ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 18, 2019

MAONESHO YA KWANZA YA KAZI ZA TEHAMA YAZINDULIWA NCHINI.

 Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akisaini mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa Maonyesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana
 Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akizungumza na Wageni waalikwa kutoka makampuni mbali mbali yaayojihusha na Tehama, Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walisoma mambo ya Tehama na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana.  
 Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akisalimiana na baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana.  
Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbalibali walisoma mambo ya Tehama wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana.  

Wednesday, July 17, 2019

MARAIS 16 KUKUTANA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 39 WA SADC

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC utakaofanyika mwezi Agosti mwaka 2019 jijini Dar es salaam. 

 Mkutano huo utatanguliwa na vikao vya awali kwaajili ya maandalizi na kutangulia kwa wiki ya maonyesho ya bidhaa za ndani ujulikanao kama wiki ya viwanda ya SADC 22-26 Julai. Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa nchi 16 zinazounda jumuiya ya SADC. 

 Mara ya mwisho nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo ilikuwa mwaka 2003 ambapo Rais Benjamini Mkapa alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

WATEJA WATANO WA TIGO KUSHUHUDIA FAINALI ZA AFCON NCHINI MISRI

 Meneja Mawasiliano wa Tigo , Woinde Shisael (Kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akitangaza washindi 5 wa tiketi za kwenda kushuhudia mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri kupitia promosheni ya SOKA LA AFRICA inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, (Kushoto) Mtaalamu wa Huduma za ziada kutoka kampuni hiyo, Ikunda Ngowi.
 Mmoja wa washindi wa tiketi ya ndege kwenda nchini Misri kupitia promosheni ya SOKA LA AFRICA inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Lukundo Samuel Sikombe, kutoka mkoani Arusha akipokea stakabadhi ya kusafiria (boarding pass), kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Tigo , Woinde Shisael (kulia) katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa washindi wa tiketi ya ndege kwenda nchini Misri kupitia promosheni ya SOKA LA AFRICA inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Lukundo Samuel Sikombe, kutoka mkoani Arusha, akipokea stakabadhi ya kusafiria (boarding pass),  kwa  niaba ya washindi wenzake (waliosimama nyuma) kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Tigo , Woinde Shisael (kulia) katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
---
Baada ya kuwezesha wateja wake watano kushuhudia mechi za ufunguzi za michuano ya mataifa ya Afrika, kupitia promosheni yake inayoendelea ya SOKA LA AFRIKA, leo Tigo imetangaza washindi wengine watano watakaogharamiwa safari za kwenda Misri kushuhudia mechi za fainali mubashara.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, amewataja washindi hao watano ambao sasa wanakamilisha idadi ya washindi kumi wa promosheni hiyo kuwa ni Kaunda John Petro, kutoka Zanzibar, Mohabe Noah Senso, (Dar es Salaam), Jafari Abdallah Zitto, (Tanga), Shabani Msafiri James (Dar es Salaam), na Lukundo Samuel Sikombe, (Arusha).

“Tigo,  tunayo furaha kuona promosheni  hii ya SOKA LA AFRIKA inawezesha wateja wetu wengine kujishindia safari ya kwenda kuona mechi za fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika sambamba na kuwezesha wateja kujishindia  fedha taslimu kwa siku,wiki na kwa mwezi kuanzia laki moja hadi milioni 10.Vilevile tumefanikisha dhamira yetu ya kuwashukuru  kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kununua bidhaa na kutumia huduma zetu”,alisema Shisael.

Kupitia promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu washiriki wataendelea kujishindia zawadi za fedha taslimu kila siku, kwa wiki na kwa mwezi. Ili kushiriki kinachotakiwa ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15670 au tembelea tovuti ya  www.tigosports.co.tz  na kujibu maswali kuhusiana na michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.     

