ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 21, 2018

RC MONGELA AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA WATENDAJI IDARA ZA AFYA KUJA NA MPANGO KAZI WA KUTEKELEZA KAMPENI YA UHAMASISHAJI UPIMAJI AFYA ILI KUBAINI MAAMBUKIZI VVU.



GSENGOtV/-/MWANZA.
Mwezi mmoja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya “Furaha yangu, Pima, Jitambue, Ishi’ jijini Dodoma kwa ngazi ya kitaifa sasa kampeni hiyo inazinduliwa hapa ikiwa ni Julai 21 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kwa ngazi ya mkoa.
Zaidi ya matarajio, viongozi na wananchi wake kwa waume hata watoto wamejitokeza kwa wingi ili kupima na kutambua afya zao.
Mabanda ya kupima maradhi mbalimbali yamesimikwa katika viwanja hivi ambapo ni fursa sasa kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella kuyatembelea mabanda hayo kujionea shughuli za afya na elimu zinazofanyika hata ikibidi naye kupima afya.
Hizi ni Dawa mpya zenye uwezo wa kufubaza na kukinga maambukizi dhidi ya VVU kwa asilimia 99 zilizoanza kutumika katika baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika, na sasa zimekuja ukanda huu wa Afrika Mashariki ndani ya Tanzania. Badala ya kumeza vidonge vingi sasa muathirika atapaswa kumeza tembe moja tu kujikinga na maambukizi.
Naam mara baada ya kupata elimu ya kutosha Mhe. Mongella hakusita kupima afya ambapo majibu yalitoka papo hapo.
 Akizungumza  wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Mwanza Dk Pius Masele amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi yameongezeka na kufikia asilimia 7.2 kutoka asilimia 4.2, mwaka 2011
 Kwa mujibu Dk Masele amesema ongezeko hilo linaufanya mkoa huo kuwa wanne ukitanguliwa na Njombe,Iringa na Mbeya.
Dk Masele ameeleza mikakati ya kupunguza maambukizi hayo ni  kuzifikia 90 tatu, ifikapo kwama 2030.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, amewataka watendaji  wa idara za afya katika wilaya zote za mkoa huo kuhakikisha wanaandaa mpango kazi utakaoainisha jinsi watakavyo tekeleza kampeni hiyo ili iwe na tija.

Kampeni ya furaha yangu inafadhiliwa na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) Tanzania kupitia mradi wake wa FHI360- Tulonge Afya wa miaka mitano,  Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS)  na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia kipengele cha kusaidia wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 45 kwa kipindi cha miezi sita .








MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI SONGWE


GSENGOtV

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili Mkoani Songwe na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa katika uwanja wa Ndege wa kimataifa Songwe mapema leo asubuhi ili kuanza ziara ya kikazi ya siku tano.

UKIONA MTU ANAKUJA KWENU BILA UTAMBULISHO PIGA BAKORA

GSENGOtV
NJOMBE

Licha ya kuwepo kwa taarifa za waganga wa tiba asili na tiba mbadala kutumia utaalamu walio nao kuwatapeli wagonjwa pindi wanapo hitaji huduma zao,hivi sasa hali imekuwa tofauti ambapo kumelipotiwa kuwepo kwa matapeli wanao tumia mgongo wa serikali kuwatapeli waganga wa tiba asili mkoani Njombe.

Kutokana na wimbi hilo la matapeli wanaodai kutoka serikalini kumemsukuma mratibu wa waganga wa tiba asilia na tiba mbadala kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa idara ya afya MATHIAS GAMBISHI, kuwaagiza waganga mkoani Njombe kuwaadhibu kwa viboko huku wakiwapeleka polisi mtu yeyote atakayebainika ni tapeli huku akijinadi kutoka serikalini.

