A 72nd minute Davis Mwape goal was enough to earn Young Africans a 1-0 win over their traditional rival Simba in a Mainland Premier League match at the National Stadium in Dar es Salaam today.
The Zambian striker used weaknesses in central defender Juma Nyoso to beat Juma Kaseja in the game which was clouded by nail biting tension.
Saturday, October 29, 2011
HABARI
Wendesha mashtaka wa kimataifa wamekuwa na "mawasiliano yasiyo rasmi" na mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi. Mahakama ya uhalifu ya Kimataifa (ICC) imesema watu wa kati wametumika katika mazungumzo hayo yasiyo rasmi na Saif al-Islam.
Waendesha mashtaka wamesema mahakama imeweka wazi kwa mtoto huyo wa Gaddafi, kuwa anatakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, na kuwa hana hatia hadi itakapo thibitishwa mahakamani.
Washirika
Saif al-Islam, ambaye alidhaniwa kuwa huenda angerithi utawala wa baba yake, amekuwa akijificha kwa miezi kadhaa.
Taarifa za hivi karibuni zinadai kuwa alikuwa kwenye msafara unaoelekea kwenye Jangwa la Libya karibu na mpaka na Niger, nchi ambayo washirika wengine wa Gaddafi wamekimbilia.
Lakini taarifa hizo hazijathibitishwa, na ICC imesema haifahamu yuko wapi.
Ofisi ya mwendesha mashtaka imeweka wazi kuwa iwapo atajisalimisha kwa ICC, atakuwa na haki ya kesi yake kusikilizwa mahakamani, na hana hatia hadi itakapothibitishwa.
Chanzo: bbc swahili
Friday, October 28, 2011
BANGO
"Blogu hii inakutakia kila la kheri katika siku yako hii, iwe njema yakukumbukwa daima"
Jembe ikibidi ufike hapa....tehe-te!
HAPPY BIRTHDAY.
WOCHIT''''''!!!!!
Video by Leshontee' Shuku and Supeb' Ngahyoma
Thursday, October 27, 2011
SIASA
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema hana ndoto ya kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015.Kauli hiyo ya kwanza ya Sitta ambaye pia ni kada wa CCM, imekuja wakati ambao kuna mpasuko mkubwa ndani ya chama chake hicho ambao unahusishwa na mbio za urais wa 2015, huku yeye akitajwa kuwa mmoja wa wenye nia ya kushiriki mbio hizo.
Kauli yake imeingia katika orodha ya kauli za makada wengine kadhaa ambazo zimetikisa siasa za CCM huku nyingi zikiwa na sura ya mvutano tena zikitolea nje ya vikao rasmi vya chama hicho tawala nchini.
Hata hivyo, juzi usiku akijibu swali kama ana ndoto ya kuwania urais au la, Sitta alisema: "Hapana! Sina ndoto ya kuwania urais kwa sasa, wapo vijana watajitokeza, wapo wazuri, tutawaunga mkono tu".
Sitta alifafanua kwamba matumaini yake mwaka 2015 watakuwapo wagombea wenye uwezo wakiwemo vijana, na kuongeza, "wale wazalendo wenye maadili wataungwa mkono".
Ingawa, Sitta amesema hana ndoto ya kuwania urais kwa sasa, lakini amekuwa akitajwa kama mmoja wa watu wanaoutaka baada ya Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015, kutokana na nguvu zake kubwa alizojijengea kwa umma.
Sitta aliweza kujipatia umaarufu mkubwa kisiasa baada ya kuongoza kwa mafanikio Bunge la Tisa ambalo alikuwa na kauli mbiu yake ya Bunge la Kasi na Viwango.
Kuhusu chuki ya watu aliowaita mafisadi, Sitta alisema watuhumiwa hao walifanya mbinu mbalimbali kuhakikisha hafanikiwa katika malengo ya kurejea kwenye uspika wa Bunge la Kumi kwani waliendesha hujumu nzito dhidi yake.