Mashindano ya promosheni ya SOKA LA AFRIKA ni sehemu ya jitihada za Kampuni ya Tigo kuwashukuru wateja wake kwa kutumia bidhaa na huduma za Kampuni. Pia promosheni hii ni sehemu ya ubunifu ambao umelenga kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wateja.

ATCL KUANZA SAFARI KUTOKA DAR ES SALAAM HADI MUMBAI, INDIA.


Waziri wa Ujenzi. Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe ametangaza kuanzia leo Jumatano, Julai 17 Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) litanzindua safari yake ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai, India na safari hiyo itaanzia katika Uwanja Mpya wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA, Terminal III.

Waziri Kamwelwe alisema hayo mwishoni mwa juma alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Taifa la Ufaransa, kwenye makazi ya Balozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Kamwelwe alisifu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa na kuwakaribisha wawekezaji wa Ufaransa kuja kuwekeza nchini katika sekta za usafirishaji, kilimo, mifugo na uvuvi na kuongeza kuwa Tanzania ni sehemu salama.

NATOA SIKU SABA KITUO CHA AFYA IBABA KIANZE KAZI-BRIGEDIA MWANGELA

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela akizungumza na viongozi katika humba cha upasuaji katika kituo cha Afya Ibaba ambapo ameagiza huduma zianze kutolewa ndani ya siku saba.
 Majengo ya Kituo cha Afya Ibaba, Wilaya ya Ileje yaliyojengwa kwa fedha za serikali shilingi milioni 400 ambayo yamekamilika lakini huduma za Afya hazijaanza kutolewa.
 Majengo ya Kituo cha Afya Ibaba, Wilaya ya Ileje yaliyojengwa kwa fedha za serikali shilingi milioni 400 ambayo yamekamilika lakini huduma za Afya hazijaanza kutolewa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amempa siku saba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ahakikishe kuwa kituo cha Afya cha Ibaba Wilayani humo kinatoa huduma za Afya hususani huduma za Mama na mtoto,
Brigedia Mwangela ametoa agizo hilo mara bada ya kukagua maendeleo ya ujenzi katika kituo hicho na kukuta miundombinu yote muhimu ikiwa ni pamoja na majengo yote yakiwa yamekamilika lakini huduma za afya hazitolewi.
“Mkurugenzi nakups siku saba akina mama na watoto waanze kupata huduma hapa, kituo hiki kimekamilika isipokuwa kwa mambo machache ambayo yapo ndani ya uwezo wenu”, amesisitiza Brigedia Mwangela.
Amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa Daktari aliyepaswa kuhudumia kituo hicho anafika siku ya Jumatatu na pia halmashauri ihakikishe ujenzi wa njia za wagonjwa (walkways) wenye thamani ya shilingi milioni 20 unakamilika mapema.
Aidha Brigedia Mwangela amewataka wananchi wa Ibaba kukitunza na kukitumia hicho na endapo kutakuwa na ucheleweshwaji wa kuanza kutolewa huduma watoe taarifa ofisini kwake.
“Wananchi wa Ibaba nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya ndio maana kumekuwa na ujenzi wa Kituo hiki, sasa ikifika Jumatatu Daktari hamjamuona hapa mnitaarifu na mkiona imefika siku ya ijumaa akina mama na watoto hawapati huduma hapa nijulisheni”, amesema Brigedia Mwangela
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya amesema serikali imetoa shilingi milioni 400 zilizojenga majengo ya upasuaji, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, wodi ya wazazi na nyumba ya daktari pia imepeleka vifaa vya kutolea huduma vyenye thamani ya shilingi milioni 92.2 katika kituo hicho.
Dkt. Kagya ameeleza kuwa kwa majengo ambayo tayari yamekamilia na vifaa vilivyokwisha tolewa kituo hicho kinaweza kutoa huduma za mama na mtoto isipokuwa huduma ya upasuaji ambayo itahitaji uwepo wa njia ya kupitia wagonjwa (Walkways).
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa watazingatia maagizo yake na kuhakikisha wananchi wa Ibaba wanapata huduma za Afya katika kituo hicho ndani ya siku ya saba walizopewa.