Tarifa kutoka Njombe inasomwa na AMIRI KILAGALILA

Gambishi ametoa agizo hilo alipokuwa akisimamia uchaguzi wa viongozi wa waganga wa tiba mbadala na tiba asilia waliopo katika chama cha TAMETO na kuwaonya waganga kutokubaliana na faini ambazo zimekuwa zikitozwa na baadhi ya matapeli bila wao kuhoji na kupata taarifa zao kamili kwa kuwa serikali inapotuma maafisa hutumia utaratibu maalumu ikiwemo uthibitisho wa barua wenye nembo ya taifa.

insert......mratibu wa waganga

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RENATHA MZINGA askari SSP A.M.HAULE amesema kumekuwepo na matukio ya waganga kutapeliwa fedha hadi kiasi cha milioni mbili hali ambayo inaweza kujenga uhasama ndani ya jamii.

Aidha kamanda Haule ametoa wito kwa waganga kuacha kukaa na nyara za serikali ikiwemo pembe za wanyama ndani ya nyumba zao kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria hivyo endapo nyara hizo zimekuwa zikitumiwa katika shughuli zao ni vema kupata kibali kutoka kwa maafisa mali asili ili kuepukana na adhabu pindi watakapobainika.

insert.........kamanda haule

Nao baadhi ya waganga akiwemo ALLY MUHAGAMA maarufu kwa jina la dk.sagasaga na Saidi mlwale ambaye ni makamu mwenyekiti wa TAMETO mkoa wa Njombe wameiomba serikali kutoa vyeti vya uponyanyi kwa baadhi ya wahubiri ambao wamekuwa wakijinasibu wanaponya huku baadhi yao wamekuwa wakiipotosha jamii.

insert........waganga akiwemo dk saga saga

Aidha kwa upande wake RAISI wa chama cha waganga wa tiba asili na tiba mbadala TAMETO nchini Tanzania SHALIF WIKETYE amewagiza waganga waliopo katika chama hicho kujisajili katika ofisi ya mratibu wa waganga mikoani mwao ili kuepukana na utapeli pamoja kukamtawa kwa makosa kutoa huduma zao bila vibali kutoka serikalini. 

Friday, July 20, 2018

GUNDUA MENGI MTAANI KUPITIA KAMPENI YA FURAHA YANGU


Kampeni ya uhamasishaji watu kupima Afya imeendelea tena leo katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza, wilaya za Ilemela na Nyamagana zimehusishwa na mpango huo.
Mmoja wa balozi wa uhamasishaji kutoka mradi wa Furaha Yangu Bi. Zainab akitoa elimu ya kunini tunapaswa kupima na kuzijua afya zetu, na hapa ni katika eneo la kituo cha mabasi Nyakato Buzuruga jijini Mwanza.
Maswali ya kitaalamu yataulizwa jumamosi hii ya tarehe 21 viwanja vua Furahisha jijini Mwanza ambapo ndiko kwenye shughuli za upimaji na tiba kwa maradhi mbalimbali kama vile kifua kikuu, moyo, presha, upimaji wa vvu na magonjwa mengine.
Chakufurahisha suala hili limekuwa na mvuto kwa watu wa kila rika, nayo maswali hayakukosekana.
Uhamasishaji na uelimishaji kwa maswali madogo umefanyika sanjari na kuwahamasisha wadau kuibuka Jumamosi hii viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Swali la kwanza, swali la pili na swali la............
Naam vijana nao wameukubali mpango huu wa kujua afya.
Katikati ya wadau.
Ubishi na ubishani hapa palinoga.
Bodaboda akajishindia kofia kwa kujibu vyema maswali.
Mama huyu alijishindia fuko la mama kwa kuhamasisha watu kujitokeza kupima akitumia lugha ya Kikerewe.
Wanafunzi nao wamevutiawa na mpango huu wa kupima.
Kamanda akajinyakulia zawadi ya Tshirt.
Vaaaa mwanangu.
Tokelezea.
Kofia kwa rasta.......
Pima Jitambue Ishi..........!!

AMNESTY WAPINGA HUKUMU YA KIFO KWA MISS MAGEREZA.



Shirika la Amnesty International limetoa wito wa kubatilishwa kwa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya malkia wa urembo gerezani nchini Kenya Ruth Kamande.

Mwanamke huyo alihukumiwa kifo Alhamisi baada ya kupatikana na kosa la kumuua mpenzi wake miaka mitatu iliyopita katika mtaa wa Buruburu, Nairobi.

