ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 15, 2022

WANANCHI WAASWA KUTOA USHIRIKIANO THABITI KATIKA UTAFITI WA VVU NCHINI

SERIKALI imezindua Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS 2022-2023) na kueleza kuwa kiwango cha maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI kimeshuka na kufikia asilimia 4.7.


Pia imedhamiria kudhibiti maambukizi ya VVU kwa kuongeza uelewa kwa wananchi,kujua hali zao za maambukizi ya VVU, kujiunga na huduma za matibabu ya VVU,kuongeza uelewa na ujuzi wa kukabiliana na janga hilo nchini.

Aidha utafiti uliofanywa mwaka 2016/17 ulionyesha idadi ya wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliojitambua ilikuwa 61%, waliokuwa kwenye tiba 92% na waliofikia ufubazaji VVU 87%, matokeo ambayo umuhimu wake ulisaidia kuunda mkakati wa Kitaifa wa mwitikio wa VVU na UKIMWI.

01
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene akizungumza na wadau wa masuala ya afya na ukimwi (hawapo pichani) kabla ya kuzindua Utafiti wa Viashia na Matokeo ya Ukimwi Tanzania.
Akizindua utafiti huo mnamo October 1, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene amesema utaiwezesha serikali kufahamu tabia hatarishi zinazochangia kuenea kwa VVU na viashiria vinavyotoa taarifa hizo vitazingatia umri,jinsia, maeneo na nchi kwa ujumla.

“Tunafahamu takwimu bora ni muhimu katika kufahamu ukubwa wa janga la UKIMWI katika nchi yetu,tunaendelea kukusanya takwimu bora zitakazotupa uelewa wa hali ya maambukizi na namna ambavyo programu na afua za VVU zinavyofanya kazi ili kufikia malengo ya 95 ya Shirika la UKIMWI duniani na kudhibiti janga hili ifikapo 2030,”amesema.

Simbachawene amesema,serikali inahitaji kuendelea kutathmini na kufuatilia kiwango cha maambukizi mapya,idadi ya watu wenye maambukizi ya VVU na walio kwenye matibabu ya ARV za kufubaza VVU.

“Utafiti wa viashiria vya VVU na UKIMWI mwaka 2022/2023 utakuwa wa tano kufanyika nchini baada ya utafiti wa mwaka 2016/2017 uliotoa mwanga juu ya namna tulivyoelekeza nguvu zetu kufikia malengo yaliyokusudiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI,”amesema.

Pia utafiti huo ulionyesha kiwango cha maambukizi nchini, kushuka na kufikia asilimia 4.7 na ulionyesha idadi ya wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliojitambua 61%,walio katika tiba 92% na waliofikia ufubazaji VVU 87%.

Simbachawene amesema tangu mwaka 2018,serikali inatekeleza kwa kasi afua zinazolenga kuwatambua wanaoishi na virusi vya Ukimwi na kuwaunganisha kwenye tiba za ARV wafikie ufubazaji wa VVU,hivyo serikali ina jukumu la kuwahakiki wanaoishi na virusi vya Ukimwi kupitiatafiti ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema serikali kwa utafiti huu kama ulivyokuwa wa mwaka 2016/2017 utatoa takwimu za VVU zitakazotupa uelewa zaidi wa kukabiliana na janga la UKIMWI,takwimu zitatuongoza kuboresha mipango ya afya na mgawanyo wa rasilimali fedha katika program mbalimbali za VVU.

Waziri huyo amesema si kila mtu anayeishi na VVU nchini anafahamu hali yake,hivyo THIS 2022-2023 utatoa fursa kwa kaya takriban 19,000 kupimwa VVU majumbani na kujua hali zao siku hiyo hiyo,watapimwa ugonjwa wa homa ya ini ‘B’ na ‘C’ na watakaokutwa na maambukizi watapata huduma za afya.

“Watakaokutwa na maambukizi ya VVU kwenye utafiti huu wataunganishwa na vituo vya afya watakavyochagua ili kuanza matibabu,huduma za ARV zinapatikana bure katika vituo vyetu vya afya,na matibabu yanasaidia watu wanaoishi na VVU kuishi maisha marefu yenye afya na kupunguza hatari ya kuambukiza watu wengine,”amesema.