SONGWE DC WAONGEZE NGUVU KUKAMILISHA UJENZI WA VITUO VYA AFYA

 Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia Opulukwa (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu chumba cha upasuaji kutoka kwa  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya (katikati) wakati alipotembelea Kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi ili kujifunza kwa vitendo ukamilishaji wa Vituo vya Afya, Kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songwe Humphrey Masuki.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela na Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia Opulukwa wakisikiliza maelezo kuhusu chumba cha kuhifadhia maiti kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya wakati wa ziara Katika Kituo cha Afya Isansa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela ameutaka Uongozi wa Wilaya ya Songwe Kuongeza jitihada na nguvu Zaidi katika kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya vya Magamba na Mbuyuni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya hiyo.
Brigedia Jenerali Mwangela ameyasema hayo leo mara baada ya kupokea taarifa ya mpango wa ukamilishaji wa miradi hiyo kutoka kwa uongozi wa Wilaya ya Songwe na kisha kuwapeleka katika Mradi uliokamilika wa Kituo cha Afya ya Isansa Wilaya ya Mbozi na ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili waweze kujifunza kwa vitendo.
“Baada ya kupokea taarifa yao ya ukamilishaji wa miradi ya ujenzi ya Wilaya ya Songwe, nimeona ni vema waje wajifunze kwa vitendo kwakuwa ukamilishaji wa miradi yao ya ujenzi umekuwa ukienda taratibu mno pia wajifunze kufanya kazi za serikali kwa teamwork”, amesisitiza Brigedia Mwangela.
Brigedia Jenerali Mwangela amesema miradi ya ujenzi ya Wilayani humo mingi bado haijakamilika na muda umewaishia hivyo kwa ziara hiyo wajifunze kuwa wenzao wamekalisha miradi hiyo  na inahudumia wananchi na pia kazi za serikali zinapaswa kukamilika kwa muda.
“Wao vituo vimechelewa sana kukamilika wamekuja wajifunze na waongeze nguvu ili waweze kukamilisha mapema, wameniambia wamejifunza kitu lakini pia wanapaswa kutambua kuwa kazi za serikali unapewa fedha, vifaa na muda maalumu wa kukamilisha”, ameeleza Brigedia Mwangela
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia Opulukwa amesema wamejifunza kuwa wenzao wameweza kumalizia ujenzi wa Vituo vya Afya kwa viwango vizuri na wao watafanya hivyo ili wananchi waanze kupata huduma.
“Tumeona wenzetu wamekamilisha vizuri nasi tutajitahidi kukamilisha vizuri vituo vyetu ya Afya vya Magamba na Mbuyuni pamoja na hospitali ya Wilaya ili tuweze kutoa huduma kwa wananchi wetu ifikapo Julai 30, 2019”, amesema Opulukwa.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songwe Humphrey Masuki amesema wamejionea namna nzuri ya umaliziaji wa vituo vya Afya ili viwe na ubora na kutoa mfano kuwa wamejifunza namna nzuri ya upangaji makabati katika chumba cha kuhifadhi maiti na upangaji wa makabati na meza katika jengo la maabara.

TABD YAPATA TUZO YA MANUNUZI BORA 2017/2018

 Meneja Mawasiliano, Bi Chaba Rhuwanya (mwenye miwani kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo (wa pili meza kuu) wakati wa hafla ya utoaji tuzo iliyotolewana PPRA ya mnunuzi bora kwa mwaka 2017/2018.
Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania, imepokea kwa furaha kubwa tuzo iliyotolewana PPRA ya mnunuzi bora kwa mwaka 2017/2018. 

 Akipokea tuzo hiyo Meneja mawasiliano, Bi Chaba Rhuwanya ambaye amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TADB bwana Japhet Justine amesema wameipokea tuzo hiyo kwa fahari sana, kwa sababu tuzo hiyo nikielelezo cha uongozi bora na usimamizi mzuri wa fedha za umma kwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha katika manunuzi. 

