadhi ilikuwa imepondeka vibaya na kukatika viungo akiwemo mtoto wa miaka minne, Raphael Simon aliyekufa pamoja na baba yake Saimon Paschal(35), wakazi wa Usagara.

Kamanda Mulowola aliwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Eliakim Fredrick mkazi wa Igogo Mwanza, Stephen Mungisa (hatambulika makazi), Dismas Mpange (Usagara)na wanawake wengine wawili ndugu Shobo Lumecha na Gaudensia Lumecha, wakazi wa Geita. 

“Abiria 15 walijeruhiwa katika ajali hiyo akiwemo dereva wa Hiace Anthony Maige (52) na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando lakin dereva wa Basi la allys Elias Charles alikimbia tunamsaka.” Alieleza Kamanda huyo na kubainisha kuwa daladala hiyo ilikuwa imejaza watu kupita kiasi.
Basi la Ally's lililoigonga daladala na kusababisha vifo vya watu 9.
Basi la Bunda Express lililomgona mwendesha baiskeli.
Katika ajali nyingine iliyotokea saa 11 jioni katika eneo la Mitindo Misungwi, Basi la Bunda T.234 BZK aina ya Scania likiendeshwa na Emmanuel Mashauri, limemgonga mwendesha baiskeli Shilaga Thomas (20) na kusabaisha kifo chake palepale na kumjeruhi abiria wa baiskeli hiyo Machwenda Komanya.

Kamanda Mulowola amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ya basi la Bunda lililokuwa likitoka Dodoma kwenda Musoma, ni mwendo kasi na ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu na wazingatie sheria za usalama barabarani wanapotumia vyombo vya moto.

MAMA REGINA LOWASSA ASHIRIKI CHAKULA CHA MCHANA PAMOJA NA WATOTO WENYE ULEMAVU JIJINI ARUSHA

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akishiriki kuhudumia chakula watoto wenye ulemavu  katika Kituo cha Huduma ya Walemavu kinachomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha kilichopo Monduli wakati alipokwenda kushiriki nao Ibada ya X-Mass pamoja na kuzungumza na kula nao chakula cha mchana.

MAWAZIRI WANNE WANG'OKA.

CHANZO: MWANANCHI.
Dar es Salaam / Dodoma. Ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira iliyowasilishwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma, imewang’oa madarakani mawaziri wanne ambao wizara zao zilishindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kung’oka kwa mawaziri hao kulitangazwa bungeni jana usiku na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wao baada ya kuwasiliana naye kwa mashauriano akiwa nchini Marekani kwa matibabu.
Mawaziri waliong’olewa kutokana na ripoti ya kamati hiyo iliyoongezewa shinikizo na michango ya wabunge wengi ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa  Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Waziri wa  kwanza kutangaza kujiuzulu alikuwa ni Kagasheki huku uamuzi wa mawaziri watatu kujiuzulu ukitangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Kagasheki alitangaza kujivua wadhifa huo sa 2:09 usiku alipokuwa akichangia majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli ambaye ni Mbunge wa Kahama (CCM).
Katika maelezo yake Kagasheki alisema: “…Mimi ni mtu mzima nimesikia hisia nzito sana kwa waliyoyasema wabunge.  Rais Kikwete aliponiteua ilikuwa ni kwa furaha yake na operesheni hii, yaliyotokea yametokea hali ya wanyama huko si nzuri;
Mimi mwenyewe nimewasikia na nachukua fursa hii kuteremka ngazi hii ya uwaziri na nitachukua taratibu za kawaida kuijulisha sehemu inayohusika(Rais).
Baada ya Kagasheki kutangaza hatua hiyo, Spika aliwaita mawaziri Dk Nchimbi na Nahodha kuchangia hoja hiyo, hata hivyo hawakuwepo ndipo alipoitwa Dk Mathayo na kutoa maelezo yake.
Katika maelezo yake Dk Mathayo alisema kuwa ripoti hiyo haikumtendea haki kwani kamati ya Lembeli haikumwita kumhoji na kwamba hata ripoti nzima haikueleza kuhusika na kashfa hiyo. Hata hivyo akihitimisha hoja hiyo Lembeli alisema Dk Mathayo ameshindwa kusimamia mapendekezo tisa, yakiwemo matatizo    ya wafugaji aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete Januari 18, 2006 alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Akitoa maelezo ya kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Niliona nimtafute mkuu wa nchi (Rais Jakaya Kikwete), nilimpa picha yote ya kinachoendelea, alikubali ushauri wa Bunge; ..amekubali kuchukua ya uamuzi wa kutengua uteuzi wao(mawaziri).”
Akihitimisha mjadala huo wa ripoti ya kamati yake, Lembeli alisema: “...Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii nao wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao na unyama uliotokea kwenye mpango wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Rushwa iliyopo ndani ya wizara hiyo ni kubwa inakusanywa kwa kutumia simu, hivyo Serikali izichunguze simu zao kuanzia leo.”

Friday, December 20, 2013

SKYLINGHT KUFUNGA MWAKA 2013 MELINI NA WANA MWANZA.

MPANGO MZIMA BOFYA PLAY:-

KWA MARA YA KWANZA ...IN THE ROCK CITY... SKYLIGHT ENTERTAINMENT NA MKOMBOZI ENTERTAINMENT WANAWALETEA....

CRUISE PARTY...KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA..

TUNAKARIBISHA MWAKA MPYA KWENYE FERRY BOAT  KWA KUFURAHI NA MUZIKI WA LIVE MKALI NA SKYLIGHT BAND,BENDI YAKO YA KIJANJA..