Bi Kamande, 25, amekuwa akizuiliwa rumande katika gereza kuu la wanawake la Lang'ata jijini Nairobi ambapo mwaka 2016 aliibuka kuwa malkia wa shindano la urembo lililoandaliwa humo gerezani.

Mkurugenzi mkuu wa Amnesty International nchini Kenya Irungu Houghton amesema mwanamke huyo anafaa kusaidiwa kujirekebisha badala kuhukumiwa kifo.

"Tunasikitika kwamba Kenya inaendelea kutoa adhabu hii katili, isiyo na utu na iliyopitwa na wakati. Hukumu hii ni pigo kwa rekodi nzuri ya Kenya ya kuendelea kubadilisha hukumu za kifo kuwa hukumu za vifungo jela," amesema.

"Hakuna ushahidi wowote wa kuaminika kwamba hukumu ya kifo huwazuia watu kutekeleza uhalifu zaidi ya adhabu za aina nyingine. Hukumu hii ya kifo inafaa kubatilishwa mara moja na Ruth Kamande asaidiwe kurekebisha tabia."

Ingawa huku ya kifo huendelea kutolewa kwa makosa ya mauaji na wizi wa kutumia mabavu nchini Kenya, haijatekelezwa kwa mfungwa yeyote nchini Kenya katika kipindi cha miaka 30.

Rais Uhuru Kenyatta na mtangulizi wake Mwai Kibaki walibadilisha hukumu ya wafungwa wengi waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita na kuwa vifungo vya maisha jela.

Wafungwa takriban 6,747 wamenufaika kupitia hatua hiyo.


Hukumu ya kifo iliondolewa katika mataifa 139 duniani lakini bado kuna nchi zinazotekeleza hukumu hiyo zikiwemo Marekani, China, Pakistan na Saudi Arabia.

SAUTI - CHADEMA NJOMBE WALAANI VIKALI WAGOMBEA WAO KUKATALIWA NA WASIMAMIZI CHANZO WATAJWA KUWA SI RAIA



GSENGOtV
NJOMBE

Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoani Njombe kimelani Vikali Kitendo cha wasimamizi wakuu wa Uchaguzi katika halmashauri ya Wilaya ya Makete na Wanging'ombe kwa kuyaondoa Maajina ya mwagombea wake wawili wa udiwani katika Kata ya Isapulano na Itulahumba kwa madai ya kwamba wamekosa sifa za kuwania nafasi hiyo.

Msmamizi mkuu wa uchaguzi wilayani Makete ambae pia ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo Fransis Namaumbo Anatajwa kumuondoa mtia nia wa Chadema katika kata ya Isapulano ndugu Dadiso Tweve kwa madai ya kwamba sio mkazi huku mkurugenzi wa halmashauri ya Wanging'ombe Amina Kiwanuka Akimuondolea Sifa ya kugombea Mgombea wa Kata ta Itulahumba Mgute Yohane kwa madai ya kutilia shaka mihuli iliyopigwa kwenye fomu yake.

TAARIFA KUTOKA NJOMBE INASOMWA NA AMIRI KILAGALILA


Kata ya Isapulano ya wilayani Makete inalazimika kurudia uchaguzi Augost 12 baada ya diwani wake kujiuzuru na kujiunga na chama cha mapinduzi huku katika kata ya Itulahumba ya wilayani Wanging'ombe ikirejewa baada ya diwani wake kufariki dunia.

BAADA YA HUKUMU YA WEMA WAKILI WAKE ANENA HAYA.

Wakili wa wema sepetu Albert msando amedai kuwa iwapo wema hata badilika baada ya mahakama kumkuta na hatia na kuhukumiwa mwaka mmoja jela au kulipa faini ya shilingi millioni 2 atakuwa ni mtu wa ajabu.

Vilevile amedai kuwa amemsahauri wema awe balozi mzuri na kuwa na wajibu wa kuwa balozi wa kulisemea swala hili la madawa  ya kulevya na kulikemea na ameendelea lusema kuwa changamoto kubwa ya wasanii wanaigia na kujikuta hawana mambo mengi ya kufanya.