Sitta aliwatuhumu watu hao akisema: "Mafisadi hawanitaki, wananichukia wako tayari hata kuniua".
CHANZO: Mwananchi
Thursday, October 27, 2011
BANGO
Wapenzi wadau na wasomaji wa napenda kuwafahamisha kuwa Geofrey Mwakibete wa MO BLOG ambaye amebahatika kuchaguliwa kuwa miongoni mwa washiriki wa shindano la SWAHILI FASHION WEEK AWARDS katika kundi la Wapiga picha bora wa Mitindo.
Bila nyinyi asingefanikiwa kupata nafasi hii hivyo tunaomba tuendelee kumpa sapoti na hamasa kwa kumpigia kura GEOFREY MWAKIBETE kupitia mtandao
http://www.swahilifashionweekawards.blogspot.com
Asanteni kwa Ushirikiano wenu.
Thursday, October 27, 2011
ELIMU
From one of Irina secondary School, English teacher: "The girl goes to school, goesn't she?
From Brits, somewhere in one of Mbeya School teacher: ” Both of you three come here!"
An irritated Songea School teacher to a student: "Tomorrow I want you to come with your father, your mother and both your parents!"
On seeing twins enter his office, the deputy principal at a certain school (Serious Senior Secondary School) at Makuyuni said: " You look together; are you twice"
Notice at a store in Sinza: "Open seven days a week and weekends"
Bwana majimarefu admonishing two boys who were arguing: "Don't speak so twice together, man, Speak once upon a time!"
Stay well Blessed!!!
Thursday, October 27, 2011
BANGO
KWANZA KABISA Tunapenda kuchukuwa nafasi Hii kuwasalimu watu wote Wakubwa Shikamoo na wadogo Mambo vipi, Umoja wa Matukio na wanavyuo Tanzania (http://www.tzwanavyuo.blogspot.com/) inayo furaha kuwaletea habari njema wale wanafunzi wote ambao walikosa nafasi za kujiunga na vyuo katika mchakato mzima wa awamu ya kwanza na awamu ya pili.
Lakini sasa baadhi ya vyuo vikuu vikiwemo Teofilo Kisanji University, Stefano Moshi Memorial University College,St. Augustine University of Tanzania, Ruaha University, National Institute of Transport, Iringa University College, Institute of Finance Management, Eskerforde Tanga University, University of Dodoma na Ardhi University vimetangaza baadhi ya nafasi hizo.
Nafasi zimeelezewa vema na pia mwaweza tazama wapi unataka kujiunga. Fungua sasa na ufuate maelekezo na kutuma maombi yako bila kuchelewa Tunawatakia mafanikio mema wale wote ambao wataenda kujiunga.
Mwisho tunapenda kuwakumbusha kwamba ule mtandao wenu wa wanavyuo Bado unakungoja wewe ambae haujajiunga na SOCIAL NETWORK YENU jiunge sasa na kama mna matukio mbali mbali ya vyuoni kwa wanavyuo wote watanzania waliopo nje na Ndani ya Tanzania na Watumishi wa vyuo kama mna matangazo ama matukio mnataka kuyaposti pia tutumieni kupitia twanavyuo@live.com
Kutazama nafasi mpya za masomo bofya hapa: http://www.tzwanavyuo.blogspot.com/
Kwa niaba ya Wenzetu ni sisi,
Matukio na wanavyuo Crew
Wednesday, October 26, 2011
HABARI
Tuesday, October 25, 2011
HABARI
Watu kadhaa wamefariki dunia katika ajali mbaya ya basi la abiria iliyotokea kibaha mkoani pwani kamanda wa polisi wa mkoa huo ERNEST MANGU amesema kwamba idadi ya vifo kwa ajali hiyo iliyo husisha gari la Deluxe lililokuwa likitokea jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Dodoma liliungua na kuteketea kabisa kwa moto.
Habari ambazo hazijathibitishwa inasema kuwa idadi ya waliokufa inaweza kuwa zaidi ya watu ishirini.