Mkurugenzi Mkazi wa ICAP,Haruka Mayaruma amesema utafiti huo ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na ICAP unalenga kuongeza jitihada za kupambana na VVU zisingefanikiwa bila serikali,Kituo cha Dharura cha Magonjwa cha Marekani kwa kuwezesha tiba na matunzo kwa wanaoishi na VVU ili kupunguza vifo na maambukizi mapya.

Amesema kaya 20,000 sawa na watu 40,000 wa umri kuanzia miaka 15 na kuendelea kote nchini zitafikiwa na utafiti huo utakaosaidia kufikia malengo ya 95-959-95.

Balozi wa Marekani nchini,Dr. Donald Right amesema jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania zitasaidia mapambano dhidi ya UKIMWI ingawa eneo la mambukizi ya mtoto kutoka kwa mama hatufanya vizuri na kusistiza tujifunze kwa matokeo ya nyuma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kifua Kikuu na UKIMWI,Fatuma Towafiq alisema Bunge litaendelea kuishauri na kuisimamia serikali itenge bajeti ya VVU na anaamini utafiti huo ukifanyika kwa weledi na umakini utatoa matokeo sahihi yenye tija na kuwawezesha Watanzania kuwa an afya bora.

Naye Naibu Katibu Mkuu Seif Shekilaghe, kwa niaba ya Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu, amesema utafiti huo wa tano kufanyika utaonyesha namna ya kutekeleza mapambano ya VVU na utangalia magonjwa mengine ikiwemo homa ya ini ili kufikia malengo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr.Leonard Maboko amesema za mwaka 2017 zilionyesha watu milioni 1.4 walikuwa na maambukizi mapya na mwaka 2021 watu milioni 1.7 walikadiriwa kuwa na maambukizi ya VVU.

“Asilimia 84 wanafahamu hali zao,73 asilimia wanafikiwa na huduma za afya na 66 asilimia wanatumia dawa za kufubaza virusi (ARV),hivyo takwimu za THIS 2022-2023 zitasaidia kutupima na kuwa na ujuzi wa masuala ya VVU,”amesema Maboko.

Henry Karugendo wa Taasisi ya Takwimu la Taifa (NBS) amesema watashirikiana na Wiara ya Afya kupanga mipango ya afya kwa kutumia takwimu bora za VVU ambazo ni nyenzo muhimu ya kuiwezesha serikali na wadau kuandaa sera, mipango na takwimu rasmi za mapambano ya VVU kuhakikisha watu wanapata huduma za matibabu.

“Takwimu za utafiti wa THIS 2022-2023 zitaonyesha kiwango cha maambukizi mapya ya VVU, kiwango cha watumiaji dawa, kiwango cha homa ya ini B na C na uelewa wa wananchi na kuisaidia serikali kuboresha huduma za afya,VVU na ustawi wa wananchi,”amesema.

Bugingo awapa somo maafisa habari Pwani kutumia taaluma yao kusaidia kuboresha elimu ya awali


  Afisa elimu Mkoa wa Pwani Sara Mlaki  wa pili kutoka kulia aliyeketi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki katika moja ya warsha hiyo.

Na Victor Masangu,Pwani 

Maafisa Habari wa Halmashauri za Mkoani Pwani pamoja na Waandishi wa habari wametakiwa kuwa wazalendo na kutumia kalamu zao kwa weledi katika kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kujiunga katika vituo vya utayari kwa lengo la kupata fursa ya  kujiunga na darasa la kwanza mwaka 2023.


Kauli hiyo imetolewa na Afisa habari wa Mkoa wa Pwani  Zablon  Bugingo  wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ambayo imeandaliwa kwa lengo la kujadili mpango wa utayari ambao unalenga kuwasaidia watoto na kupata elimu ya awali kabla ya kujiunga na darasa la kwanza.


Bugingo alisema kwamba maafisa habari hao wanapaswa kuwa mstari ww mbele kwa kushirikiana na jamii nzima ya Mkoa wa Pwani kuwaelimisha kupitia mafunzo hayo waliyoyapata ili kuweza kufanikisha mpango huo wa utayari kwa watoto kujiandaa kwa ajili ya  kuanza darasa la kwanza kwa mwaka ujao.