Amemalizia kwa kusema kuwa utofauti wa kesi ya wema na wakina TID ni kwamba swala la wema lilihitaji ushahid na kuthibitishwa ndio mana lmechukua muda mrefu hali kuwa swala la wakina TID wao walikubali moja kwa moja

BILIONI MBILI KUWEZESHA WAHITIMU WA FANI ZA KILIMO SUA KUANZISHA MIRADI YA KILIMO BIASHARA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay akiongea katika hafla ya makubaliano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo iliyofanyika chuoni hapo mjini Morogoro. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini halfa hiyo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda akitoa shukrani zake za pekee kwa Taasisi binafsi ya kusaidia Sekta ya kilimo nchini (PASS) jinsi walivyojitoa kuwasaidia wajasiliamali kujikwamua katika kilimo kibiashara ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa elimu.
Wageni pamoja na wakuu wa idara mbali mbali katika chuo kikuu cha SUA mjini Morogoro wakimsikiliza kwa makini makamu wa chuo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay (katikati waliokaa) na Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda (kwanza kushoto) wakiasaini mkataba wa makubaliano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa PASS na Chuo Kikuu cha SUA.
Wakibadilishana mkataba wa makuabaliano.
Wakionyesha mkataba kwa furaha.
Picha ya pamoja baina yao.
Wakiagana kwa furaha mara baada ya tukio la makabidhiano kumalizika.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Taasisi binafsi ya kusaidia Sekta ya kilimo nchini (PASS) imetenga kiasi cha shilingi Bilioni mbili kwa ajili ya kuwawezesha Wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kuweza kuanzisha miradi ya Kilimo Biashara .

Upatikanaji wa fedha hizo umelenga uanzishwaji wa miradi 100 ya majaribio katika Chuo hicho kupitia mpango wa Maalumu utoaji wa Mazoezi na Majaribio kupitia Vituo Maalum (Incubators)  vyenye lengo la kutoa uzoefu kwa Wajasiliamali Vijana .

Hatua hiyo imebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay baada ya kuingia makubaliano  na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya  kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo.

“Baada ya kuona uwepo wa changamoto ya Wahitimu katika masuala ya kilimo pamoja na fani nyinginezo wakishindwa kushiriki katika shughuli za kilimo-biashara baada ya kukosa mitaji PASS kupitia Idara yake ya Agribusiness Innovation Center (AIC)  imeona ije na mpango huu”

Amesema mpango huo  utawawezesha Wajasiliamali vijana kupata mitaji pamoja na nyenzo mbalimbali katika maeneo maalumu kwa lengo la kuwaandaa kuwa Wajasilimali watakao weza kumiliki Miradi ya Kilimo-Biashara.

Bwana Bohay amesema kipaumbele kitatolewa kwa Wajasiliamali Vijana watakaojihusisha na uzalishaji wa mbogamboga kwenye mahema (greenhouse), ufugaji wa samaki, Kuku, mbuzi, usindikaji na viwanda vidogo vya kuzalisha bidhaa zinazotokana na kilimo kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

“Wenzetu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine (SUA)  wametoa eneo la kutoshereza wa miradi ya Wajasiliamali Vijana kwa lengo la kuhakikisha vijana wetu wanapata mahali pa kuanzia kabla ya kujitegemea” alisema Bwana Bohay.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof, Raphael Chibunda amesema kuwa ushirikiano huo na Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo PASS umekuja wakati muafaka na kuwataka wahitimu pamoja na watafiti chuoni hapo kuchangamkia fursa hiyo.

“ Kwetu sisi mradi huu wa kuwalea wahitimu wetu kwa kuwapatia mitaji, nyenzo na ushauri na maeneo maalumu ya kutekeleza kile walichokisoma darasani kwa vitendo ni faraja sana kwani siku zote tumekuwa tukiwaandaa vijana wetu waweze kukabiliana na changamoto za Maisha huko mtaani kwa kutumia elimu waliyoipa hapa chuoni”

“Sasa tunawapa fursa hiyo hapahapa chuoni kabla hawajaingia huko mtaani……,wataondoka hapa wakiwa ni wajasiliamali mahili wa kilimo Biashara na mchango wao Kiuchumi kwa taifa na jamii utaongezeka sana. alisema Prof Chibunda .