Imeelezwa kwamba idadi ya abiria walioondoka na basi hilo kutoka katika kituo kikuu cha mabasi ya mikoani Ubungo jijini Dar es salaam walikuwa arobaini na mbili lakini basi hilo linauwezo wakubeba abiria sitini na tano.
Hata hivyo msemaji wa hospitali ya Tumbi mkoani Kibaha Rose Mtei amesema kuwa mpaka jioni hii wamepokea majeruhi thelethini na tano wa ajali hiyo ambapo kumi na tatu wameruhusiwa, wengine wakiendelea kupatiwa matibabu zaidi.
Fredrick Katulanda mchana wa leo katualika lunch na hii ndiyo menyu husika.
Tuesday, October 25, 2011
BANGO
SALAM,
Napenda kutoa shukurani zangu za pekee kwa Mwenyezi Mungu, Familia yangu, Marafiki zangu, mashabiki wangu, wadau na watanzania wote kwa ujumla walioweza kunipigia kura ambazo zimefanikisha blog ya MissJestinaGeorge kuibuka kidedea na kunyakua ushindi mkubwa wa kuwa ''BLOG BORA YA MWAKA 2011'' katika tuzo za BEFFTA zilizofanyika nchini UK mapema wiki iliyopita.
Mchakato mzima wa kumtafuta mshindi ulikuwa na changamoto lukuki ukizingatia ya kwamba kulikuwa na jumla ya blogs 15 za kimataifa kutoka nchi mbali mbali Duniani. Kutokana na ushirikiano wenu mzuri mmeiwezesha blogu yetu kupata ushindi mnono na vile vile kunipatia fursa nzuri ya kuiwakilisha vyema Tanzania Ughaibuni.
Ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja kwa mchango wenu uliosadia kuwezesha blog yetu kunyakua ushindi mkubwa ingawa ningependa kuwatambua wafuatao: kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu zote za dhati kwa timu ya URBAN PULSE CREATIVE kwa mchango wao mkubwa waliotoa, wanachama wenzangu wa AMTTA (Amka Mwanamke Twende Tujikomboe Afrika) kwa kuwa na mimi bega kwa bega nawapenda sana. Pia natoa shukrani kwa Bloggers wenzangu wote, tovuti mbalimbali, TONE RADIO popote pale walipo kwa michango yenu.
Nawasihi sana tuendelee kushikamana, kupendana na Kusaidiana kwa hali na mali ili isiwe tu kuleta maendeleo nchini kwetu bali pia kupeperusha bendera ya nchi yetu Tanzania Duniani kote.
Napenda kuitoa wakfu tuzo hii kwa dada yangu mpendwa Kissa George aliyetutoka ''I miss you so much Sis'' najua kama angekuwa hai angefurahia sana.
Mwisho namshukuru sana binti yangu Iman ambae amekuwa nguzo na muhumili mkubwa katika maisha yangu kwa kunipatia nguvu za kuendelea mbele siku hadi siku.
Binadamu kushukuru ni wito ila leo umekuwa ni wajibu wangu.
Asanteni sana,
Mungu awabariki sana na ninawapenda sana
Jestina George
Monday, October 24, 2011
SIASA
CHUNGULIA KIDEO:Ni sehemu ya majibu kupitia maswali aliyoulizwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Mnauye wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika ziara yake aliyoifanya hivi majuzi jijini Mwanza.
“Ni suala la maadili na ujumla wake, maadili yanapimwa na nini? Maadili yanapimwa na imani ya Chama Cha mapinduzi, ukiapa kule nyuma unasema ‘Rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa, Cheo ni dhamana sito tumia cheo changu wala cha mwingine..’ Kwa hiyo siyo suala la Nape wala la nani, hili ni suala la Chama, Nape atakufa yatabaki haya"
"Yamekuwepo mimi sijazaliwa, nimezaliwa nimeyakuta, nitayasimamia nitaondoka nitayaacha……”
“Sasa tukimaliza huku tutaelekeza nguvu zetu Serikalini ambako nako kuna watu ambao hawafanyi sawa…..”
