ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 4, 2023

WIZI WA MISUMARI HOSPITALI YA WILAYA YA PANGANI WAMCHEFUA MWENYEKITI WA CCM TANGA ATOA AGIZO KWA JESHI LA POLISI

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhamani kushoto akikagua nyaraka za manunuzi wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ukarabati wa Hospitali ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika wilaya hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman kushoto akisisitiza jambo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Panganai kulia wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani kulia akionyeshwa maeneo mbalimbali ya Hospitali ya wilaya ya Pangani na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo wakati apofanya ziara ya kushtukiza

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhamani kushoto akisisitiza jambo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani kushoto akimuonyesha maeneo yanayoendelea na ukarabati katika hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza ya Mwenyekiti huyo


Na Oscar Assenga,PANGANI.



MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rajab Abdurhamani amekerwa na wizi wa misumari katika Hospitali ya wilaya aya Pangani Mkoani Tanga huku akiliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na watakaowabaini walihusika kwenye tukio hilo hatua kali za kisheria zichukuliwe.

Hayo yalibainika wakati wa ziara yake wilayani hapa ya kushtukiza iliyokuwa na lengo la kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara yake hivi karibuni ambapo alisema pamoja na hayo wachukuliwe hatua za kinidhamu na asionewe mtu huku akisisitiza aliyetia mkono wake kuiba vifaa hivyo ashughulikiwe.

Akiwa Hospitalini hapo baada ya kukagua ukarabati wa Hospitali hiyo ambao unagharimu milioni 900 ndipo alipoelezwa wizi huo na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah wakati akipopata nafasi ya kuzungumza.

Mwenyekiti huyo alisema lazima washughulikiwe kwa kuchukuliwa hatua kali ili iweze fundishwa kwa watu wengine wenye tabia za namna hivyo maanaa zikivumiliwa vitakwamisha juhudi za kimaendeleo ambazo zinafanywa na Serikali.

“Kwa maana tutawapa lawama ndugu zetu waliopewa nafasi ya kusimamia miradi ikiwemo Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya na katika hili nikutake Mkuu wa wilaya usicheke na mtu na ukiacha hilo ninazo taarifa nyegine nimeweka watu wangu nitakapozithibitisha nitachukua hatua kuna vifaa viliibwa hapa hospitali lakini jana usiku baada ya kusikia ninakuja vimerudishwa watu hawaogopi wala hawana haya hilo halikubaliki”Alisema

Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kusimamia mradi huo wa ujenzi wa Hospitali huku akionyesha kuridhika nao kwa kiasi kikubwa kwa sababu thamani ya fedhana kinachoonekana kinaendana.

“Niwaombe wananchi wenzangu lazima tumhurumie Rais Wetu Dkt Samia Suluhu kwa maana anahangaika usiku na mchana muda wowote siku zote halali kwa sababu ya kuwasaidia Watanzania kuwaondolea adha zinazowakabili pia mbunge wetu anapambana sana kujenga hoja kwamba hospitali yetu na hapa Hospitalini ameleta Milioni 900 kwa ajili ya ukarabati hivyo tusiwakatishe tamaa viongozi wetu”Alisema

Aidha alisema kwa maana wakati miradi inapotekelezwa zinatumika fedha nyingi ambazo zimeletwa kwenye wilaya yenu katika utekelezaji wa miradi hiyo lazima wananchi wawe waaminifu ili lengo liweze kutimia lakini inapojitokeza watu wanaiba misumari inakwamisha juhudi hizo.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa wabunifu katika maeneo yao ikiwemo kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu anayejali matatizo ya wananchi anaowaongoza.

Mwenyekiti huyo aliwataka wananachi hao kuhakikisha mwaka 2025 hawana Rais mwengine zaidi ya Dkt Samia Suluhu mambo anayoyafanya ni makubwa ya kimaendeleo watapata muda kwenda kuyaelezea.

Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alimueleza Mwenyekiti huyo kwamba Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu aliwapelekea million 900 kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali ya wilaya hiyo huku akieleza wakati anapofanya ziara na kamati ya usalama kukagua ujenzi huo ndipo walipobaini uwepo wa wizi huo.

Alisema baada ya kulibaini hilo alimuelekeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya hiyo (DMO) aweze kuchukua hatua kutokana na kupotea magunia mawili ya misumari lakini hawakuripoti katika Jeshi la Polisi ili uchunguzi ufanyie na hatua zichukuliwe.