Mpango huu unatajwa kuwa suluhu ya changamoto ya ajira kwa Wahitimu hususani wa masuala ya Kilimo ambapo kwa vijana watakao pitia katika vituo maalumu vya uwezeshaji (Incubators) watakuwa na uwezo wa kujiajiri na kujiendeleza kiuchumi.

UJUMBE WA AFYA KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA MWANZA


Jumamosi hii 21 July 2018 ndani ya viwanja vya Furahisha jijini Mwanza tukutane pale.


WAZIRI MKUU WA KOREA KUTUA NCHINI KWA MUALIKO WA MAJALIWA.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon atafanya ziara ya kikazi nchini kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kuanzia tarehe 21 hadi 23 Julai 2018. Ziara hiyo itakuwa ya kwanza kufanywa na kiongozi wa ngazi ya juu kutoka Jamhuri ya Korea tangu nchi zetu mbili zianzishe mahusiano ya kidiplomasia mwaka 1992.

Madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kufungua zaidi fursa za ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi katika ngazi na sekta mbalimbali.

Waziri Mkuu Lee atafuatana na ujumbe mzito wa maafisa wa Serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa. Ujumbe wa wafanyabiashara utakaoongozana na Lee unatarajiwa kukutana na wenzao wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Wafanyabiashara uliopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 23 Julai 2018. Mkutano wa kwanza ambao ulikuwa na mafanikio makubwa ulifanyika Seoul mwezi Februari 2018.

Lee Nak-yon atawasili nchini saa kumi na mbili na nusu jioni (12:30) ya tarehe 21 Julai 2018 na atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku inayofuata, Waziri Mkuu Lee na mwenyeji wake Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), watafanya mazungumzo rasmi jijini Dar es Salaam na baadaye watashuhudia uwekaji saini wa mkataba wa kuondoa hitaji la visa kwa wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za utumishi (diplomatic and official/service passport).

Aidha, Lee atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa ajili ya kusalimiana.

Jamhuri ya Korea ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania ambapo kupitia  Shirika la Kimataifa la Maendeleo (KOICA) na Mfuko wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (EDCF) yamekuwa yakitoa misaada na mikopo mingi ya masharti nafuu kwa Tanzania ikiwemo misaada ya fedha katika bajeti, ujenzi wa miundombinu ya jamii, mafunzo ya muda mfupi na mrefu, wataalamu mbalimbali wa kujitolea, vifaa na mashine kwa ajili ya sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.

Baadhi ya miradi ambayo imegharamiwa na Serikali ya Korea ni pamoja na Mradi wa kuboresha Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Chanika, Mradi wa Mfumo wa Usajili wa Meli na Mabaharia kwa Njia ya Mtandao Zanzibar, Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Taifa ya Taaluma na Tiba (MUHAS) kampasi ya Mloganzila na ujenzi wa daraja katika mto Malagarasi.

Vile vile, Korea ni mshirika mkubwa katika kusaidia maendeleo ya Bara la Afrika ambapo hivi karibuni katika mkutano wa Sita wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na Africa (KOAFEC VI) uliofanyika mwezi Mei 2018, Busan, Korea ambapo Serikali ya Korea ilitangaza msaada wa Dola za Marekani bilioni 5 kwa ajili ya Bara la Afrika kwa kipindi cha mwaka 2018/2020. Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika na msaada huo.

Thursday, July 19, 2018

WANAUME MWANZA WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUPIMA VVU NA MKUU WA MKOA.




  GSENGOtV
Wakati takwimu za kitaifa, zikionesha kuwa zaidi ya Watanzania milioni 1.4 wanaishi na VVU huku mikoa inayoongoza na asilimia yake kwenye mabano ikiwa ni Njombe (11.4), Iringa (11.3), Mbeya (9.3) na Mwanza kwa asilimia 7.2.

Katika takwimu za mkoa wa Mwanza kufikia lengo la Tisini tatu (90,90,90) zinaonyesha kwa 90 ya kwanza ni asilimia 53 tu ya WAVIU wanafahamu hali zao, huku idadi kubwa iliyobaki hawajui hali zao za maambukizi hivyo hawajaanza kutumia dawa za kufubaza VVU.




