ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 11, 2012

MEXICO YAIBANJUA BRAZIL

Timu ya kandanda ya Mexico imewashangaza mashabiki wa mchezo huo kwa kuichapa Brazil kwenye fainali ya Kombe la Olimpiki katika uwanja wa Wembley mjini London.
Oribe Peralta aliipatia Mexico bao la kwanza ikiwa ni sekunde 29 baada ya kipenga cha kuanza mchuano kupulizwa.

Peralta litumia fursa iliyotokana na kosa la beki wa Brazil kuchezea katika nusu ya uwanja kwa upande wa Brail na kuikandika Brazil bao la haraka lililozipeleka pande hizi hadi mapumziko kwa hesabu ya 1-0 kwa Mexico.

Bao la Peralta...
Hili ni bao la kwanza kufungwa haraka zaidi katika kipindi cha miaka 36 ya mashindano ya soka ya Olimpiki. Mshambuliaji huyo huyo alirudi kutikisa nyavu za Brazil mnamo dakika ya 75 kwa mpira wa kichwa.

 Brazil ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia mshambuliaji Givaldino Hulk zikisalia dakika kama tatu hivi kufikia mwisho wa mechi lakini Mexico ikashikilia mabao yake mawili hadi kipenga cha mwisho.

Machungu ya Neymar...
Kabla ya mechi hii, watangazaji wa idhaa ya kiswahili walitabiri ushindi wa Brazil, lakini Mexico ilikuwa na mipango tofauti na fikra za wengi.

Hivyo basi historia inabaki pale pale kwa Brazil kuondoka mashindano haya ya Olimpiki bila medali ya dhahabu ingawa itaondoka na fedha. Jumla ya watu 86,162 wameshuhudia pambano hili ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kuhudhuria mechi yoyote kwenye mashindano haya ya Olimpiki ya London 2012. Jumla ya watu milioni 2,186,930 wamehudhuria mashindano ya mpira ya wanawake na wanaume kwenye Olimpiki hizi.
Maandishi kwa hisani ya bbc Swahili.

NEW SONG MTOTO WA FISADI BY KINGKAPITA aka RICHBOI

 Sikiliza hapa.... AJE AJE MDAU NI YULE YULE MKALI WA HIPHOP ALIYETISHA KWENYE ILE NYIMBO YA MTOTO MLITO SASA KARUDI RICHBOI AKA KINGKAPITA NA SOLO PROJECT INAITWA MTOTO WA FISADI AMBAPO ANAONGELEA MAISHA YA JAMII YA TANZANIA UPANDE WA MTOTO WA FISADI NA UPANDE WA WATOTO WA MASKINI...NAOMBA SUPPORT YAKO POPOTE ULIPO ASANTE SANAAA

MWANZA HOTEL YAFUTURISHA

                                         Kilichozungumzwa Futarini.
Mkurugenzi wa New Mwanza Hotel Bw. Christopher Mwita Gachuma akihojiwa na mtangazaji wa Metro Fm mara baada ya kufuturu, pembeni akishuhudiwa na Mwakilishi wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza (RPC) Kamanda Rashidi na moja kati ya Wazee Maarufu jijini Mwanza.


Shekhe Mkuu wa Mkoa na Kadhi wa mkoa wa Mwanza Alhaji Fereji akitoa salamu kwa waislamu na wageni waalikwa baada ya futuru jana jioni ndani ya Mwanza Hotel.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya futuru iliyoandaliwa na Bw. Mwita Gachuma.


Baadhi ya waalikwa wakipata futari...


Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza (kushoto), katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Bi. Joyce Masunga, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS) Bi. Doroth Mwanyika, Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mwanza Bi. Sumari na Katibu msaidizi CCM Sekretarieti ya Maadili Mkoa baada ya kupata futari iliyoandaliwa na Gachuma katika ukumbi wa Makutano uliopo ndani ya Mwanza Hotel jana. 


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumzia kuhusu Sensa baada ya kumaliza kupata futari.