 Amesema usimamizi huo mzuri ndio unaowezesha Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuweza kutoa huduma kwa wadau wetu wakubwa ambao ni Wakulima, Wafugaji, na wavuvi na walioko kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo ikiwemo wenye viwanda. "Ni ahadi yetu kuwa tutaendelea usimamizi mzuri katika manunuzi yetu ili fedha ziweze kuendeleza na kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Sisi Benki ya Maendeleo ya Kilimo tunaamini Kilimo Kinabenkika," amesema Bi. Ryuwanya.

Tsh Milioni 125 zilizokusanywa na Wafugaji kusaidia kaya Masikini Ngorongoro



Zaidi ya Tsh. Milioni 125 zimekusanywa na Wafugaji katika tarafa ya Ngorongoro wakishirikiana na Viongozi wa kisiasa na Taasisi za umma na binafsi ambazo zitatumika kuimarisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa (Vikoba ) ili kusaidia kaya masikini kujikwamua kiuchumi.

Edward Maura ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji  wafugaji kutoka vijiji vya tarafa ya ngorongoro amesema kuwa  wamekutana na kuanza kuchanga zaidi ya Tsh. Milioni 100 huku wengine wakijitolea mbuzi ng’ombe na kondoo, wafikika hatua hiyo baada ya kuona kuwa hakuna sababu ya kusubiri misaada kutoka nje wakati wenyewe wanauwezo wa kutatua changamoto zao kwa kuunganisha nguvu pamoja.

William Ole Nasha ni Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Ngorongoro  amesema kuwa hatua ya kusaidia vikundi hivyo itasaidia katika kupunguza umasikini kwa wafugaji hao kwa kutumia Vikoba ambavyo vimekua vikileta matokeo makubwa katika uchumi wa wananchi.

James Ole Millya ni Mbunge wa Simajiro amesema kuwa uwezweshaji wa kundi la wafugaji wanaoshi katika mamlaka hiyo utasaidia pia katika kuibua vyanzo vipya vya mapato mbali na mifugo na pia na pia kuona umuhimu wa kuhifadhi rasilimali za wanyamapori na mazingira.

MAGUFULI ALIPOTINGA GEREZA LA BUTIMBA MWANZA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akitekeleza majukumu ya kiserikali

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YASEMA MKAKATI WA SERIKALI NI KUENDELEZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI



Na Ripota,Michuzi TV-Morogoro

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji imesema kuwa mpango mkakati wa Serikali ni kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Marco Ndonde akiwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro ambako yeye,Wataalamu  na maofisa wengine wamekwenda kuangalia shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinazofanyika katika Shamba la Skimu za Umwagiliaji Dakawa,Mvomero mkoani Morogoro, ambayo miundombinu yake imeboreshwa kupitia ufadhili wa fedha wa Serikali ya Marekani.

Hivyo amefafanua kuwa mpango kazi ambao umefanyiwa mapitio mwaka 2018 ni kwamba Serikali imejipanga kufanya kilimo cha umwagiliaji kwa kutotegemea mvua, kwa kuwa na miundombonu ya maji hasa kwa kuvuna maji kupitia mabwawa.

"Hivyo katika mpango kazi tumepanga kujenga mabwawa kwa awamu mbili 
awamu ya kwanza ni kuanzia mwaka 2018- 2025 mabwawa 51 na awamu ya 2026 hadi mwaka 2035.

"Kwa ujumla wake tunatarajia kujenga na kukarabati jumla ya mabwawa 112 na kwa kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2035 na lengo ni kuwa na skimu za umwagiliaji ambazo zinapata maji kwa muda wote na zinakuwa zinavuna maji kupitia mabwawa ambayo yatakuwa yamejengwa,"amesema.