"Mpango huu ni vema ukaenda Sambamba na kuwaelimisha wazazi,walezi pamoja na jamii kwa ujumla hivyo maafisa habari wote ambao wameweza kupata fursa hii ya mafunzo sasa ni jukumu lao kutoa sapoti ya Hali na mali na ikiwemo kuandika habari hizi kwa wingi,"alisema Bugingo.


Kadhalika alibainisha kuwa watoto hao wanaandaliwa katika vituo hivyo vya utayari na wanapaswa kusoma kwa kipindi cha muda wa wiki 12 lengo ikiwa ni kuwandaa kupata uelewa juu ya mambo ya shule kabla ya kujikinga rasmi na elimu ya darasa la kwanza.

Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo akiwemo kaimu mkuu wa kitengo cha habari Wilaya ya Kisarawe Waziri Waziri ameahidi kuyatendea haki mafunzo hayo waliyoyapata kwa kuelimisha jamii juuu ya mpango huo wa utayari.


Naye Afisa habari wa Halmashauri ya Kibaha Innocent Byarugaba amesema kuanzishwa kwa mpango huo ni mkombozi mkubwa katika kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngaziza chini ili kuwasaidi  watoto hao kupata elimu ya awali  na hatimaye kujiunga na dara


Naye Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Hellen  Kulwa amewataka Maafisa habari hao  wa halmashauri  kwenda kuzingatia Umri wa Watoto Ili Mwalimu asiache kazi ya kufundisha na kuanza kulea Watoto.


Mpango wa Shule Bora ni Program ya Serikali ya Tanzania ya Kuboresha Elimu ya awali na Msingi Kwa Ufadhili wa mfuko wa Ukaid wa Serikali ya Uingereza  unatekelezwa Katika Mikoa Tisa ya Tanzania.


Katika  warsha hiyo ya  siku moja  ambayo imeandaliwa na ofisi ya Elimu Mkoa wa Pwani imeshirikisha maafisa habari wa halmashauri zote,maafisa maendeleo ya jamii na maafisa ustawi wa jamii.


Thursday, October 13, 2022

WAZIRI MKUU KUFANYA ZIARA JIJINI MWANZA

 

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa anaetarajia kufanya ziara Mkoani Mwanza 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima (kulia) akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya ujio wa Waziri Mkuu.



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambapo ata kagua miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 13,2022  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima, amesema Waziri Mkuu atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Daraja la Magufuli,mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),mradi wa stendi ya kisasa ya mabasi Nyegezi na kuzindua jengo la huduma ya macho kwenye Hospital ya Kanda ya Rufaa Bugando.

“Oktoba 17,2022 Waziri Mkuu atatembelea Wilaya ya Ukerewe ambapo atawasili kwenye kisiwa cha Irugwa kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya,ujenzi wa shule ya sekondari Irugwa”, ameeleza Malima

Katika hatua nyingine Malima ametoa rai kwa madereva na wamiliki wa magari kuwa na utaratibu wa kuondoa magari pindi yanapoharibika barabarani ili kuepusha msongamano unaoweza kusababisha ajali zisizokuwa za lazima.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi, ameeleza mikakati mbali mbali iliyopo ya kuhakisha wanapunguza ajali za barabarani ikiwemo askari kusimamia maeneo ya watembea kwa miguu.

MKOA WA PWANI WAJIZATITI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KWA KUJEGA VITUO VYA WATOTO.


Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani Sara Mlaki akizungumza na washiriki wa warsha hiyo hawapo pichani iliyofanyika Wilayani Kibaha.

 Na Victor Masangu, Pwani 

Serikali mkoani Pwani katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi za chini imejenga vituo vya utayari vipatavyo 36 katika halmashauri zote lengo ikiwa ni kuwapatia elimu watoto waliosahaulika kupata fursa ya elimu ngazi ya awali.


Hayo yamebainishwa na Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani wakati wa kufungua warsha ya mpango maalumu kwa ajili ya kuwandaa watoto hao waweze kuandaliwa vizuri katika  elimu ya awali kabla awajajiunga na darasa la kwanza.