Mzee maarufu akiwa anafuatilia kwa makini salamu za Kadhi Mkuu na Shekhe wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Fereji.

TAFF YATOA TAMKO JUU YA MAHARAMIA WA FILAMU

Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo juu ya wizi mkubwa uliotokea hivi karibuni uliofanywa na Kampuni ya Steps Entatainmenti kwa kushirikiana na wasanii wwenyewe na kudai kuwa tabia hii ikomeshwa kwa maalamia wa kazi za wasanii kulia ni Msanii Vicent Kigos 'Ray' na Mwenyekiti wa Shilikisho la Filamu Tanzania 'TAFF' sIMON mWakifwamba. 


Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama katikati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam baada ya wasambazaji kuungana na wasanii kwa ajili ya kutoa tamko la kupambana na malamia wa kazi za sanaa kushoto ni msanii Muhsin Hawadhi na Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' . 

Msanii wa Filamu Nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto akizungumza na waandishi wa habari wakati walipokuwa wanatoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuwa wameungana kupambana na maalamia wa kazi zao za sanaa kushoto ni 
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na msanii Muhsin Hawadh.

Hizi ni moja kati ya kazi feki....
Picha na 
www.burudan.blogspot.com


SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.

Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.

“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao” 
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.

Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.
Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.

Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubalina kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo. 

Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwebnda kwa haki ili wasanii wapate na wao wawe ni watu wa kusaidi wasanii kusambaza kazi zao

Friday, August 10, 2012

PROF MAHALU KUWATAKA WAANDISHI WASOME ZABURI 17 NI UJUMBE KWA NANI?


Jana baada ya hukumu alipoulizwa maoni yake kuhusu hukumu ya mahakama dhidi ya mashtaka aliyokabiliwa nayo Prof. Costa Mahalu aliwaomba waandishi wasome zaburi 17.


Zaburi 17 inasema:  
1. Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.

2. Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili.

3. Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku, Umenihakikisha usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,

4. Mintarafu matendo ya wanadamu; Kwa neno la midomo yako Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.

5. Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa.

6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.

7. Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwa okoae wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kuume, Uwaokoe nao wanaowaondokea.

8. Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;

9. Wasinione wasio haki wanaonionea, Adui za roho yangu wanaonizunguka.

10. Wameukaza moyo wako, Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.

11. Sasa wametuzunguka hatua zetu, Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.

12. Kama mfano wa simba atakaye kurarua, Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake.

13. Ee Bwana, usimame, umkabili, umwinamishe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya.

14. Ee Bwana, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana,
huwaachia watoto wao akiba zao,

15. Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.

AIRTEL TANZANIA YAPELEKA NYOTA WAKE MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS AFRICA.

Afisa Habari wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jane Matinde(kulia)akizungumza na waadishi wa habari wakati wa kutangaza kikosi cha timu ya soka cha Airtel Rising Stars kitakachoshiriki michuano ya Inter-continental yatakayofanyika Nairobi, Kenya mwezi  huu. Amefuatana na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando(kulia)

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jackson Mmbando(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kikosi cha timu ya Airtel Rising Stars kinachokwenda kushiriki michuano ya Inter-continental itakayofanyika Nairobi, Kenya baadaye mwezi huu. KAtikati ni Afisa Habari wa kampuni hiyo Jane Matinde na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA).


Taarifa kwa Vyombo vya Habari 
Airtel yapeleka Kikosi cha wachezaji nyota wa Airtel Rising Stars Nairobi Timu ya Yoso bora 16 kuwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Airtel Rising Stars  Afrika, Airtel Tanzania kupitia mpango wake maalum wakuvumbua na kukuza vipaji vya soka nchini ujulikanao kama Airtel Rising Stars leo wametangaza kikosi cha wachezaji 16 watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel yatakayofanyika Nairobi kuanzia Agosti 19 hadi 25, 2012.

Wachezaji hao walichaguliwa na jopo la makocha kwa kushirikiana na shirikisho la mpira TFF na chama cha mpira cha Dar es Saalam DRFA wakati wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam mwezi Juni na kushirikisha timu kutoka mikoa ya Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Temeke na Kinondoni.


Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za TFF leo, Afisa Maendeleo wa mpira wa miguu nchini Salum Madadi aliwataja vijana watakaowakilisha Tanzania kuwa ni Denis Richard, Juma Hamza, Abdul Selemani, Ishaka Shekolowa na Bakari Ally kutoka mkoa wa kisoka wa Temeke.


Wengine ni Abdulatif Mohamed, George Joseph na Badilu Said (Lindi), Said Kassim, Amos Ikungula, Paul Balama na Goodluck Mabiku (Ilala), Joel Kasimula na Ibrahim Mtenga (Mbeya), Sntkony Angelo na Suleiman Yunus (Arusha).


Mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkali yatashirikisha wachezaji wengine nyota wa ARS kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, DRC, Congo Brazzaville, Nigeria, Ghana, Zambia, Niger, Gabon, Burkina Fasso, Sierra Leone, Chad, Madagascar na Tanzania.


Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kimataifa ni kuwapa vijana fursa zaidi ya kuendeleza vipaji vyao na kupata uzoefu. "Vile vile Airtel Rising Stars inatoa nafasi kwa wanasoka hawa chipukizi kuweza kupanua jiografia yao na kujenga urafiki na vijana wenzao kutoka nchi mbali mbali", alisema Singano.


Michuano hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo pia itafanyika Nairobi chini ya walimu wa soka la vijana kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United ya Uingereza. Kliniki kama hii ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa kisasa wa soka jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya, Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.


Katika kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji sita miongoni mwao ni wavulana watatu na wasichana watatu ambao walioibuka kuwa wachezaji bora wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam mwezi Juni.


Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wanaochipukia barani Afrika. Walengwa ni wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata fursa ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya waatalum wa mpira wa miguu wa kitaifa na kimataifa.

MWAUWASA SOON WATAKUWA HAPA PA KISASA ZAIDI

Ni mjengo mpya unaochipuka toka ardhini ukielekea juu unaotajwa kuwa utakuwa wa ghorofa nane, mjengo mali ya Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) na hapa panatajwa kuwa ndipo patakuwa Makao makuu ya mamlaka hizo ambapo ofisi zake zote zitahama kutoka eneo lake la awali karibu na mahakama ya mwanzo wilaya ya Nyamagana. 

Wadau...

Kwa nyuma ...Mjengo huu ukikamilika itakuwa ni heshima kubwa kwa Mamlaka hiyo inayofanya katika majengo ya ofisi zilizo choka kwa kitambo sasa, huku ikiwa na rasilimali  watu na vyanzo vya kutosha kwa upatikanaji maji tofauti na  halmashauri nyingi hapa nchini.

Thursday, August 9, 2012

“JIANDAE KUHESABIWA 26 Agosti 2012”


Bofya hapa juu kumsikiliza Afisa Mkuu Uhamasishaji Sensa Sensa Makao makuu Bw. Said J. K. Ameir  kupitia mahojiano aliyofanya na blogu hii mara baada ya mafunzo kumalizika hivi karibuni jijini Mwanza.

Historia ya Sensa Tanzania.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603.

Kwa habari zaidi tembelea:-
http://www.nbs.go.tz/sensa2012/

"HUJAFA HUJAUMBIKA"“Hujafa…hujaumbika”
Na Devota Mwachang’a
Beatrice Shimende Kantimbo (48) anaomba msaada wa pesa kwa ajiri ya matibabu ya maradhi ambayo vipimo vya kitabibu vimegundua kuwa ni matende (elephantiasis), ili kufanikisha safari yake kwenda India kwa matibabu.

Kantimbo anasumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, kwahivi sasa yamemtoa kwenye mstari wa maisha yake ya kujitegemea na kumfanya awe tegemezi kwa watoto wake na mumewe ambao hata hivyo kipato chao si cha uhakika.