Ameeleza kazi zote za ujenzi wa miundombinu na ukarabati wa skimu ni fedha ambazo zimetoka Serikali ya Marekani na kwamba jumla ya Sh.bilioni 24 zimetumika ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu , kuweka pampu na kusakafia mifireji.

"Nitoe shukrani kwa Serikali ya Marekani kwani kupitia ufadhili wao tumeweza kuboresha miundombinu kwenye skimu hii na leo hii faida yake tunaiona.

"Huko nyuma tulikuwa tunaboresha skimu juu juu tu lakini hivi sasa tumeziboresha kwa kiwango kikubwa sana,"amesema Ndonde na kueleza kuwa Serikali kupitia JICA kuna mradi wa kusaidia wakulima wadogo, ambao huo nao utawezesha kukamilika kwa skimu nyingine na mkakati uliopo ni kuhakikisha skimu zote zinakuwa na miundombinu iliyoboreshwa.

Ndonde amesema na ili kufikia hatua hiyo ni vema wakawa wanatengeneza miundombinu kwa skimu chache chache badala ya kufanya katika skimu nyingi kwa wakati mmoja.

Hata hivyo amesema kuna sera ya Taifa ya umwagiliaji inayoshauri na kueleza kuwa mifereji mikuu yote isakafiwe , hivyo wanakwenda na sera hiyo.
 Mfereji mkubwa wa kusambaza maji katika mashamba ya Mpunga,ukiwa umesakafiwa vizuri kuhakikisha maji yanayotumika kumwagilia mashamba hayo hayapotei tena,kufuatia ukarabati mkubwa kufanywa katika miundo mbinu ya Skimu za Umwagiliaji  ndani ya mashamba hayo.
Moja ya Shamba la Mpunga.

   Mwenyekiti wa Ushirika Wakulima Wadogowadogo  Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa,Mvomero mkoani Morogoro Bwa.Thomas Kakema  akimuonesha Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya  Umwagiliaji Bwa.Marco Ndonde namna Miundombinu ya Skimu za Umwagiliaji zilivyoboreshwa katika shamba hilo la Ushirika.
 Pichani wa pili kulia,Kaimu Mkurugenzi Tume ya  Taifa ya Umwagiliaji Bwa.Marco Ndonde akimsikiliza Mwenyekiti wa Ushirika Wakulima Wadogowadogo  Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa,Mvomero mkoani Morogoro Bwa.Thomas Kakema alipokuwa akimuonesha namna Miundombinu ya Skimu za Umwagiliaji zilivyoboreshwa katika shamba hilo la Ushirika.
 Sehemu ya mashine za kusukuma maji na kupeleka kwenye mashamba ya Mpunga kupitia mifereji ambayo kwa sasa imekarabatiwa na kuwa bora zaidi,kuhakikisha maji hayapotei 

KUBORESHWA KWA MIUNDOMBINU SKIMU ZA UMWAGILIAJI KWAPAISHA BAJETI YA HALMASHAURI MVOMERO MKOANI MOROGORO.


Na Ripota, Michuzi TV-Morogoro

HALMASHAURI ya Wilaya Mvomero mkoani Morogoro imesema asilimia 30 kati ya asilimia 33 ya bajeti ya halmashauri hiyo inategemea mazao ya kilimo na hasa cha umwagiliaji.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Florent Kyombo mbele ya Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Marco Ndonde.

Wakurugenzi hao wapo katika wilaya hiyo ya Mvomero kwa lengo la kuangalia shughuli za kilimo cha umwagiliaji kinachotokana na skimu zilizopo wilayani humo ikiwa ni jitihada za Serikali kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.

Akifafanua zaidi Kyombo amesema mchango wa kipato kinachotokana na kilimo cha umwagiliaji kwa halmashauri ni mkubwa na asilimia 33 ya bajeti ya halmashauri inategemea mazao ya kilimo na kati hizo 30 ni mazao ya umwagiliaji.

