Friday, August 22, 2025
Thursday, August 21, 2025
"MUSTAKABALI WA TAIFA LETU HUPIMWA KUPITIA CHAGUZI TUNAZOFANYA" DC MAKILAGI
“𝙈𝙪𝙨𝙩𝙖𝙠𝙖𝙗𝙖𝙡𝙞 𝙬𝙖 𝙏𝙖𝙞𝙛𝙖 𝙡𝙚𝙩𝙪 𝙝𝙪𝙥𝙞𝙢𝙬𝙖 𝙠𝙪𝙥𝙞𝙩𝙞𝙖 𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙯𝙞 𝙩𝙪𝙣𝙖𝙯𝙤𝙛𝙖𝙣𝙮𝙖.”.
Nikiwa kama kiongozi mwanamke, nachukua nafasi hii kuhamasisha wanawake wote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.
Tunapozungumzia mustakabali wa Tanzania, tunazungumzia uongozi bora—uongozi unaojali usawa wa kijinsia na unaomgusa mwanamke katika kila nyanja ya maisha.
Ni wajibu wa kila mwanamke kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi. Tuna mfano hai na wa kuigwa, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kupitia nafasi yake ameonesha kuwa mwanamke anaweza, ana haki na ana mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
Jitokeze. Shiriki. Chagua kwa uelewa. Tanzania ni yetu sote. — Mhe. Amina Makilagi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Kupitia kipindi cha Kazi na Ngoma
.
.
#KaziNaNgoma
@jembefmtz
SASA RASMI, SERIKALI YAONGEZA UMILIKI MRADI WA DHAHABU NYANZAGA.
Mwanza. Serikali ya Tanzania, kupita Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), na Kampuni ya Perseus Mining Limited, zimesaini rasmi mkataba wa nyongeza wa umiliki wa hisa katika Mradi wa Dhahabu wa Nyanzaga, hatua inayochukuliwa kuwa ni kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
Mkataba huo uliosainiwa Agosti 20,2025 katika hafla iliyofanyika katika Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, unaongeza umiliki wa Serikali, kupitia OMH, kutoka asilimia 16 hadi 20 katika Kampuni ya Ubia ya Sotta Mining Corporation Limited, ambayo inasimamia utekelezaji wa mradi mkubwa wa dhahabu unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Perseus na Serikali.
Mkataba huo ulisainiwa na Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, kwa upande wa Tanzania, na Mkurugenzi wa Kampuni ya Perseus, Bi. Lee-Anne de Bruin, mbele ya Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde.
Bw. Mchechu alisema kuwa nyongeza ya hisa inaashiria dhamira ya Serikali ya kuhakikisha sekta ya madini inawanufaisha Watanzania kwa njia endelevu na ya uwajibikaji.
Bw. Mchechu pia alieleza kuwa usainiaji wa mkataba huo umetokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya Serikali na wawekezaji, na kwamba Serikali itaendelea kutengeneza mazingira rafiki ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi huo unafanikishwa kwa mafanikio makubwa.
Kwa upande wake Mhe. Waziri wa Madini, aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alieleza kuwa mkataba huo ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa Serikali na Kampuni binafsi katika sekta ya madini.
Aidha, alisema kuwa mradi huo utaongeza ajira, mapato ya Serikali, na huduma za kijamii kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema na taifa kwa ujumla.
"Utekelezaji wa Mradi wa Dhahabu wa Nyanzaga utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Leo tunahakikishia Watanzania kuwa mradi huu utaendeshwa kwa manufaa yao," alisema Waziri Mavunde.
Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa zaidi ya Sh1 trilioni zinatarajiwa kuwekezwa kwenye mradi huo, na kwamba Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wake kwa karibu kuhakikisha wananchi wanapata fursa za ajira, ushiriki wa wananchi kupitia huduma na bidhaa, na mapato makubwa kupitia kodi na gawio la hisa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Perseus, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha mazungumzo na kusaini mkataba huo wa nyongeza unaowezesha kuanza uzalishaji mwanzoni mwa mwaka 2027.
"Tunamshukuru Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kuendeleza mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyochangia mafanikio haya," alisema Bi. Lee-Anne.
RMO MWANZA ATAKA UBUNIFU KUFIKISHA ELIMU YA MALEZI, MAKUZI KWA JAMII
![]()
Ametoa wito huo Agosti 19, 2025 wakati akifungua mkutano wa maandalizi ya kikao cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kitakachofanyika mapema mwezi Septemba 2025 chini ya uongozi wa Katibu Tawala wa Mkoa.
Amewataka wadau hao kuhakikisha wanatumia fursa ya ratiba ya wizara ya mwezi huo wa uelimishaji unaoambatana na wiki ya ustawi wa jamii kwenda kutoa elimu kwenye jamii kwa kutumia mbinu mbalimbali kama redioni na mikusanyiko vijijini kuhusiana na malezi na ukatili wa kijinsia kabla ya kuchukua sheria kwa wakaidi.