Kabla ya hapo alikuwa ni mama 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa ikiwemo biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele ambapo yeye mwenywe ni msusi mzuri wa nywele na kwa ucheshi wake na kujiamini pia alikuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC) kwenye sherehe kadhaa akifahamika kama MC Kimbaumbau.

Ila kwa sasa, tofauti na hapo awali alipoitwa MC na mama mchakariji, Kantimbo hawezi kufanya lolote amebakia ni mama wa kukaa mahali pamoja tu kuanzia asubuhi hadi jioni.

Kwa uchungu anasimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.

"Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na malaria.

"Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali. Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba. Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"


Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka  kuvimba na maumivu makali yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza. Anasema:

"Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligunduliwa tatizo kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.

"Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.

Kwa mawasiliano namna ya kumsaidia piga simu namba 0716 850350, 0784 861031.

POLISI MORO 2 FALCON ZNZ 0 DIMBA LA KIRUMBA

Mgeni rasmi Inspector Rashidi kutoka ofisi ya RPC Mwanza akiikagua timu ya Polisi Morogoro katika mchezo baina yake na Falcon Zanzibar, hadi mwisho Polisi iliibuka na ushindi wa bao 2-0.

Akiwa ameambatana na mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mwanza, Jacson Songoro (kushoto) mgeni rasmi Inspector Rashidi kutoka ofisi ya RPC Mwanza akiikagua timu ya Falcon katika mchezo wa ligi Super 8 baina yake na Polisi Morogoro, uliochezwa leo katika dimba la CCM Kirumba, hadi mwisho Polisi iliibuka na ushindi wa bao 2-0.

Polisi Morogoro.

Falcon Zanzibar.

Ni ligi ya Super 8 kituo cha Mwanza inayodhaminiwa na Benki ya ABC.

BREAKING NEWS: KIJANA MMOJA AUAWA KUIBA KUIBA KOKI YA BOMBA LA MAJI. TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI.

Ni ukatili gani huu...?Mwili wa marehemu.Wananchi wa maeneo hayo wakiangali huku wakijiuliza maswali ya kwanini matukio ya kujichukulia sheria mikononi bado wanaendekezwa na Wananchi.


Koki aliyokutwa nayo marehemu Hassan Stanley.


Mwandishi wa habari Fabian Fanuel kutoka FPLUSS BLOG  akiwa na Mwandishi wa habari wa Kwaneema Fm Joshua Dede wakimhoji mwenyekiti wa mtaa wa Chanmwenda bi. Lucy Kapombe.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiloleli bwana Joshua Josia Mnana akiwatoa maelezo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kifo cha Hassan Stanley.Kaka yake Marehemu Hassan akimfunika kanga mdogo wake baada ya kukutwa na tukio la kuuawa kwake..


Mwili wa marehemu Hassan Stanley akiwa amefunikwa kanga na kaka yake.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Stanley asubuhi ya kuamkia leo majira ya saa kumi na moja  katika maeneo ya uwanja wa mbuzi Kiloleli jijini Mwanza, ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na kuchomwa moto hadi kupelekea mauti yake.

 Mwenyekiti wa mtaa wa maeneo tukio lilipotokea Bi Lucy Kapombe amesema kuwa haya ni matokeo na hasira walizokuwa nazo wananchi ambao wamekuwa wakilalamikia matukio ya wizi wa koki za maji maeneo mbalimbali katika jiji la Mwanza.

Amesema yeye binafsi hauingi mkono mwizi yeyote kuuawa bali wananchi wanatakiwa kuiacha sheria ifuate mkondo wake katika watuhumiwa wanaokuwa wamekamatwa kutokana na matukio mbalimbali ya uhalifu katika jamii yetu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kiloleli b bwana Joshua Josia Mnana ameto wito kwa vijana wanohusika katika uhalifu mbalimbali kuacha ili wasije wakapatwa na matukio kwa hayo yaliyompata mwenzao.

Marehemu Hassan Stanley aliye na umri wa kati ya miaka 22 hadi 26 alikuwa mpiga debe katika kituo cha Kiloleli na ni kazi ambayo amekuwa akiifanya mpaka anakutwa na umauti.