“Lakini nilitoe maelekezo kwa DMO achukua hatua ili sheria ichukue mkono wake lakini niliwataka lega ya vifaa vyote vinavyongia na kutoka vya zamani na vipya na hali yake ipoje bahati nzuri DMO aliniandikia taarifa na nilimueleza aende kufungua kesi na kesi tayari imeshafunguliwa kituo cha Polisi na uchunguzi unaendelea na hivi vilipotea wakati wanahamisha vifaa kutoka sehemu waliokuwa wamehifadhi kwenye stoo mpya”Alisema

Friday, November 3, 2023

AZIZ KI MCHEZAJI BORA, ROBERTINHO KOCHA BORA LIGI KUU OKTOBA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amechaguliwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Oktoba huku Mbrazil wa Simba SC, Robert Oliveira ‘Robertinho’ akishinda Tuzo ya Kocha Bora. Aziz, nyota wa Kimataifa wa Burkina Faso amewashinda kiungo mwenzake wa Yanga, Mkongo Maxi Mpia Nzengeli na mshambuliaji wa Simba, Mzambia Moses Phiri wakati Robertinho amewapiku Muargentina Miguel Gamondi wa Yanga na Mmarekani mwenye asili ya Somalia, Abdihamid Moalin wa KMC. Ungana na Jacob Mlay akiwa na George Kivumbi wa Jembe Fm. #jembefm #mwanza #samiasuluhuhassan #sports

MBUNGE MPINA ATAKA MAWAZIRI WAKAMATWE “WAZIRI HAJUI….SASA NAIBU WAZIRI ANAONGEA NINI?”

 

 

Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina akichangia taarifa tatu za kamati za kudumu za bunge za Kamati ya kudumu ya bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)na kamati ya kudumu ya bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022.

PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI (AFDP) YASAIDIA WAKULIMA KUKABILIANA NA ATHARI ZITOKANAZO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

 

Mtaalamu wa Masuala ya Ufuatilia na Tathmini Bw. Bernard Ulaya kutoka katika Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akizungumza wakati Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo (IFAD) Ulipotembea Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Nchini Mkoani Arusha (TOSCI).

Mtaalamu wa masuala ya Lishe na Jinsia kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bi. Florence Munyiri akizungumza mbele ya wataalamu hawapo katika picha, mara Ujumbe huo kutoka IFAD ulipotembelea Taasisi ya Tafiti za Mbegu za Kilimo (TARI) Seriani Arusha.


Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD),na wataalamu wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Missaile Albano Musa, kabla ya Ujumbe huo kuanza ziara ya kutembelea baadhi ya Taasisi za Kilimo zinazotekeleza Programu ya kuelendela Kilimo na Uvuvi (AFDP) Mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Missaile Albano Musa,na Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD),na wataalamu kabla ya Ujumbe huo kuanza ziara ya kutembelea baadhi ya Taasisi za Kilimo zinazotekeleza Programu ya kuelendela Kilimo na Uvuvi (AFDP) Mkoani humo.

NA; MWANDISHI WETU – ARUSHA

Imeelezwa kuwa, Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) imesaidia wakulima katika kufahamu na kutumia njia bora za kilimo cha kisasa zitakazowapelekea kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi.

Akizungumza wakati Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo (IFAD)ulipotembelea kituoni hapo Novemba 1 mwaka huu , Mtafiti kutoka Taasisi ya Tafiti za Mbegu Nchini (TARI) tawi la Seriani Arusha Bw. Shida Nestory amesema, Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi zake za Tafiti za Kilimo, (TARI) Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI) na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar, umesaidia wakulima katika kufahamu na kutumia njia bora za kilimo cha kisasa.

TARI Seriani Mkoani Arusha inatekeleza kupitia zao la maharage na Mahindi ambapo kwa mazao yote mawili mradi umewasiaidia kuwafikia wakulima ambapo mabwana shamba wanapewa mafunzo ya namna ambavyo wakulima wawaweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kupitia teknolojia mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya aina za mbegu mbazo zinaweza kustahimili kwenye maeneo ya ukame.

“Tari inawaelimisha wakulima juu ya matumizi ya teknolojia ya kuvuna maji na kuwa na uhakika wa kulima katika misimu tofauti na matumizi ya mbegu bora ambazo zinaweza kukinzana na magonjwa.” Alisisitiza

Kwa Upande wake Mtaalamu wa masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka katika Programu hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Bw. Bernard Ulaya alisema, Lengo la Timu hii ya IFAD kufanya ziara katika taasisi hizo ni kuangalia maendeleo ya program, mafanikio, changamoto zilizopo ili kama kuna maeneo yanayoweza kuboreshwa yaboreshwe.