"Hivyo tukiona skimu zinaendelezwa katika Wilaya yetu na zinafanya kazi kwa ufanisi tunaamini wananchi wetu watavuna sana na maana yake hata kwa halmashauri tunatajia mapato ya fedha za bajeti kuongezeka.

"Hivyo kupitia fedha hizo halmashauri itajenga madarasa, zahanati, itaboresha miundombinu pamoja na kuendeleza miradi mingine ya maendeleo kwa ajili ya wananchi,"amesema Kyombo.

Pia amesema kuimarika kwa miundombinu kumekuwa kukiongeza mzunguko wa fedha, kwani sehemu kubwa ya kipato cha wananchi kinategemea kilimo na mifumo. "Hivyo wananchi wakivuna utaona mzunguko wa fedha unaongezeka na shughuli za uchumi zinachangamka ikiwemo watu kwenda minadani."

Akizungumzia skimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Kyombo amesema kuna skimu 11 lakini zinazofanya kazi ni chache kwani nyingine bado hazijaendelezwa. 

"Ukiangalia hata maeneo yaliyowekwa miundombinu ni madogo ukilinganisha na ukubwa wa eneo la Skimu. Hata hivyo kupitia skimu hizo chache ukweli ni kwamba faida zake ni nyingi sana kwani kwa sasa uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka na hiyo maana yake pato la mwananchi nalo limeongezeka,"amesema Kyombo.

Amesisitiza kutokana na kuboreshwa kwa skimu hizo wakulima wa zao la mpunga wanavuna kati ya gunia 40 hadi gunia 50 kwa ekari moja wakati huko nyuma kabla ya skimu walikuwa wnavuna kati ya gunia 10 hadi 15 tu.

"Kuptia skimu ambazo tunazo , uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka.Pia imetoa fursa ya ajira kwa vijana, wanawake na wanaume na kubwa zaidi kila mmoja anaweza kujikwamua kiuchumi."Hivyo Halmashauri tumeendelea kuwa na mikakati ya kuomba fedha ili skiku ambazo bado hazijaendelezwa nazo ziendelezwe.Kwa Dakawa tunayo skimu kubwa sana ambayo uwepo wapo umefanya kuwe kunazalishwaa mpunga kwa wingi sana,"amesema Kyombo.

Pia amesema kwa halmashauri yao nao wamejipanga ili kuwa na Skimu ambayo wanaamini itasaidia kuongeza mapato na kuwa chachu kwa wakulima wa mpunga huku akitoa rai kuwa wananchi wanalo jukumu la kuhakikisha skimu ambazo miundombinu yake imeendelezwa inalindwa.Wakati huo huo ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuendeleza skimu zilizopo Mvomero kwani imekuwa ikitumia fedha nyingi kuziendeleza ikiwemo skimu ya Dakawa.

Pia amesema kuna skimu nyingi ambazo nazo miundombinu yake ipo hatua mbalimbali ya kuendelezwa na ni matumaini yao zitakapokamilika zitasaidia kuongeza upatikanaji wa mazao ya kilimo."Wananchi wamehamasika sana kutokokana na uwepo wa skimu hizi.Tunafahamu skimu kongwe zote nazo zipo kwenye mchakato wa kuendelezwa ikiwemo skimu ya Mkenge ambayo imeshawekewa banio na itaanza kutumika siku za karibuni,"amesema Kyombo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo akifafanua jambo ofisini kwake mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde, Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda wakiwa na Wataalamu pamoja na Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (hawapo pichani),kuhusu Skimu ya Umwagiliaji wilayani humo mkoani Morogoro
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo akisoma moja ya kitabu (nyenzo) kinachohusu Skimu ya mwagiliaji,alichokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde (pichani kulia) kwa ajili ya kuendelea kuimarisha Skimu ya Umwagiliaji Wilayani humo,mkoani Morogoro.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Wataalamu wapo katika wilaya hiyo ya Mvomero kupata taarifa kuhusu Maendeleo na mafanikio waliyoyapata baada ya ukarabati mkubwa wa miundombinu kufanyika katika shamba la Ushirika la Wakulima Wadogowadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWADA),Wilayani humo,ambapo ukarabati wa miundominu hiyo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada la USAID-Tanzania,aidha gharama za ufadhili huo wa Ukarabati wa Miundombinu hiyo ya shamba imegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24.
Pichani kulia Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda wakiwa na Wataalamu pamoja na Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu Maendeleo na mafanikio waliyoyapata kufuatia ukarabati mkubwa wa miundombinu uliofanywa katika shamba la Ushirika la Wakulima Wadogowadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWADA),Wilayani humo,ambapo ukarabati wa miundominu hiyo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada la USAID-Tanzania,aidha gharama za ufadhili huo wa Ukarabati wa Miundombinu hiyo ya shamba imegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24. 
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda akiomba taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kuhusu Skimu ya Umwagiliaji katika Wilaya ya Mvomero inavyofanya kazi na mafanikio yake mpaka sasa.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde (kushoto) pamoja na Wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kuhusu maendeleo na mafanikio ya Skimu ya Umwagiliaji wilayani humo.