Aidha afisa elimu huyo alibainisha kwamba nia yao kubwa katika mpango huo wa utayari ni kuwajengea uwezo na mahalifa ya katika suala zima la kuweza kujua kusoma,Kuhesabu na kuandika kabla ya kuingia darasa la kwanza.


Pia aliongeza kuwa wameamua kuwakutanisha wadau mbali mbali wa elimu wakiwemo madiwani,watendaji kata,waratibu elimu,wakuu wa shule ili tuweze kuweka mpango wa kuboresha sekta ya elimu kwa watoto hao ambao walishindwa kupata fursa ya kupata elimu ya awali.


"Lengo letu ni kuanzisha vituo vya utayari katika halmashauri zetu tisa kwa ajili ya watoto wetu wa kuanzia miaka 5 hadi 9  ili waweze kupata elimu ya awali kabla ya kuanza kujiunga na darasa la kwanza na halmashauri zetu zinatupa ushirikiano katika kufanikisha Jambo hili"alibainisha Sara.

 Kadhalika alisema kuwa mpango huo ambao umeanzishwa na serikali utawasaidia watoto ambao wamekosa fursa ya kupata elimu kuweza kujifunza zaidi katika kusoma,kuhesabu na kuandika.

 
Kwa upande wake afisa elimu ya watu wazima katika halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Hamisi Chikaula amebainisha mpango huo wa utayari wa kuanzia vituo utaweza kuwa mkombozi mkubwa wa kuwasaidia watoto kupata elimu iliyo bora kuanzia ngazi za chini.


Chikaula ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wawezeshaji katika Warsha hiyo aliongeza kuwa katika mpango huo kila halmashauri inajenga vituo vinne ambavyo vitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa watoto kupata elimu ya awali.


Kwa upande wake diwani wa kata ya mkuza Focus Bundala ambaye ameshiriki katika Warsha hiyo ameahidi kuyafanyia kazi mafunzo yote ambayo wameyapata katika suala zima la kuwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika vituo hivyo.

Diwani wa kata ya Visiga Kambi Legeza aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuanzisha mpango huo wa kujenga vituo ambavyo vitatumika katika kuwasaidia watoto ambao walikosa nafasi katika elimu ya awali.


KWIMBA WAAMUA SABANA MALINJA NDIYE MWENYEKITI CCM WILAYA

 NA ALBERT G. SENGO / KWIMBA

"Kwenye uchaguzi wowote tukubali tukatae suala la makundi, kuvutana na kusigana haliepukiki, uchaguzi umekwisha tushikamane kuhakikisha tunakijenga chama" asema mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Kwimba Sabana Malinja mara baada ya kushinda uchaguzi huo kwa kura 918, akifuatiwa na Mayala David aliyepata kura 248 huku mwingine mmoja akikacha uchaguzi huo kwa kutotokea ukumbini.

Wednesday, October 12, 2022

RAILA AANZA KUWA KARIBU NA RUTO.


Kundi la waendesha bodaboda Jumatano Oktoba 12 walikuwa na bahati baada ya kukutana na kiongozi wa Azimio Raila Odinga. 

Wahudumu wa bodaboda wakipokea zawadi ya Raila Odinga. 

Raila alikuwa kwenye kituo cha kuuza mafuta ya gari wakati alikutana na kundi hilo la wahudumu wa bodaboda. 

Alishuka toka kwenye gari lake na kuamua kuwapa zawadi katika kipindi hiki kigumu kiuchumi kwa kuwanunulia mafuta. 

Huku akiwa amejihami na bunda la noti, Raila al-maarufu 'Baba' anaonekana akilipa bili za mafuta ya kundi hilo na kuwaachia ujumbe kuwataka wachape kazi. 

WAISHI KWA WASIWASI KUFUATIA MFULILIZO WA MATETEMEKO KENYA.

 

Wenyeji wa Kiambu wamekuwa wakishuhudi mitetemeko ya ardhi tangu Jumatatu.

Baadhi ya wenyeji wa Kaunti ya Kiambu wanaishi kwa hofu baada ya kushuhudia misururu ya mitetemeko ya ardhi katika eneo hilo, kwa siku mbili mfululizo. 