“katika kituo cha Seriani program imeweza kuwasaidia kuwa na kitalu Nyumba mbacho kitaweza kuwasiaidia katika tafiti zao za kuweza kuzalisha mbegu mama na mbegu kwa matumizi ya wakulima.” Alifafanua

Wageni hao kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) pamoja na wataalam watatembelea maeneo hayo ya Kilimo katika Mikoa ya Arusha, Manyara Tabora, Morogoro na Dodoma kwa Upande waTanzania Bara Pamoja na Sekta ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu katika baadhi ya mikoa ya Unguja na Pemba.

Thursday, November 2, 2023

JINA KIBU DENIS LAIBUKA WAKATI SEKILOJO AKIICHAMBUA YANGA YA ZAMA ZAKE NA YA SASA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Alikuwa kiungo mshambuliaji mwenye akili nyingi na sifa ya kutoa pasi maridadi zilizozaa magoli, akinyumbulika dimbani akiwa na klabu yake iliyompa jina zaidi Young Africans. Hii leo Jembe Fm inapata nafasi ya kuzungumza naye machache, suala kuu likiwa ni nini utofauti kati ya Yanga ya enzi zake na Yanga ya sasa?
HISTORIA YA SEKILOJO CHAMBUA KWA UFUPI
Akitokea Tukuyu Stars Jina lake lilianza kuwika zaidi wakati wa kombe la Chalenji (Afrika Mashariki na Kati) mwaka 1992, yeye akiwa na timu ya pili ya Tanzania Bara iliyoitwa "Kaka Kuona" (timu ya kwanza iliitwa Victoria) na kocha wake alikuwa Sunday Kayuni akisaidiwa na Charles Boniface. Kundi lao lilikuwa Arusha. Walifaulu kutinga nusu fainali wakakutana na Malawi, Waliifunga Malawi 1-0 kwa mkwaju wa penati. Chambua ndiye alifunga hilo goli Fainali ilikuwa chungu kwake na Taifa kwani "Kaka Kuona" walifungwa 0-1 dhidi ya Uganda. Kadhalika Chambuka alikuwa mchezaji tegemeo wakati Tanzania Bara wakinyakua ubingwa wa Chalenji ya mwaka 1994 iliyofanyika Kenya. Kikosi hicho chini ya Sylesaid Mziray na Sunday Kayuni kiliwafunga Uganda kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Muunganiko wa Chambua, Lunyamila (Edibily) na Mohamed Hussein 'Mmachinga' iliwahi kuwa hatari kweli katika ligi kwa kufunga zaidi ya magoli 50 katika ligi.

VITUKO VYA MBWIGA MBWIGUKE NDANI YA JEMBE FM NA KIKOSI CHA PAMBA KILICHOTIKISA.

 

NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Hii ndiyo ilikuwa TP Lindanda Wana Kawekamo, shughuli ilikuwa pevu kwenyedimba la CCM Kirumba Mwanza. Ungempanga nani ungemwacha nani nje? Paul Rwechengura. Abdallah Bori. Hamza Mponda. Juma Amir Maftaha. Rashid Abdallah. George Masatu Hamis Nyembo. Khalfan Ngassa. Madata lubigisa. Ibrahim Magongo. Fumo Felician. David Mwakalebela. Rajab Risasi. Hamisi Selemani. Beya Simba,Ali Bushiri. Hussein Amani Masha. #mwanza #jembefm #sports #PAMBASPORTSCLUB #simba #yanga

"MSIONE KIMYA UMEME TUMEFIKIA HAPA" - DKT BITEKO

 NA ALBERT G.SENGO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko mnamo Oktoba 31, 2023 amewasilisha Azimio la Bunge la mapendekezo ya Tanzania kuridhia Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA). Je unafahamu kuwa kukamilika kwa mradi wa kimkakati wa Julius Nyerere kutasaidia nchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa umeme. Aidha Mhe. Dkt.Doto Biteko amesema Sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015 inatambua rasilimali kubwa ya Nishati Jadidifu iliyopo nchini na changamoto ya utekelezaji wa Nishati hizo. Tizama sasa mradi umefikia asilimia 92.74.