KUMBE MAGUFULI ALIISHI IGOGO.......


UKIULIZA wakazi wa jiji la Mwanza ni wachae sasa wasiojua historia na sifa kuu ya maisha tata, iliyo tawala  kwa miaka mingi kwa watu wa viunga vya kata ya Igogo iliyopo wilaya ya Nyamagana mkoani hapa.

Matukio ya Wizi, Uporaji wa kutumia nguvu, Ubakaji na fununu za Ushirikina ni matendo yaliyotawala kwa kipindi kirefu hasa katika miaka ya nyuma, lakini wengi wanasema huwenda sababu kuu ya matukio hayo kushamiri ikawa ni kwa kuwa eneo hilo awali lilitambulika kama makazi ya watu wa hali ya chini ambao walikuwa wamechangamana na wachache wenye kipato kizuri hivyo suala la kuoneana wivu likapata nafasi.

Sawa tutazungumza sifa mbaya lakini pia IGOGO ina mazuri yake, kwanza inapatikana kwenye moja ya vilima vya miamba ya mawe viliyotawala eneo kubwa la ardhi ya Mwanza, mpaka ikaitwa ROCK CITY.

Pili IGOGO ndilo eneo lenye idadi kubwa ya uwekezaji wa viwanda vikubwa nayo reli ya kati inapita katikati ya IGOGO.

Lakini jingine kubwa usilolijua ni hili.... Hivi unajua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alishawahi kuishi IGOGO? Msikilize yeye mwenyewe akifunguka hiyoo juzi Jumatatu ya tarehe 14 July 2019.

RAIS AFUKUWA KABURI JINGINE LA UPIGAJI FEDHA SERIKALINI.

"HATA  kuwapeleka wagonjwa nje kwenda kutibiwa ilikuwa DILI, ilikuwa ni FURSA kwa baadhi ya watendaji wa Serikali  wapo walikuwa wakipewa vibali kwa matibu ya nje kwa ugonjwa wa mafua ili mtu apate nafasi ya kwenda akiwa na akiambatana na msindikizaji  na wengine mpaka wanaenda na wake zao nayo Serikali inaingia gharama kwa wote" 

Ni moja ya makaburi ya upigaji yaliyofukuliwa JANA na Rais Magufuli wakati akifungua vitengo saba vya Huduma za tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza akidai kuwa baadhi ya fedha katika mabilioni tunayodaiwa kwa waliokuwa wakienda kutibiwa nje ya nchi hayana UHALALI.

Kwa maana hiyo Rais amemwagiza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwenda kufukua madeni na kuchunguza kama ni ya halali au laa, na kama si halali basi wadaiwa walioambatana na wagonjwa kwenda nje wakamatwe kuyalipa madeni hayo.........

Rais #JPM akiwa Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza.