Maeneo yaliyoathirika ni pamoja na mji wa Limuru na viunga vyake, Mutarakwa, Ngarariga, Manguo na Ngubi pamoja na maeneo ya Kikuyu kama vile Kerwa, Keroe na Nachu. 

Wenyeji walisema mitetemeko hiyo ya ardhi ilishuhudiwa eneo hilo siku ya Jumatatu na Jumanne, na kudumu kwa muda sekunde kumi.  

 Tukio la kwanza liliripotiwa Jumatatu asubuhi mjini Limuru, kabla ya ingine kuripoti saa sita mchana na hatimaye usiku kabla ya maji kuzidi unga asubuhi. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na jarida la People Daily, Stanley Muturi anayeishi eneo la Manguo alisema kuwa mitetemeko hiyo ilishuhudiwa saa 10.20 usiku mnamo Jumatatu, kwa sekunde kadhaa. 

Ushauri wa wataalam 

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa mazingira Kiambu David Kuria, serikali ya kaunti inashughulikia suala hilo la mitetemeko na kusaka maoni ya wataalam wa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

 Alisema ripoti za awali kutoka kwa wanajiolojia zilifichua kuwa mitetemeko hiyo haikujiandikisha kwenye mfumo wa kukagua mitetemeko ya ardhi nchini. “Sitaki kusema mengi kuhusu suala hilo ila tunasubiri majibu kutoka kwa wataalama kabla ya kutoa taarifa tukiwa serikali ya kaunti,” afisa huyo alisema. 

KOFFI OLOMIDE AJA NA MPYA NYINGINE HII

 Koffi Olomide - Apeleté (Clip Officiel)

SHIRIKA LA BRAC MAENDELEO TANZANIA LIMEJIKITA KUWASAIDIA WATOTO WA KIKE

 

Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mwanaidi Kombo akizungumza wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.



Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa siku hiyo




Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo akizungumza wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.


MRATIBU wa Watoto Jiji la Tanga Mwajuma Mustapha akizungumza wakati wa maadhimisho hayio








Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo


Na Oscar Assenga,TANGA.

MWAKILISHI wa Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo amesema kwamba wao wamejikita katika harakati za kuwasaidia watoto wa kike kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa utekelezaji wa mradi wa elimu kwa mkoa wa Tanga ili kuwawezesha waliokosa fursa hiyo kunufaika nayo.

Katika mradi huo wa elimu Shirika hilo limekuwa likitoa fursa za elimu ya awali yaani ECD kwa watoto wadogo ikiwemo watoto wa kike na elimu ya Sekondari kwa mabinti walio nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa kutumia programu ilioharakishwa Accelerated Learning Program (QT).

Hayo yalibainishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.

Isihaka ambaye ni Msimamizi wa Miradi ya Elimu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Mkoani Tanga alisema kwamba katika utekelezaji wa mradi huo wameweza kuwafikia mabinti wengi ambao wamenufaika kupitia miradi yao.

Alisema kwa upande wa wanufaika wa shule za Sekondari mabinti 926 ambao wengine wapo katika ngazi tofauti tofauti kama vile wasichana 10 wapo vyuo vikuu mbalimbali nchini, wasichana 51 wapo kidato cha sita ,wasichana 25 wamehitimu katika vyuo vya kati mbalimbali nchini na wengine wapo katika ngazi ya Sekondari katika shule huria mbalimbali hapa Tanga.

Alisema pia wanufaika takribani 1376 wamepatiwa mafunzo mbalimbali yahusuyo elimu ya Afya ya Uzazi, Athari zitokanazo na matumizi ya dawa za kulevya, Ujasiriamali nk ikiwemo kuwawezesha vifaa kwa ajili ya kuanza shughuli za uzalishaji katika Jamii kwa lengo la kujiongezea kipato katika nyanja walizosomea kama vile ushonaji, utengenezaji wa batiki, sabuni na mapishi.

"Lakini pia watoto takribani 2100 tumewapatia elimu ya awali katika vituo vyetu vya malezi na makuzi vilivyopo katika shule za Serikali za Msingi Mkoani Tanga huku watoto wengine 772 wanaendelea kunufaika na elimu hiyo nchini ya Ufadhili wa NORAD na Brac Maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa mradi huu "Alisema.