Wednesday, November 1, 2023

DC TANGA AZINDUA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO AIPONGEZA TAASISI YA ANSAAR MUSLIM KWA KUJITOA KWA JAMII

 

Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyani  wakati alipokwenda kuzindua zoezi la uchangiaji damu salama lililoratibiwa na Taasisi hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Athumani Kihara,ambapo vijana wa taasisi hiyo 600 wanatarajiwa kushiriki kwenye zoezi hilo kulia ni Mwenyekiti wa Idara ya Ustawi wa Jamii katika Taasisi ya Ansaar


MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo na kulia ni Matroni wa Hospitali hiyo Beatrice Rimoy

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Athumani Kihara akizungumza wakati wa halfa hiyo



Zoezi la Uchangiaji damu likiendelea


Zoezi la Uchangiaji damu likiendelea

Sehemu ya vijana kutoka Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji ambaye hayupo pichani


MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu mapema leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo
MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu mapema leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo

MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji katikati akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyan mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Taasisi hiyo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Athumani Kihara


Na Oscar Assenga, TANGA.

Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji leo amezindua zoezi la uchangiaji watu wanaochangia damu kwa wahitaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

Zoezi hilo lililokuwa limeratibiwa na Taasisi ya Ansaar Muslm Youth Centre kupitia Idara yake ya Ustawi wa Jamii Makao Makuu amba wameshirikiana na kituo cha Mahad Imam Shafii Tanga ambapo zaidi ya vijana 600 wanatarajiwa kuchangia damu.

Akizungumza mara baada ya kulizindua zoezi hilo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kitengo cha taasisi hiyo kutoa damu wamefanya jambo kubwa la dhawabu kuliko kitu chochote.

Alisema kwamba kwani wanapofanya hivyo wanawezesha kuwasaidia watu wengine wenye uhitaji ambao wanakumbana na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowahitaji kuongezewa damu.

“Niwapongeze sana na niwaambie kwamba jambo mnalolofanya hapa ni kubwa mnoo kutokana na kwamba unasaidia jamii yenye uhitaji”Alisema

Aidha alisema kwamba ni watu wachache ambao wanaweza kubuni jambo hilo hivyo niendelea kuiasa jamii kuwa na mwamko wa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuwa sehemu ya kusaidia wenye uhitaji.

“Niwapongeze kwa kuona umuhimu wa kuchangia damu nyie mmekuwa kuokoa maisha ya watu wengine kwani wakati mwengine wanapoteza maisha wengine hata ndugu zao wanaogopa kuwatolea damu lakini nyie mmejitoa hii ni sadaka kubwa asanteni sana”Alisema

Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba waandishi wa habari kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa jamii.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyan alisema taasisi hiyo kwa niaba ya vijana wao wameamua kujitokea damu kwa ajili ya wagonjwa.

Alisema huo ni utaratibu wao ambao wamekuwa wakiufanya mara kwa mara kusaidia jamii yenye uhitaji kwa kuhakikisha wanachangia damu katika maeneo mbalimbali.

Aidha alisema uanzishwaji wa taasisi hiyo malego yake ni kuelimisha jamii, kuhudumia jamii pamoja na kwamba ni taasisi ya kidini lakini wanatoa mafunzo hazimu ya mtume wao.

Alisema katika mafunzo hayo sio kwamba dini ni ibada tu bali ni huduma kwa jamii na yamekuja mafunzo mengi sana kuhusu umuhimu wa kuwasaidia wanyonge wa aina zote,masikini,walemavu.

“Lakini pia tunasaidia watu wenye mahitaji maalumu, waliopata matatizo ya kiafya wa aina zote za unyonge na sisi ndio mafunzo tunayopewa na mtume kuhudumia jamii na katika jumla ya kuhudumia jamii ni kuchunga afya za watu kwa sababu ibada haziwezi kufanyika kama watu ni wagonjwa”Alisema

Hata hivyo alisema pampoja na kwamba wao wamebobea katika masuala ya kielimu lakini huduma za jamii upande wa afya wameziona ni muhimu sana na walishawahi kufanya kambi mbalilmbali za kuwahudumia watu hasa wa macho kwa kutumia wataalamu wa ndani.

Pia alisema wao wamekuwa mstari wa mbele kuifikia jamii kwenye zoezi la kujitokea damu na litakuwa ni endelevu kwenye mkoa wa Tanga na nje ya mkoa huo.


