ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 28, 2012

YANGA BINGWA CECAFA 2012 BHAAAAASSsss..!!


Mashabiki wa Yanga mkoa wa Mwanza ambao walikuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia luninga kwenye hoteli ya Annox iliyopo Furahisha Kirumba jijini Mwanza, wakishangilia mara baada ya timu yao kupachika bao la pili mfungaji akiwa Said Bahanuzi katika dakika ya 90. Hadi Mwisho Yanga iliibuka kwa ushindi kwa kuifunga Azam Fc 2-0

Kipre Cheche kulia Mchezaji wa timu ya Azam FC akikokota mpira mbelea ya beki wa Yanga Nidir Haroub Canavaro wakati wa mchezo wa fainali ya kombe la Kagame inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, mpira umekwisha na timu ya Yanga imefanikiwa kutetea kombe la Kagame kwa mara ya pili mfurulizo baada ya kuitandika timu ya Azam FC goli 2-0 jioni hii.

Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya timu yao kupata goli la kuongoza katika mchezo huo.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Yanga na Azam FC pamoja na maafisa wa CECAFA na wachezaji wa timu zote mbili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akielekea kukagua timu kabla ya mchezo huo kuanza kulia ni , Crecentius Magori kushoto Makamu Mwenyekiti wa timu ya Yanga Clement Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa Azam FC mzee Mohamed Said
Timu zikiingia uwanjani kuanza mpambano huo.
PICHA NA FULL SHANGWE.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012 KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA, MAGHARIBI NA KATI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikiro.

WADAU wa vyombo vya habari pamoja na Waandishi wa Habari hapa nchini wameombwa kulipa umuhimu wa pekee zoezi la Sensa ya watu na makazi litakaloanza Agosti 26 katika maeneo mbalimbali kote nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Evarist Ndikiro alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kutoka Wilaya zote na mikoa ya Kanda ya ziwa, Magharibi na kanda ya kati ili kutoa elimu tosha ya zoezi la uhesabuji sensa kwa jamii inayowazunguka.

Msikilize mkuu wa mkoa kwa kubofya hapa.

Amesema Vyombo vya Habari vinao umuhimu mkubwa sana katika kuuandaa umma na kuhamasisha Wananchi katika kulipokea zoezi hilo na hatimaye kufanikisha malengo yaliokusudiwa na Serikali katika kupata takwimu sahihi na kuweza kupanga mipango madhubuti ya maendeleo.


Ndikilo amesema kupitia Wahariri na Waandishi wa Habari katika vyombo mbalimbali wanayo nafasi kubwa ya kuwafanya Wananchi wakaelewa lengo la zoezi hilo ambalo Serikali imewekeza fedha nyingi ili kuhakikisha inapata takwimu sahihi ili kuweza kuharakisha maendeleo yanayokusudiwa kwa Wananchi wake.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameongeza kuwa Sensa ya mwaka huu inaumuhimu wake ili kuweza kufanikisha malengo ya melenia hivyo licha ya vyombo vya Habari pekee kufanya kazi za uhamasisha Taasisi nyingine zikwemo za dini,za Serikali na zile zisizo za Serikali zinapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kufanikisha zaidi.


Wanahabari wa vyombo mbalimbali kutoka kulia ni Paschal Michael, Shomari Binda, Juma Ntono na mdau kutoka Radio Ekwizera
Ameongeza kuwa wale waliteuliwa kupata mafunzo hayo wamepewa dhamana kubwa na Serikali katika kufanya kazi hiyo hawategemei kupokea visingizio vya aina yeyote kwa yule atakayevuruga zoezi hilo na ndicho kilichopelekea kuweka mkazo kukakikisha wanakuwa makini katika kufatilia mafunzo watakayokuwa wanapewa kwa muda wote.


Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza amewataka Wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani na wasimamizi katika muda wote wa zoezi hilo litapokuwa linaendelea na kuongeza kuwa tayari wamekwisha kuziagiza kamati za ulinzi katika ngazi zote kuhakikisha kunakuwa na ulinzi kwa Wananchi na vifaa vyote vitakavyohusika katika zoezi hilo.