Tuesday, July 16, 2019

"HUU NI MRADI MMOJA LAKINI MAENEO MENGINE YANAGUSWA VIPI?" : RC MONGELLA MBELE YA RAIS MAGUFULI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwasilisha maendeleo ya mkoa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Jumatatu Julai 15, 2019 wakati wa uzinduzi wa miradi saba inayohusiana na huduma za tiba yenye thamani ya shilingi Bilioni 10.6 za kitanzania katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando.

"Nayasema haya Mhe Rais kwakuwa watu wanaweza kujikita Bugando tu!, tukasahau maeneo mengine yameguswa vipi" John Mongella.

Monday, July 15, 2019

WAZIRI MBARAWA AANZA KWA KASI UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS

 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kyaka (hawapo pichani) ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli.
 Baadhi ya wananchi wa Kyaka wakimsikiliza Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani).
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo ya utekelezaji wa mradi wa maji Kyaka kwa wataalam alipotembelea aneo linalopendekezwa kujengwa tenki la maji. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga.
 Muonekano wa Mto Kagera kutokea eneo linalopendekezwa kujengwa tenki la maji Kyaka.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa tenki la maji.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Kyaka, Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera kupata huduma ya majisafi na salama kutoka Mto Kagera ifikapo Desemba, 2019.

Kauli hiyo aliitoa Julai 12, 2019 wakati wa ziara yake Wilayani humo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Julai 11, 2019.

Akiwa njiani akitokea Wilayani Karagwe kuelekea Wilayani Chato, Rais Magufuli alisimama katika Mji Mdogo wa Kyaka kusalimiana na wananchi na walimueleza kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama.

Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Waziri Mbarawa kwa njia ya simu mbele ya wananchi hao kufika eneo hilo siku iliyofuata kuzungumza nao na kuhakikisha kero hiyo inatatuliwa na ikifika kipindi cha Sikukuu ya Krismasi mwaka huu wananchi hao wawe wamepata huduma ya majisafi na salama.

Katika utekelezaji wa agizo hilo, Waziri Mbarawa akiwa ameongozana na Watendaji na Wataalam kutoka Mamlaka za Maji Mwanza (MWAUWASA) na Bukoba (BUWASA) alisisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaondolea wananchi wake kero ya maji na aliwahakikishia wananchi wa Kyaka kwamba kero ya maji inakwenda kuwa historia.

Profesa Mbarawa alisema Mkandarasi mahiri atapewa jukumu hilo la kujenga mradi wa maji na aliwasihi wananchi hao wa Kyaka kutakapojengwa chanzo cha maji kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi atakayetekeleza mradi ili ukamilike kwa wakati na kwa kiwango.

"Tumesema sasa imetosha wananchi kuhangaika, tunawahakikishia wananchi wote wa Kyaka kuwa  mtapata majisafi na salama kutoka Mto Kagera, tunajenga mradi mkubwa wa maji ambao pia ni endelevu," alisema Waziri Mbarawa.

Waziri Mbarawa aliamuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga kushirikiana na Mkurugenzi wa Maji Bukoba, Allen Marwa na wataalam wengine kutoka Wizara ya Maji kusimamia na kuratibu haraka shughuli za awali za ujenzi wa mradi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Sanga alielezea walivyojipanga kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa mradi.

Mhandisi Sanga alibainisha kwamba shughuli za awali za utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na kumpata Mkandarasi wa ujenzi zitakamilika ndani ya muda mfupi ili kazi za ujenzi ziweze kukamilika katika muda ulioelekezwa na Rais Dkt. Magufuli. 

"Ili kukamilisha ujenzi wa mradi katika kipindi kilichoagizwa na Mhe. Rais inatakiwa taratibu za awali zifanyike kwa muda mfupi kadri iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kumpata mkandarasi atakaye jenga mradi," aliongeza Mhandisi Sanga.

Kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha wananchi wa maeneo ya Kyaka, Bunazi na maeneo mengine ya Mutukula, Kakunyu na Bubale.