Amesema serikali imeweka afua tano kuhakikisha makuzi, malezi na maendeleo ya mtoto yanakua na ustawi na kwamba programu mbalimbali zinazosawili afua hizo yanapaswa kuzingatiwa kwa gharama yoyote ili mwisho wa siku jamii iwe salama.
Vilevile, ametumia wasaa huo kuwashukuru wadau wote pamoja na kumpongeza Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa pamoja na wasaidizi wake kwa uchapakazi kwani Mwanza imepiga hatua kubwa katika kuelimisha na kupunguza matendo ya ukatili kutokana na juhudi zao za kuhakikisha elimu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto inawafikia wananchi.
Akitoa salamu za Wizara ya maendeleo ya Jamii Idara ya Mtoto bi. Mery Shila amesema wizara hiyo kwa kushirikiana na mikoa wanahakikisha mtoto kuanzia mwaka mmoja hadi minane analindwa na jamii nzima na ndio maana wanasukuma afua mbalimbali za malezi.
Aidha, amebainisha kuwa viongozi wa dini kote nchini wamekua kiungo kikubwa kwenye malezi ya watoto kwa kutoa malenzi na mafundisho ya kiroho katika kuhakikisha wanakua na tabia njema ili ikiwezekana madawati ya jinsia yakose mashauri ya ukatili.DKT. TULIA AKOSHWA NA CRDB BANK MARATHON IKIKUSANYA BILIONI 2 KUSAIDIA AFYA NA UWEZESHAJI JAMII

Dar es Salaam, 17 Agosti 2025 - Maelfu ya wakimbiaji na wapenda michezo kutoka ndani na nje ya Tanzania wamejitokeza leo katika viwanja vya The Green, Oysterbay, kushiriki CRDB Bank Marathon 2025, mbio za hisani ambazo mwaka huu zimekusanya Shilingi Bilioni 2 ili kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo, wakinamama wenye ujauzito hatarishi, na vijana kupitia programu ya iMBEJU.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, aliongoza maelfu ya washiriki kwenye msimu huu wa sita wa CRDB Bank Marathon.
Akitoa salamu zake, Dkt. Tulia alipongeza ubunifu wa CRDB Bank Foundation katika kuunganisha jamii kupitia michezo na kusaidia wenye uhitaji, akieleza kuwa mbio hizo ni mfano wa vitendo vya huruma vinavyogusa maisha ya wengi. “Ushiriki wetu katika CRDB Bank Marathon ni tendo la huruma linaloleta faraja kwa watoto na wakinamama na familia zao. Ni ushahidi kwamba tukishirikiana, tunaweza kubadilisha maisha,” alisema.
Akitoa salamu zake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, aliipongeza Benki ya CRDB na CRDB Bank Foundation kuendelea kuandaa mbio hizo. Alisema, “CRDB Bank Marathon si tu imekuwa ikikuza afya na mshikamano wa kijamii, bali pia imekuwa ikifungua milango ya ajira na fursa za kiuchumi kwa vijana wetu. Michezo ni sekta inayoweza kubadili maisha, na ninapongeza sana kitendo cha kuweka zawadi nono kwa washindi. Hizi ni fursa ambazo zinaweza kuwa mtaji wa kuanzisha biashara na kuimarisha maisha ya vijana wetu. Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kama CRDB Bank Foundation kuhakikisha michezo inakuwa chachu ya maendeleo ya taifa.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alibainisha kuwa msimu wa sita wa CRDB Bank Marathon umefanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Benki ya CRDB, na kuendelea kupanua wigo wa matokeo yake ndani na nje ya Tanzania. Kwa mara ya pili, mbio hizi zimefanyika pia nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), zikikusanya fedha kwa ajili ya miradi ya afya na ustawi wa jamii katika nchi hizo. Nsekela alisema kuwa mbio za mwaka huu zimeweza kuvutia zaidi ya washiriki 16,000, na kufanikisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 2 ambapo pamoja na kusaidia maandalizi ya mbio hizo, shilingi milioni 450, zimeelekezwa kusaidia wenye uhitaji katika jamii.
Kati ya hizo shilingi milioni 100 zimekwenda hospitali ya CCBRT kusaidia wakinama wenye ujauzito hatarishi kujifungua salama, shilingi milioni 100 zimekwenda Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kusaidia upasuaji wa Watoto wenye matatizo ya moyo, na shilingi 250 zitaelekezwa katika uwezeshaji wa vijana.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya mbio hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa, alieleza kuwa safari ya msimu wa sita imeanzia Lubumbashi, DRC, ambako zilikusanywa Dola za Marekani 70,000 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika hospitali ya Jeshi la Ruashi, na kuendelea Bujumbura, Burundi, ambapo zilipatikana Faranga za Burundi milioni 175 kusaidia bima ya afya kwa zaidi ya watu 58,000 wasiojiweza. Mwambapa alisisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya mshikamano wa kipekee wa serikali za nchi shiriki, wadhamini na washiriki, akiwashukuru wadau wote waliotoa jitokeza kuchangia ikiwamo kampuni za bima za Sanlam Life na Alliance Life ambao wamekuwa sehemu ya mbio hizi tangu kuanzishwa kwake.