VUTAPATA TUSKER LITE AU PEPSI YA BURE MLANGONI KWA WATU 100 WA KWANZA..

KUTAKUA NA SHOTS ZA TEQUILLA NA ZAWADI KIBAO...

TUTA POP CHAMPAIGNS NA KUSEREBUKA NA SKYLIGHT NA MAFATAKI YA NGUVU TUKIKARIBISHA MWAKA MPYA..

KIINGILIO..15,000 KWA MMOJA   NA 25,000 KWA WAWILI.
MAHALI PA KUPANDIA FERRY NI MWALONI NA SKYLIGHT BEACH RESORT..
MUDA: KUANZIA SAA 12.JIONI

PARTY INALETWA KWENU NA 
PEPSI,TUSKER LIGHT,MKOMBOZI ENTERTAINMENT,GOLDCREST HOTEL,KVANT,NA SKYLIGHT BEACH RESORT.

MZIGO UMESIMAMIWA NA JEMBE NI JEMBE...
USIKOSEE..

PICHA ZA HAPA NA PALE KISESA

Wakazi wengi wa eneo hili ni wakulima na wafugaji.. nazo wachuuzi wa pembejeo wameziona Fursa.
Pancha...
Pilika pilika za mashineni....
Kibanda cha muuza nguo za mitumba aka pamba, lakini leo hayupo kaenda kuchukua mzigo.
Mwenyekiti yupo?

Thursday, December 19, 2013

MAGUFULI, WASIRA NA NDIKILO WAONGOZA MAELFU KATIKA SAFARI YA MWISHO YA MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM.

Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya mazishi ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Diwani wa kata ya Kisesa hadi mauti yalipomkuta Marehemu Clement Mabina.
Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Mabina.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akito salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kwenye ibada ya mazishi ya Mabina.
Akitoa salamu za rambirambi kwaniaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarsti Ndikilo amesema kuwa, Rais Kikwete  ametoa pole kwa wananchi wa Kisesa na Mkoa wa Mwanza juu ya tukio hili la msiba wa marehemu Mabina (58) na mtoto Tevery Malemi (12) kutokana na vifo vilivyosababishwa na mgogoro wa ardhi.

Ameongeza kuwa migogoro ya ardhi inapaswa kushughulikiwa kwa uangalifu mkubwa huku hekima na busara zikitumika kushughulikia utatuzi wa migogoro hiyo badala ya kutumia hasira jambo ambalo siku zote husababisha majonzi na madhara makubwa kwa jamii.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wasira akitoa salamu za rambirambi.
Sehemu ya wanafamilia na viongozi wa Vyama vya siasa na serikali wakishiriki ibada ya mazishi.
Ni sehemu tu ya waombolezaji waliofika katika viwanja vya Red Cross kushiriki ibada hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Jimbo la Magu naye alitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo.
Katibu wa uhamasishaji wa Chipukizi UVCCM Taifa Paulo Makonda (kushoto) alishindwa kujizuia kuficha hisia zake na kububujikwa na machozi, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja naye akipiga dua la kumuombe amarehemu Mabina.
Mkuu wa wilaya ya Magu Jackline Liana akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo.
Huku akibubujikwa na machozi na kuangua kilio, Mbunge wa Jimbo la Magu Festus Limbu akimpa mkono wa pole mjane wa marehemu Mabina.
Katibu wa uhamasishaji wa Chipukizi UVCCM Taifa Paulo Makonda akiwasilisha salamu za rambirambi.
Askofu Mstaafu wa kanisa la AICT Paulo Nyagwaswa naye alipata fursa ya kutoa neno kwa maelfu ya waombolezaji waliojitokeza leo kwenye ibada hiyo ya mazishi.
Sehemu ya makada wa Chama cha Mapinduzi.
Ulinzi na utaratibu ulizingatiwa na kamati ya mazishi.
Ni moja kati ya eneo la mti wa historia ndani ya viwanja hivyo ambapo baadhi ya waombolezaji waliketi wakifuatilia mwenendo wa ibada.
Kusalimiana na kupeana pole kwa viongozi.
Umati ukisubiri kuuaga mwili wa marehemu Mabina.
Uwanjani ilikuwa hivi.
Kutoka juu.
Ndugu wa karibu na marehemu wakiongozwa na baadhi ya watawa kutoka eneo la ibada ya mazishi tayarikuelekea eneo la maziko kitongoji cha Kanyama.
Mbunge Chenge akitoa ushuhuda kwa wanahabari alivyomfahamu marehemu mabina.
Mkurugenzi wa Global Publisher Erick Shigongo akimwelezea marehemu Mabina.
Bodaboda nazo zilitoa huduma ya usafiri.
Sasa ni safari kuelekea makaburini.
Msafara.
Mwili wa marehemu Mabina ukiwasili eneo la maziko kitongoji cha Kanyama.
Ibada ya mwisho kabla ya mazisho eneo la kaburi.
Jeneza la mwili wa marehemu Mabina likishushwa kwenye nyumba yake ya milele.
Viongozi wakiongozwa na Mh. Magufuri wakiweka mchanga kwenye kaburi. 
Mh. Wasira na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata wakiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Mabina.
Mjane wa marehemu Clement Mabina,  Bi. Judith Mabina akiweka shada la maua kwenye kaburi la  marehemu mumewe.
Vijana. 
Kumbukumbu.
Kwaheri Clement Mabina, Tunakuombe rehema za Mwnyezi Mungu upumzike kwa amani.