Said Ameir Afisa Uhamasishaji Sensa makao makuu kwa upande wake amesema kuwa Sensa haina maana ya kuhesabu watu tu bali ni mchakato mzima wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha au kusambaza takwimu, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote nchini na makazi yao kwa kipindi maalum.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mwanza.

Friday, July 27, 2012

BIBI ANAYEFUGA MISUKULE ACHOMEWA NYUMBA

Nyumba ilichomwa moto na kuvunjwa vunjwa.
Nyumba ya bibi Irene iliyo teketezwa leo kwa moto kwa tuuma za uchawi. Bibi huyo ambaye  amekuwa akisadikiwa kuwa na tabia ya kuwachukuwa watoto wa majirani zake kwa nguvu ya giza ameumbuka leo baada ya mtoto mmoja aliye potea kwa muda mrefu kwao na kutajwa kuwa alishafariki dunia kisha leo kijana huyo ana kwa ana akakutana na ndugu yake.

Mshangao ulitawala kwa ndugu huyo ambaye kwa ujasili alianza kumuuliza unaishi wapi na kijana yule ndo akamwelekeza kua nipo kwa bibi mmoja anaitwa bibi Irene na tunaishi na wenzangu wengine ambao nilikutana nao pale kwa bibi wakiongezeka siku baada ya siku.

Bibi huyo ambaye anatajwa kuwa mkali katika vitendo vya ushirikina, kakutwa na hilizi kibao na mara baada ya kupata kichapo ambacho hata ivyo akikuonyesha kumdhuru kwa licha ya kupigwa na mawe, bakora na hata vitu vingine vigumu vya hatari hakutokwa na damu, kuvimba nundu wala kuonyesha makovu ya majeraha mwilini mwake, aliwambia wananchi kua watoto wengine wapo ndani na alipo ambiwa awatoe nje alifanya mandingo yake na walio toka ni bata na kuku.

Kwa sasa bibi huyo anashikiliwa na jeshi la police jijini Mwanza kwaajili ya usalama wake.

PICHa zaidi zaja

BREAKING NEWS BARAZA LA MADIWANI JIJI LA MWANZA LAMNG'OA MEYA MANYERERE WA CHADEMA

Aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza kupitia CHADEMA Bw.Josephat Manyerere akitoa neno lake la Mwisho baada ya upigwaji kura ya kutokuwa na imani naye.

HATIMAYE BARAZA LA MADIWANI WA JIJI LA MWANZA WAMNG'OA MEYA MANYARERE (CHADEMA) KWENYE WADHIFA WAKE KWA KUPIGA KURA ZA KUTOKUA NA IMANI NAYE.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo limeng'oa kwenye wadhifa wake Meya wa Jiji hilo Bw.Josephat Manyerere(CHADEMA) kutokana na madai ya wajumbe wa baraza hilo kupitia barua walioiwasilisha Mei 24 mwaka huu iliyokuwa ikimtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kuitisha kikao cha dharula ili kumsomea Meya mashitaka yake.

Madiwani waliojiorodhesha na kufikia theluthi mbili ya wajumbe wapatao 17 kati ya wajumbe 33 wakiwa halali wa vikao vya baraza la madiwani wa Jiji hilo ambalo ilidai ni suala la kisheria na kanuni ya 80 za kudumu za halmashauri hiyo ambayo ipo wazi na inasomeka .

“Halmashauri inaweza kumuondoa Mwenyekiti au Meya madarakani kwa azimio linaloungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe kutokana na sababu yoyote ya sababu hizo ni (a) Kutumia nafasi yake vibaya(b),Kushiriki vitendo vya rushwa(c),Kushindwa kazi(d),Mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu na(e) lemavu wa kimwili aidha kiakili kwa kiasi cha kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti ama Meya.”ilifafanuliwa kanuni hiyo.
Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw.Kabwe ambaye kimsingi ndiye Katibu wa kikao hicho aliwasilisha kwa wajumbe ajenda moja tu iliyokuwa mezani ya wajumbe kutokuwa na imani na Meya hivyo kanuni ya 80 ya kumuondoa madarakani waliomba itekelezwe lakini kabla ya kufanya uamuzi huo baraza hilo lilitakiwa kujibadili na kukaa kama kamati.