Naye kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Athumani Kihara aliwashukuru Taasisi ya ya Ansaar Muslim Youth Centre kwa jambo ambalo wamelifanya kwa kujitolea huduma ya damu kwa wahitaji.

Dkt Kihara ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wakina mama na Uzazi alisema kwamba jambo wanalo lifanya ni muhimu sana kwa jamii kutokana na kwamba katika idara ambazo zinaathirika sana suala la damu ni la uzazi.

Alisema wamekuwa wakipata matatizo mengine ya wakina mama wamekuwa wakipata kutokana na upungufu wa damu kipindi cha ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua matatizo mengi yakiwemo moyo na figo .

Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Maabara Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Sinde Mtobu alisema mwaka huu hamasa imeendelea kuwa kubwa kwa mwezi sasa wastani wanapata chupa 600 .

Alisema hali hiyo imepunguza gepu la wahitaji ingawa bado wapo wahitaji  hivyo aliwapongezea sana Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre na wanawaomba waendelee kuwa pamoja nasi.


Hata hivyo alisema ikiwa kwenye Taasisi kila jamii yenye watu ikiwa na tukio la kuchangia damu mara moja tu kwa mwaka hakika changamoto ya damu itakuwa imekwisha hivyo wataendelea kushirikiana.

Sunday, October 29, 2023

TaSUBa KITOVU CHA MAFUNZO TASNIA ZA SANAA NA UTAMADINI NCHINI-DKT. BITEKO


#Amefunga tamasha la 42 la Kimataifa la Utamaduni Bagamoyo


#Aipongeza Wizara kwa kutangaza utamaduni wa nchi


#Sanaa iwe nyenzo kuunganisha wananchi


Imeelezwa kuwa, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ni kitovu cha mafunzo katika tasnia za Sanaa na Utamaduni nchini na Serikali imeendelea kuiboresha taasisi hiyo kwa kutoa fedha za kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. 


Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alipomwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na TaSUBa mkoani Pwani Oktoba 28, 2023.


"Niwapongeze Wizara kwa kuitangaza nchi yetu kwa kupitia kazi mbalimbali za utamaduni, sanaa na michezo. Aidha nakupongeza Waziri na wafanyakazi wa Wizara yako kwa kazi kubwa mnayoifanya kila mwaka katika kuliandaa na kuliendesha Tamasha hili kwa kipindi cha miaka 42 sasa," amesema Dkt. Biteko.



Ameongeza kuwa, tamasha hilo lina hadhi kitaifa na kimataifa kwani limehusisha ushiriki wa vikundi vingi vya sanaa vya hapa nchini na vya kutoka nje ya nchi zikiwemo Zambia, Kenya, Burundi, Uganda, Botswana, Afrika Kusini, Canada na nyinginezo.


Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameipongeza taasisi hiyo kwa kukuza utalii wa kiutamaduni (cultural tourism) hapa nchini jambo linalofanya kuendelea kuvutia utalii wa ndani na nje ya nchi.


 "Nawakaribisha na kuwahimiza vijana wote wa kitanzania wenye vipaji vya sanaa kuchangamkia fursa hii kwani sanaa sasa ni ajira hivyo tuitumie vyema kupitia taasisi hii," amesisitiza Dkt. Biteko.


Vile vile, Dkt. Biteko ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa na Mipango mikakati ya kuwasaidia wasanii nchini ili kupitia sanaa hiyo waweze kunufaika kiuchumi na kuitangaza nchi. Amesisitiza wapewe ushirikiano ili Sekta hiyo iwe na mchango mkubwa katika Pato la Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa, tamasha hilo limekua na mafanikio makubwa kwa Bagamoyo na mkoa wa Pwani. Amesema wadau wamejitokeza kwa wingi na kulifanya liwe tamasha bora nchini.

Naye, Katibu Mkuu  Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema kuwa, tamasha hilo ni fursa ya kutangaza utalii uliopo nchini kwa kuwakutanisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi. Amesisitiza kuwa mwaka 2024 tamasha litakuwa kubwa kwa kuwaleta wadau wengi zaidi nchini.






Wengine walioshiriki kilele cha tamasha hilo ni Mkuu wa Chuo TaSUBa, Dkt.Herbert Makoye, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash na Watendaji wa Taasisi za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wadau wa Sanaa na Utamaduni. Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka yalianza rasmi tarehe 26 mwezi huu na kilele chake ilikuwa Oktoba 28, 2023.