Monday, October 24, 2011
BANGO
Kinyume na matarajio ya Wengi, Man United walishindwa kabisa kuhimili vishindo vya majirani zao na mahasimu wao wa jadi. Hadi mapumziko City walikuwa wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Mario Balotelli.
Man United walicheza karibu kipindi chote cha pili wakiwa na mchezaji mmoja pungufu baada ya beki Jonny Evans kupewa kadi nyekundu kwa kumzuia Balotelli kwenda kumuona kipa wa United David De Gea.
Baada ya kutolewa kwa Evans, karamu ya magoli ilianza kwa City. Balotelli aliongeza bao la pili katika dakika ya 60. Sergio Aguero akafunga bao la tatu katika dakika ya 69. Edin Dzeko baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba alifunga bao la nne katika dakika ya 90, David Silva bao la tano na Dzeko tena kupiga msumari wa mwisho katika filimbi ya mwisho ya mchezo.
Bao pekee la kufutia machozi la United lilifungwa na Darren Fletcher katika dakika ya 81.
Matokeo haya yanaipa City pointi tatu ambazo zinaifanya kuendelea kuongoza kwa pointi tano zaidi ya United.
Mada Maugo (kushoto) na Joseph Odhiambo wakitambiana.
BONDIA Machachari nchini Mada Maugo amesema kuwa atamchapa kipigo cha mbwa mwitu bondia mwenzake kutoka nchini Kenya, Joseph Odhiambo kwenye shindano la raundi nane la ngumi linalotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba kesho(leo).
Aliyasema hayo jana muda mfupi mara baada ya kufanyika zoezi la kupimwa uzito kwa mabondia wote 12 watakaoshiriki katika pambano la leo.
Mada Maugo.
Huku akionekana kujiamini akitumia kauli yake ya uzawa, Maugo alisema kuwa yuko bomba na amewataka watanzania na wapenzi wa ngumi hususani wale wa Kanda ya ziwa wajitokeze leo kwa wingi kuupata uhondo na kushuhudia jinsi ambavyo anamshikisha adabu jirani yake bondia kutoka nchini Kenya Joseph Odhiambo.
Maugo v/s Odhiambo
Naye Joseph Odhiambo kutoka nchini Kenya, licha ya kukiri kumfahamu Mada Maugo katika ulimwengu wa masumbwi na kuwashukuru wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa, alisema kuwa hana hofu juu ya pambano hilo kwa madai kuwa ametoka mbali na anaamini atashinda katika pambano hilo la raundi 8 kwa uzito wa kilo 72 (middle weight).
Joseph Marwa.
Jumla ya mabondia 12 watashiriki, ambapo pambano la utangulizi litakuwa ni kati ya mabondia maarufu nchini Rashid Matumla ambaye atacheza na Bondia kutoka mkoani Mara Emma Kichele katika uzito wa kg 79 light weight na Joseph Marwa atafungua dimba na bondia Irandi Chacha naye kutoka Musoma katika uzito wa kg 83 cruiser weight.
Kiingilio katika pambano hilo kitakuwa ni Sh. 5,000 jukwaa kuu, Sh. 3,000 mzunguko na Sh. 1,000 kwa watoto.
Mabondia wengine watakaoshiriki na uzito wao kwenye mabano ni Elias Amos(56kg) VS Said Mazola(55kg), Pande Yusuph(55kg) vs Gabriel Paulo(56kg), Gasto Rweyunga(60kg) vs Deo Msangi(59), Ibrahim Wegoro(59) vs Nassor Ally(60kg). Mabondia wengine wanaotarajiwa kusindikiza pambano hilo ni pamoja na Frank Jofrey(64kg) vs Alex Nyakalungu(63kg) na Saliboko Juma(66kg) vs Danny William(68kg).
Katika pambano hilo, wasanii wa kizazi kipya John Walker, Ras Lion na D nob wanatarajiwa kuwatumbuiza wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na wapenzi wa mchezo kutoka mikoa jirani ya kanda ya ziwa.