Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika
kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya
kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017. Picha na Mathias Canal
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mhe Gelasius Gasper Byakanwa akimuonyesha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa jinsi magunia yalivyopangwa kwa ustadi ktika gala la kuhifadhia
Korosho la Mtanda mara baada ya Mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi
Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba
17, 2017.
Badhi ya wakulima wa
zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU)
wakifatilia mnada wa tano wa korosho katika kijiji na kata ya Chiungutwa,
Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara. Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa
wakiwasili Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kwa ajili ya
kujionea Mnada wa Korosho unavyoendeshwa, Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa (Wa Tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wazee
maarufu wa kijiji cha Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Wengine ni
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa (Wa Kwanza Kushoto), na
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia (Wa Kwanza Kulia).
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper
Byakanwa wakati wa Mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia
wakati wa ukaguzi wa ghala la Buko Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani
Mtwara wakati wa ziara yake ya kikazi
Mkoani Humo, Jana Novemba 17, 2017
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza ushauri sambamba na pongezi kwa kushiriki Mnada
wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Humo,
Jana Novemba 17, 2017
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa
wakikagua magunia ambayo tayari yamewasili katika Ofisi ya Ofisi ndogo ya Makao
Makuu ya Chama Kikuu cha ushirika mara baada ya kumalizika kwa mnada wa tano wa
Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Na Mathias Canal, Mtwara
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary
Machuche Mwanjelwa leo Novemba 18, 2017 amemuagiza Mrajisi wa vyama vya
ushirika kukamilisha haraka kazi ya uchunguzi kwenye Bodi za vyama vya ushirika
vya Mkoa wa Mtwara ili kubaini sababu zilizopelekea kuuzwa kwa magunia
kiholela.
Alisema kuwa kumalizika kwa
uchunguzi huo kutarahisisha kuchukuliwa haraka hatua kali za kisheri kwa wale
wote watakaobainika kukiuka sheria No 17 ya vyama vya ushirika.
Naibu waziri alitoa agizo hilo
wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa,
Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kugundua kuwa kuna viashiria vya
ukiukwaji wa taratibu katika upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia korosho
wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.
Sambamba na hilo Naibu waziri Mhe
Mwanjelwa wakati wote wa mkutano huo ameshuhudia malalamiko kutoka kwa wakulima
wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd
(MAMCU) kuhusu ucheleweshwaji wa upatikanaji wa maguni kutoka kwa mzabui,
Mapungufu ya kilo kati ya PDA na WHRs ghala kuu, ikiwa ni pamoja na kuchelewa
kwa malipo ya wakulima kwa njia ya benki kutoka kwa wanunuzi.
Katika ziara yake hiyo kilio cha
wananchi wengi na wakulima walisiitiza zaidi kuhusu kukosekana kwa magunia hayo
huku wakieleza kuwa wakati mwingine kuchelea kufika ama kutowafikia kabisa
jambo ambalo linachangia kupunguza thamani ya zao la korosho.
“Nataka Mrajisi ufanye na ukamilishe
kazi yako ya uchunguzi na baada ya kuipata taarifa hiyo hatua stahiki
zitachukuliwa kwa wale wote watakaogundulika kukiuka sheria ya nchi”
Amekaririwa Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa
Mbali na agizo hilo Naibu Waziri
pamoja na wabunge wa Mkoa wa Mtwara walipata nafasi ya kujionea mnada wa tano
wa ununuzi wa korosho unavyoendelea.
Hata hivyo Mnada wa tano
ulishuhudiwa Kilogramu 7,524,104 za korosho zikiuzwa kwa thamani ya zaidi ya
Bilioni 30.
Wakati huo huo Naibu Waziri Mhe
Mwanjelwa amesema Wizara itayafanyia kazi haraka mapendekezo ya tume iliyoundwa
na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa kufanya uchunguzi kuhusu
mwenendo mzima wa magunia pamoja na upatikanaji wake.