Eti jamani koki tu! inanunua uhai wa mwanadamu? 
Blogu hii inalaani sana sana na kupinga matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

CHANZO:-  fpluss.blogspot.com

WAKATI PAMBA QUEENS WAKITAWAZWA KUWA MABINGWA NETIBOLI NYAMAGANA, MTEKATEKA KUZIWEZESHA TIMU SITA ZILIZOINGIA ROBO FAINALI

Licha ya kuahidi kuyaboresha zaidi mashindano hayo mwakani kwa vifaa bora vya kimichezo na nyenzo mbalimbali, Mhasibu mkuu wa jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Noel Mtekateka jana kupitia fainali za mpira wa pete (Netiboli) kwa wilaya ya Nyamagana ameahidi kuwa ataziwezesha timu zote sita zilizo ingia hatua ya robo fainali kwa kuzipatia shilingi laki moja moja kwa kila timu kama sehemu ya zawadi ili kuwapa changamoto washiriki kuwa na mapenzi kwa mchezo huo. 

Ligi ya Polisi Jamii wilaya ya Nyamagana iliyobuniwa na Jeshi la Polisi Nyamagana kupitia polisi jamii na kubatizwa jina la Nyamagana Cup imehusisha mpira wa miguu na mpira wa pete na kushindanisha timu 12 kutoka kata zote za wilaya hiyo, ambapo katika siku ya jana Timu ya Isamilo Queens imenyakuwa ubingwa kwa kuitandika Mkolani Queen.

Mgeni rasmi  Noel Mtekateka akikagua kikosi cha washindi wa pili mpira wa pete kwenye mashindano ya Nyamagana Cup, Mkolani Queens.

Washindi wa pili Nyamagana Cup iliyomalizika jana Mkolani Queen katika picha ya pamoja.

Pamba Queen mabingwa wa Netiboli (mpira wa pete) wakiwa katika picha ya pamoja.

Meza ya kutunza kumbukumbu za michezo ikiwajibika wakati wa fainali hizo zilizofanyika jana viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza. Lengo la mashindano hayo ni kupunguza vitendo vya uhalifu, kuwaondosha vijana vijiweni na mitaani na kuwaweka vijana pamoja kubadilishana mawazo na kujifunza mambo ya msingi ili kupunguza vitendo vya uhalifu.

Mchezo wa fainali ukiendelea baina ya Mkolani Queens na Pamba Queens ambapo mwisho wa siku Pamba Queens iliibuka kuwa Machampioni wa netiboli Nyamagana.

Kwa mara ya kwanza mashindano hayo yamevunja rekodi kwa kutokuwa na mchezaji yoyote aliyezawadiwa kadi nyekundu hadi yakifikia tamati hii ikimaanisha kuwa suala la nidhamu limezingatiwa kwa hali ya juu na washiriki wa mchezo huo. Mpango mzima Washindi watakabidhiwa zawadi zao mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Line Polisi Mabatini. Tuwe sote..

Wednesday, August 8, 2012

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTION YAKAMATA MITAMBO NA KAZI FEKI ZA WASANII MJINI DODOMA

Mkurungezi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ,Bwa.Alex Msama pichani akifafanua jambo kwa Wanahabari (hawapo pichani), kuhusiana na tukio zima la kama kamata ya wezi wa kazi za wasanii iliofanyika mjini Dodoma.
Mkurungezi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ,Bwa.Alex Msama pichani mwenye fulana ya mistari akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) Cd za video na Audio Cd za Muziki wa aina mbalimbali pamoja na Kompyuta za kudurufu kazi za wasanii kwa njia ya wizi kwenye  kituo kikuu cha Polisi mkoani Dodoma,mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaka na kuwakamata wezi  wa kazi za wasanii,ambapo jumla ya Cd na Computer zenye thamani ya shilingi milioni Sitini na saba zilikamatwa kwa msaada wa Jeshi la Polisi mkoani humo. (PICHA ZOTE NA DIRA MEDIA).