  Baada ya kukubalika kwa hoja hiyo Mkurugenzi Bw.Kabwe aliwataka wajumbe wasiyo wa kikao hicho cha Kamati kutoka nje ya ukumbi huku viongozi waalikwa waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo,RAS Bi Dorothy Mwanyika na Wakuu wa wilaya za Nyamagana Bw.Baraka Konisaga na Bi.Amina Masenza  wakitakiwa kubaki kwa mujibu wa taratibu za Halmashauri.


Hatimaye baraza lilirejea kama kawaida yake baada ya kusikiliza utetezi wa Meya Bw.Manyerere ambapo katika madai kumi yaliyowasilishwa ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili kusomewa naye kujitetea kisha ukafanyika uamuzi wa kumpigia kura za wajumbe ili kumuondoa madarakani aidha kumuacha aendelee na nafasi yake ya Umeya.

Naibu Meya wa Jiji hilo Bw.Charles Chichibela(CHADEMA) ambaye ni Diwani wa Kata ya Mahina alitangaza matokeo ya kura hizo za wajumbe kama ifuatavyo alisema kwamba idadi ya wajumbe waliohudhulia kikao hicho wapatao 28 kati ya 33 ambao ndiyo halali lakini kutokana na wengine kuwa katika majukumu mengine ya kitaifa.

Akitangaza matokeo Naibu Meya wa jiji la Mwanza Bw. Chichibela alisema kuwa madiwani waliosema kwamba Meya Bw.Manyerere Ang’oke kwenye wadhifa huo ni wajumbe 20 na waliosema aendelee kubaki ni wajumbe nane tu (8 ) hivyo kwa mujibu wa matokeo hayo Manyerere hana tena sifa za kuwa Meya wa jiji la Mwanza.
Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye hapa ilikuwa awali kabisa akiendesha kikao hicho kabla ya 'kuvulishwa joho'.


Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye akitoa neno la mwisho nmara baada ya 'kuvulishwa joho'.

WABUNGE MLIKUWA WAPI KUTETEA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAKATI HOJA IKIPITISHWA?


MABADIKO ya Sheria ya Hifadhi za Mifuko ya Jamii ya mwaka 2012, iliyopitishwa Aprili mwaka huu, imeendelea kuzua mtafaruku sehemu mbalimbali nchini, huku wabunge wakishinikiza kuwa, sheria hiyo inapaswa kurejeshwa bungeni ili ijadiliwe upya.

Hata hivyo, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola alitofautiana na wenzake pale aliposema kuwa sheria inayolalamikiwa ilishapitishwa na Bunge hilo hilo, hivyo angependa kujua uhalali wa kujadiliwa tena bungeni.

Hapo ndipo twapaswa kujadili umakini wa wawakilishi wetu tuliowachagua kutuwakilisha mjengoni... yaani kwa hili lenye kugusa maslahi ya wengi kupitishwa kirahisi rahisi ... duh

Bofya hapa kusikiliza.

Thursday, July 26, 2012

WALIMU WA MICHEZO MARA WAMPASHAVU BULAYA

Kushoto ni Mbunge wa viti maalum vijana (ccm) Ester Bulaya.

Na Shomari Binda,
Musoma


Walimu wa michezo wa Shule za msingi na Sekondari Mkoani Mara wamemtumia salamu za pongezi Mbunge wa viti maalumu vijana (CCM) Esther Bulaya kwa kuona umuhimu wa suala la kutengewa bajeti nzuri ili kurudisha hadhi ya michezo ya Shule za Msingi na Sekondari Umitashumta pamoja na Umiseta.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati kikao cha Bunge la bajeti ya Wizara ya Habari,Vijana,Utamabuni na Michezo kikiendelea,Walimu hao walisema Mbunge huyo ameliona suala la msingi na kuweza kulizungumzia alipokuwa akichangia katika Wizara hiyo.

Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Msingi Kamnyonge A na mwalimu wa timu ya komani ya Umitashumta ya Wilaya ya Musoma Mjini Jedi Kunyenga alisema baada ya kurudishwa kwa michezo hiyo Mashuleni bado imekosa hamasa kutokana na kukosekana fedha za kutosha katika kuendeshea mashindano hayo ambayo yamekuwa yakiibua vipaji kutoka ngazi ya chini.

Alisema katika mashindano ya Mwaka huu kuanzia ngazi ya Shule,Kanda za Wilaya hadi Mkoa yaliyofanyika hivi karibuni yaliendeshwa kwa hali duni na kupelekea kukosa hamasa huku baadhi ya michezo ikishindwa kufanyika kwa kiwango kizuri na kupelekea baadhi ya wanamichezo kushindwa kuonyesha vipaji vyao.

Kwa upande wake Mwalimu wa michezo katika shule ya Sekondari Mmazami iliyoko Wilaya ya Butiama Mugisha Garibona alisema hata kwa upande wao hufikia hatua walimu kuchangishana pesa kwa kila Shule ili kuweza kufanikisha mashindano hayo kutokana na kukosa bajeti ya kuendeshea.

Alisema mashindano ya Wilaya waliyaendesha kwa ukata mkubwa na hata ilipofikia wakati wa kupeleka timu ya Mkoa katika mashindano ya Taifa Kibaha Mkoani Pwani iliwalazimu kupitisha tena bakuli ili kuweza kuwapeleka vijana kushiriki mashindano hayo ya Kitaifa.

Kwa pamoja Walimu hao walidai Mbunge Bulaya aliona mbali katika kuzungumzia suala la bajeti ya michezo mashuleni ili kuweza kuleta ufanisi katika mashindano hayo ambayo ni ndio chimbuko la kuibua vipaji vya michezo mbalimbali na badae kulitangaza Taifa kupitia michezo

Katika kuchangia Wizara hiyo ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Bulaya aliitaka Serikali kuweka bajeti kwa ajili ya michezo kwa shule za msingi (UMITASHUMTA) na sekondari (UMISETA).

Alisema pamoja na Serikali kurudisha michezo mashuleni lakini haifanyiki kwa ufanisi kutokana na ufinyu wa bajeti inayotolewa kwa michezo hiyo licha ya serikali kuamua kuirudisha mara baada ya kuifuta kipindi cha nyuma.

Mbunge Bulaya alitaka kujua Serikali imejipanga vipi kibajeti kuhakikisha inarudisha michezo mashuleni kama ilivyokuwa hapo zamani.

Akimjibu Mbunge huyo Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Amos Makalla alisema ni kweli ni kweli Serikali ilirudisha michezo shuleni na kumuomba Bulaya kupitisha bajeti ya Wizara yake ambayo pia imelenga kuendeleza michezo mashuleni.

NI YANGA V/S AZAM FAINALI CECAFA CUP 2012

Yanga


Azam Fc

Na Prince Akbar

BAO pekee la mwanasoka bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 110, jioni hii limeipa Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo, na sasa itamenyana na Azam FC keshokutwa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kiiza alifunga bao hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna Niyonzima ambaye alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia maamuzi ya refa, baada ya Kiiza kuangushwa.

Yanga waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo. Dakika tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.

Ikumbukwe mwaka jana, Yanga iliifunga Simba SC katika fainali bao 1-0 na kutwaa taji la nne la michuano hiyo, baada ya awali kutwaa Kombe hilo 1975, 1993 na 1999.

Mapema katika Nusu Fainali ya Kwanza, Azam FC iliitoa AS Vita kwa kuifunga mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na John Bocco ‘Adebayor’ na Mrisho Ngassa, wakati la Vita ya DRC lilifungwa na Mfongang Alfred.

Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Shamte Ally/Juma Seif, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Godfrey Taita, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende.