Awali akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana alitoa wito kwa watoto wa kike wasikubali kurubuniwa.

Dkt Sipora alisema kwamba Rais Samia Suluhu amewajali sana watoto wa kike ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa bilioni 580 kwa ajili ya madarasa 29 na mwaka jana alitoa Bilioni 1.8 zaidi ya hapo alitoa Bilioni 2 ya madarasa.

Alisema pia Rais Samia alitoa fedha nyengine zaidi ya Bilioni 700 kwa ajili ya watoto wa kike timiza malengo kila mtoto 250,000 kwa ajili ya kuanzisha miradi ili kuepukana na vishawishike watoto wa kike waliopo mitaani .

"Lakini pia bado kwenye mapato ya ndani Rais Samia ametoa asilimia 10 ya mapato inaenda kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu huko ndani wengi ni wanawake watoto wa kike"Alisema.

Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mwanaidi Kombo bado watoto wa kike wana jukumu la kufanya ili kuondokana na adha ya kukosa maendeleo.

" Kama mlivyomsikia MC hapa amesema kwamba wapo watoto wenyewe wanawashawishi wajomba acheni tabia na tambueni jukumu lenu la kuleta maendeleo endelevu" Alisema

Naibu Meya huyo alitoa wito kwa watoto wa kike kuhakikisha wanasoma kwa bidii maana elimu pekee ndio inaweza kuwakomboa na watambue kwamba hakuna bahati ila waamini kwamba elimu ndio itawawezesha kuwakwamua .

Hata hivyo aliwatoa hofu watoto wa kike kwamba Serikali imeendelea kuuunga mkono juhudi za watoto wa kike kuhakikisha wananufaika na uwepo wa fursa mbalimbali zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi.

LANDESA:UWEKEZAJI WAJIBIFU WA ARDHI YA JAMII UTAPUNGUZA MIGOGORO

 

Mkurugenzi wa Landesa Tanzania, Godfrey Massay akipekua baadhi ya taarifa za ardhi wakati wa mafunzo ya wanahabari na wadau wa ardhi yaliyofanyika mjini Morogoro

Baadhi ya washiri wa warsha ya wanahabari na wadau wa ardhi.

Mtaalamu wa Ardhi wa Landesa, Masalu Luhula akichangia mada katika mafunzo ya wanahabari na wadau wa ardhi yaliyofanyika mkoani Morogoro

 

Na Tumaini Godwin, Morogoro

SHIRIKA la Kimataifa linalojihusisha na masuala ya Ardhi la Landesa limesema Uwekezaji Wajibifu wa ardhi ya jamii utasaidia kupunguza migogoro hasa baina ya wakulima na wawekezaji.


Akifungua mafunzo ya wanahabari na wadau wa sekta ya ardhi, Mkurugenzi wa Landesa Tanzania, Godfrey Massay  amesema ili uwekezaji uwe na tija lazima kuwe na uwajibikaji wa pande zote muhimu hasa Serikali, jamii na wawekezaji.  


Amesema moja ya masuala muhimu kwenye Uwekezaji Wajibifu ni ushirikishwaji wa makundi yote muhimu wakiwemo Wanawake, vijana na walemavu.


Kulingana na Massay, Landesa wameamua kuja na Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Wajibifu kwenye ardhi ya jamii kama dira ya kusaidia kufikia malengo ya uwekezaji huo


"Mwongozo huu ukitumika utasaidia kumaliza migogoro ya ardhi kwenye maeneo mengi," amesema Massay.


Afisa Ardhi wa Landesa, Masalu Luhula amesema zipo sababu nyingi zinazochangia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wawekezaji na wananchi hasa vijijini.


Ameeleza kuwa miongoni mwa hizo nu uelewa mdogo kuhusu masuala ya ardhi kwa baadhi ya wananchi na ushirikishwaji hafifu.


Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameomba kuendelea kupewa elimu kuhusu masuala ya ardhi.


"Wanakuja wawekezaji mnaongea kiswahili halafu wanaleta mikataba ya kingereza, ukisaini tu basi mnajikuta kwenye mgogoro. Kumbe ulisaini kitu hukielewi," amesema