Mbele ya waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameyatanabaisha hayo hii leo akiongeza kuwa kwa 90 ya pili, waliopimwa na kugundulika kuwa na VVU na kuanza kutumia dawa ni asilimia 74, na takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wapo wengi kuliko wanaume. Kwa 90 ya tatu, takwimu za mkoa zinaonesha kuwa ni asilimia 72 tu ya walioanza kutumia dawa na kuwa na ufuasi mzuri wa dawa na wamefanikiwa kufubaza virusi ambao hata hivyo idadi kubwa ni wanawake ndiyo wanaotimiza masharti.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wapo katika picha nyingine na kulia ni John Bosco Basso Mtaalamu Mwandamizi wa Mabadiliko ya tabia ya jamii USAID Tulonge. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wapo katika picha nyingine na kushoto kaketi Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza Dr. Thomas Rutachunzibwa, na kulia ni John Bosco Basso Mtaalamu Mwandamizi wa Mabadiliko ya tabia ya jamii USAID Tulonge. 
Habari tukioni.
Kampeni hii ina dhamira ya kutoa taarifa, kuelimisha na kuisaidia jamii kupima virusi vya ukimwi na kutoa matibabu yanayorefusha maisha iwapo watagundulika kuwa na maambukizi ya VVU.
Mkoa wa Mwanza umepokea agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu ambapo uzinduzi rasmi wa Kampeni utafanyika Jumamosi ya tarehe 21 July 2018 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

NAIBU WAZIRI KANDEGE AAGIZA KITUO CHA AFYA LUBANDA KIKAMILIKE KWA WAKATI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Josephat Kandege (aliyevaa koti jeupe) akitoka kukagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Lubanda kinachoonekana  nyuma yake na kuhimiza ujenzi wa kituo hicho ukamilike kwa wakati uliopangwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Josephat Kandege akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kabla ya kuanza ziara ya kikazi kukagua ujenzi wa Vituo vya afya.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Josephat Kandege jana amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Ileje kukagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Lubanda na kuagiza ujenzi wa kituo hicho ukamilike kwa wakati uliopangwa.
Kandege amesema uwepo wa mvua nyingi ambazo huanza mapema katika wilaya hiyo utakwamisha kituo hicho kukamilika mapema endapo hawatautumia muda huu ambao hauna mvua kumalizia ujenzi kwa haraka.
“Ninaamini kama isingekuwa mvua nyingi kunyesha pamoja na kuharibika kwa barabara nimatumaini yangu ujenzi wa kituo hiki cha Afya ungekuwa umekamilika, sasa jitahidini kumaliza haraka kabla ya mvua kuanza, ili mradi huu ukamilike na uanze kuwanufaisha wananchi wa Lubanda na maeneo ya jirani”, amesisitiza Kandege.
Aidha amemuelekeza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ileje Enock Mwambalaswa kubana matumizi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ili fedha zitakazobaki zitumike kumalizia jengo  la wazazi na wagonjwa wa nje ambalo lilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na kujenga nyumba nyingine za watumishi.
Kandege amemuelekeza pia Mhandisi wa Halmashauri ya Ileje kuangalia uwezekano wa kuunganisha wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji ili kuendana na ramani mpya za vituo vya afya, aidha ameelekeza utaratibu wa kufikisha umeme kituoni hapo hasa kupita mpango wa REA uanze kufanyika haraka.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi amemueleza Naibu Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandege kuwa halmashauri ilipokea shilingi milioni mia tano kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Lubanda na mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 95 na matarajio ni kuwa kituo hicho kitakamilika ifikapo Julai 25, 2018.
Mnasi amemshukuru Naibu Waziri Kandege kwa kufanya ziara ya kukagua kituo hicho na amemuhakikishia kuwa atazingatia maelekezo ya kuwapangia watumishi wapya wa sekta ya afya watakaoajiriwa hivi sasa katika vituo vya afya vinavyojengwa ili vitoe huduma kwa wananchi mara baada ya kukamilika.