APR; Jean Ndoli Claude, Olivier Karekezi, Suleiman Ndikumana, Mugiraneza Jean, Johnson Bogoole, Lonel St Preus, Ngabo Albert, Iranzi Jean Claude, Mbuyu Twite, Dan Wagaluka na Tuyizere Donatien.

JOSE CHAMELEONE AFANYA MAANDAMANO KUSHINIKIZA AREJESHEWE NA SHIGONGO PASPOTI YAKE


Mwanamuziki maarufu Afrika Mashariki Jose Chameleone akiwa na wafuasi wake nje ya mjengo wa ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Uganda akishinikiza apatiwe paspoti yake inayodaiwa kushikiliwa na mtanzania Erick Shigongo (PICHA zote kwa hisani ya facebook ya Jose Chameleone)  

Sekeseke nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.

'Nahitaji paspoti yangu', 'Tanzania naomba mnisaidie',  'Eric Shigongo je uko juu ya sheria?' ni baadhi ya maneno yanayosomeka kwenye mabango ya waandamanaji hao.

Bado hakijaeleweka.


PINDA KUONGOZA MAZISHI YA MWALIMU WA MWALIMU J.K NYERERE

Enzi za uhai wake marehemu Mzee James Irenge ambaye alikuwa mwalimu wa baba wa taifa Julias Kambarage Nyerere katika shule ya Msingi Mwisenge, amefariki akiwa na umri zaidi ya miaka 120 na ameacha watoto 12, wajukuu 30 na vitukuu 15.
Na. Shomari Binda: Musoma

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda amewasili Mjini Musoma mchana huu kwa ajili ya kuongoza viongozi wa Serikali katika kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwalimu wa Mwalimu Nyerere mzee James Irenge aliyefariki dunia nyumbani kwake maeneo ya Mwisenge katika Manispaa ya Musoma.

Katika uwanja wa ndege Mjini musoma waziri pinda amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara john Tuppa,waziri wa nchi ofisi ya Rais Stevin wasira,mbuge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Wananchi.

Mzee Irenge, aliyekuwa na umuri wa miaka zaidi ya 120, alimfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge, kati ya mwaka 1934-1936. Hadi mauti yanamfika,

licha ya umri wake mkubwa, bado alikuwa na uwezo wa kusoma na kuandika mwenyewe bila kutumia miwani wala kusaidiwa.

Wiki kadhaa zilizopita, aliandika barua yake ya mwisho kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akimshuru kwa kumwezesha kumlipia fedha za dawa na chakula mambo yaliyokuwa kilio chake cha siku nyingi.

Mwalimu James Irenge atazikwa katika kijiji cha Busegwe kilichopo katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara jioni ya leo.


TSC WAANDALIWA DINNER KUPONGEZWA KWA KUCHUKUA UBINGWA NCHINI UJERUMANI


Shaffih Dauda (mwenye miwani ) akiwa na baadhi ya wachezaji wa TSC Mwanza wakipa msosi. Hapa ilikuwa ni saa tatu usiku ya Ujerumani. Kwa wale wanaojua baadhi ya nchi za ulaya jua huwa linachelewa kuzama.


Wadau wakipata maakuli kwenye hafla hiyo waliyoandaliwa vijana wa TSC

Mara menyu mara kamera...

Misosi full draft

Huyu ndiye mpishi


Maakuli hayoooo -  kwa wengine ndiyo ikawa sehemu ya futari.


Mmoja wa makocha wa TSC akipata msosi


Hi...


M-m-m...


Frank Sekule akigonga menu

GUNDUA KITU NA USIKU.....

Ni hali tulivu na mishemishe za kuhesabu katika barabara ya Posta jijini Mwanza ndani ya msimu huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni jana usiku majira ya saa 1:45.

Pembezoni mwa kingo kuelekea eneo la mataa barabara ya Nyerere nakutana na viumbe hawa wakiwa wametandazwa chini wakiuzwa.

Wengine tundikoni.

Chekshia kwa face..

Mdau akajichukulia mzigo...
Swali ni jeh umegundua chochote.

Mwanza hotel ground flow.

Geti kuu la Mz Hotel kuelekea Pizeria .