Saturday, May 8, 2010
SEMINA YA BIASHARA YAFANYIKA MWANZA LEO.
TANZANIA OYEEE!

KUPITIA MKUTANO MKUBWA WA DUNIA WA UCHUMI ULIOFANYIKA NA KUMALIZIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM HAKIKA TAIFA LETU LIMEFUNGUA UKURASA MPYA WA FURSA YA KIUCHUMI.
MKUTANO HUU WA 20 MAHUSUSI KWA BARA LA AFRIKA, ULIRATIBIWA NA JUKWAA LA UCHUMI DUNIANI LENYE MAKAO MAKUU HUKO GENEVA USWISI.
MKUTANO UMEFUNGUA MILANGO YA KIUCHUMI KWA TAIFA LETU, KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA SASA TUMEINGIAKTK RAMANI YA UCHUMI WA DUNIA KWA KUFANYIKA MKUTANO HUU HAPA NCHINI KWANI KWA KIPINDI KIREFU MIKUTANO MINGI IMEKUWA IKIFANYIKA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA NCHI HIYO KUWA NA MIUNDOMBINU BORA ZAIDI YA KUHUDUMIA WAGENI WENGI KWA PAMOJA, KIGEZO AMBACHO TANZANIA IMEKITIMIZA HATIMAYE IKAWA MWENYEJI WA MKUTANO HUO ULOMALIZIKA KWA UFANISI.
ZAIDI YA WAGENI 1000 KUTOKA NCHI 85 WAKIWAMO WAKUU WA NCHI 11 WAMESHIRIKI MKUTANO HUU, DHAHIRI HALI IKIONESHA KUWA KUTOKANA NA MKUTANO HUU MIKUTANO MINGINE YA KIMATAIFA ITAKUWA IKIFANYIKA HAPA NCHINI KWANI WAGENI WANASIFA YETU NA UZOEFU WETU KTK KUFANIKISHA MIKUTANO MIKUBWA KAMA HUU ULIOISHA.
LENGO LA MKUTANO PAMOJA NA KUJADILI NA KUBADILISHANA UZOEFU WA KUJENGA UCHUMI NA KUIMARISHA UHUSIANO WA KATI YA MATAIFA YENYE UCHUMI MKUBWA NA YALE YA AFRIKA MAARUFU KAMA SOUTH - SOUTH CO - OP - ERATION.
Friday, May 7, 2010
Thursday, May 6, 2010
KAUTARATIBU KAPYA.
UKIPIGWA BASI UMETAKA MWENYEWE!
BGML YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 50 KWA WAHANGA WA MAFURIKO.

PICHANI Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Meja mstaafu Bahati Matala, wa pili kutoka kulia mstari wa mbele akipeana mkono na Meneja Mahusiano na Serikali wa African Barrick Gold, Philbert Rweyemamu.
HABARI KAMILI:-Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetoa msaada wa shilingi milioni 50 kwa waathirika wa mafuriko wilayani Bukombe na pia kusaidia wilaya hiyo katika kuanzisha Mfuko wa Maafa.
Akikabidhi hudi ya fedha hizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Meja mstaafu Bahati Matala, Meneja Mahusiano na Serikali wa African Barrick Gold, Philbert Rweyemamu, amesema kampuni imeguswa na maafa hayo ya mafuriko katika wilaya ya Bukombe.
“African Barrick Gold haiko nchini kwa ajili ya kuchimba madini pekee, bali pia kuisaidia jamii katika shughuli za maendeleo na kubwa zaidi wakati wa matatizo pia,” alisema Rweyemamu.
Rweyemamu alisema ABG kama mwekezaji katika sekta ya madini nchini Tanzania, itaendelea kufanya kazi na serikali katika kuhakikisha kuna maendeleo endelevu katika jamii inayozunguka migodi yake na kutoa msaada wa aina yoyote kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya aliipongeza BGML kwa kuitikia haraka wito wa kutoa msaada na kuongeza kuwa fedha hizo zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Alifafanua kwamba, msaada huo utazilenga kaya 421 katika vijiji vya Lelembela na Kabanga kata ya Ikunguigazi ambazo nyumba zao zilibomolewa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zilizonyesha Aprili 2 2010.
Kadhalika mvua hizo pia zilisababisha vifo vya watu watatu na daraja lililopo kati ya Runzewe na Ushirombo katika barabara kuu iendayo Rwanda na Burundi kusombwa na maji, hali iliyosababisha barabara hiyo kufungwa kwa siku mbili.
Jumla ya hekari 4,700 za mazao pia ziliharibiwa na mvua hizo.
Msaada huo wa fedha utatumika kununulia mahitaji muhimu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na madawa, chakula, mahema na vitanda.
Wednesday, May 5, 2010
MWALONI LEO.
Tuesday, May 4, 2010
SAFARI HII WATU WATAKULA MCHELE.

KWEA PIPA 3 YAPATA WENGINE MWANZA .
HEPI BORZDAY DJ VENTURE!!
MLUME NDAGO LONG TIME KWENYE GAME, UMRI? MWALIMU WA FANI SASA. MWENYEZI MUNGU AKULINDE AZIDI KUWEKA MIKONO KATIKA KAZI YAKO, AKUONGEZEE HEKIMA NA UJUZI KADRI UNAVYO ISHI.... SAFI! HAPPY BORZDEY BROO.
Monday, May 3, 2010
Sunday, May 2, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)