NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
"Siri yangu ni Mwenyezi Mungu tu ndiye anayenipa moyo, ingawa mara nyingine nakata tamaa hasa pale bidhaa zangu zinaposhindwa kwenda sokoni kimauzo kwasababu soko ninalolitegemea ni mtandaoni na wateja kupata ni changamoto lakini sikati tamaa naendelea kutengeneza bidhaa nzuri za viwango" anasema mwanadada mjasiliamali Suki's Craft, Mtanzania mwenye asili ya Asia anayeishi jijini Mwanza akishiriki Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ya TCCIA yanayofanyika katika viwanja vya Furahisha kata ya Kirumba. Kisha akaongeza "Nimejiunga kwenye magroup mengi ya whatsaaap hivyo kila maonesho yakiitishwa naziona fursa za kushiriki" Jeh! nini ombi lake kwa Serikali na vipi siku akikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atamwambia nini? #jembefm #samiasuluhuhassan #ikulumawasiliano #tanzania #maoneshoyabiasharaFriday, September 1, 2023
Wednesday, August 30, 2023
WAZALISHAJI NAMBA MOJA WA VIFAA VYA UJENZI TOKA NCHINI UGANDA WASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA MWANZA
NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Tukiwa bado tuko katika maenesho ya wafanyabiashara Afrika Mashariki (EAC) yanayoendelea katika viwanja vya Furahisha Mwanza yakiandaliwa na TCCIA tunakutana na mwekezaji huyu anayetoka nchini Uganda anayejihusisha na zana za ujenzi toka kampuni ya EA ROOFING . Pamoja na wenyeji Tanzania, washiriki wengine ni kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).Tuesday, August 29, 2023
YANGA WAENDELEZA PALE WALIPOISHIA WAIKUNG'UTA JKT RUVU 5-0
"WANANCHI MNARA UNASOMA 5G TU."
RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SOKO LA CRDB KIZIMKAZI DIMBANI, KUSINI UNGUJA ZANZIBAR
SIKU 4 KABLA YA TUKIO TIKETI ZIMEBAKI CHACHE COUPLES MEET SINGLES MWANZA
𝙅𝙐𝙈𝘼𝙈𝙊𝙎𝙄 ya Tarehe 2 September 2023 chagua uiweke akilini au moyoni?
. 𝗨𝗸𝘂𝗺𝗯𝗶:- Villapark Social Hall Kirumba Mwanza. ‘Couples Meet Singles’ Tutagonga pichaz za kutosha kwa Red carpet. . . 𝗞𝗶𝗶𝗻𝗴𝗶𝗹𝗶𝗼: - Single 70,000 na double 100,000. . Tiketi zinapatikana duka la BJ FASHION iliyopo Furahisha Kirumba pamoja na Ofisi za Jembe Fm Mwanza zilizopo Furahisha Kirumba jijini Mwanza au piga simu namba 0763 74 92 86 au 0759097744.MBUNGE MAIMUNA PATHANI UTAJIRI WA LINDI UPO KWENYE MADINI
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan amesema Lindi utakuwa mkoa tajili Tanzania kutokana na uwepo wa madini ya Kila aina katika ardhi ya mkoa huo.
Akizungumza wakati wa kongamano la madini lililofanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi,Mbunge Maimuna Pathan alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Lindi wanatakiwa kuzitumia vilivyo fursa za uwepo wa madini katika ardhi ya mkoa huo ambao utakuza uchumi wa taifa zima.
Pathan alisema kuwa baada ya miaka mitano kila mtu anatakuwa anazungumzia utajiri wa madini uliopo katika katika mkoa wa Lindi tofauti na ilivyokuwa awali.
Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa zote zilizopo kwenye sekta ya madini ili kukuza uchumi wao na kupata maendeleo kutokana uwepo wa madini mbalimbali.
Pathan alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na utunzaji wa mazingira kwenye maeneo ambayo madini yanachimbwa
Monday, August 28, 2023
BRELA "TUMEJIZATITI KUHAKIKISHA WATEJA WANAOSAJILI MAKAMPUNI MAJINA HAYAGONGANI"
NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe leo ametembelea banda la BRELA katika maenesho ya wafanyabiashara Afrika Mashariki (EAC) yanayofanyika katika uwanja uwanja Furahisha Mwanza yakiandaliwa na TCCIA Kutoka viwanja hivyo jijini hapa Jembe Fm inazungumza na wadau wa banda hilo wakati ukaguzi wa bamanda ukiendelea.MABAKI YA MWILI YALIYOKAA MOCHWARI SIKU 190 YAZIKWA.
Baada ya mabaki ya mwili wa Josephine Mngara (27), mkazi wa Mtemboni, Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kukaa Mochuari kwa siku 190 sasa familia yake imekabidhiwa mabaki ya mwili huo na kwenda kuyazika katika makaburi ya Mereseni yaliyopo katika Mji mdogo wa Himo.