Washindi wa mbio za mwaka huu upande wa Tanzania kwa Kilometa 42 upande wa wanawake ni Joyloyce Kemuma kutoka Kenya, upande wa wanaume mshindi ni Abraham Kiptum kutoka Kenya. Kilometa 21 upande wa wanawake ni Catherine Syokau kutoka Kenya, na upande wa wanaume ni Joseph Panga kutoka Tanzania. Kilometa 10 upande wa wanawake ni Silia Ginoka kutoka Tanzania, na upande wa wanaume ni Boayi Maganga kutoka Tanzania.
Joseph Panga mshindi wa mbio za Kilometa 21 upande wa wanawake ameeleza furaha yake kushiriki katika mbio hizo na kusema kuwa ushindi wake ni sehemu ya kusaida matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo na matibabu ya wakinamama wenye ujauzito hatarishi hospitali ya CCBRT.
“Mimi kama Mtanzania najisikia fahari kubwa kushiriki kusambaza tabasamu kwa watoto na wakinamama. Ni muhimu watu kufahamu kuwa afya bora ni haki ya kila mtoto, na hakuna mama anayestahili kupoteza maisha wakati wa kujifungua. Tunawashukuru CRDB Bank Foundation kwa kutuleta pamoja katika harakati hizi za kuokoa maisha,” amesema.
CRDB Bank Marathon imekuwa jukwaa muhimu la kuchochea ustawi wa kijamii katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na kati hivi karibuni ikipata heshima ya kutambuliwa kimataifa kwa kushinda tuzo ya jukwaa bora la taasisi za fedha katika kusaidia kusaidia jamii.
Sunday, August 17, 2025
TAASISI YA BAOBAB KUCHELE YAFANYA BONANZA BABU KUBWA LA KUKUZA VIPAJI KWA SHULE 12 ZA SEKONDARI
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala zima la kuboresha sekta ya michezo uongozi wa shule ya sekondari Baobab pamoja na chuo cha afya cha Bihas vilivyopo Kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo imeamua kufanya bonanza kubwa la michezo ambalo limeshirkisha jumla ya shule 12 za sekondari lengo ikiwa ni kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi wa kike na wakiume.
Bonanza hilo ambalo limehudhuliwa na viongozi wa serikaali, walimu kutoka shule mbali mbali, wadau wa michezo pamoja na wanafunzi kutoka maeneo mengine ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo washindi katika mchezo wa soka wameweza kuzawadia zawadi mbali mbali ikiwemo kupatiwa vikombe pamoja na medali ikiwa pamoja na wale wanafunzi wa kidato cha sita ambao wamefanya vizuri katika taaluma.
Amebainisha kwamba katika bonanza hilo ameweza kubaini kuwepo kwa vipaji mbali mbali kutoka kwa wanafunzi wa kike na wakiume katika mchezo wa soka sambaambaa na vipaji na uwezo mkubwa katika mashindano ya kitaaluma ambayo yameweza kuonyeshwa na wanafunzi mbali mbali.
"Napenda kutoa pongezi kubwa kwa uongozi mzim wa taasisi ya Baobab ambaapo leo tumeweza kushuhudia bonanza ili kubwa ambalo limeambatanaa na michezo mbali mbali pamoja na uzinduzi wa chuo cha afya naa sisi kama serikali tutaaendeleaa kushirikiaanaa beg kwa bega kwa lengo la kuwez kuleta maatokeo chaanyaa katika sualaa laa kukuza taalumu pamoja naa kukuza vipaaji kwa wanafunzi,"amebainisha Suleman.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya Baobab Shani Swai amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuendelea kukuza michezo na kwamba watajitahidi sana kuhakikisha wanajenga mazingira rafiki kwa lengo kuwawezesha wanafunzi waweze kucheza viwanjaa vyenye ubora ambao unatakiwa.
Naye Mkuu wa chuo cha afya cha Baobab Nelsen Rahul amebainisha kwamba dhumuni la bonanza hilo ni kuendelea kuwashirikisha watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi pamoja na watoto wenye ulemavu kwani michezo na kwamba mikakati yao ni kuendeleza kufanya mabonanza zaidi kwa lengo la kukuza vipaji na kuimarisha afya.
Katika bonanza hilo ambalo limeweza kugonga nyoyo za wanafunzi timu ya shule ya sekondari Shushila wameweza kubuka na mabingwa wa jumla baada ya kuwachapa wapinzani wao wenyeji wa shule ya Sekondari Baobao kwa bao 1-0 katika mchezo mkaali uliokuwa wa vuta ni kuvute kutokana ana wachezaji wote kuonyesha vipaji vya hali ya juu.
Baadhi ya shule za sekondari ambazo zimeweza kupata fursa ya kipekee katikaa kushiriki katika Bonanza hilo ni pamojaa na wenyeji shule y Sekondari Baobab,Dunda Sekondari, Mapinga, Dunda, Nia njema,Kerege, Kingani, Fukayosi.
.jpg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)






.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)