Mwanamke huyo ambaye aliyekuwa akiishi na mpenzi wake Mtaa wa Mtemboni wilayani hapa inadaiwa kuuawa kikatili na mpenzi wake usiku wa kuamkia Februari 19, mwaka huu kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.Februari 23, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori aliiambia Mwananchi kuwa usiku wa kuamkia Februari 19 kuna mwili ulikutwa umechomwa moto na kutelekezwa kwenye pagale ambapo polisi katika kuchunguza walikuta michirizi ya damu kutoka nyumba jirani kuelekea eneo ambalo mwili ulikokutwa umeungulia.
Alisema mabaki ya mwili huo, ikiwemo mifupa na sehemu nyingine imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) kwa ajili ya taratibu nyingine za kiuchunguzi ikiwemo vipimo vya vinasaba (DNA) ambavyo vilipelekea kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kujiridhisha na mabaki ya mwili yaliyokutwa eneo la tukio.
Hata hivyo, siku chache baadaye wakati Jeshi la Polisi likimsaka mtuhumiwa huyo, alituma ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwa mama mkwe wake, Theodora Msuya, mama mzazi wa binti huyo akiomba radhi na kusema roho ya yake inamuuma kwa kujihusisha na mauaji hayo.
"Mama samahani sio kosa langu, nilimkuta ...na mke wangu kwangu nikavunja mlango tukaaza kupigana na ... mimi nikashika panga na yeye akachukuwa mpini wa jembe akawa anarusha nikakwepa ndiyo akampiga mke wangu mpaka chini, akanipa nauli akanambia sepa niachie mimi ataua mtu, mulize (...) mama mimi sijui roho yangu inauma sana mchana mwema," ilisomeka meseji hiyo kwenye simu ya mama mkwe.
Hata hivyo, Mei 18, mwaka huu baada ya miezi mitatu kupita Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanikiwa kumtia mbaroni Erasto Gabriel (31) mkazi wa Mtemboni aliyekuwa akiishi na mwanamke huyo (marehemu) kwa madai ya kuhusika na mauaji hayo.
Mama wa marehemu, Theodora Msuya amesema tukio hilo limewaumiza sana familia na ameacha pengo kubwa kwa familia na kwamba marehemu amemwachia watoto wanne wadogo na kwamba hajui atawalea vipi kwa kuwa maisha yake ni duni.
"Tunamshukuru Mungu tumezika mabaki ya mwanangu lakini hili tukio limetujeruhi sana maana hata sijui pakuanzia, mwanangu kaniachia watoto wanne wadogo na hata sijui nawaleaje maana sina uwezo hapa nilipo," amesema.
Mama huyo ameiomba serikali kupitia mamlaka zake kuitendea haki familia hiyo ikiwemo kumchukulia hatua za sheria aliyehusika na mauaji ya mwanaye.
Anna Juma, ambaye ni dada wa marehemu ameziomba mamlaka zinazohusika kumchukulia hatua kijana huyo kwa kukatisha uhai wa ndugu yake ili iwe ni fundisho kwa vijana wengine.
RAIS SAMIA ATEUA BOSI MPYA USALAMA WA TAIFA.
Rais Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa leo Agosti 28, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Massoro aliteuliwa kushika nafasi hiyo Januari 3 mwaka huu na kudumu kwenye ofisi hiyo nyeti kwa miezi nane kabla ya kuteuliwa kuwa balozi.
Kabla ya kupewa jukumu hilo Massoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Balozi Siwa ameapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam tayari kuitumikia nafasi hiyo nyeti na muhimu kwa Usalama wa Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Balozi Siwa alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) nafasi aliyohudumu tangu Septemba 20, 2018.
Kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda kwa takribani miaka mitatu kuanzia 2015 hadi 2018.
KUTANA NA MASHINE RAHISI YA KUFANYA USAFI NA KUVUTA UCHAFU, NYUMBANI NA KWENYE MAGARI - BEI POA SANA
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
JEMBE FM inakutana na Shimomo international Pte LTD ambao wao wamekuja na mashine ya kuvuta uchafu na vumbi kwenye carpet za majumbani, za kwenye magari na madirisha ni moja kati ya wadau wanaoshiriki Maonyesho haya ya 18 ya Biashara ya Afrika Mashariki (MEATF) yanayofanyika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kwa wiki moja kuanzia Agosti 25, 2023 hadi Sepetemba 3, 2023. Pamoja na wenyeji Tanzania, washiriki wengine ni kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).RAIS SAMIA AMEKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA POSTA AFRIKA IKULU DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Chief Moyo wakati alipofika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Chief Moyo wakati alipofika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Chief Moyo wakati alipofika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Chief Moyo mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Chief Moyo (kulia) na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti, 2023.